Hiyo sio kweli kwa Tanzania, Huku kwetu hata mzanzibar anaweza kuwa Rais wa Tanzania yote , hiyo Tanganyika inawezaje kuimeza Zanzibar? Mbona Tanganyika imemezwa na Tanzania bila kuona tabu yoyote? Makabila, milima mbuga, kahawa nk viko palepale ilipokuwa Tanganyika. Tueleze Zanzibar itakavyomezwa na Tanzania kama muungano utakuwa wa serikali moja TU. Watanganyika wamepoteza utanganyika (identity) Yao kwanini isiwe wazanzibar pia?Kwa sababu nchi kubwa kuzitawala nchi ndogo kwa kigezo cha muungano huku wao wakijifanya kuwapa serekali feki nchi ndogo huku wao wakichukua mamlaka yote muhimu ya kila nchi
Wamerekani wako stable kwasababu majimbo Yao yana uhuru wa kujiamulia baadhi ya mambo Yao mengi, ukifuata muungano wa marekani huna budi kuirudisha serikali ya Tanganyika na kuwa na muungano wa serikali tatu. Kuna wakati watanganyika wanaopinga mzanzibar kuwa Rais wa Tanzania ninawaelewaelewa hivi.Yes ni kweli, tunaona masuala ambayo Texas wameleta na baadhi ya majimbo kutaka kujitenga lakini wenzetu wamesimika mizizi imara tofauti na sisi
Hapa Wanaingiaje, kwa green cards?
niambie kitu kimoja tu, Tanganyika imefaidika na nini kwenye muungano?Manufaa ya muungano tumeyaona, ni matamu sana kwa watanzania walio wengi. Kila kijana mzanzibar anatamani kwenda kuishi Tanzania bara, na wako watanzania bara ambao wanatamani kwenda Zanzibar kwasababu moja au nyingine. manufaa ya muungano kila mtu anaweza kuyasimulia bila kuambiwa wala kusoma pahala popote.
Mwalimu Nyerere na Karume nina uhakika wote au mmojawapo alitaka muungano wa serikali moja, na wako wazee ambao wanajua dhamira ya muungano na aina ya muungano ambayo waasisi waliukusudia lakini kwa unafiki na woga wao wamenyamaza kimya na hatimaye kufa na siri hiyo.
Wazee wa hivi hawafai kupewa heshima tunayowapa, maana ni wanafiki, waoga na wasioona mbele. Nyerere sio mjinga kuifuta serikali ya Tanganyika na asiifute ya Zanzabar, lazima kuna jambo ambalo tunafichwa na kupewa sababu za kijinga na uongo juu ya muungano wa serikali mbili. G55 hawakuwa wajinga kudai kuirudisha serikali ya Tanganyika; bila shaka ilikuwa kujibu mkwamo wa kupata serikali moja.
Wakati tunaelekea kuadhimisha sikukuu ya Muungano ni aibu nchi moja kuwa na serikali kamili mbili bila kuwepo ya Tanganyika. Wazee kama Pius Msekwa, Warioba, Butiku, Mongella, Msuya, Sumaye, Kikwete, na wengine ambao wanafahamu sababu za kweli na halisi juu ya kwanini serikali ya tanganyika ilifutwa na ya zanzibar akabakizwa waitoe siri hiyo kabla hawajaiaga dunia na kuondoka nayo hata kama kwakufanya hivyo kutaleta shida kwao. maana watoto wajao hawataujua ukweli halisi juu ya kwanini kuna serikali 2 badala ya 1 au 3.
Ni muhimu sana badala ya hivi ilivyo sasa ambavyo muungano wa aina hii utahojiwa na kila kijana wa leo na wa kesho mwenye akili timamu. Hii haitaleta afya ya muungano siku zijazo wakati wazee wote wanaoijua siri ya muungano watakapokuwa wameondoka duniani.
Nje ya muungano tusingewakuta mapemba wako kule lukozi, Lushoto wanatafuta makabichi mashambani. Hoja ni kwamba nje ya muungano waunguja na wapemba wasingezikanamkuu hata mungeeka hizo taratibu, wapemba wengekuepo na wangeishi na kufanya biashara zao, Kwa hoja ya muungano isiwe kama ni kigezi kuwa eti munawasaidia wapemba. Acheni roho mbaya. Leteni hoja za muungano na sio ishu za kipuuzi
Uko sahihi, ukweli ni kwamba hakuna mwananchi mtanganyika wa kawaida yeyote anayeweza kukueleza kwake binafsi faida aliyoipata kutokana na huu Muungano bali tu wote wanaeleza maneno ya kulishwa kikasuku kuwa ni ulinzi kwa nchi yetu, hoja ambayo haina mashiko kwani hata kama Zanzibar ingekuwa huru bado Tanganyika tungekuwa salama kama tunavyopakana na mataifa mengine.niambie kitu kimoja tu, Tanganyika imefaidika na nini kwenye muungano?
1. Mtanganyika zanzibar hamiliki ardhi vs Mzanzibar anamiliki ardhi bara apendavyo.
2. Mtanganyika haajiriwi serikali ya zanzibar, vs wazanzibar wameajiriwa wengi bara.
3. mzanzibar anaweza kuwa mbunge kwao na kwetu pia, Mtanganyika ni bara tu.
4. Mtanganyika akienda kule anaitwa chogo vs mzanzibar anaitwa mtanzania
taja kimoja tu.
Hii ni hoja ya kukariri, eleza faida yako au ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida wa Tanganyika kama ambavyo wazanzibar wanazopata kibinafsi kama vile ajira, uongozi, ardhi, utaifa, nk.Muungano wetu una faida nyingi hasa ulinzi na usalama, tuulinde kwa gharama yoyote.
Acha kufananisha vituo tofauti, China ulikuwepo kabla ya hongikong na hakuna kati yao hao aliyepoteza jina lake. Pili faida ni kwa wananchi wa pande zote tofauti na kwetu wazanzibar tu ndiyo wanaonufaika na miungano, embu tueleze wewe kama wewe unanufaikaje na miungano huu kama ni mtanganyika uache wimbo wa kikasuku wa ulinzi.muungano wetu ni kama china na hongkong,
hakuna athari zozote zanzibar wakiendelea kujitawala...
Nje ya muungano tusingewakuta mapemba wako kule lukozi, Lushoto wanatafuta makabichi mashambani. Hoja ni kwamba nje ya muungano waunguja na wapemba wasingezikana
Bonafsi NITAULINDASasa mara mutaulinda muungano usivunjike mara uvunjike kwa kweli hamueleweki, Munasimama na Hoja Gani?
Faida halisi na kweli (tangible and palpable) ya muungano wanaipata wazanzibar. Mzanzibar inaepinga muungano anafanya hivyo kwa misingi ya dini na kuzuiwa ruhusa ya kurudisha tena waarabu Zanzibar kufanya hili na lile.Uko sahihi, ukweli ni kwamba hakuna mwananchi mtanganyika wa kawaida yeyote anayeweza kukueleza kwake binafsi faida aliyoipata kutokana na huu Muungano bali tu wote wanaeleza maneno ya kulishwa kikasuku kuwa ni ulinzi kwa nchi yetu, hoja ambayo haina mashiko kwani hata kama Zanzibar ingekuwa huru bado Tanganyika tungekuwa salama kama tunavyopakana na mataifa mengine.
Kabla ya kuwalaumu na kuwashutumu wazanzibar tumshutumu Nyerere na kundi lake la akina msekwa kuifuta Tanganyika prematurely harakaharaka. Hata hivyo Iko siku itafika muungano utakuwa wa watu badala ya nchini, tuendelee kuoana, kuoleana na kuzaliana sanaDunia nzima hakuna Muungano wenye Serikali moja.
Kipindi hiko Zanzibar ilikua mbele ya muda kuliko Tanganyika.Kabla ya kuwalaumu na kuwashutumu wazanzibar tumshutumu Nyerere na kundi lake la akina msekwa kuifuta Tanganyika prematurely harakaharaka. Hata hivyo Iko siku itafika muungano utakuwa wa watu badala ya nchini, tuendelee kuoana, kuoleana na kuzaliana sana