Muungano: Dkt. Mpango na Waziri wa Afya, hili si la Muungano. Msiliingize kinyemela!

Kuna wakati wengine tunakaa pembeni na kuwaachia akina Pascal Mayalla, watambe humu wanavyopenda na kujizolea sifa kama mpembuzi yakinifu.
Mkuu, kuna upotoshaji wa jamii kwa 'exploitation' ya Wananchi ambao licha ya kuwa 'literate' bado wanakosa ''perspective analysis'' kwa maana ya kuyaangalia mambo kutoka 'angle' tofauti.

Wanaofanya 'exploitation' wana access na media. Wasomaji hawana uwezo wa kuchambua nini kimeandikwa au kusemwa na gazeti au TV kama maoni au ukweli . Wanafahamu kila lisemwalo au kuandikwa ni 'fact'
Nitafafanua upotoshaji
Niongezee, hata CCM haina 'structure' ya chama kimoja. Kuna kamati maalumu ya CCM Zanziba (CCM Zanzibar)
Ndani ya CCM Union kuna Wazanzibar. Swali linabaki , Chama kimoja kuwa na sehemu 2, kama nchi moja serikali 2

Wapotoshaji na nina uhakika wanajua kwamba wanapotosha wanasema Serikali 2 za Tanzania na SMZ ndio kigezo cha kufanya Muungano 'adhimu na adimu''. Maneno yanatumika kufunika ukweli hakuna jibu la kuwa na Serikali 2 .

Upotoshaji umepewa utetezi mwingine, kwamba tuna Union kimataifa halafu tuna Federation ndani ya nchi.

Fikiria hivi kwamba kuna Federation ya Tanzania na Zanzibar! na hili linasemwa bila aibu haya wala soni.
Ikifika hapo Wananchi wetu wasio na ''perspective analysis' wanabaki kuamini yanayoandikwa.

Tena wanaofanya upotoshaji huo wanapewa access na media nyingi tu kufanikisha lengo la upotoshaji.
CCM kama niliyoeleza mwanzoni wanasema ni Moja, ukiangalia ni mbili kwa jina la kamai maalumu Zanzibar.
Kwa maana kwamba kinachokosekana ni CCM Tanganyika.

Mtririko huo wa makosa ndio unatuletea kituko kingine cha Serikali 2, yaani ya Muungano ikiwemo Zanzibar halafu ya Serikali ya Zanzibar lakini ya Tanganyika imekufa.

Kuna wakati Serikali ya JMT yenye Wazanzibar inajadiliana na Serikali ya Zanzibar!
Matatizo ya Muungano yanatokana na 'structure' isiyo na majibu akina Pascal wakisema 'adhimu na adimu''

Vituko havijaishia hapo, mwaka huu Serikali ya JMT imeingia MoU na SMZ kuhusu nishati na madini.
Rais wa JMT ikiwemo Zanzibar anasaini MoU na sehemu ya JMT ambayo ni Zanzibar na Rais wa SMZ.

Vituko havina mwisho, Katiba ya JMT inapokuwa na mamlaka kidogo kuliko katiba ya Zanzibar''
Sheria zinazotungwa Dodoma Wazanzibar wakiwemo zikivuka hazina maana hadi Wazanzibar wazipitie!

Kuna tatizo na halitakuwa na jibu bila uwepo wa Tanganyika.

Kwa structure ya sasa ya Muungano hakuna mtu anayefikri sawa sawa atakayeweza kuitetea, of course Chawa na Wadudu can say, write or do anything!
 
ACT WAZALENDO
HAKI YA WAZANZIBAR KUSEMA CHOCHOTE YAJIDHIHIRI
MANSOOR HIMID ASEMA '' WAO NI WAUNGWANA''

Chama cha ACT Wazalendo ni washirika wa CCM katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar
Siku za karibuni ACT imeeleza nia ya kujitoa serikali ya kitaifa kwasababu kadhaa

Viongozi wa ACT wamekuwa mstari wa mbele kuisema serikali ya Rais Hussein Mwinyi kikamilifu

Katika hali isiyo ya kawaida ACT wanalaani CCM Zanzibar wamekuwa 'wasemaji na watetezi' wakubwa wa CCM Taifa chini ya Rais SSH. Ilipotokea hoja kuhusu Rais SSH utetezi mkuu unatoka ACT Wazalendo.

Wachunguzi wa duru za kisiasa nchini wanaona 'uswahiba' wa ACT Zanzibar na Rais SSH katika jicho pana zaidi
Kutokana na hali hiyo, kuna tetesi na uzushi usio na ithbati mitaani kwamba SSH anamtazamo wa sera za ACT.

Katika mkutano wa ACT Wazalendo, kiongozi mwandamizi Mansoor Himid ameonekana tena jukwaani baada ya ukimya. Masoor alizungumzia mengi kubwa ni kusema '' Hakuna watu wanaotekwa au kupotea, mikutano imeruhusiwa na hayo ni kwasababu ya Rais SSH. Bw Himid akasema kupotea, utekaji na kuzuiwa mikutano hayatokeikwasababu SISI NI WAUNGWANA.
Mansoor akasema je ikitokea akaletwa mtu mzigo mwingine kama uliopo hapa Zanzibar...''

Kuna hoja muhimu tukiyataza maneno ya mansoor
Kwanza, Wazanzibar wamepewa haki ya kutukana , kutusi, kubagaza na kusema chochote kuhusu Muungano !
Haki hiyo hana Mtanganyika. Hapa kuna ushahidi

1. Kauli kwamba sisi ni Waungwana ikimaanisha '' Rais SSH na Wazanzibar'' ni tusi kwasababu inaonyesha Ma-Rais wengine waliopita hawakuwa Waungwana kwa maana ya kinyume chake ''washenzi''

Laiti kauli hiyo ingetolewa na raia wa Tanganyika tungesikia ACT, CCM, Serikali na kila awaye akifungua kinywa na kulaani. Ikiwa kusema ' Rais SSH ni Mzanzibar'' ililkuwa tusi ingalikuwa vipi kusema '' sisi ni waungwana, wo ni washenzi.''

2. Kitendo cha kusema Rais Mwinyi ni mzigo ulioletwa kina maana mbili
Kwanza, kwamb, ni mtu kutoka ''Tanganyika'' kwa baba yake kule Mkuranga''

Ni kweli kwasababu licha ya kuwa Mzanzibar Mwinyi aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga. Swali, huu si ubaguzi ?
Pili, kusema ni mzigo kwa Mzanzibar ni kumbagua na hapa tunaona ufa wa '' Wazanzibar na Wazanzibara''

3. Mansoor na ACT Wazalendo wameshirikiana na CCM kupindisha mchakato wa katiba mpya, wao wakidai tume huru ya uchaguzi. Hii inaonyesha ushahiba wa ACT na CCM lakini kupitia Rais SSH kama kiungo!!!

ACT wazalendo wamesahau mwaka jana kiongozi wao alifuatwa na wasiojulikana , kupigwa na kufia Hospitali.
Kwamba leo hali nchi imekuwa shwari ?

ACT hawana habari za kelele zinazoendelea kuhusu watu kutoweka katika maizngira tata
ACT wanadhani mikutano ni hisani na si haki yao kikatiba na hivyo wanamshukuru Rais kwa Hisani
ACT wanatumaini kwamba uungwana wa Rais ni muhimu kuliko sheria na taratibu na hivyo katiba haina maana
 
UFAFANUZI KUHUSU '' ELIMU YA JUU KUWA SUALA LA MUUNGANO''

Katika ukurasa wa X mdau ameeleza ksuala la elimu ya juu kutokuwa la muungano na jinsi Wazanzibar wanalitumia kama la Muungano. Habari hiyo ilichukua sura katika mabandiko ya JF kwa mijadala na hisia kali

Suala la elimu ya juu limeleta taharuki kwa Wazanzibar wakitetea ni la Muungano. Wazanzibar wale wale wanaolalamika mambo yameongezwa na kufikia 22 au 40 (ACT na OMO) leo wanatamani Elimu ya Juu!!

Ufafanuzi ;
Kuna mambo 11 katika mkataba wa Muungano 1964. Miongoni mwake ni Bandari , mafuta na gesi.
Tunataja Bandari , mafuta na gesi kwasababututakayoieleza.

Elimu ya Juu haipo katika mambo 11, ilifanywa jambo la Muungano mwaka 1967.

Rasimu ya Warioba haikutaja Elimu ya Juu. Zanzibar ina Wizara , Bajeti na bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu ZHSLB
Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010 iliondoa moja ya mambo 11, BANDARI, MAFUTA NA GESI bila kushirikisha Tanganyika.

Hoja ya Watanganyika, ikiwa Zanzibar iliondoa mafuta na gesi na Bandari yakiwa ni mambo ya Muungano kwasababu yanafaida, na Wazanzibar wanalalamika kuongezwa kinyemela, kwanini wasiondoe Elimu ya Juu!

Ni Elimu ya Juu kwasababu ni jambo lenye gharama. Bodi ya mikopo ya Tanganyika kwa jina la Tanzania ( HESLB) inatoka katika kodi za Watanganyika kwa Vijana wa Tanganyika kama ZHESLB inavyotoa kwa Vijana wa Kizanzibar.

Tatizo; HESLB inatumiwa na Wazanzibar kama ''Tanzania' kwa msemo '' ni Watanzania na Wazanzibar''.
Hivyo, Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wanapata mikopo pande zote kama Watanzania na Wazanzibar

Kijana wa Kizanzibar ana fursa tatu, kama Mtanzania, Mzanzibar na fungu maalumu la Uzanzibar
Akiwa Mtanzania anapata HESLB, halafu ana sehemu maalumu ya Wazanzibar ndani ya HESLB na kisha kama Mzanzibar anapata ZHESL mahususi kwake. Kijana wa Tanganyika ana fursa moja pekee

Vijana wa Tanganyika hawana fursa hata ya bahati mbaya kupata mikopo kupiitia ZHESLB
Hawawezi kupata kupitia ubaguzi wa kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi ambacho ni lugha nyepesi ya kuwatambua Wazanzibar dhidi ya Wtanaganyika

Kwa maana hiyo Vijana wa Zanzibar wanaziba nafasi za vijana wa Tanganyika kupata mikopo

Lakini pia kuna maswali, Wazanzibar wanarudishaje mikopo hiyo ?

Katika bajeti ya 2022/2023 Waziri wa SMZ alisema '' Wanamshukuru Rais SSH kwa kumaliza changamoto za udhamini wa Elimu ya Juu kupitia HESLB''. Hii inaeleza jambo moja, Marais waliopita hawakushughulikia suala hilo lisilosemwa!
Ni jambo gani hilo na kwanini ni kwa Wazanzibar tu? Kwanini halikuwekwa wazi na kwanini ni kipindi hiki!

Tumalizie kwa kusema Elimu ya Juu si suala la Muungano. Vijana wa Tanganyika wapewe fursa zao na Wazanzibar kupitia Wizara yao ya Elimu ya Juu na ZHESLB washughulikie vijana wao. Upendeleo maalumu ni dhulma kwa Watanganyika

Muhimu zaidi, kwavile Wazanzibar wanalalamika mambo kuongezwa nje ya mkataba wa 1964 na Elimu ya Juu imeongezwa mwaka 1967 ni wakati Elimu ya Juu iondolewe kwasababu ni kero kwa Wazanzibar na Watanganyika.
 
KAULI YA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KUHUSU MUUNGANO YALETA UTATA

Kama kuna viongozi wanaotajwa na kusifiwa Zanzibar ni Waziri wa Fedha wa Tanganyika Dr Mwigulu Nchemba na Makamu wa Rais Dr Mpango. Ushiriki wao katika mambo ya muungano umewafanya wajizolee sifa Visiwani.

Akiwasilisha Bajeti ya Fedha ya JMT 2024/2025 kinyume na tamaduni, Waziri wa Fedha alitumbukia katika mjadala wa Muungano badala ya Bajeti ambayo ni mwelekeo wa maisha ya Watanzania kwa mwaka wa fedha ujao

Katika mazingira ya kushangaza, Waziri Nchemba alikaririwa na gazeti la Mwananchi akitaja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ni nadra kusikia viongozi wa CCM wakitamka Tanganyika sasa hali inabadilika taratibu.

Siku za nyuma kulikuwa na mjadala wa 'hovyo' kwanini Rais SSH hatumii nembo ya Taifa ya Adam na Hawa.
Swali hilo lilizuka baada ya kuona nembo inayotumika ni ile ya Ikulu tofauti na Marais Watangaulizi.
Chaguo la nembo halikuwa suala kubwa lakini mazingira yanalikuza na hivyo kulipa mvuto hata usiohitajika.

Makamu wa pili wa Rais wa SMZ Bw Maulid na baadhi ya viongozi wa CCM na SMZ wana kauli inayotumika siku hizi kuliko wakati mwingine. Kwamba '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar'

Pengine matumizi ya nembo ya Taifa yanazingatia hilo. Kwamba kwa Wazanzibar , Uzanzibar kwanza na Utanzania baadaye. Umuhimu wa nembo ya Tanzania kwa Wazanzibar ni chaguo! lakini Uzanzibar si chaguo!!!

Katika hali nyingine Waziri Nchemba amesema '' Bila Tanzania Bara hakuna Muungano wa Tanzania''
Kauli hii ina utata , kwamba Tanzania Bara ndio Muungano au Tanzania Bara ndio imebeba Muungano au jina la Tanzania Bara ndilo liemebaba muungano!!!

Na mwisho, Waziri Nchemba amelaani viongozi wa vyama vya siasa akisema vinawagawa Watanzania.
Alichoshindwa kusema ni ukweli kwamba ubaguzi mkubwa mwaka huu umefanyika ndani ya Bunge alilosimama.
Pengine anafahamu lakini Wazanzibar wana haki ya kusema, si Watanganyika.

Swali linalozunguka vichwani ni kuhusu Muungano na haki ya Tanganyika.
Makamu wa Rais Dr Mpango na Waziri Mwigulu wamejipambanua kuhakikisha kero za Wazanzibar zinamalizwa.

Je, viongozi hao ndio wawakilishi wa ''Tanganyika''? Na kama siyo Tanganyika inawakilishwa na nani?
Na kama ni ndiyo , mamlaka ya kuizungumzia Tanganyika na rasilimali zake wamepata wapi?
 
SEHEMU YA MAELEZO YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR
BAJETI YA 2023/2024

'' 17. Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeendelea kwa juhudi kubwa kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Fedha zinazotoka kwa Washirika wa Maendeleo, hupokelewa kupitia njia
tofauti ikiwemo Miradi ya moja kwa moja ya Kisekta (Direct Project Financing), Mifuko ya Pamoja (Basket Funds) pamoja na Misaada ya Kibajeti (General Budget Support - GBS).
Kupitia utaratibu wa GBS, Zanzibar kwa kipindi kirefu imekua ikipokea kiwango kidogo cha asilimia 4.5 ambacho hakikuweza kuakisi mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Kupitia Awamu mbali mbali, SMZ imekua ikifanya juhudi mazungumzo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Tanzania kuangalia uwezekano wa kuongeza kiwango hicho ili
kiendane na hali halisi ya mahitaji yaliyopo.''

Hoja: Maneno muhimu ni ''kipindi kirefu na kupitia awamu mbali mbali'' . Kwanini ilichukua muda mrefu na kwanini ilikuwa awamu mbali mbali!

18. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua , umuhimu wa suala hili kisiasa, Viongozi wetu Wakuu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, waliagiza kwa pande zote mbili kukaa pamoja na kuangalia misingi na vigezo vya kitaalamu vitakavyokuwa bora katika ugawaji wa rasilimali hizo kwa pande zetu mbili. Baada ya Kamati za Kitaalamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukaa kwa pamoja na kulifanyia kazi suala hilo, mapendekezo yaliyozingatia vigezo vya kiuchumi, kiutawala pamoja
na uwezo wa kukopa, yamewasilishwa na kupokelewa na Serikali ambapo kuanzia sasa, mgao wa GBS kwa Zanzibar umeongezeka na
kufikia asilimia 9 badala ya asilimia 4.5 iliyokuwepo awali.

Hoja: Kwamba mgao ulichukua muda mrefu na awamu mbali mbali limemalizwa awamu hii kwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo kisiasa. Kero hiyo imemelizwa ili '' kuwaridhisha' Wazanzibar kisiasa bila kujali athari zake kwa upande wa Tanganyika kwasababu hakuna serikali wala mtetezi.

Ni kwasababu za kisiasa Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mh Jaffo mwezi February alisema kero zimebaki 2 lakini tarehe 20 March 2024 akasema zimebaki 7 na miongoni mwake ni hisa za Zanzibar BoT.
Wazanzibar wanatumia mwanya wa siasa kuleta madai na kwavile viongozi wanaona umuhimu kisiasa kero zao zinamalizwa. Je, ni kweli kwamba Tanganyika hakuna kero? Nani anasimamia?

Ukisoma taarifa, Waziri wa Fedha Mh Mkuya anasema '' Viongozi wetu wakuu Dr SSH na Dr H.Mwinyi wameagiza pande zote mbili kukaa pamoja''. Hiki ni kituko, pande mbili ni zipi?

JMT haiwezi ikawa upande kwasababu ndani yake wamo Wazanzibar.
Mfano, kuna wakati Wizara ya Ujenzi ya JMT iliongozwa na Waziri na Katibu mkuu wote Wazanzibar.
Hivi kama kuna kamati inayoshughulikia masuala ya rasilimali nani atasimamia Tanganyika?

Lakini pia Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar wanawezaje kuwa wasuluhishi wa suala la upande mmoja! Tanganyika haipo, msulhishi ni Tanzania, anayedai ni Zanzibar, wasimamizi ni Wazanzibar.
Kanuni za asili 'natural justice' hazikubaliani na hilo na hata ingekuwa Zanzibar wasingekubaliana nalo

Taarifa inasema kamati za kitaalam za JMT na SMZ!! Jamani hiki ni kituko!
JMT ina Wazanzibar inakuwaje upande wa Pili?
Pande mbili ni Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar, na msuluhishi ni JMT.

Kiwango kimeongezwa na kufikia 9%. Kuna Wazanzibar takribani milioni 1.2 kwa mujibu wa Profesa Makame wa SUZA wanaoishi Tanganyika. Hawa wana 'strain resources' yaani wanaongeza mzigo wa huduma Tanganyika.
Kwanini sehemu ya rasilimali za Tanganyika iwe ya Muungano halafu Zanzibar ipewe 9%
Uko wapi mgao wa Tanganyika?

Inaendelea
 
19. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, nachukua fursa hii, kuipongeza kwa dhati, Kamati ya Wataalamu waliolisimamia jambo hili hadi kufikia makubaliano. Aidha, tunawashuruku na kuwapongeza kwa dhati, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa
umahiri na umakini wao pamoja na uthubutu wa kusimamia uchumi, ustawi wa jamii na maendeleo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nikweli usiofichika kuwa Zanzibar inafaidika ikiwa ni
sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…
…….!! ”Kazi Inaendelea”…... na hakuna atakaebisha kuwa Yajayoooo…! “Ni Neema Tupu”….!!


Hoja: Kwavile suala la Muungano 'hoja moto'' kamati ya Watalaam ya JMT inaundwa na akina nani?
Je, kamati hiyo inawakilisha maoni ya Watanganyika! na kama ni hivyo itakuwaje katika maeneo ambayo watoa maamuzi ni Wazanzibar!

Na swali la msingi linarudi, ni kwa mantiki gani Muungano unajadiliana na Zanzibar?

Kwa maelezo juu Waziri wa Fedha anaongoza kamati. Naye kama Makamu wa Rais wa JMT na Waziri ofisi ya Makamu , kwa pamoja wanashiriki vikao kama Wajumbe wa JMT dhidi ya Wajumbe wa Zanzibar.

Ni ''turufu'' yenye utata. Kwa muda mfupi wamefanikiwa (short gain) lakini ikiwa ni lengo ni muda mrefu katika siasa, watakumbuna na changamoto na maswali mengi kutoka kwa Watanganyika, iwe muundo wa S2 au S3 kwa kuwa Watanganyika wana mtazamo tofauti kuhusu muungano, nje na ndani ya CCM

Ushiriki wa Makamu wa Rais na Waziri wa Fedha na matarajio ya kisiasa una kitu kinaitwa '' make or break' lakini likely break!!! Watakumbana na changamoto ya jinsi walivyomtetea Mama Tanganyika au walivyoshiriki namna tofauti. Muda utaeleza kwa ukubwa na upana wake! kwasasa ni turufu dhaifu

_________________________________________________________

Bandiko lijalo tutajadili ongezeko la madai ya Wazanzibar kuhusu
1. Shea za BoT
2. Kuingiza Sukari
4. Bei ya Umeme
5.Kuingiza maziwa kupitia Bahresa
6. Kuingiza mgari kutoka Zanzibar
7. Double Taxation ya Wafanyabiashara

Hizo zinaitwa kero za Zanzibar! kama alivyosema Waziri Mkuya katika Bajeti ya SMZ 2023/2024 katika hotuba ya Bajeti 2023/2024

''18. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua , umuhimu wa suala hili kisiasa, Viongozi wetu Wakuu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, waliagiza kwa pande zote mbili kukaa pamoja na kuangalia misingi na vigezo vya kitaalamu vitakavyokuwa bora katika ugawaji wa rasilimali hizo kwa pande zetu mbili ''

Maamuzi ya kuongeza GBS 4.5% hadi 9% yemefanywa na Dr SSH na Dr Mwinyi kwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo kisiasa '' kwa maana kwamba hoja nzima iliongozwa na siasa

Kwa kuzingatia umuhimu wa kisiasa Wazanzibar wanaongeza kero tajwa 5 hapo juu kama zilivyothibitishwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais katika gazeti la Mwananchi na akijibu swali March 20, 2024. Kabla ya hapo yaani Feb 2024 Waziri alinukuliwa akisema kero za Wazanzibar zimebaki 2.

Kuna Kero za Muungano na kero za kipuuzi za Muungano. Hizo 7 hapo juu ni kero za kipuuzi za Muungano

Upuuzi unatokana na neno puuza kwa maana 'ignore'.
Kero za sukari na maziwa n.k. ni za kipuuzi,hazifai kujadiliwa na watu wenye kufikiri sawa sawa.
Tutafafanua
 
KERO ZA KIPUUZI ZA MUUNGANO

Tumejadili hoja ya Wazanzibar kwamba ''Sisi ni Nchi moja' pale wanapotaka kuitumia Tanganyika.
Bandiko#50 tumeorodhesha kero za kipuuzi zinazopigiwa upatu na Wazanzibar

1. Shea za BoT
Ni kweli ilipovunjika Bodi ya Sarafu ya A.Mashariki 1966 shea za Zanzibar 11% ziliingizwa kama mtaji wa BoT.

Ni ukweli pia shea za BoT hazioti kama uyoga! Mtaji wa BoT uilikuzwa na uchumi wa Tanzania

Aliyekuwa Gavana wa BoT Marehemu Beno Ndulu alithibitisha, kwa zaidi ya miaka 40 Zanzibar haina mchango wowote. Kauli hiyo ilishabihiana na ya Waziri wa Fedha Marehemu B.P. Mramba kwamba Mishahara ya Watumishi wa SMZ ilitoka Dar es Salaama kuanzia nayakati za Komandoo, Karume n.k.

Zanzibar haina gharama zozote katika Bajeti zake zilizopita za kuhudumia huduma za Muungano.
Kuna JWTZ, Bajeti ya 2024 ni 3.3 Trilioni, hakuna mahali Bajeti ya SMZ inaonyesha mchango wake kwa JWTZ
Ndivyo ilivyo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani yenye Polisi na Uhamiaji
Ipo Wizara ya Mambo ya Nje
Kuna Wabunge wa Zanzibar wanaolipwa na fedha kutoka Tanganyika, hakuna Bajeti ya namna hiyo Zanzibar
Kuna Taasisi za Muungano ambazo mzigo ameubeba Mama Tanganyika
Kuna 9% ya GBS inayokwenda Zanzibar
Kuna madeni ya Zanzibar yanayolipwa na JMT ambayo ni Tanganyika
Orodha inaendelea

Wazanzibar wana haki ya kuzungumzia shea lakini haki inakuwa na mantiki zaidi ikiwa wataangalia mambo wanayonufaika nayo , pili, wataangalia wamechangia nini baada ya huo mtaji.

Tunaita kero ya kipuuzi kwasababu Wazanzibar wanataka kugawana tu hawana kuwajibika.

Gharama za kuendesha Muungano na taasisi zake na usaidizi wanaoupata si busara kufikiria mgao

Mfano, ikiwa Zanzibar itapewa shea na faida wanazodai BoT na kisha kupigiwa hesabu za kila jambo walilonufaika nalo, wataweza?

Ikiwa wataambiwa wachangie 5% ya Bajeti ya Wizara tatu, Ulinzi mambo ya ndani, na nje wataweza?

Hii ni kero ya kipuuzi hakuna mtu anayejua hesabu anayeweza kuiweka mezani kirahisi.
Hata hivyo, tumeambiwa na Waziri kuna kamati inayohsughulikia!

Hatudhani kamati hiyo haifahamu, lakini kama alivyosema Waziri wa Fedha wa SMZ '' Kwamba KERO zinaamuliwa kwa umuhimu wa kisiasa' hili nalo litaangaliwa kwa jicho hilo ili kuwaridhisha Wazanzibar

Kwa bahati mbaya Tanganyika haina mtetezi! ikiwa ndio watuhumiwa na ndio waliobeba Muungao.

Bandiko lijalo tutaangalia kero ya kipuuzi ya Sukari
 
KERO ZA KIPUUZI ZA MUUNGANO

2. KERO YA SUKARI
Katika mwendelezo wa kero za kipuuzi, ipo moja ya Wazanzibar kutaka kuingiza sukari kutoka Zanzibar

Hii si kero mpya , imekuwepo tangu Rais SSH akiwa Makamu wa Rais wa JMT
April 2018 Mbunge wa Konde Hatibu Haji alisema '' ...Mnamdhalilisha makamu wa Rais SSH anayekaa vikao kila siku kutafuta sulugu'' - Rejea Hansard za Bunge.

Zuio la sukari kutoka Zanziabar limekuwepo tangu utawala wa Rais Kikwete

Ili kupata uelewa wa suala hili, n Kiwanda cha sukari Zanzibar kilianzishwa 1970 kikiaendeshwa na SMZ.
1978 serikali ilishindwa kukiendesha na kupewa mwekezaji (Expoer trading group) .
Kiwanda cha Mahonda kinazalisha tani 8,000 kwa mwaka, mahitaji ya Zanzibar ya tani 17,000-20,000 kwa mujibu wa Waziri Ashantu Kijazi katika Bunge la April 2018, akijibu swali la Mbunge wa CUF Yusuf Hussein

January 9 2028 Meneja wa kiwanda cha Mahonda Rajesh Kumar alikaririwa na gazeti la Mwananchi '' tunataka kuuza Bara kwasababu ya bei. Zanzibar mfuko ni Tsh 60,000 na mfuko huo ni Tsh 100,000 Tanzania Bara.
Meneja anasema wameajiri watu 235 na wanataka soko la uhakika la Bara

Waziri wa Biashara (2018) balozi Amina Salum anasema , kuzuia sukari ni kinyumr na matakwa ya Muungano. Balozi anakiri sukari inayozalishwa Zanzibar haitoshelezi mahitaji lakini wanataka kuuza popote!!
Waziri Amina akasema madai kwamba sukari inatoka nje hayana msingi wowote

Hoja
Kwanza, kiwanda cha Mahonda ni mali binafsi, kuingiza suala la watu binafsi katika Muungano ni upuuzi

Pili, kiwanda cha Zanzibar hakitoshelezi mahitaji wanaagiza tofauti kutoka nje ya nchi.
Hoja ya Balozi Amina haina maana wala mantiki na inashadidia kero za kipuuzi. Tutafafanua.

Balozi Amina alipaswa kuelewa kuna mamlaka na Wizara tofauti na kwamba sukari haipo katika mkataba wa Muungano kwahiyo hakuna ukiukwaji wa matakwa ya Muungano. Balozi alipaswa kulielewa hili vema! sad

Tatu, Zanzibar wana mamlaka za kodi. Mwaka 2024 wameondoa VAT ili kukidhi haja zao. Hii ina maana sukari kutoka Zanzibar ni bei rahisi.

Nne , Zanzibar wana shirika la viwango (ZBS) tofauti na TBS. Kwahiyo viwango si suala la Muungano

Kwa mantiki , Wazanzibar wanataka kuingiza sukari kwa magendo katika soko la Tanganyika kwa kisingizio cha Muungano. Kinachofanyika ni Wafanyabiashara binafsi kuitumia SMZ kushinikiza JMT ili matatizo binafsi yawe ya Muungano. Suala la sukari za magendo lilikokataliwa na viongozi wote kuanzia Nyerere hadi Magufuli

Kwanini limerudi kwa kasi?

Viongozi waliokataa walielewa upuuzi wa hoja wakizingatia kinachofanyika ni biashara za watu binafsi kuingizwa katika masuala ya Muungano. Walielewe kuingiza sukari kimagendo kuna madhara kadhaa;
1. Kuleta bidhaa chafu zisizoweza kuhakikiwa kwa kisingizio cha Muugano na kumtwisha mlaji madhara ya afya
2. Kuua soko la viwanda vya Tanganyika kwa sukari za nje kupitia Zanzibar na athari za ajira na kodi
3. Kuinyima TRA mapato kwa Wafanyabishara kutumia Zanzibar kama uchochoro wa kukwepa kodi

Suala la sukari si la Muungano na linashughulikiwa na serikali tofauti. Ni suala linalohusu watu binafsi.
Ikiwa tatizo ni soko kwanini SMZ isiwasaidie Wafanyabiashara wa Zanzibar kuuza Comoro, Kenya, Rwanda n.k

Suala hili halihitaji kamati au utaalamu, lipo wazi kwamba kuingiza sukari ya Zanzibar inayoagizwa kutoka kusikojulikana kuna madhara kwa Tanganyika. Hii ni kero ya kipuuzi maana haihitaji utaalamu bali akili kidogo

Nani anatetea masilahi ya Tanganyika?

Bandiko lijalo, kero ya kipuuzi ya Maziwa ya ng'ombe!
 
KERO ZA KIPUUZI ZA MUUNGANO

3. UINGIZAJI MAZIWA
Ni mwendelezo wa kero za Muungano za kipuuzi kama zilizvyoanishwa awali
Ni Kero miongoni mwa zile 7 '' uingizaji wa maziwa kutoka Zanzibar ''

Kilimo si suala la Muungano, Zanzibar wana Wizara na taasisi zao (ZALIR) na Tanganyika (TALIR)

Sheria za vibali vya mazao ya mifugo kwa pande mbili ni tofauti na hazitambuliwi na pande hizo

Jambo la kushangaza JMT ambayo ni serikali mama sheria zake hazitambuliwi na Zanzibar
Hoja ya kwamba ni ''Nchi moja' kama wanavyodai Wazanzibar wakitaka soko la Tanganyika inafia hapo

Zuio la kuingiza maziwa ni yale ya ''UNGA' kupitia kampuni ya Bakhresa.
Kama ilivyokuwa hoja ya sukari tatizo si kati ya SMZ na JMT bali Wafanyabishara wanaotumia SMZ na kutumia kero za muungano kuingiza bidhaa za Tanganyika.

Kama livyosema waziri Mkuya katika Bajeti ya SMZ 2023/2024 '' .. kero zinatatuliwa kwa umuhimu wak kisiasa hasa kwa upande wa Zanzibar''. Ili kupata fursa kila kero ya Wazanzibar hata kushinda na njaa ni ya Muungano.

Bakresa ni mwekezaji nchini, hajawahi kunyimwa haki Tanganyika kwasababu ya Uzanzibar.
Suala la maziwa ni la kisekta lingemalizwa kati ya kampuni za Bakhrea na Wizara ya Kilimo.
Hakuna sababu za kulifanya ni kero za muungano kwasababu Kampuni za Bakhresa si sehemu ya SMZ wala JMT.

Uingizaji wa bidhaa za mifugo unaongozwa na sheria tofauti za pande. Wazanzibar kwa kupitia Wizara ya kilimo walikataza ndizi za Tanganyika kuingia Zanzibar kwa hoja kwamba sheria zilizotumika ni za Zanzibar.
Wazanzibar hao hao wanatumia jina la Tanzania kukiuka sheria za Tanganyika wakidai ni ''nchi moja''

Taasisi zinazodhibiti ubora wa bidhaa ni tofauti kati ya Zanzibar na Tanganyika.
Hivyo, maziwa yanayotoka nje ya nchi kupitia Zanzibar hayawezi kupewa kibali kwa jina la Tanzania tu.

Hoja ya Wazanzibar kwamba sisi ni nchi moja ni ya kipuuzi. Maziwa yakiagizwa kutoka Kenya yanakaguliwa mpakani na mamlaka za Tanganyika iwe taasisi ya viwango au mamlaka ya chakula.
Bidhaa hiyo itauzwa popote Tanganyika kwasababu imekaguliwa na mamlaka ya nchi moja Tanganyika.

Hali hiyo ni tofauti na Zanzibar kwasababu taasisi za bara hazitabuliwi na hivyo za visiwani hazitabuliwi pia.

Kuruhusu bidhaa za maziwa kuingia Tanganyika kwa kisingizio cha nchi moja kuna madhara;
1. Kunafungua mlango wa ukwelpaji wa kodi kupitia Zanzibar
2. Uingizaji wa bidhaa hafifu za nje kupitia Zanzibar utaua soko la maziwa Tanganyika
3. Bidhaa hafifu ni hatarishi kwa matumizi ya walaji wa Tanganyika.

Muhimu zaidi, hii si kero ya Muungano! ni kero ya kipuuzi ya Muungano na wanaoileta wapuuzwe kwa upuuzi.
Kama kuna kamati ya kushughulikia suala hili kama kama kero kamati hiyo itakuwa inashughulika na upuuzi.
 
Kero ya Muungano ya kipuuzi-sukari sehemu ya II

Kabla ya kuendelea na ''kero ya kipuuzi ya umeme' turejee kuhusu maziwa

Wadau wanasema maziwa ya unga yanayozuiliwa kuingizwa Tanganyika kutoka ni ya kampuni ya Bakhresa

Bakhresa ni mfanyabishara Tanganyika akimiliki viwanda, mashamba na kuagiza bidhaa kwa kiwango cha meli nzima. Bidhaa hazijawahi kukatawaliwa kuingia bandarini Dar es Salaam au kwingineko.
Swali , kwanini maziwa yapitie Zanzibar kabla ya kuingizwa Tanganyika na sikuagiza kama anavyofanya kwa bidhaa zingine !

Kwanini Bakhresa atumie viongozi wa SMZ kuleta hoja ya maziwa kama tatizo la Muungano wakati ambapo anapata huduma zote akiwa Tanganyika? Kwanini suala la kisekta lisilo la kisera lifanywe kero za Muungano?

Suala la maziwa na Sukari ni mambo ya wafanyabiashara binafsi lakini kwa kutambua kwamba likipewa '' hadhi ya kero za Muungano' litatoa fursa ya kukwepa kodi kwasababu lina ''uzito' kero inatumiwa kama neno muhimu . Ikiwa si hivyo kwanini Wafanyabiashara wa Maziwa na Sukari wasiagize moja kwa moja kupitia bandari za Tanganyika?

Viongozi wanaolibeba kama kero ni sehemu ya 'mfumo' wa kutaka kukwepa kodi kwa kupitishia bidhaa Zanzibar kwa kisingizio cha '' nchi moja' wakati ukweli si 'nchi moja' tuna mifumo tofauti ya ushuru wa forodha, kodi , ukaguzi wa bidhaa na viwango. Je, hawa viongozi wanapata nini kusimamia hili!!

Ikiwa Wafanyabiashara wa Zanzibar wanaona kero kufuata taratibu za Tanganyika , wana uhuru wa kuuza bidhaa zao za maziwa Kenya, Comoro , Msumbiji , Somalia na Mauritius.

Ndio maana tunasema hizo zinazoitwa kero ni kero za kipuuzi za Muungano!
 

Tunapoelekea kujadili hoja ya 'kipuuzi ya kero za Muungano'' kama tulivyozianisha Bandiko#50 , ni vema tukarejea bandiko #11 na 13 hapa chini ili kuelewa kwanini suala la Umeme ni kero ya Kipuuzi.

Tunaendelea kusisitiza, upuuzi si tusi ni neno linalotokana na puuza '' ignore' kwa maana ya kupuuzwa au upuuzi.
 
Hili ni bandiko#13.

Kwanini umeme ni kero ya kipuuzi? Bandiko linafuata
 
UMEME- KERO YA KIPUUZI YA MUUNGANO

Ni kero inatitajwa kubaki ikitafuriwa ufumbuzi kama ilivyoelezwa bandiko#50
Hoja ya Wazanzibar ni tofuati ya bei tukiwa ''Nchi Moja''. Kwamba Bei ya Tanga ni tofauti na Zanzibar

Tunarejea pale pale kukiwa na mafao Wazanzibar hujitanabahisha kama 'Nchi Moja' , nje ya hapo ni Wazanzibar si Watanzania, hii ni ' abuse' ya Muungano na Unafiki

'' Sisi si nchi moja'' na hili tumelieza mara nyingi si kwa nadhari bali kwa kauli na matendo ya Wazanzibar
Ikiwa katiba ya Zanzibar haitambui sheria za JMT , ni nchi moja kwa namna gani?
Ikiwa tuna sheria zinazoongoza chumi tofauti , sisi tunakuwaje nchi moja?
Ikiwa Watanganyika ni wageni Zanzibar kama Nigeria au Guinea, sisi ni nchi moja kivipi?
Ikiwa Mbunge anaukana Utanzania ndani ya Bunge na viongozi wa nchi wapo kimya, sisi ni nchi moja gani?
ikiwa tuna taasisi tofauti zenye majukumu sawa kama TANESCO na ZESCO sisi tunakuwaje nchi moja?

Nishati na madini si ya Muungano. Wazanzibar waliondoa mafuta na gesi ukiwa ni ushahidi jambo hilo si la Muungano. Umeme si jambo la Muungano Tuna mashirika mawili tofuati, ushahidi si jambo la Muungano

Katika hali ya kushangaza kumesainiwa MoU yaani hati ya makubaliano ya ushirikiano katika nishati kati ya Nchi ya ''Tanzania na Nchi ya Zanzibar''. Jambo hili halijawahi kutokea awamu yoyote tangu Muungano uasisiwe.

Huu ni ushahidi kwamba sisi si Nchi moja na kwamba masuala ya umeme na nishati si Muungano

Matokeo ya MoU kati ya Nchi ya ''Tanzania na Nchi ya Zanzibar'' yamewezesha Tanzania kutoa pesa za kujenga miundo mbinu ya umeme (soma bandiko#58) nchini Zanzibar na si Wizara ya Nishati na madini ya Zanzibar!!

Nchi ya Tanzania iliyoingia MoU na Zanzibar inaitwa Tanganyika! suala lisilo la Muungano limeingizwa Kinyemela katika Muungano. Wazanzibar wanaolalamika kuongezwa mambo kinyemela wamekaa kimya kwa unafiki

Mfumo wa wa kupeleka umeme Zanzibar umekarababatiwa na serikali ya JMT na siyo SMZ

MoU ni njia iliyotumika kuwezesha Wizara ya Nishati na Madini ya Tanganyika kufanya kazi Zanzibar
Ni kupitia MoU hiyo masuala ya umeme yanaingia pia kama ujenzi wa njia za umemeo kule Zanzibar

Bei ya umeme Tanga na Kigoma haziwezi kuwa tofauti kwasababu zipo chini ya shirika moja la Tanesco

Bei ya Umeme Zanzibar lazima itaongezeka kwasababu kuna mashirika mawili Tanesco na Zesco
Kuna mamlaka tofauti za kodi TRA na ZRA
Kuna gharama za kupeleka umeme kwa njia ya Bahari kule Unguja na Pemba
Kwa taratibu za kiutawala mashirika mawili yana gharama za kuendesha kuliko shirika moja

Ongezeko la gharama ni kutokana na uwepo wa ZESCO na mengine tajwa hapo juu.

Swali la kujiuliza ni kwanini Tanesco ichukue majukumu ya kufikisha umeme Zanzibar halafu liwepo shirika jingine la umeme. Zesco ni eneo la kutengeneza ajira, haina maana yoyote kwasababu haizalishi umeme na gharama zote za ''uzembe' wa Zesco zinabebwa na Tanesco kupitia wateja wake kama ilivyotokea kwa deni la Bilioni 60

Wazanzibar wanapolalamika kuhusu bei ya umeme kuwa kubwa si kweli.
Ukubwa unatokana na uwepo wa shirika lisilo na kazi la Zesco na mamlaka tofauti za ukusanyaji kodi.

Deni la Bilioni 60 lililofutwa limerudi kwa Tanesco na JMT na kuwabebesha mzigo Wananchi wa Tanganyika kwa kutumia jina la Tanzania na MoU na Nchi ya Zanzibar.
Ndio maana hii ni kero ya kipuuzi kwasababu imetengenezwa tu kwa kukosa maarifa.
 
KODI-KERO YA KIPUUZI YA MUUNGANO

Tunamalizia kero 7 kama zilivyoanishwa katika bandiko#50.
Wazanzibar wanasema '' sisi ni Nchi moja' kuna TRA moja kwanini bidhaa kutoka Zanzibar zitozwe kodi Bara.
Kwa mshango zaidi, Wazanzibar wanauliza kwanini bidhaa kutoka Tanga hazitozwi kodi zikienda Mbeya!

Hutuhitaji kurudia maana ya ''Sisi ni nchi moja'' tumeeleza sababu lukuki zikitengenezwa na Wazanzibar zikionyesha pasi na shaka ''Sisi si nchi moja'' Kwa kodi 'sisi si nchi moja', kuna mamlaka mbili, TRA na ZRA

TRA inakusanya mapato Zanzibar yasiyovuka bahari. Mwaka 2023/2024 Bajeti ilionyesha makusanyo ya takribani Bilioni 450 zikibaki Zanzibar. Hakuna kuonyesha Zanzibar inachangia pato la kodi katika Muungano.

Upo ushahidi wa Gavana wa BoT marehemu Ndulu akisema Zanzibar haijachangia Muungano kwa miaka zaidi ya 40. Bajeti ya SMZ haionyeshi mapato ya Zanzibar kuingia Muungano. Mapato ya ZRA yanabaki Zanzibar

Tuna mamlaka tofauti za Viwanja vya ndege na Bandari. Kuna Tozo na ushuru wa forodha tofauti kati ya Tanganyika na Zanzibar. Kuna mamlaka za viwango na udhibiti wa rushwa tofauti .

Ni upungufu wa uelewa kudhani kwamba suala la kodi linaweza kuwa sawa kati ya chumi mbili

Tumeeleza ushuru unaotozwa Zanzibar kwa bidhaa zinazoagizwa ni mdogo.
Gharama za Kontena moja la bidhaa ni tofuati katika ya Tanganyika na Zanziba kwenyer gharama kidogo sana.
Kuna ukwepaji wa kodi mkubwa Zanzibar unaofanya bidhaa kuwa rahisi hasa zikiingizwa Bara.

Tofauti hizo zinalazimu bidhaa za Zanzibar zitozwe kodi zikiingia Bara. Kodi zinazotozwa ni kidogo kuliko bidhaa ile ile ikiingia moja kwa moja Bara. Kuacha kotoza kodi ni kuruhusu ukwepaji kodi , bidhaa hafifu kwa viwango kuingia Tanganyika kupitia Zanzibar.

Ni kuua biashara za Watanganyika wanaoingiza bidhaa zao moja kwa moja na kuchangia pato la Taifa .
Kubwa zaidi ni kupunguza mapato na kumtwisha Mtanganyika mzigo wa kodi

Hoja ya kutozwa kodi mara mbili ni ya kupuuzwa kwasababu ni ya kipuuzi.
Wazanzibar waelewe panapokuwepo na Mamlaka za ; Bandari, Viwanja vya ndege, Kodi, ushuru n.k. tofauti huwezi kufanya '' Harmonization' ya kodi.

Pia waelewe 'harmonization' itaumiza soko la Tanganyika kwasababu bidhaa zinatoka Zanzibar kuja Bara.

Wazanzibar walipiga marufu uingizaji wa ndizi tu za kula kwasababu ya kulinda soko lao.
Ni sheria kama hizo zipo Tanganyika na haiwezi kuwa ''mlango wazi' kama pango la wakwepa kodi kupitia Zanzibar, kuingiza bidhaa hafifu kwa kisingizio cha Muungano

Kuhusu bidhaa kutoka Tanga kwenda Mbeya kutotozwa kodi, Wazanzibar waelewe tuna mamlaka moja ya Bandari na viwanja vya ndege, mamlaka moja ya kodi na ushuru na hakuna Mkoa wa Tanganyika wenye mamlaka yake. Bidhaa ikitoka eneo moja inachangia pato la Tanganyika popote ilipo.

Zanzibar siyo Tanga au Mbeya kwasababu kuna mamlaka na sheria zake kama Nchi na wala sheria au mamlaka za Tanganyika hazina uwezo Zanzibar .

Wanaoweka sheria hizo kama kuondoa Bandari, mafuta na gesi ni Wazanzibar! ''Sisi si nchi moja'' , wanaosema na kutenda hayo ni Wazanzibar. Kutumia jina Tanzania kuingiza bidhaa ni ku 'abuse' Muungano!
 
KUINGIZA MAGARI -KERO YA KIPUUZI YA MUUNGANO
K kinachoitwa kero ya kuingiza magari kutoka Zanzibar. Hoja yao ni kwamba magari kutoka Zanzibar yaingie Tanganyika kama ambavyo magari kutoka Mbeya yanakwenda Moshi kwasababu ''Sisi ni Nchi moja'' . Kauli mbiu ya ''nchi moja' tumeieleza ubutu na upotofu wake

Tunarudia, kuna mamlaka tofauti za kodi, forodha, ushuru n.k. Tuna mamlaka tofauti utoaji wa Leseni ikiwemo kuendesha magari. hazitambuliki Zanzibar kwasababu sisi 'si nchi moja' kwa mujibu wa Wazanzibar.

Magari kutoka Tanga, Mtwara, Arusha, Bukoba, Musoma , Mbeya n.k. yanaingia kupitia chanzo kimoja ' Border post' ya serikali. Mamlaka ya kodi ni moja ''TRA'' hivyo gari kutoka mkoa mmoja lipo nchi moja ya Tanganyika.
Gari kutoka Zanzibar limelipiwa kodi Zanzibar na leseni Zanzibar ! si sawa na kutoka Tanga

Kuruhusu magari kutoka Zanzibar kwa kisingizio cha matumizi binafsi ni utaratibu ule ule wa kutokuwa na uadilifu. Wafanyabiashara wanatumia SMZ na CCM kufanya suala ni kero!.

Wafanyabiashara wanata kuingiza magari kwa kutumia Familia zao kisha kuuza Tanganyika.
Watafanya hivyo kila siku na mwisho wa siku watafanikiwa kukwepa kodi za Tanganyika.

Tunarudi kule kule kuruhusu magari kutoka Zanzibar kutumika kama ya Familia ni uchafu wa Wafanyabiashara wanaowatumia wanasiasa na viongozi wa SMZ kuiita ni kero. Tuna mamlaka tofauti za kodi na udhibiti wa bidhaa

Kuingiza magari kutoka Zanzibar ni njama za Wafanyabaishara tu. si kero ni jambo la kupuuzwa na ni upuuzi wa kero za Muungano
 
Bandiko lijalo tutajadili ongezeko la madai ya Wazanzibar kuhusu
1. Shea za BoT
2. Kuingiza Sukari
4. Bei ya Umeme
5.Kuingiza maziwa kupitia Bahresa
6. Kuingiza mgari kutoka Zanzibar
7. Double Taxation ya Wafanyabiashara

Kutoka bandiko#50 kero zimeorodheshwa ikisemwa zinatafutiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Waziri anayeshughulikia Muungano. Tumezipitia na tuhitimishe ;

Tunaposema kero za kipuuzi za Muungano tunamaanisha ' kero za kupuuzwa' au kuwa ''ignored''

Kero ni jambolinaloleta sintofahamu kati ya pande za Muungano kutokana na sera.
Kero s matatizo binafsi ya watu kutoka pande moja ya Muungano yanayofanywa ''sera'

1. Shea za BoT- Ni hoja mujarabu kwasababu ipo kisera. Ikiwa inaangaliwa na Wataalam kinachopaswa kuangaliwa si Shea za Zanzibar tu bali mzigo alioubeba Tanganyika kwa miaka yote ya shea .
'Disadvantage' iliyopo ni kwamba hakuna msimamizi wa Tanganyika!

2. Zanzibar haizalishi sukari ya kuitosheleza.Ni ujinga kudhani inaweza kuuza sukari Tanganyika.
Ikiwa kuna Wafanyabiashara wa Zanzibar wanaotaka kuagiza sukari na kuingiza Tanganyika, ni wajibu wafuate Taratibu za JMT zinazotawala Tanganyika ili kuzuia ukwepaji wa kodi na udhibiti wa viwango.
Hii si kero ni mbinu ya Wafanyabiashara kutumia Serikali 2 kwa kuzitisha ni kero. Ipuuzwe haina maana

3. Bei ya umeme ni matokeo ya kuwa na mashirika mawili. Nishati haijawahi kuwa Muungano.
Tanesco ni shirika linalohitaji kujiendesha kibiashara. Misamaha ya umeme kwa Zanzibar inadhoofisha shirika na kuwabebesha Wananchi wa Tanganyika mzigo wa kuliendesha.
Nishati umeme ukiwemo si jambo la Muungano, kama Wazanzibar hawaridhiki watafute chanzo kingine.
Kuwabebesha walipa kodi wa Tanganyika mzigo wa Zanzibar kwasababu hawana serikali, si kuwatendea haki

4. Maziwa ya Bakhresa ni suala binafsi linaloweza kumalizwa na Wizara ya Kilimo na mamlaka ya kodi.
Si suala la Muungano na wala haligusi Wananchi wa Zanzibar. . Kampuni inaweza kuingiza maziwa bandarini Dar es Salaam bila kupitia Zanzibar. Hii si kero ya sera ni wafanyabiashara wanatumia Serikali mbili kulifanya ni kero.

5. Kuingiza magari ni mbinu ile ile ya sukari na maziwa. Wafanyabiashara kuitumia SMZ na Viongozi wa CCM kueleza ni kero bila kujali athari zake kwa uchumi wa Tanganyika.
Hii si kero ya Muungano ni jambo la kupuuzwa kwasababu ni upuuzi wa kero za muungano.

Inashangaza kwamba mambo haya yana kamati inayoyashughulikia. Hizi si kero za kisera ni Wafanyabiashara wanataka kutumia neno ''kero' ili kutisha muungano wakitokea Zanzibar. Na kwavile hakuna Tanganyika, Zanzibar inaogopwa na hivyo kila jambo kuwa kero hata kama mtu anaumwa tumbo kwa kula hovyo!

Lakini mambo haya yanasukumwa kwa kasi sana awamu hii, kulikoni?
Nani anasimama kutetea masilahi Tanganyika?

Bandiko lijalo:
Baada ya kero, kamati gani inayoshughulikia mchango wa Zanzibar katika Muungano?
 
BAADA YA KERO, ZANZIBAR INAWAJIBIKA WAPI NA KIVIPI KATIKA MUUNGANO?

Tumeona kinachoitwa kero, si kero bali mbinu za Wafanyabiashara wanaitumia JMT, SMZ na Bunge kutisha uwepo wa ''kero feki'' za kuvunja Muungano

Ipo kamati ya Watalaam kushughulikia '' kero'' zinazopaswa kupuuzwa ''ignored'
Hakuna mantiki ya kamati , isipokuwa kujenga uhalali wa kero za Wafanyabiashara.

Kamati inashughilikia kero za Wazanzibar tu kwasababu ''Watanganyika'' hawana ''platform''
Kamati ya Wataalam inayosemwa ni ya JMT haiwakilishi masilahi ya Watanganyika.

Kamati yoyote ya JMT ina Wazanzibar kwasababu ni ya Muungano, halafu kuna uwakilishi wa Zanzibar.
Hakuna mtetezi wa masilahi ya Tanganyika ndio maana zinasikika kero za Zanzibar tu, kila siku

Haina maana Watanganyika hawana kero! la hasha. Kero za Watanganyika ni kubwa na nyingi zikianikwa hadharani hizi za sukari , chumvi, makaimati na maziwa zinabaki kuwa 'upuuzi'

Kwa mfano, Watanganyika wana kero ya kubeba muungano peke wakihudumia kwa rasilimali zao zilizogeuzwa kuwa za JMT. Mapato yote yakiwemo kodi, Nishati, Madini, Utalii na vyanzo vingine zinazingizwa katika Muungano.

Sehemu ya rasilimali hizo zinapelekwa Zanzibar kwa ''formula'' iliyoamuliwa bila kujadiliwa Bungeni.
Hakuna sheria yoyote inayoeleza Zanzibar ipate 9% ya fedha kwa kisingizio cha GBS.

Ipo kero ya fursa pia. Kwavile kila cha Tanganyika kimegeuzwa cha Muungano hilo linajenga ''uhalali'' unaotumiwa na Wazanzibar siku hizi wa kusema ' Kila Mzanzibar ni Mtanzania na si kinyume chake''

Hii ni abuse ni tusi kubwa kwa Watanganyika, kwa maana kwamba '' Chenu ni chetu, chetu ni chetu''
Haya yanaongewa na Viongozi wa SMZ si Wananchi bila kujali uzito wake. Ni maneno makali kama ya Waziri Mstaafu aliyesema '' Rais SSH aweke formula ya kugawana mapato ya Tanzania '' kwa jina la Muungano.

Mambo mengi yanayohusu fursa za Watu wa Tanganyika yanapewa ''mgao maalumu' kwa Zanzibar.
Mambo hayo hayo yakiwa upande wa Zanzibar , Mtanganyika anaonekana kama mgeni kutoka Burkina Faso.

Msingi wa kero za Watanganyika upo kisera ukihusisha rasilimali na Fursa zao. Hoja inayoingia katika vichwa vya Watanganika si mantiki bali maswali yanayohitaji majibu yakinifu;
1. Kwanini tuliungana
2. Tanganyika inafaidika na nini katika Muungano
3. Nani anasimamia masilahi ya Tanganyika yasitumiwe vibaya
4. Kwanini Tanganyika inalaumiwa kwa kubeba Muungano

Wakati kuna kamati ya kutatua kero za Wazanzibar, ni wakati sasa Wazanzibar waeleze na kuweka wazi katika Muungano huu wanaonufaika nao nini wanacholeta mezani.

Swali la nini Zanzibar inaleta katika Muungano linachagiza uwepo wa maswali 4 hapo juu. Watanganyika wanapata kitu kinachoitwa '' fatique' yaani kuchoshwa. Kila wakitazama ni nini Wazanzibar wanaleta katika Muungano ili nao wanaufaike hawaoni ! Lakini pia licha ya kutumia rasilimali zao wamelaumiwa.

Hakuna jibu la mkato, ni wakati sasa Wazanzibar waeleze nini wanaleta katika Muungano ambacho raia wa Tanganyika atasimama na kusema ''naam' hizi ni faida za Muungano! kutoka Zanzibar
 
DAWA SI KUSHUGHULIKIA KERO NI KUJIBU HOJA NA MASWALI
Ufumbuzi wa tatizo hupatikana kwa kuangalia chanzo 'root cause' na si kuangalia dalili ''symptoms''

Inasemwa kero za Zanzibar karibu zi kuamlizwa lakini haziwezi kuisha, muungano ni jambo endelevu

Kuna utamaduni wa kufanya mjadala wa Muungano kama ni mwiko 'taboo'' ukinakshiwa na maeno ya tunu ya Taifa, adhimu na adimu, wa kipekee n.k. Haya ni kweli kwa kizazi kilichopita kilichoamini fikra za Viongozi

Kizazi cha leo ni cha kuhoji ndio maana tunaona maswali magumu na mazito yanayohusu Muungano.
Ni maswali yanayohitaji majibu na si kuwekewa bendeji juu ya donda 'band aid'.

Ufumbuzi wa kero ni bendeji juu ya kidonda na si suluhu ya kudumu.

Kwanza, kosa ni kero kumalizwa na 'mamlaka' na si uwakilishi. Suluhu inabaki makubaliano tu yasiyo na nguvu kisheria. Kero hazikupitia uwakilishi wa Wananchi Bungeni kwa kuogopa kujadiliwa ''taboo''.
Ikiwa atatokea Rais Mwingine kama ilivyotokea nyakati tofauti na jinsi ''kero'' zinaweza kurudi

Pili, kero ni za Zanzibar, Tanganyika inafunikwa ili kuzima hoja nzito ingawa ndiyo iliyobeba Muungano 100%.
Hoja na maswali ya Watanganyika yasipojibiwa ni jipu lililovia tu wakati wowote litapasuka na kuleta taharuki

Tatu, jitihada za kuzuia watu kuujadili hasa Watanganyika na kutumia vitisho kama uchochezi havitasaidia.
Wazanzibar wana 'uhuru' wa kujadili, kutusi au kutukana Muungano lakini kwa Tanganyika inaitwa uchochezi.

Wapo waliofungwa siku za nyuma kwa lengo la kuzima sauti zao, leo sauti ni kubwa kuliko huko nyuma.
Tunakumbuka G55, Marhum Jumbe, Maalim Seif, Shaaban Mloo n.k.

Nne, majibu rahisi ya kudanganya au kuogofya watu kwa kutumia baadhi ya Wazee hayashabihiani na haja ya Hoja au maswali kutoka kizazi cha leo , kizazi kisichowajuawWaanzilishi wa Muungano labda kupitia maktaba.

Wazee wanaojibu hoja kwa lugha za ''adhimu na adimu, ni muungano wa kipekee' n.k. hawana hoja zinazojibu haja na hoja za nyakati tulizonazo. Ni watu wanaotumia lugha za kutisha lakini hawana majibu ya hoja.

Kizazi cha leo kina maswali mengi. Mfano, ikiwa hoja na kero za Zanzibar zinashughulikiwa zimalizwe lini kero za Tanganyika zitaanza kushuhulikiwa? Nani atasimamia masilahi ya kero za Tanganyika?
Zanzibar inaleta nini katika meza ya Muungano ?
 
'WAHAMIAJI HARAMU'' KUTOKA TANZANIA BARA KWENDA ZANZIBAR'

Katibu Mkuu wa SMZ alipoita Watoto ''Wahamiaji Haramu Zanzibar


Gazeti, The Citizen la 23 July 2024 limemnukuu Katibu mkuu Wizara ya Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto wa SMZ Bi Abeida Rashid akisema kuna Watoto wa mitaani 66 walioingia Zanziar kwa '' NJIA HARAMU''

Bi Rashida alisema uhamiaji haram unachagizwa na ' Umasikini na unyanyasaji'' Abeida aliyasema katika kongamano la Umoja wa Mtaifa kuhusu Wahamiaji na kueleza Watoto hao wanavyolelewa kwa mahitaji.

Kauli ya Bi Rashida imezua mazungumzo na hisia kali katika mitandao ya jamii ikiwemo JF.
Kauli za Abeida zinaamsha hisia katika jamii kuhusu muungano!!

Mh Mbowe, M/Kiti wa Chadema Taifa alitahadharisha suala la DP. Kauli yake iliitwa ya kibaguzi ikalaaniwa na viongozi wa ngazi zote. Mh Tundu Lissu akamzungumzia Rais SSH kama Mzanzibar, naye alilaaniwa kwa ''ubaguzi'

Hakuna aliyeonyesha wapi Mbowe au Tundu Lissu walifanya ubaguzi kwa hoja! walilaaniwa tu kwasababu ni Watanganyika na ni mwiko kwao kuzungumzia Muungano au Zanzibar!

Mbunge Suleiman wa Zanzibar alisimama Bungeni Dodoma akisema '' Yeye si Mtanzania ni Mzanzibar''. Wabunge wa Zanzibar walikuwa kimyaa ishara ya kumuunga mkono, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na viongozi wa juu wa JMT na SMZ Kimyaa! Hatuskusikia yale ya Mbowe au Tundu Lissu

Kuna utamaduni uliojengeka wa kipuuzi, kwamba, Wazanzibar wana haki ya kusema chochote au lolote kuhusu Muungano, akisema Mtanganyika yale yale kavunja mwiko ''taboo''.
Utamaduni huo umejenga hasira na hisia kwa Watanganyika kwamba hawana pa kusemea ! wamefungwa midomo. Ni kwa hisia hizo, kauli ya Bi Abeida kuhusu '' Watoto wahamijai haramu' wa Tanganyika imezua mjadala na hisia kali katika kipindi hiki chenye hisia za Utanganyika na Uzanzibar

Tanzania ni Nchi moja kwa mipaka, Uhamiaji n.k. . Hakuna Raia anayetoka sehemu moja ya nchi kwenda nyingine akaitwa 'Mhamiaji haramu''. Raia anaweza kuitwa ''mhamiaji' lakini hakuna Uharamua, ni RAIA wa Tanzania. Kuita Watoto wadogo''Wahamiaji haramu'' ni kukosa hekima busara na utu!

Kwa mujibu wa Prof Makame wa SUZA, kuna Wazanzibar takribani 1.2 Milioni wanaoishi Tanganyika.
Idadi hiyo ni kubwa kuliko Wazanzibar wanaoishi Zanzibar kwa wakati wowote.

Wazanzibar wanaoishi Tanganyika hawaitwi '' Wahamiaji haramu'' kwasababu zile zile wanazosema Wazanzibar '' wao ni '' Watanzania na Wazanzibar'
Ikiwa ni hivyo, watoto 66 wanakuwaje '' Wahamiaji haramu'' Zanzibar?

Wazanzibar hulalamika kwamba bidhaa kama sukari, maziwa, TV na zingine zinazopitia Zanzibar kwa njia za magendo na zingine zenye viwango duni ziingie Tanganyika bila kodi kwasababu '' sisi ni nchi moja''.
Ikiwa ni kweli, Watoto wa Tanganyika wanakuwaje '' wahamiaji haramu' Zanzibar ambako '' sisi ni nchi moja''

Pili, Bi Rashid anaaminisha dunia Watoto hao 66 wanakimbia Umasikini na unyanyaswaji Tanganyika.
Abeida hatambui wala hana fahamu kwamba Wazanzibar 1.2 Milioni wanaishi Tanganyika.
Kwamba Tanganyika ndiyo nchi iliyobeba Wazanzibar wengi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Bi Rashid haelewi takribani 10% ya Bajeti ya SMZ inalipwa na kodi za Wazazi wa hao Watoto anaaowaita wahamiaji haramu achilia mbali gharama za kubeba Muungano pekee.
Abeida hatambui Wizara ya Uhamiaji ipo mambo ya ndani ya JMT ikigharamiwa na Watanganyika.

Tatu, Wazanzibar takribani 1.2 Milioni wanaishi Tanganyika wanatumia huduma zote ikiwemo elimu na matibabu kama Watanzania na si '' wahamiaji haramu kutoka Zanzibar'' . Bi Rashid hana ufahamu na hili!

Kitendo cha kuwasema Watoto 66 wa Tanganyika ni udhalilishaji. Watoto 66 ni kidogo sana ukilinganisha na maelfu ya Watoto wa Zanzibar wanaoishi Tanganyika na Familia zao wkifaidika na fursa zilizopaswa kuwahudumia hao 66 anaowabagaza bila kujali hakuna '' uhamiaji haramu kwa watoto'' au minors

Kwa kiwango au mtazamo wowote , kauli za Katibu mkuu Bi Abeida Rashid ni za kudhalilisha, zilizojaa chuki.
Ni kauli zinazopanda chuki kama inavyosemeka katika mitandao, Watanganyika wakighadhibika sana

SMZ itoke kauli na kuomba radhi kuhusu kauli ya Bi Abeida Rashid
Muhimu ni viongozi wa Serikali zote kumkemea. Laiti kauli angezisema Mtanganyika zingeitwa za kichochezi.

Bi Abeida Rashid amewakosea Watanganyika, awaombe radhi. kutoomba radhi kuna panda mbegu itakayochipua kwa gharama kubwa ! Hisia mitandaoni ni kali, hata kama zitafumbiwa macho chuki itabaki

Abeida amewakosea Watanganyika!

Aug 23 2024


sept 06





View: https://www.youtube.com/watch?v=Ei3gPVd7yjE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…