Muungano Wa NASA wamtangaza Raila Odinga kugombea Urais na Musyoka Makamu wa Rais

Muungano Wa NASA wamtangaza Raila Odinga kugombea Urais na Musyoka Makamu wa Rais

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance NASA, umemteua aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu

Bw. Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia Chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili

Makamu wa Rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubali kumuunga mkono mgombea huyo mmoja

"Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa", alisema

Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake

Mgombea mwenza wa Bw. Odinga atakuwa Makamu wa Rais wa zamani Bw. Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Wiper.

Waziri mkuu mratibu wa shughuli za Serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi

Naibu Waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Watengula

Kiongozi wa chama mashinani CCM Isaac Ruto atakuwa Naibu Waziri mkuu atakayesimamia utawala wa huduma za jamii

Bw. Odinga ni Mwanasiasa aliyesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika mstari wa mbele kuunda vyama vya muungano na wanasiasa ambao ni mahasimu wake.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Fungueni Citizen Kenya kwenye luninga sasa hivi muwaone utitiri wa watu.
 
Vipi moses watangula,Isaac Ruto,Musalia Mdavadi,mana hao ndo wanaunda ile big five ya NASA,wao wamepewa nyadhifa gani mkuu???
Musala Mudavadi Chief Minister
Moses Wentangula Chief Secretary to the Govt.
Isack Ruto Deputy chief sectretary to the govt.
 
This is how it is going down
C-a_xHzXYAIgUR8.jpg
C-a7RPTXkAAHR0z.jpg
C-a7q5jXYAIPrC3.jpg
C-a99jPXgAAnpi-.jpg
C-Z_qf5W0AA-6IP.jpg
 
Alianza jomo na giramong giramong akachemsha. Uhuru na Raila Raila akachemsha mara ya kwanza bado nafikiri hii vita itaenda mpaka vitukuu
 
Raila Odinga - Mgombea urais
Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu
 
Raila Odinga - Mgombea urais
Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu

Mkuu, hivi sasa waziri Mkuu wa Kenya ni nani? Au kupeana ulaji tu?
 
Unaogopa nini? Mbona kwetu bado, au unaona upepo?
Halafu huyu wanasema ni rafiki wa JUMA PONDA MALI maana kuna sikukuu fulani alialikwa jiji la CHATTLE akakaa huko akila raha karibu wiki nzima. Sasa nashangaa wafuasi wa bwana YULE wanaanza kumpiga mawe, why!! Kwa nini?
 
mh hi aina ya uongozi Africa mashariki hatari sana,wakenya msifanye makosa bakieni na Kenyatta la sivyo mtajutaaaaa
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu mno. Kama mtu atashinda margin itakuwa ndogo mno. Mimi nafuagilia sana siasa za Kenya. Ngoma ya mwaka huu ni ngumu.
Siasa za Kenya ni za kikabila. Kura zina mirengo ya kikabila n kikanda. Uwepo wa Hassa Joho Mombasa ni threat kubwa kwa Uhuru Kenyatta. Hali kadhalika Isaac Ruto mkoa wa rift valley. Kuhama kwa Isaac Ruto kwenda upinzani kutagawanya kura za Rift valley ni pigo lingine kwa Uhuru Kenyatta na VP Ruto. Kingine Nairobi central zone itakuwa balaa Kidero (governor wa Nairobi) n Raila wanakubalika sana esp katika eneo la mabanda (slums) Kama Kibera Mathare nk though Uhuru nae amejitahidi kujiweka karibu na slums lkn bado Raila ana nguvu mno Nairobi
 
Back
Top Bottom