Muungano gani huu wa KIBAGUZI?

Wahuni hawajui nguvu kubwa iliyotumika kumdhibiti Nyerere. Nyerere aliondoa ukabila, udini, ukanda, matabaka.

Aliunganisha Taifa. Mtu amekaa kama Rais zaidi ya miaka 25 hajaiba hata senti tano. Leo analinganishwa na Samia.
 
Marekani kila miaka kumi ina target ya kuwaondoa viongozi wasumbufu kwa maslahi yao au taifa linaloweza kuwa kubwa duniani.

Ukiwa na rasilimali nyingi kama Uarabuni, Iran, lazima wazilimiliki. Au njia ambapo meli nyingi za biashara zinapita. Walijipanga waondoe watawala wa Somalia, Iran, Iraq, Libya, Yemen, Syria, Lebanon, Sudan. Watatumia vibaraka, mapinduzi, uuaji.

Tatizo lao lingine ni hawataki ushindani kwahiyo China na Urusi lazima warudishwe chini, wasie tatizo. Otherwise watatengenewa zengwe kama Ukraine, Taiwan.
 
Tanganyika imedhulumiwa saaana...kwa ajili ya siasa njaa za CCM......shame,shame!!
 
Imetosha, kama hawataki muungano wakweli kila mmoja ajitegemee.
Nikuulize wewe, na huyu mkuu 'Ngongo': Kwani waTanganyika wanayajuwa haya; na bado wanayo furaha kubwa na mategemeo ya CCM kuwaletea kiongozi huyo huyo ayaendeleze haya mnayo yalalamikia?
WaTanganyika wanaonyesha haya kwao hayana maana, ndiyo sababu Samia haoni shaka juu ya wao kuendelea kumwamini katika uongozi wake huu!

Kwani katika haya mliyo eleza hapa, kuna ugumu gani wa mTanganyika wa kawaida kuyaelewa na kuchukua uamzi anaoona unafaa?

Naomba nieleweke. Haya ni mambo mazito sana, lakini sielewi kwa nini watu hawayachukulii kwa uzito stahiki.
 
Ila mkuu nawe unagubu, tanganyika yote hii hadi uende zenji kutafuta kiwanja?

Omba uraia huko wa kudumu upate kitambulisho cha mkaazi uone kama hautapata kaplot😀.
Hana cha kiwanja wala shamba, anataka kufikisha ujumbe tu ambao wameshashindwa wengi hata kabla ya kuanza hizo harakati

Muungano bado upo sanaaaa
 
Tatizo mnachelewa sana kuvuka bahari. Mkiambiwa mpiganie Tanganyika yenu hamuelewi
 
Necta, nimr, tantrade, tpdc kote huko ni wapemba. Kiufupi tunapigwA.
Maneno machache haya yamenirudisha nyuma na kuwaza kinyume nyume.
Chukulia mipango ya "muda mfupi na muda mrefu".
Samia hawezi kuwa kwenye nafasi hiyo zaidi ya miaka mitano mingine...! "Muda mfupi"; kaandaa mipango ya "muda mrefu, hata kama yeye hajui ; miaka kumi na kuendelea; mia na zaidi. Tanganyika hii haiwezi kamwe kukosa viongozi wenye "DIRA" na maono ya muda mrefu...!

Sasa sijui kama ninaeleweka vizuri. Kama umenielewa, basi na wewe eleza kivyako unavyo nielewa ninacho kimaanisha hapa.
 
Sasa Kama wátanganyika hamna akili zenu mnataka wazanzibar wàfanyeje? Huoni mmeletewa wabunge, rais, mawaziri wakuu wa mikoa na wilaya nk toka Zanzibar kwenye akili wawatawale? Tulieni hivyo hivyo.
 
Nani anamwamini mtu ambaye si raia wetu?
Mkuu 'Vichekesho', usikwepe swali kirahisi hivyo. Iwe "kuaminiwa" au vinginevyo utakavyo ionekane; CCM hawana mbadala wa Samia... Sasa umenielewa ninacho kizungumzia? Usisahau, waTanganyika kama waTanganyika huwezi kuwatofautisha na CCM, au nakosea? (Hao wachache ninao warundika huko naomba mniwie radhi), nazungumza kijumla hapa.
 
Sasa Kama wátanganyika hamna akili zenu mnataka wazanzibar wàfanyeje? Huoni mmeletewa wabunge, rais, mawaziri wakuu wa mikoa na wilaya nk toka Zanzibar kwenye akili wawatawale? Tulieni hivyo hivyo.
EEEeeeeHEEEEEeee!
Bahati nzuri sana, binafsi huwa ninakuelewa vizuri haya unayo andika hivi. Lakini chunga sana; hao jamaa wasi akili wanaweza kuwa na akili ndefu zaidi ya uielewavyo; hata ikiwa ni akili ya kubahatisha tu mara moja moja. Usikurupuke, nielewe vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…