jumuiya ya africa mashariki inawekwa rehani kwa huu urafiki wa Magu na Raila, hizi chokochoko za kuzuia gesi ya tz kuingizwa kenya zinachombezwa na huu uchaguzi.
sielewi UKAWA watakuwa upande gani kama magu atasupport upinzani wa NASA na wao wataendea kuunga mkono mabadiliko kama ilivyo agenda ya upinzani kenya
Kwa vile Rift Valley ndio nyumbani kwa Ruto na amejijenga kisiasa kwa muda mrefu kunakipa chama cha Jubilee nafasi na pia Raisi Mstaafu Moi anatokea huko na amemwidhinisha Uhuru kwa mara nyingine,yeye pia ana ushawishi, Kikuyu + Kalenjins ni bonge la support kwa Uhuruto na pia uchaguzi ujao mpango ni Uhuru amwachie Ruto awe raisi so kwa kifupi pia Ruto ni president in waiting...so indicators za kuwa favour hawa wawili ni nyingi, wakipata kura za Rift Valley na Central aafu wadokoe kwa Waluhya hapo watakua wamejipa nafasi zaidi, ICC walishdwa kuwazima uchaguzi uliopita na wakenye wakaona ni bora wao waedeshe nchi kwa Skyp kuliko CORD...so pia awamu hii watakua na mbinu mbadala...kazi ipoteh teh
technically ndio kivipi
nadhani anaye leta kura nyingi awe flag bearer.
wao wamesema watakuwa wakiamua wote kama group, so naamini kama wakenya hawamtaki Uhuru they will rejwct him ila kama wana mtaka hakuna kusingizia eti oo RAO is this, so ngoja tuone uchaguzi utakuwaje
why you guys mna siasa za identity!? it sucks kwa kweliKwa vile Rift Valley ndio nyumbani kwa Ruto na amejijenga kisiasa kwa muda mrefu kunakipa chama cha Jubilee nafasi na pia Raisi Mstaafu Moi anatokea huko na amemwidhinisha Uhuru kwa mara nyingine,yeye pia ana ushawishi, Kikuyu + Kalenjins ni bonge la support kwa Uhuruto na pia uchaguzi ujao mpango ni Uhuru amwachie Ruto awe raisi so kwa kifupi pia Ruto ni president in waiting...so indicators za kuwa favour hawa wawili ni nyingi, wakipata kura za Rift Valley na Central aafu wadokoe kwa Waluhya hapo watakua wamejipa nafasi zaidi, ICC walishdwa kuwazima uchaguzi uliopita na wakenye wakaona ni bora wao waedeshe nchi kwa Skyp kuliko CORD...so pia awamu hii watakua na mbinu mbadala...kazi ipo
Kasema yupo kwa uhuru wewe acha kusikiliza huku wakimbia wwNimemsikia Waziri mkuu mstaafu wa Tz Mh Lowasa amewaasa wale wabunge kutoka Kenya walipomtembelea Monduli kuwa "Safari hii msifanye makosa tena"
Tafsiri ni kuwa Lowasa anaukubali umoja wa NASA.
Maana yake ni kuwa Raila anakubalika kwa Magu na kwa Lowasa.
ni kweli unayoyasema ila hakuna kitu ambacho hawa watu wa opposition wako nayo ya kuletea wananchi...hawana sera...they are just power hungry...mabo ya kuleta sijui premier CS..i even thought itakua speaker for Wetangula...anyway, they have nt even won the thing yet..kwa hiyo tusubiri tuone matokeo...maybe they will lose
Upo sahihiShida ya Kenya ni makabila. Raila ana nafasi kwa sababu mwaka uliopita mudavadi hakuwepo kwenye muungano wao sasa ameongeza nguvu.
Happ ulipaswa kumpa hiyo elimuMcheza Ngoma uvuta kwake! Mrandi wewe ni jubilee povu utatoa tu! Kazi ya elimu ipo
Ana watu wa kabila lake (luhya) so never underestimated him.mudavadi hana lolote..ni kawaida yake kuotea hivyo..yani hajatoka siku akafanya kampeni ila hujishirikisha kwa kiongozi anayefikiri ataibuka ili apate kufaidi...
Tunafuatilia siasa za Kenya kwa sababu ni siasa zinazovutia na zenye ushindani wa hali juu tofauti na mataifa mengine ya kiafrika.
Siasa za Kenya zimekuwa ni darasa kwa wananchi na wanasiasa wa Tanzania hasa chaguzi za ndani ya vyama "primary elections".
Kwani kumekuwa na ushindani mkubwa kiasi kwamba ingekuwa ni Tanzania tungeshuhudia vyama vikivunjika kwa tamaa ya madaraka lakini kwa Kenya hali imekuwa shwari.
Tuna mengi ya kujifunza kutoka Kenya - aina ya siasa na wanasiasa.
Hasa maana halisi ya maneno "siasa ni maendeleo". Kwetu sisi haya maneno bado ni msamiati lakini kwenu mmefanikiwa kufanya siasa zenye tija na maendeleo kwa taifa la Kenya.
Happ ulipaswa kumpa hiyo elimu
NASA Wana Hoja zipi Kupelekea kuchagulia
Naona hata wewe umetokwa na Povu
Raila Odinga mwaka 2007 aliibiwa wazi kabisa, na hata 2013 kulikuwa na figisu figisu,, Odinga ni namba nyingine,,ni mtu pekee aliyeweza kuwaunganisha watu wa makabila mbalimbali kenya kwenye uchaguzi na kuwa pamoja. Mwaka huu pia ameweza kuwaunganisha hao watano, Raila, musalia,Kalonzo, Ruto na Wetangula. Hakuna mwanasiasa mwenye upeo mkubwa kama Odinga katika eneo zima la Kusini mwa Jangwa la sahara na kuvuka mto Limpopo. Usifananishe Raila na Zepumba.Kwa maoni yangu Raila angepumzika tu amuachie Steven Kalonzo Musyoka. Amegombea sana kwa miaka mingi bila mafanikio. Mwishowe sasa anataka kuwa kama Lipumba wa Tanzania.
Lowassa amesema yuko upande wa Kenyatta. Magu yuko upande wa odingaNimemsikia Waziri mkuu mstaafu wa Tz Mh Lowasa amewaasa wale wabunge kutoka Kenya walipomtembelea Monduli kuwa "Safari hii msifanye makosa tena"
Tafsiri ni kuwa Lowasa anaukubali umoja wa NASA.
Maana yake ni kuwa Raila anakubalika kwa Magu na kwa Lowasa.
NASA WATASHINDA 63%
Mpaka Sasa Raila Odinga anapewa nafasi Kubwa ya Kupeperusha Bendera ya NASA.
Kolonzo Musyoka Ametajwa katika nafasi ya Makamu wa Rais japo wengi wanataka yeye ndiye agombee Urais.
Musalia Mudavidi anatajwa katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu kama NASA wakishinda.
KTN wana Stream Live Viongozi wa NASA wanatarajia Kufikia hapa Uhuru Pack majira ya Saa nane Kamili Mchana Huu. Ulinzi Umeimarishwa KFU wanafanya Kazi Vizuri Ikumbukwe Uhuru Pack Ipo 200M kutoka Serena Hoteli. Vijana Ni Wengi sana na Askari wapo wengi Kulinda Interference yeyote wakihakikisha Barbara inayoelekea Serena na Kulinda Usalama Wa Raia.
Watu ni Wengi sana Inanikumbusha Mafuriko ya Chama Fulani cha Siasa Pale Jangwani lakini Kikatoka Mikono Mitupu. Msaga Sumu hayupo hapa Kuna Wasanii Wengine.
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.
Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.
Makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubalina kumuunga mkono mgombea huyo mmoja.
"Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa," amesema.
Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake, kama ilivyokuwa kwenye rasimu hiyo ya katiba.
Mgombea mwenza wa Bw Odinga atakuwa makamu wa rais wa zamani Bw Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement.
Waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi.
Naibu waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto atakuwa naibu waziri mkuu atakayesimamia utawala na huduma za jamii.
Mpangilio wa Upinzani
Bw Odinga ni mwanasiasa anayesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika msitari wa mbele kuunda vyama vya miungano na wanasiasa ambao ni mahasimu wake.
- Raila Odinga - Mgombea urais
- Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
- Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
- Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
- Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu
Odinga ni nani?
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1997 ambapo Raila alishikilia nafasi ya tatu, kufuatia kuundwa kwa muungano wa chama chake (NDP) na chama cha rais wa zamani Daniel moi (KANU), aliteuliwa kama waziri wa kawi katika serikali ya muhula wa mwisho wa Moi.
Mwaka 2002, baada ya Moi kumuunga mkono uhuru Kenyatta, kama mrithi wake, Raila na maafisa wengine wa KANU ikiwemo Kalonzo Musyoka na wafuasi wengine, walipinga ungwaji mkono wa Kenyatta kugombea Urais.
Waliungana na kiongozi wa upinzani Mwai Kibaki na na kuunda muungano wa National Rainbow Coalition (Narc) ambao baadaye ulishinda uchaguzi wa mwaka 2002.
Raila aliungana na Rais Mwai Kibaki kuunda serikali ya Muungano ya NARC baada ya kumuondoa mamlakani rais mstaafu Daniel Moi.
Mwaka 2005 aliungana na Uhuru Kenyatta aliyekuwa kama kiongozi rasmi wa upinzani, ili kushinda kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba chini ya serikali ya Rais Kibaki .
Wakati Kibaki alipomfuta kazi na washirika wake, aliunda chama cha ODM ambacho kilipiga kura ya 'La' dhidi ya rasimu ya katiba mpya ambayo ilishindwa mwaka 2005.
Aliongoza kampeni mwaka 2007 na kwa shingo upande kukubali ushindi wa rais Kibaki Katika uchaguzi uliokumbwa na utata, ghasia na mauaji.
Lakini hatimaye alilazimika kujiunga na Kibaki katika serikali ya Muungano.
Disemba mwaka 2012, Raila alilazimika kupiga moyo konde na kurudiana na Kalonzo Musyoka chini ya muungano wa CORD, kwani daima husema katika siasa, hakuna maadui wa kudumu.
Raila anaamini kuwa Wakenya wanastahili kuhudumiwa vyema zaidi kuliko ahadi wanazopewa na kwamba chini ya utawala wake.
Raila anaahidi kuleta mageuzi na kuhakikisha uongozi bora.
Chanzo: BBC Swahili
Wanaridhishana kikabila yaani kila kabila na eneo lipate muwakilishiinawezekana ikawa haisumbui katiba
lazima wali consult legal officers kabla ya kutangazana hivo
sema tu inawaonesha kama they are there for vyeo kiaina
hahaaWanaridhishana kikabila yaani kila kabila na eneo lipate muwakilishi
labda watafanya mabadiliko maana nimeshangaa walivyo jipa vyeo kama wamechanganyikiwa vile hahahahaHalafu hii ya kusema kuwa Musalia Mudavadi Atakuja Waziri Mkuu ni kwa mujibu wa katiba ipi?? Au hawa NASA wakishinda watafanya marekebisho ya katiba ili kuunda cheo cha PM?? Kwa kufanya hivi hawaoni kuwa huu muungano wao ni wa kugawana vyeo badala ya kuwaletea wananchi maendeleo?? Waangalie wasije ishia kama NARC.
hahahahaha vituko tupuRaila Odinga - Mgombea urais
Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu