Muungano unatutafuna! Iweje bara Umeme uwe shilingi 350 kwa unit wakati Zanzibar ni shilingi 130?

Sina uhakika, nadhani, zanzibar hakuna tanesco,, yaani huko umeme unasambazwa na kampuni ya huko,, hivyo kwenye bei, ya 350,ondoa gharama za kusambaza umeme na uendeshaji, mishahara, vipuli, etc
 
Sina uhakika, nadhani, zanzibar hakuna tanesco,, yaani huko umeme unasambazwa na kampuni ya huko,, hivyo kwenye bei, ya 350,ondoa gharama za kusambaza umeme na uendeshaji, mishahara, vipuli, etc
TANESCO ya kule inaitwa ZECO (ZANZIBAR ELECTRICITY CORPORATION).
 
Sote tunajua huu muungano wetu una matatizo makubwa, muundo wake hautufai kwa 100%.
Wazanzibar walishasema huu muungano hawautaki kwa kuwa unaingilia uhuru wao.

Watanganyika leo wanalalamika kuwa muungano huu ni mzigo mzito wa kiuchumi kwao kwa kuwa umekaa kumnufaisha mzanzibar kwa gharama ya mtanganyika.

Suluhisho ni nini?
Tuamue kuachana na huu muungano sasa, kwa kuwa sote hatuutaki. Sasa tujadili namna ya kupambana ili kuachana nao.
 
TANESCO ya kule inaitwa ZECO (ZANZIBAR ELECTRICITY CORPORATION).
Sawa, wao zeco ndo wanasambaza umeme baada ya kuutoa Tanesco,, wanalipa vibarua, magari, spare, etc,, na unategemea Tanesco iwauzie bei ya reja reja? 😲
Wao wanauziwa na tanesco bei ya jumla, my thinking
 
Nimekueleza vizuri matatizo zaidi ya Muungano.

Kwamba hata bara hatununui umeme kwa bei inayotakiwa.

Wewe bado umekwama kwenye Muungano.

Inaonekana una tatizo lako na Muungano, si bure.
Huwezi sema tu kwamba hatulipii garama halisi bila kuonyesha mchanganuo wake.

Unajua kama mgao wa umeme unalipiwa?
 
Ni upumbavu mtupu. Halafu kwa sauti za kurembua utawasikua mafuta sio suala la muungano. Kisa wanajua kuna mkondo wa mafuta huko
😑😑😠😠😈😈
 
Wazanzibar wao ni wananchi daraja la juu wanahitaji upendeleo maalmu
 
Huwezi sema tu kwamba hatulipii garama halisi bila kuonyesha mchanganuo wake.

Unajua kama mgao wa umeme unalipiwa?
Nimeweka jedwali linaloonesha bei za umeme kwa nchi za Afrika. Angalia link ya mwisho post # 33.

Hata baada ya kulipia mgao wa umeme, bado gharama za umeme Tanzania kwa mfano tu, kulinganisha na Kenya, ni nusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…