Muungano uwe wa serikali moja tu, kama sio hivyo ufe tu

Shida ni kuwa Zanzibar haipo tayari kufuta serikali yao, kwahiyo muamue either iendelee kukuepo au muvunje muungano
Kushikilia msimamo kama huo ni kutokuwa tayari na muungano ambao umedhihirika kuwa na faida kubwa kwa wazanzibar. Faida kubwa kuliko yote wanayoipata wazanzibar kwenye muungano huu ni ardhi na makazi, Tanganyika ni kubwa sana kuliko Zanzibar na wazanzibar wanazaana sana kupitiliza. Faida ya pili ni uchumi, vijana wengi wa Zanzibar wako bara kujitafutia maisha bila mashariti yoyote. Faida ya tatu kubwa na huduma na vyakula kutoka bara kwa bei nafuu.

Wanasiasa wakuu wengi kama sio wote Zanzibar wamewekeza bara, wanawahadaa watu wao kuhusu muungano.
 
Nchi zote East Africa zinataka muungano na Tanganyika kwaajili ya ardhi na bamdari zake. Zanzibar inafaika na ardhi lakini Wana jeuri sana. Tunataka watanzania wote tuwe kwenye ukurasa mmoja, kama Kuna nafuu iwe kwa wote na kama Kuna shida iwe ni kwa raia wote. Hivi Sasa raia wa Tanzania Kuna wenye nafuu na wasio na nafuu yaani Cha Zanzibar ni chetu na Cha Tanganyika ni chetu pia. Wengine Cha Zanzibar ni chao na Cha Tanganyika ni chao pia.
 
Nimekwambia, fanya stadi ujiridhishe aina za miungano na changamoto zake. Unaweza ukafikiri Marekani wametulia kumbe Wana yao!
Yes ni kweli, tunaona masuala ambayo Texas wameleta na baadhi ya majimbo kutaka kujitenga lakini wenzetu wamesimika mizizi imara tofauti na sisi
 
Tumechoka kuwabembeleza wazenj iko wazi kua Zanzibar haitaki kabisa swala Hilo la muungano
Aidha iwe serikali moja au waachiwe wawe kama Comoros. Huu ni utumwa mamboleo sio muungano.
 

HIo sio hoja kabisa mkuu, wazanzibari wangekuwepo Bara hata bila ya Muungano, walishakuepo toka kabla ya muungano, wazanzibar wengi ni watu wakutembea wakutaafuta fursa za kimaisha, Wengi sana wapo Oman, Dubai, Msumbiji, Kenya, U.K Canada, U.S, Uganda, Ila kote huko hakuna Muungano.

KInachopiganiwa na wazanzibari hapo ni utambulizi wao, au dignity yao. Mkuu dignity ni zaidi ya mafanikio ya kiuchumi.
 
Mimi kinachonishangaza ni ardhi, mimi wa bara sio rahisi kupata kipande cha ardhi Zanzibar kama ilivyo wao kupata ardhi bara.
Hii hata kwa wao wenyewe wazanzibari, ni rahisi kwao kupata ardhi bara kuliko Zanzibar.

Usishangae, Zanzibar ni visiwa, hakuna ardhi ya kutosha, na hilo ndio jambo lililopelekea wawe na sheria ngumu za kumiliki ardhi.
 
Nakubaliana na wewe yote isipokua suala la chakula, hawakipati kwa bei rahisi, hawakipati kwa sababu ya muungano, na hapo anaefaidika zaidi ni mkulima wa bara kupata soko la uhakika. Wakenya na wengineo wananunua kwetu kama wazanzibari bila muungano.

Kawaida mwenye pesa anachagua popote anapotaka kununua, ndio maana Zanzibar kuna mafuta ya kupikia kutoka Oman, mchele kutoka Thailand, Pakistan na Vietnam, na sisi hapa Bongoland tunakula ngano kutoka Russia na Ukraine wala hatuna muungano nao.
 
Yes ni kweli, tunaona masuala ambayo Texas wameleta na baadhi ya majimbo kutaka kujitenga lakini wenzetu wamesimika mizizi imara tofauti na sisi
Nani kasema sisi hatujasimika mizizi? Yaani mtu mmoja mmoja kama wewe au Chadema au CUF akisema hataki Muungano ndio kutosimika mizizi? Ahahahahaha!!!!
 
Nani kasema sisi hatujasimika mizizi? Yaani mtu mmoja mmoja kama wewe au Chadema au CUF akisema hataki Muungano ndio kutosimika mizizi? Ahahahahaha!!!!
Usiwe na fikra fupi, tofautisha kusimika mizizi na fikra za mtu mmoja au wawili na hata kadhaa kama sio wengi wasioutakia heri Muungano wetu

Sijamaanisha TZ haijasimika mizizi, vinginevyo usingekuwepo mpaka leo ila wametuacha mbali katika eneo hilo kutokana na misingi waliyoiweka tokea kuasisiwa kwa muungano wao
 
Sijaelewa umeandika nini. Ila kama wewe umeelewa basi inatosha! Ahahahahaha!
 
Huu muungano ni wa ccm na siyo wa wananchi.Ukiwagusa au ukahoji uhalali wa huu muungano hutapewa jibu kwa sababu uko kwa maslahi yao zaidi ili waendelee kugawana madaraka.Labda wajivu wa siasa watuambie aina hii ya muungano uko ktk nchi gani duniani ambao nchi moja inauliwa wkt nyingine inaachwa hai na kupewa Mamlaka kamili
 
Acha uongo mkuu, wasingekuja bila utaratobu na kukaa bila utaratibu na kuchukua bila bila utaratibu kama ilivyo Sasa.
 
Chakula wananunua na kusafirisha kama raia wengine TU. Hawahotaji kwenda kununua kwenye maghala ya serikali kama bashe alivyowataka wakenya na wageni wanataka chakula tz
 
Hatutaki muungano unaotegemea ulinzi wa CCM TU kuwa madarakani. Tunataka muungano unaolindwa na watanzania wote. Waliotengeneza jina la Tanzania lenye herufi za Tanganyika na Zanzibar walikuwa na maana gani? Mbona swali rahisi kama hili linapatiiwa majibu ya kijanja kijanja TU?
 
muungano wetu ni kama china na hongkong,
hakuna athari zozote zanzibar wakiendelea kujitawala...
 
Acheni upumbavu....hapa nchi ni moja tu....miaka ya mbeleni tutapata Rais wa kutaka nchi moja....vilianza kuvunjwa vyama vya siasa TANU NA ASP kuwa CCM, hata hiyo zanzibar serikali yake itakufa.....mtulize mshono
 
Ni swala la muda tu. Wabunge sasa mmoja mmoja anaanza kutikisa kiberiti.
 
Kwa sababu nchi kubwa kuzitawala nchi ndogo kwa kigezo cha muungano huku wao wakijifanya kuwapa serekali feki nchi ndogo huku wao wakichukua mamlaka yote muhimu ya kila nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…