Ni jambo zuri kuungana lakini lazima tutathmini kwa kina na kujiuliza kwanza kabla ya kuungana nao kwa maana kuungana maana yake ni kufungua mipaka
kama warundi wenyewe kwa uchache wao kuna msuguano mkubwa na mauaji ya kikabila japokuwa wana Makabila makubwa mawili je?
Itakuwaje wakija na kuchanganyika kwenye jamii yetu watanzania wenye makabila zaidi ya 120?
Wataenea masokoni, Vyuoni, kwenye Ajira, Masokoni nk...
Je wanaweza kustaarabika na kujizuia kwa upole na uvumilivu kama watanzania...?
Je kukitokea uchaguzi na akapita kiongozi asiyekubalika kwao watakubali kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida bila vurugu kama watanzania?
Muungano ni jambo jema lakini linahitaji umakini wa hali ya juu sana....