Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

sisi wazanzibar hatuna shida na serikali 1 km hamtaki serikali 3 basi tugawane mbao hatuna shida ya muungano badala ya kutafuta tanganyika yenu munangangania muungano tu
 
The United States of Tanzania.one country with two states namely tanganyika and zanzibar.tuwe na mfumo kama wa marekani
 
mimi hata sasa huo muungano wenyewe kichefu chefu tu,kila m2 kwao inatosha.
 
Kwa hotuba ya Rais ni kwamba hakuna muungano tena, sisi wa Bara hatutaki tunataka Tanganyika yetu. hawa Wazanzibar hatuwataki huku waondoke warudi makwao,wanadai hawataki muungano lakini nchi yetu wameifanya shamba la bibi yaani kila mtu anakuja kuvuna,hii imetosha. na kama kweli Wazanzibari hamuutaki muungano anzeni kuondoka kwa makundi ndipo tutajua kuwa hampendi lakini hii mambo bana ya " baniani mbaya kiatu chake kizuri" hapana bana sasa imetosha.ondokeni mrudi pemba na unguja
 
Utangulizi: Zanzibar kiuchumi inapata asilimia 4% kwenye mchango wa taifa ingawa wanachangia kiasi kidogo kiuchumi kuliko wanachopata. Hivyo kutaka asilimia 4% iongezwe ni kwasababu gani hasa? Idadi yao vilevile ni ndogo kuliko asilimia 4%.
Mambo ya Mafuta na madini: Zanzibar wanataka mambo ya mafuta na madini yatolewe kwenye mambo ya muungano lakini kwa sasa kwenye asilimia 4% wanayopata kuna mchango wa madini na mafuta ambayo inajumuisha gas. Sasa kama wanataka basi asilimia ya mchango nayo ipunguzwe kwa asilimia ya mchango wa sekta hizo. Kama mafuta na madini mfano yanachangia asilimia 20% basi mchango wa uchumi ushuke kutoka 4% ya sasa mpaka 3.8% na wakipata gas, mafuta, na madini ni ya kwao.
Serikali Mbili: Tukisema serikali mbili zibakie na je ni mabadiliko gani sasa Zanzibar wanataka na Tanganyika itanufaika vipi? Inavyoelekea Zanzibar inataka zaidi tu bila kunufaisha taifa wala Tanganyika mfano wanataka mchango wapewe asilimia 25% je ni kwa misingi ipi?, wanataka kujitegemea zaidi kiserikali kwa ufupi hawataki ndoa bali wanataka pesa zaidi. Hivyo muungano wa serikali mbili hutabadilisha kitu zaidi ya Tanganyika kutoa zaidi na zaidi bila misingi yeyote ya uchumi na kunyonya watanzania wengi wenye umasikini kwa kufurahisha wachache . Pesa za uchumi zinatumika kutunza viongozi Zanzibar wakati wananchi wake wengi wanacheza bao tu siku nzima.
Serikali tatu: Wanaotaka serikali tatu wanajua fika kwamba muungano utavunjika lakini wamechoka kuendelea kutoa na kutoa hivyo hii italeta nchi mbili tofauti kabisa na Tanganyika ikizaliwa haitakufa.
Serikali Moja: Serkali moja ndiyo soluhisho kama nchi hizi mbili zinataka kufuta ubaguzi na kuwa na maendeleo ya kweli. Serikali mbili na usawa na haki kwa wote.
Muungano kuvunjika: Serikali mbili vilevile zitaleta muungano kuvunjika kwasababu itafika wakati Tanganyika wanaona upendeleo wa hali ya juu na kama serikali haitafanya mabadiliko basi wananchi ipo siku watafanya mabadiliko kwa nguvu.
 
Mimi nakubaliana na ww, kuwe na nchi moja serekali moja, lakini jina la nchi iitwe Zanzibar na makao makuu ya serekali ya wepo Zanzibar
 
Umenisoma bila ya hivo, ukivunjika muungano Zanzibar tunajipanga miaka mitano then tunai Dar es salam, mtwara, tanga, bagamoyo, mombasa kuwa ni maeneo halali ya Zanzibar kabla ya kuja mjerumani Tanganyika, uaije ukashanga wa zenji watakapo kuja na full document
 
Mgawo wa Zanzibar ni asilimia 4.5% ya misaada ya nchi wafadhili!.
Dawa ya hili ni serikali 3, kila mmoja aubebe mzigo wake!, au serikali moja tuibebe jumla hiyo Zanzibar iwe reduced to mkoa wenye wilaya 2, rais wao awe ni RC tuu!.
Pasco
 
Mimi nikokinyume na wadau wengi ambao wanashadadia serikali mbili kwa tatu. Mimi ninasema kama nchi ni moja basi hata serikali iwe moja tu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Rais awe mmoja na pasiwe na cheo cha makamu wa rais badala yake waziri mkuu atoke upande wa pili wa muungano ambao haukutoa rais. Rais atawale miaka 8 kwa mhula wa 4 by 2, kisha upande wa pili wa muungano ndio uwe na haki ya kutoa rais. Baraza la mawaziri liwe 2/3 kwa 1/3 Tanganyika wawe 2/3 na Zenji wawe 1/3 ya mawaziri wote. Bunge liwe moja tu la muungano. Mikoa iwe majimbo na Zenji iwe na majimbo pia. Jeshi liwe moja na pasiwe na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano yote yawe ya muungano maana nchi ni moja yenye serikali moja. Ni mtazamo wangu japo unaweza kubezwa na watu kadhaa.
 
Nimekuwa nikifuatilia malumbano na mijadala mbalimbali inayohusu muundo upi wa muungano unafaa kwa nchi yetu. Malumbano makubwa yapo kwenye ama muundo wa serikali 3, hiyo ni kwa mujibu wa Tume ya mabadilko ya Katiba baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi au muundo wa serikali 2 kwa mujibu wa CCM.

Kwakuwa malumbano haya yanayoendelea kwenye bunge maalumu la Katiba hayalekei kupatiwa ufumbuzi maana kila mmoja anavutia kwake, Napendekeza tuanze kuelekeza nguvu zetu kwenye Muundo wa serikali moja. Muundo wa serikali moja hautakuwa na changamoto zote zilizotajwa kwenye Muundo wa serikali 2 na 3.

Kama kweli tuna nia ya dhati ya kuulinda huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi SERIKALI MOJA NDIO SULUHISHO LA KUDUMU.

Nawasilisha.
 
Unaongea IMPOSSIBLES, jaribu ku-analyze situation kwanza kabla ya kutoa ushauri. Unataka kusema kama wazinzibar wameamua kubadilisha katiba yao ambayo inatambua kuwa kuna nchi mbili ndani a jamhuri ya Tanzania, wataweza kukubali kwenda kwenye serikali moja??!!!
 
Mtoa mada hajayasikia maneno haya ?
  • zanzibar kumezwa
  • Historia ya watu wa zanzbar kupotea
  • wazanzibar hawataki

Hayo mawili ya mwanzo hutolewa mpaka na jumuiya za kimataifa kama marekani na uingereza, juzi pinda kazema hivyo na kikwete aliyasema na warioba aliyasema. kwa conclusion hiyo MUUNDO HUO HAUPO NA HAUTEKELEZEKI. hata uingereza imeungana inaheshimu historia ya wales na scotland hayo ni muhimu kuyajua.
 
zanzibar ni moja ya miji yenye historia ya dunia,hivyo wanaamini kufanya serikali moja kutazua kushindwa kutunzwa kwa historia hiyo kama ilivyoshindwa bagamoyo,dar,tabora na kigoma. kote kuna historia kama ya znz lakini imepotea kutokana na high movement of people and rapid change.kumbuka tabia za waznz hazibadiliki wote ni vile vile
 
Kama ni kwa KUFIKIRIKA NA KUSADIKIKA ni wazo zuri sana- serikali moja. Lakini kama ni KUTEKELEZEKA, ni wazo lisilitekelezeka kwa sasa. Heri kungangania 3 u kwa sasa!
 
Nakubaliana na wewe...serikali moja ndio muafaka...huyo Seif nae anatuchanganya serikali ya mkataba!!...halafu jamaa ametawaliwa na jazba he can not even control his feelings ha ha ha haaaaaa...
 
Back
Top Bottom