Muungano uwe wa serikali moja tu, kama sio hivyo ufe tu

Naomba unichague kuwa waziri mkuu wako siku ukiwa Rais ili nikusaidie kuitengeneza Tan/zan/ia ya kweli ambayo mtanzania ni mtanzania TU mwenye haki na fursa sawa ndani ya muungano. Huo ndio muungano aliokuwa ameikusudia Nyerere. Nadhani Mzee Jumbe ulimtesa sana kwa kuukataa muungano wa aina hii.

Hakuna mtu Yuko tayari kuwaambia wajukuu wetu sababu halisi za ugomvi wa aboud Jumbe na serikali/CCM.
 
Ndugu bara Gdp inasoma 79bilion vs zenji2bilion +1.5population.
 
Kaka hakuna kitu kibaya kwa akili na fikira kama kula ugali wa Mahindi.
 
Kipindi hiko Zanzibar ilikua mbele ya muda kuliko Tanganyika.
Na kuunga mkono, exposure ya Karume na wazanzbar ilikuwa kubwa kuliko ya Nyerere na watanganyika, wazanzibar wengi walikuwa na elimu japo ya kusoma na kuandika kuliko watanganyika. Hata Leo hii wazanzibar wanafikiria vizuri kuliko watanganyika. Kuna tofauti kubwa kati ya Marais wetu watanganyika na Marais wazanzibar katika kuiongoza Tanzania.
 
Ingekuwa ni uwezo wangu, tungekuwa na serikali moja halafu Zanzibar ingekuwa mkoa wa Tanzania.

Nimemaliza 😎
Kwani wakati wa Nyerere SI ilikuwa hivyo? Wakati wa mwalimu Rais wa Zanzibar hakuwa na sauti popote kokote. Leo hii anapigiwa na kupiga mizinga 21.
 
Naunga mkono hoja
P
 
Nimewahi kukaa na wazanzibar, Hawa jamaa na watu wa Bara ni watu wawili tofauti kabisa
 
Muungano usivunjike...


Cc: Mahondaw
Miaka 60 ya muungano kuvunjika sio kazi rahisi sana, lakini tunaweza kuufanya uwe imara zaidi kwa kuwa na serikali moja TU. Tuondoe dhana ya kufikirika kuwa Kuna upande utamezwa na upande mwingine. Wanaosema watuambie umezwaji huo utakakuwa kwenye nini, hewa, jua, maji, ardhi, maendeleo, watalii, kilimo, matibabu, uongozi au nini? Hata kwenye serikali moja Zanzibar itabakia kuwa Zanzibar na wakazi wake ma mitaa yake na Dodoma itaendelea kuwa Dodoma na wakazi wake na mitaa yake
 
Huo hautakuwa muugano tena, kuungana lazima kuwa na walioungana zaidi ya moja. Kama ndio hivyo litafutwe jina lengine sio muungano.
 
Huo hautakuwa muugano tena, kuungana lazima kuwa na walioungana zaidi ya moja. Kama ndio hivyo litafutwe jina lengine sio muungano.
kuungana ni kuunganika na kuunganika ni kuchanganyika. Watu wetu wameunganika na kuchanganyika, na mchanyiko huu unaonekana zaidi Bara kuliko visiwani. Leo hii muungano ukivunjika paap!! ni rahisi mno kuwarudisha watanganyika walioko Zanzibar kurudi nyumbani kuliko kuwarudisha wazanzibar kutoka Bara kurudi kwao Zanzibar. Kilio cha wazanzibar kitasikika dunia nzima kuliko kilio cha watanganyika kurudishwa kwao. Wacheni mchezo wenu.

Muungano wetu ni zaidi ya muungano na article ya muungano, umefika mbali sana hasa kwa maisha ya visiwani. Mzanzibar kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni faraja na muujiza kwake kuliko Mzanzibar kuwa Rais wa Zanzibar. Muungano huu umewapa haki wazanzibar kuwa sehemu ya pande kuuuubwa la ardhi (Tanganyika). Nchi kama Rwanda na Burundi wanaililia fursa hii lakini hawaipati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…