Muungano uwe wa serikali moja tu, kama sio hivyo ufe tu

Kuna uwezekano hakutakuwa na nchi inayoitwa tanzania miaka 50 ijayo....maana matatizo sugu hayatatuliki yapo tu...wameyafumbia macho
 
Faida pekee ninayoiona ya Muungano ni kuongeza idadi ya watu wetu kwenye kupata soko la ndani la bidhaa zetu na kumiliki na kudhibiti eneo kubwa bahari kiuchumi na kiulizi. Hii haina mjadala.
Sasa kama ni kwaajili ya ulinzi simngeungana na mataifa yote kwani hawawezi kupitia congo?.
 
Kuna uwezekano hakutakuwa na nchi inayoitwa tanzania miaka 50 ijayo....maana matatizo sugu hayatatuliki yapo tu...wameyafumbia macho
Jina litakuwepo tu! Siunajua tuna madini ya Tanzanite?.
 
Kuna uwezekano hakutakuwa na nchi inayoitwa tanzania miaka 50 ijayo....maana matatizo sugu hayatatuliki yapo tu...wameyafumbia macho
Ni upuuzi upuuzi tunaoambiwa tangu tukiwa watoto kuwa jina Tanzania linabeba majina ya Tanganyika na Zanzibar tayari, lakini Zanzibar bado ipo tena. Yaani Zanzibar Iko hai mara mbili ; Tanzania na Zanzibar. Ni wapuuzi TU watakaokubali hadithi kama hizo.
 
Sasa kama ni kwaajili ya ulinzi simngeungana na mataifa yote kwani hawawezi kupitia congo?.
Wakati tunaungana lilikuwa hakuna supersonic missiles na satellites za kivita. Siku hizi unaweza kupigwa kutoka Lebanon moja kwa moja. Lakini sio vizuri baharini jirani yetu kukawa na majimeli na nyambizi za kivita za adui. Usalama wa bamdari zetu ni mihimu sana.
 
Sawa mr
Seme nimda sana toka tanzania tumeshuhudia vita apa nchini.
 
Sasa kama ni kwaajili ya ulinzi simngeungana na mataifa yote kwani hawawezi kupitia congo?.
Mambo ni mengi sana, tunataka wazanzibar na watanganyika wote wawe na usawa kama watanzania kwenye nchi yao mpya Tanzania. Yaani raia wote wa Tanzania wawe kitu kimoja na fursa sawa kuliko ilivyo sasa. Mfano, Zanzibar ina watu kama 1.3m. Katika idadi hii tu ya watu ndani ya muungano lakini wana Rais, makamu 2 wa rais, waziri kiongozi, mawaziri, manaibu waziri, makatibu wa wizara, watumishi wizarani, mikoa 5, wilaya, tarafa, na kata kadhaa, shule za msingi na sekondari, vyuo vikuu, mabenki, majeshi, na mataasisi kadhaa, wabunge, wawakilishi, spika, nk. Hii maana yake kila wazanzibar 10 kuna wazanzibar 6-8 ambao wana ajira ya kudumu ya serikali na sekta binafsi. Hii nitofauti na Tanganyika kwenye nchi hiyohiyo moja ya tanzania.
 
Hivi Tanganyika kwa sasa inaraisi?.
 
Mimi kinachonishangaza ni ardhi, mimi wa bara sio rahisi kupata kipande cha ardhi Zanzibar kama ilivyo wao kupata ardhi bara.
Ukiuliza hilo utaambiwa zanzibar ni ndogo, jibu la kipuuzi. Kama mtu wa zanzibar atakosa ardhi si ataenda kuipata Tanga, Mkuranga, Dar es salaam au kokote kule Tanzania? Tunataka Tanzania ya aina hii, kila mtanzania yuko huru kabisa kununua, kuuza au kuishi popote kama mtanzania popote ndani ya jamhuri.
 
Absolutely
 
Kuna uwezekano hakutakuwa na nchi inayoitwa tanzania miaka 50 ijayo....maana matatizo sugu hayatatuliki yapo tu...wameyafumbia macho
Wale wazee wanaofahamu kuwa Nyerere alikusudia munngano wa aina gani na Karume alitaka muungano wa aina gani wamekaa kimya kwa faida zao binafsi. Lakini kwavyovyote vile maswali yataendelea kuulizwa na wajukuu, vitukuu na vilembwe vyao, na wakiendelea kukosa majibu watajaza majibu yao watakayoona ni sawa kwa usawa (unguided).
 
Wanasiasa ndio wanaotuzubaisha sisi raia tunaotaka full muungano. Hata Mzee karume Kuna siku alisemaga Afrika yote inahitaji kuungana kuwa nchi moja, sisi Tanzania muungano wetu umeshaenda mbele nusu na robo, bado robo moja TU kukamilisha full muungano. Sasa tangu afariki sisi tuliobaki tushindwa kumalizia Ile robo ya safari aliyoiacha.
 

Shida ni kuwa Zanzibar haipo tayari kufuta serikali yao, kwahiyo muamue either iendelee kukuepo au muvunje muungano
 
Kabla hujafikia hitimisho hilo, ungejishughulisha kujua kwanini kuna aina tofauti tofauti za miungano. Mwanadamu ni yule yule na sababu ni zile zile. Usifikuri sababu za UK, US, USSR, SPAIN, FRANCE na kwingine ni tofauti na za Tanganyika na Zanzibar.
πŸ‘ŒπŸ‘πŸ‘πŸ‘ŠπŸ€πŸ™πŸ†’
 
Manufaa ya muungano tumeyaona, ni matamu sana kwa watanzania walio wengi. Kila kijana mzanzibar anatamani kwenda kuishi Tanzania bara, na wako watanzania bara ambao wanatamani kwenda Zanzibar kwasababu moja au nyingine

Manufaa ya muungano tumeyaona wewe na nani ???

What a freaking Tanzania Baran dunderhead
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…