Muungano wa changu changu, ila chako changu hauwezi kudumu

Muungano wa changu changu, ila chako changu hauwezi kudumu

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Moja ya mambo utu uzima hutufunza ni kuwa hakuna wa muhimu sana kwenye haya maisha. Huu ndio ukweli unaotufanya tukishakuwa watu wazima, kutokulazimisha mahusiano tena.

Binafsi ni muumini wa muungano. Sio tu wa Tanzania bara na Zanzibar, bali wa jumuiya ya Afrika Mashariki nzima. Hakuna faida wananchi wa Afrika Mashariki wanayoipata kwa kubeba mzigo wa kuhudumia marais 9 na serikali zao.

Tutafakari, kama leo tungekuwa na nchi moja ya Jumuiya ya Afrika mashari, ambapo mkulima wa mahindi wa Mbiga, anakwenda kuuza mahindi yake Nairobi kama anavyokwenda Kariakoo. Au mfanyabiashara wa vitenge kutoka Kampala akapeleka mzigo wake Mtwara kama anavyokwenda Masaka? Halafu tukawa na serikali moja ndogo tunayoihudumia; Je, ni faida ngapi za kiuchumi tungezipata?

Sasa hapa kwetu hata huu muungano tu tulionao wanasiasa visiwani wanawadanganya wananchi wao kuwa muungano ndio unawaletea ukosefu wa ajira kwa wazawa hali ikiwa hao wazawa wao wamejazana huku bara, sio tu kwenye taasisi za muungano bali hata zisizo za muungano.

Kama kweli wazanzibari mmewachoka wabara, mfukuzeni kichaa pamoja na makopo yake. Sio mnaleta habari za baniani mbaya ila kiatu chake dawa. Hakuna ndoa ya changu changu, na chako changu inayodumu. Hakuna atakayekufa kwa muungano kuvunjika.

Rai yangu, huu muungano unafaida kwetu sisi wananchi ambao tungetamani biashara baina na uguja, pemba na bara istawi. Hawa viongozi wanachotaka ni nafasi za kula. Nyerere alishawahi sema, kila walipotaka tuwe na nchi moja Africa mashariki, waliopinga ni viongozi kwakuwa kila mmoja alikuwa anahoji tukiungana mm nitakuwa nani, na sio wananchi watapata nini?

Wenzetu Ulaya wanaungana, sisi akina kapuku tumekazana kuvurugana.
 
Moja ya mambo utu uzima hutufunza ni kuwa hakuna wa muhimu sana kwenye haya maisha. Huu ndio ukweli unaotufanya tukishakuwa watu wazima, kutokulazimisha mahusiano tena.

Binafsi ni muumini wa muungano. Sio tu wa Tanzania bara na Zanzibar, bali wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Hakuna faida wananchi wa Africa Mashariki wanayoipata kwa kubeba mzigo wa kuhudumia marais 9 na serikali zao.

Tutafakari, kama leo tungekuwa na nchi moja ya Jumuiya ya Africa mashari, ambapo mkulima wa mahindi wa mbiga, anakwenda kuuza mahindi yake Nairobi kama anavyokwenda Kariakoo. Au mfanyabiashara wa vitenge kutoka kampala akapeleka mzigo wake Mtwara kama anavyokwenda Masaka? Halafu tukawa na serikali moja ndogo tunayoihudumia; Je, ni faida ngapi za kiuchumi tungezipata?

Sasa hapa kwetu hata huu muungano tu tulionao wanasiasa visiwani wanawadanganya wananchi kuwa muungano ndio unawaletea ukosefu wa ajira wazawa wao hali ikiwa hao wazawa wao wamejazana huku bara, sio tu kwenye taasisi za muungano bali hata zisizo za muungano.

Kama kweli wazanzibari mmewachoka wabara, mfukuzeni kichaa pamoja na makopo yake. Sio mnaleta habari za baniani mbaya ila kiatu chake dawa. Hakuna ndoa ya changu changu, na chako changu inayodumu. Hakuna atakayekufa kwa muungano kuvunjika.

Rai yangu, huu muungano unafaida kwetu sisi wananchi ambao tungetamani biashara baina na uguja, pemba na bara istawi. Hawa viongozi wanachotaka ni nafasi za kula. Nyerere alishawahi sema, kila walipotaka tuwe na nchi moja Africa mashariki, waliopinga ni viongozi kwakuwa kila mmoja alikuwa anahoji tukiungana mm nitakuwa nani, na sio wananchi watapata nini?

Wenzetu Ulaya wanaungana, sisi akina kapuku tumekazana kuvurugana.
Huu muungano ni bora uvunjike then labda kufanyike opinion polls huku vipengele muhimu vyote vikiwa vimeainishwa, majority wakiukubali it's well and good na wakikataa ni kheri pia.
 
Kama ccm walishindwa kumuachia nchi Maalim kwa maiaka yote hy kwa njia ya karatasi bhs mpishi wa matatizo mshamjua.
 
Back
Top Bottom