Muungano unatutafuna! Iweje bara Umeme uwe shilingi 350 kwa unit wakati Zanzibar ni shilingi 130?

Muungano unatutafuna! Iweje bara Umeme uwe shilingi 350 kwa unit wakati Zanzibar ni shilingi 130?

Yaani Zanzibar wauziwe unit moja ya umeme kwa tsh.130 kama alivyoeleza Waziri wa Nishati na Madini Zanziber wakati sisi huku bara tunauziwa shilingi 350 na senti kadhaa.

Na wale wataosema Zanzibar ni wanyonyaji wanakosea, Tukumbuke kwamba Bara ndio inang'ang'ania sana huu muungano matokeo yake ndio haya sasa inabidi waipe Zanzibar kipaumbele kuzidi Bara iwe ni kwenye ajira, vyeo, huduma, n.k.

Bara tumebaki kuubeba mzigo mkubwa sana kwenye muungano huu
Sina uhakika, nadhani, zanzibar hakuna tanesco,, yaani huko umeme unasambazwa na kampuni ya huko,, hivyo kwenye bei, ya 350,ondoa gharama za kusambaza umeme na uendeshaji, mishahara, vipuli, etc
 
Sina uhakika, nadhani, zanzibar hakuna tanesco,, yaani huko umeme unasambazwa na kampuni ya huko,, hivyo kwenye bei, ya 350,ondoa gharama za kusambaza umeme na uendeshaji, mishahara, vipuli, etc
TANESCO ya kule inaitwa ZECO (ZANZIBAR ELECTRICITY CORPORATION).
 
Sote tunajua huu muungano wetu una matatizo makubwa, muundo wake hautufai kwa 100%.
Wazanzibar walishasema huu muungano hawautaki kwa kuwa unaingilia uhuru wao.

Watanganyika leo wanalalamika kuwa muungano huu ni mzigo mzito wa kiuchumi kwao kwa kuwa umekaa kumnufaisha mzanzibar kwa gharama ya mtanganyika.

Suluhisho ni nini?
Tuamue kuachana na huu muungano sasa, kwa kuwa sote hatuutaki. Sasa tujadili namna ya kupambana ili kuachana nao.
 
TANESCO ya kule inaitwa ZECO (ZANZIBAR ELECTRICITY CORPORATION).
Sawa, wao zeco ndo wanasambaza umeme baada ya kuutoa Tanesco,, wanalipa vibarua, magari, spare, etc,, na unategemea Tanesco iwauzie bei ya reja reja? 😲
Wao wanauziwa na tanesco bei ya jumla, my thinking
 
Nimekueleza vizuri matatizo zaidi ya Muungano.

Kwamba hata bara hatununui umeme kwa bei inayotakiwa.

Wewe bado umekwama kwenye Muungano.

Inaonekana una tatizo lako na Muungano, si bure.
Huwezi sema tu kwamba hatulipii garama halisi bila kuonyesha mchanganuo wake.

Unajua kama mgao wa umeme unalipiwa?
 
Wakikopa mikopo yao eti wanagawana 50/50

yaanibtaifa lenye watu milioni 60 ligawane na kataifa kenye watu milioni 1 sawa kwa sawa

Yaani zikija milionni 100 eti wagawane 50/50.

Halafu Sasa kwenye kulipa Taifa lenye watu milioni 60 ljnalioa karibia asilimia 99 ya mkopo sababu hako kataifa kenye watu milioni kwanza hakazalishi Hela Wala Kodi na hata kama wanazalisha haiwezi hata kuwalisha wenyewe.

Huu muungano ni unyonyaji nashauri uvunjwe au urekebishwe kwa staili ya kwamba Kila mtu afaidike kwa urefu wa kamba yake kama mama yao anavyosemaga.

Muungano wa kinyongaji kwa TANGANYIKA.

Mi Wala Sina hamu nao.
Ni upumbavu mtupu. Halafu kwa sauti za kurembua utawasikua mafuta sio suala la muungano. Kisa wanajua kuna mkondo wa mafuta huko
😡😡😠😠😈😈
 
Huwezi sema tu kwamba hatulipii garama halisi bila kuonyesha mchanganuo wake.

Unajua kama mgao wa umeme unalipiwa?
Nimeweka jedwali linaloonesha bei za umeme kwa nchi za Afrika. Angalia link ya mwisho post # 33.

Hata baada ya kulipia mgao wa umeme, bado gharama za umeme Tanzania kwa mfano tu, kulinganisha na Kenya, ni nusu.
 
Back
Top Bottom