Hao uliowataja kama Msingi wa hoja yako ndio walioandika katiba unayohisi ni sawa kubadilishwa sasa kwanini suala la muungano unapinga mawazo mapya Boss?
Katiba hii tuliyonayo sisi kizazi cha sasa tudhani kuwa walikosea vitu vingi kwakuwa hatukuwepo wakati wanaiandika, hivyo hatujui kwanini wameiandika kama hivi. Hata pale Marekani wapo watu na majimbo wanahoji Muungano wao wakitaka marekebisho kwenye baadhi ya vipengele kama namna uchaguzi unavyofanyika na mshindi kupatikana; baadhi ya majimbo yanapewa hadhi kubwa na mengine hadhi ndogo. Kaka kuunda muungano kati ya nchi mbili zilizo huru kabisa sio jambo rahisi; lazima kuna kero na neema zitajitokeza kwenye upande mmoja au pande zote. Jambo la msingi ni kujikita zaidi kwenye faida zinazopatikana kuliko hasara. Wachumi wana kitu wanakiita the opportunity cost, sijui kwa kiswahili inaitwaje.
Anaetaka kuandika Katiba Mpya kwanza ajiridhishe na atavukaje kile kizingiti kilichoukwamisha mchakato wa uandishi wa Katiba mpya uliokwama, kabla hayaalika watu kuandika katiba mpya.
Sikuwepo wakati wanaiandika, lakini Katiba hii ya 1977 ndiyo iliyotuweza kufanya yafuatayo:
1. Kuyaunganisha makabila yote ya tanzania
2. Kiswahili kuwa lugha ya taifa na kuzungumzwa na makabila yote
3. Watu wa dini zote kuishi pamoja bila shida
4. Kujenga vijiji vya ujamaa
5. Makabila kuweza kuishi popote na kumiliki ardhi za makabila mengine bila vikwazo
6. Ilisaidia ukombozi wa Afrika
7. Ilimsaidia Nyerere asiuliwe au kupinduliwa na makaburu, wareno na watu wengine kama ilivyokuwa kwa viongozi wengine wa Afrika waliouawa.
8. Ndio sababu ya amani na utulivu tunaouona Tz sasa hivi kulinganisha na mataifa mengine kama DRC, Sudan, Somalia, Libya na kwingine; haikuzalisha wakimbizi wengi kwenda mataifa mengine.
9. Imeifanya tz kupokea wakimbizi wengi kutoka mataifa mengine
10. Ni chanzo cha kuwa miongoni mwa nchi zisizofungamana na upande wowote.
11. Ni sababu ya Tz kuwa na jeshi kubwa imara na lenye nidhamu.
12. Ni sababu ya huduma za kijamii kama shule, zahanati, maji, umeme, barabara kutawanywa nchi nzima.
13. Ni sababu ya Muungano wetu kusalia/kudumu kwa muda mrefu Afrika
14. Ni sababu ya hata mtoto wa masikini kupata elimu na ajira itakayomkutanisha na mtoto wa tajiri sehemu moja.
Hasara pia zipo za Katiba hii, lakini, lakini sio nyingi na kubwa, siku nyingine nitaziorodhesha pia.