Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #41
Mkuu, kuna upotoshaji wa jamii kwa 'exploitation' ya Wananchi ambao licha ya kuwa 'literate' bado wanakosa ''perspective analysis'' kwa maana ya kuyaangalia mambo kutoka 'angle' tofauti.Kuna wakati wengine tunakaa pembeni na kuwaachia akina Pascal Mayalla, watambe humu wanavyopenda na kujizolea sifa kama mpembuzi yakinifu.
Wanaofanya 'exploitation' wana access na media. Wasomaji hawana uwezo wa kuchambua nini kimeandikwa au kusemwa na gazeti au TV kama maoni au ukweli . Wanafahamu kila lisemwalo au kuandikwa ni 'fact'
Nitafafanua upotoshaji
Niongezee, hata CCM haina 'structure' ya chama kimoja. Kuna kamati maalumu ya CCM Zanziba (CCM Zanzibar)Kuna hili dude CCM. Chama cha Mapinduzi ni muunganiko wa kilichokuwa, chama tawala Tanganyika, TANU na chama tawala Zanzibar Afro-Shirazi Party. Baada ya miaka 60 baada ya huo muunganiko, tuna chama kimoja, CCM lakini serikali bado ziko mbili.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kuna taifa linaitwa Tanzania. Ndani ya taifa hilo kuna chama tawala CCM. Ndani ya nchi hiyo hiyo moja hicho chama tawala eti kimeunda serikali mbili tofauti! Jamani nawauliza wachambuzi popote mlipo, hali hii inawezekanaje?
Ndani ya CCM Union kuna Wazanzibar. Swali linabaki , Chama kimoja kuwa na sehemu 2, kama nchi moja serikali 2
Wapotoshaji na nina uhakika wanajua kwamba wanapotosha wanasema Serikali 2 za Tanzania na SMZ ndio kigezo cha kufanya Muungano 'adhimu na adimu''. Maneno yanatumika kufunika ukweli hakuna jibu la kuwa na Serikali 2 .
Upotoshaji umepewa utetezi mwingine, kwamba tuna Union kimataifa halafu tuna Federation ndani ya nchi.
Fikiria hivi kwamba kuna Federation ya Tanzania na Zanzibar! na hili linasemwa bila aibu haya wala soni.
Ikifika hapo Wananchi wetu wasio na ''perspective analysis' wanabaki kuamini yanayoandikwa.
Tena wanaofanya upotoshaji huo wanapewa access na media nyingi tu kufanikisha lengo la upotoshaji.
CCM kama niliyoeleza mwanzoni wanasema ni Moja, ukiangalia ni mbili kwa jina la kamai maalumu Zanzibar.Dude hili CCM liliunda serikali ya Muungano (Tanganyika na Zanzibar) halafu dude hilo hilo likaunda serikali ya pili (Zanzibar) Sasa kama TANU na Afro-Shirazi ziliunganika tukapata CCM, kwa nini serikali mbili? Kama ya Zanzibar ipo, je ya Tanganyika iko wapi?
Kwa maana kwamba kinachokosekana ni CCM Tanganyika.
Mtririko huo wa makosa ndio unatuletea kituko kingine cha Serikali 2, yaani ya Muungano ikiwemo Zanzibar halafu ya Serikali ya Zanzibar lakini ya Tanganyika imekufa.
Kuna wakati Serikali ya JMT yenye Wazanzibar inajadiliana na Serikali ya Zanzibar!
Matatizo ya Muungano yanatokana na 'structure' isiyo na majibu akina Pascal wakisema 'adhimu na adimu''
Vituko havijaishia hapo, mwaka huu Serikali ya JMT imeingia MoU na SMZ kuhusu nishati na madini.
Rais wa JMT ikiwemo Zanzibar anasaini MoU na sehemu ya JMT ambayo ni Zanzibar na Rais wa SMZ.
Vituko havina mwisho, Katiba ya JMT inapokuwa na mamlaka kidogo kuliko katiba ya Zanzibar''
Sheria zinazotungwa Dodoma Wazanzibar wakiwemo zikivuka hazina maana hadi Wazanzibar wazipitie!
Kuna tatizo na halitakuwa na jibu bila uwepo wa Tanganyika.
Kwa structure ya sasa ya Muungano hakuna mtu anayefikri sawa sawa atakayeweza kuitetea, of course Chawa na Wadudu can say, write or do anything!