Muungano Wa NASA wamtangaza Raila Odinga kugombea Urais na Musyoka Makamu wa Rais

Muungano Wa NASA wamtangaza Raila Odinga kugombea Urais na Musyoka Makamu wa Rais

Wakenya msije mkajilaumu. Nasa imewaletea jembe lenye NIA, SABABU NA UWEZO WA KUWA RAIS. The ball is on your court. Msije baadaye mkaanza kulia lia eti mafisadi hayashughulikiwi... The guy who know nonsense is around the corner. It's your turn to grub opportunity. Wenzenu tunafurahia matokeo mazuri sasa.
 

Mpaka Sasa Raila Odinga anapewa nafasi Kubwa ya Kupeperusha Bendera ya NASA.

Kolonzo Musyoka Ametajwa katika nafasi ya Makamu wa Rais japo wengi wanataka yeye ndiye agombee Urais.

Musalia Mudavidi anatajwa katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu kama NASA wakishinda.

KTN wana Stream Live Viongozi wa NASA wanatarajia Kufikia hapa Uhuru Pack majira ya Saa nane Kamili Mchana Huu. Ulinzi Umeimarishwa KFU wanafanya Kazi Vizuri Ikumbukwe Uhuru Pack Ipo 200M kutoka Serena Hoteli. Vijana Ni Wengi sana na Askari wapo wengi Kulinda Interference yeyote wakihakikisha Barbara inayoelekea Serena na Kulinda Usalama Wa Raia.


Watu ni Wengi sana Inanikumbusha Mafuriko ya Chama Fulani cha Siasa Pale Jangwani lakini Kikatoka Mikono Mitupu. Msaga Sumu hayupo hapa Kuna Wasanii Wengine.



Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.

Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.

Makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubalina kumuunga mkono mgombea huyo mmoja.

"Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa," amesema.

Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake, kama ilivyokuwa kwenye rasimu hiyo ya katiba.

Mgombea mwenza wa Bw Odinga atakuwa makamu wa rais wa zamani Bw Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement.

Waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi.

Naibu waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.

Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto atakuwa naibu waziri mkuu atakayesimamia utawala na huduma za jamii.

Mpangilio wa Upinzani

  • Raila Odinga - Mgombea urais
  • Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
  • Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
  • Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
  • Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu
Bw Odinga ni mwanasiasa anayesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika msitari wa mbele kuunda vyama vya miungano na wanasiasa ambao ni mahasimu wake.

Odinga ni nani?
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1997 ambapo Raila alishikilia nafasi ya tatu, kufuatia kuundwa kwa muungano wa chama chake (NDP) na chama cha rais wa zamani Daniel moi (KANU), aliteuliwa kama waziri wa kawi katika serikali ya muhula wa mwisho wa Moi.

Mwaka 2002, baada ya Moi kumuunga mkono uhuru Kenyatta, kama mrithi wake, Raila na maafisa wengine wa KANU ikiwemo Kalonzo Musyoka na wafuasi wengine, walipinga ungwaji mkono wa Kenyatta kugombea Urais.

Waliungana na kiongozi wa upinzani Mwai Kibaki na na kuunda muungano wa National Rainbow Coalition (Narc) ambao baadaye ulishinda uchaguzi wa mwaka 2002.

Raila aliungana na Rais Mwai Kibaki kuunda serikali ya Muungano ya NARC baada ya kumuondoa mamlakani rais mstaafu Daniel Moi.

Mwaka 2005 aliungana na Uhuru Kenyatta aliyekuwa kama kiongozi rasmi wa upinzani, ili kushinda kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba chini ya serikali ya Rais Kibaki .

Wakati Kibaki alipomfuta kazi na washirika wake, aliunda chama cha ODM ambacho kilipiga kura ya 'La' dhidi ya rasimu ya katiba mpya ambayo ilishindwa mwaka 2005.

Aliongoza kampeni mwaka 2007 na kwa shingo upande kukubali ushindi wa rais Kibaki Katika uchaguzi uliokumbwa na utata, ghasia na mauaji.

Lakini hatimaye alilazimika kujiunga na Kibaki katika serikali ya Muungano.

Disemba mwaka 2012, Raila alilazimika kupiga moyo konde na kurudiana na Kalonzo Musyoka chini ya muungano wa CORD, kwani daima husema katika siasa, hakuna maadui wa kudumu.

Raila anaamini kuwa Wakenya wanastahili kuhudumiwa vyema zaidi kuliko ahadi wanazopewa na kwamba chini ya utawala wake.

Raila anaahidi kuleta mageuzi na kuhakikisha uongozi bora.

Chanzo: BBC Swahili

Wasiwasi wangu ni hawa behind the scenes backers ambao wamekua na Raila tangu 2007 wakimpa pesa za maana ili kuedesha campaign zake...sasa hawa akifanikiwa kupata huo Uraisi watahakikisha pesa zote zinarudi...kwa mfano S.K Macharia wa Citizen TV ni mmoja wa hawa watu...siasa za Kenya zinaedeshwa na ma kitchen cabinet wenye maslahi binafsi na ndio maana pesa itatumika kwa mabilioni kutoka kwao wakitegemea kuja kuvuna baada ya ushindi...cartel are realy development parasite na watakua kila wizara kuvuna tenders...kwangu naona Uhuru angemaliza tena miaka hii mitano ila ajiongeze tena sana kutatua kero za rushwa kwenye idara za serikali na kuangamiza hizi cartels kabisa...
 
Wasiwasi wangu ni hawa behind the scenes backers ambao wamekua na Raila tangu 2007 wakimpa pesa za maana ili kuedesha campaign zake...sasa hawa akifanikiwa kupata huo Uraisi watahakikisha pesa zote zinarudi...kwa mfano S.K Macharia wa Citizen TV ni mmoja wa hawa watu...siasa za Kenya zinaedeshwa na ma kitchen cabinet wenye maslahi binafsi na ndio maana pesa itatumika kwa mabilioni kutoka kwao wakitegemea kuja kuvuna baada ya ushindi...cartel are realy development parasite na watakua kila wizara kuvuna tenders...kwangu naona Uhuru angemaliza tena miaka hii mitano ila ajiongeze tena sana kutatua kero za rushwa kwenye idara za serikali na kuangamiza hizi cartels kabisa...
Raila Born Loser Uchaguzi Umeshaisha Jubilee wanajipatia Miaka Mingine Kalonzo ndo alikua Perfect fit.
 
Huyu Laila odinga hana tofauti na wakina Maalim Seif Sharif au Lipumba , kila uchaguzi lazima wa contest wao utafikiri hakuna binadamu wengine zaidi yao.
 
Kwahiyo Magufuli ataenda kumpigia kampeni kipenzi chake toka moyoni
jumuiya ya africa mashariki inawekwa rehani kwa huu urafiki wa Magu na Raila, hizi chokochoko za kuzuia gesi ya tz kuingizwa kenya zinachombezwa na huu uchaguzi.

sielewi UKAWA watakuwa upande gani kama magu atasupport upinzani wa NASA na wao wataendea kuunga mkono mabadiliko kama ilivyo agenda ya upinzani kenya
 
Today
Uhuruto
C-bazRcWAAAtBes.jpg


Vs NASA
C-bVm1BXcAAtrp0.jpg


It takes the whole opposition to unite to bring down Uhuru, still it will not be easy, i know what lies ahead, proper campaigns like never seen before,

Otherwise i love those costumes, very patriotic
 
Hivi vyeo vimeanza kupingwa na Baadhi ya watu kuwa havipo kwenye Katiba
 
Today
Uhuruto
C-bazRcWAAAtBes.jpg


Vs NASA
C-bVm1BXcAAtrp0.jpg


It takes the whole opposition to unite to bring down Uhuru, still it will not be easy, i know what lies ahead, proper campaigns like never seen before,

Otherwise i love those costumes, very patriotic

Kazi ngumu sana
na mkiwa na imani hii mtaelekea kubaya,
Nikazi kubwa kumuondoa Uhuru
 
kutangazwa kwa raila flag bearer is the beginning of their defeat ,raila can't beat Uhuru
 
kutangazwa kwa raila flag bearer is the beginning of their defeat ,raila can't beat Uhuru
its a 50 50 thing right now...it is ifficult to tell who will win...but it is very hard for a Luo to win a presidency....u will see how Kikuyus will turn out to vote in large numbers
 
Back
Top Bottom