Nimeiweka hii thread ili kuwatahadharisha ndugu zangu Wazanzibar na athari ya maneno hayo wanyoongea. Hasa huyo Raza na Shamhuna. Wasidhani kuwa kwa kuuvunja muungano watapanda vyeo au kuwa maarufu zaidi. Wajue kuwa hofu ile ile iliyofanya Mzee Karume akaamua kuungana na Tanganyika wakati ule ipo mpaka leo. Wajue kuwa mhimili mkubwa unaofanya Zanzibar kuna amani (hata hiyo kidogo iliyopo) ni huu Muungano. Kinyume chake watachinjana kama kuku. Wanalijua hilo ila ni kiburi chao tu.
 
Raza ni mtu hatari sana kwa swababu akili yake haijafikia upeo wa kujua uzito wa kitu anachokijadili. Anatakiwa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo, la sivyo, harakati za Wazanzibari zitaonekana zina lengo baya
 

Naamini si busara kuufananisha Muungano wetu na ndowa kwani tutafika pahala tuanze kuuliza nani mume katika muungano huu.
Aidha pia si jambo sahihi kuwaona Wazanzibari wakilalamika kuwa mfumo wa muungano hauwatendei haki na kuwapaka ubaya. Naomba nikujuulishe kuwa Wazanzibari hawataki kuvunja Muungano bali wanataka haki ya kujiamulia mambo yao kwani hilo lilikwishawekwa wazi na hiyo katiba inayoelezwa,
Hata wakati wa hao wazee unaosema walitufungisha ndowa na hadi leo Zanzibar imeachiwa kujitegemea kimaisha lakini tatizo nni kuwa wanawekewa vizingiti katika harakati za kujitafutia riziki za kujiendeleza na wakati huo huo hawapewi mahitaji ya kujikimu.
Kama Zanzibar si nchi maana kubwa ni kuwa haiwezi kujitegemea na kama ni sehemu ya Muungano inahitaji gao sawa sawa na sehemu nyengine ya Muungano. Huu usehemu wa Muungano ni upi na nafikiri hadi sasa hata hao wataalamu wa Katiba na Viongozi hawajatwambia. Jee sehemu hiyo ni sawa sawa na sehemu kama mkoa mfano wa Mwanza, au wilaya kama Kinondoni au tarafa kama Mbagala? Zanzibar na ipewe hadhi ya mojawapo ya sehemu hizo yaani mkoa, wilaya au Tarafa nafikiri kinachofuata ni kumuona Rais wa Tanzania na Bunge la Tanzania wakifanya kama wanavyoifanyia Mwanza (kujengwe mabarabara na Kikwete aende kule na fuko la Pesa), Ifanyiwe kama Kinondoni (TAMISEMI na ionekane wilaya ya Zanzibar) au na ifanywe kama Mbagala (konoike afike kule kujenga barabara)
Hayo yote hayafanywi na Serikali ya Muungano kule Zanzibar na badala yake Karume (aliyefananishwa na Madega) na SMZ (Yanga) ndio wanaofanya hayo yaliyopaswa kufanywa na hiyo Serikali ya Nchi inayotambulika (Tanzania). Kwa mwenye akili na fikra angejiuliza hii maana yake nini? Kwa kuchukua mfano wa hiyo ndowa tuliyoambiwa tuithamini, hii ni sawa sawa na kuowa mke ukamuweka ndani asiende hata shamba huku ukishindwa kumuhudumia yeye na watoto wake na huku unawapigia makelele wanaume wenzio wasisogee kwani wew una cheti cha ndoa kutoka kwa shekhe au kanisani.
Watanganyika hawana sababu ya kuulalamikia Muungano kwani kwa mfano wa ndowa wao ni nyumba ndogo na Rais wetu wote na Bunge letu tukufu wamekazania kuihudumia nyuma ndogo huku Zanzibar ikiachwa ijtegemee yenyewe.
 

Nafikiri mtu wa hatari pengine ungekuwa wewe kwani Mwiba anatowa maoni yake na wala hachochei kama unavyodai. Kama uchochezi basi tusingekuwa tukijadili ufisadi na uozo mwengine. Wewe una haki yako ya kutowa mawazo yako na hivyo hivyo Mwiba na kinachojionesha ni kuwa kuna tofauti za pande mbili . Ufumbuzi si kupakana uchochezi wala kutishana bali ni kukaa na kujadili lipi la kufanywa ili kila upande uridhike na hilo likishindikana itakuwa Muungano hauna maana na MIND YOU Zanzibar itasurvive na itakushangaza.
 

Nashindwa kufahamu Quote yako inaiacha na kurukia point nyengine. Hebu Challenge asili ya Muungano Wa Tanzania na hiyo mifano unayoieleza. Pia hebu tupe ushauri wako wa nini Zanzibar ifanye ili kuwapatia Wananchi wake Huduma. Na jee uko tayari kuitaka hiyo Soverignity iihudumie Zanzibar kwa kila hali kwa vile Zanzibar si nchi?
 
Raza ni mtu hatari sana kwa swababu akili yake haijafikia upeo wa kujua uzito wa kitu anachokijadili. Anatakiwa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo, la sivyo, harakati za Wazanzibari zitaonekana zina lengo baya

Ndugu zangu watanzania na wazanzibari wenzangu naomba tuyapuuzie maneno ya Raza kwani hayaoneshi kujenga zaidi ya kubomoa.

Wanzazibari wa kawaida kabisa wamekuwa na mahusiano mema na ndugu zao wa bara kwa muda mrefu sana hata kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ni vema basi tukaona maslahi ya jamii zetu yanalindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo na wala si vinginevyo. Tutayarishe ardhi hii ( Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) iwe ni mahali pazuri kwa ajili ya watoto wetu. Tamaa zetu tuziweke nyuma maslahi ya taifa tuyape kipaumbele.
Leo hii sisi vijana wa Bara na Visiwani tunaishi kama ndugu moja, tumekwenda shule pamoja, tunafanya kazi pamoja na isitoshe hata familia pia tumezijenga bila ya kuzingatia maeneo tunayotoka. Sasa kwa Raza ambaye fikra zake ni kubomoa zaidi basi hatutakii mema.
Ni vema matatizo ambayo yanajitokeza kama haya tuwaachie wataalam wayazungumze na wayamalize lakini hakuna haja ya kuleta ushabiki usio kuwa na maana.
 

Kamsome vizuri mwenzio uelewe anachozungumzia. Sina muda wa kuweka mabandiko kutoka maandishi yake lakini amezungumzia kuhamishia mapambano bara, kuwa na maandamano madogo madogo na mambo mengine. Anachodai ni kiti Umoja wa Mataifa, kiti ambacho kinakaliwa na nchi huru yenye full sovereignty( wachina wameitilia ngumu taiwan kwa sababu hiyo hiyo). Halafu mnajidai hamtaki kuvunja Muungano? Leo Raza anawabeza watanganyika kwa kuwang'ang'ania bila kukaripiwa! Hivi mnadhani ni watanganyika wote wanaoufurahia Muungano? Wengi wao wangependa tutengane. Bila shaka mta'survive'. Kama mlivyo'survive' mara baada ya mapinduzi. Mtakaa waunguja na wapemba baada ya mtawala mtanganyika kuondoka na kusahau tofauti zenu! Tunawatakia kila la heri.

BTW, mfahamishe mwenzio kuwa Zanzibar haijawahi kumg'oa muingereza. On the contrary, katika kitabu cha Guiness book of records, vita fupi kuliko zote duniani ilitokea Zanzibar, ambapo mara baada ya merikebu za uingereza kupiga mzinga mmoja Sultan alisalimu amri. Mwaka 1963 nchi alikabidhiwa Sultan na mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa dhidi yake na siyo muingereza. Tusidanganyane!
 

Wazanzibari ni vema wakumbuke kuwa Zanzibar haitakuwepo bila Muungano bali itakuwapo Jamhuri ya Pemba na Serikali ya Mapinduzi ya Unguja. Waangalie yanayotokea sasa katika nchi zilizounda USSR kwa kuangalia mambo yanayoendelea huko Jamhuri ya Georgia ambapo mkoa mmojawapo unataka kujitenga.

Huko Zanzibar kuna vikongwe wanawaburuza wenzao- wote wanaochangia za kujitenga ni wale waliozaliwa kabla ya Mapindizi ya 1963 na hapo ndiyo tujiulize kwa nini wao ndo wanaopiga kelele za kutaka kujitenga ni si waliozaliwa baada ya Muungano? Vijana hawaijui nchi ya Zanzibar, wanaijua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; vijana wa Zanzibar nao waseme ikiwa wanaunga mkono Vikongwe kura ya Maoni ipigwe.

Iwapo watataka kujitenga waachwe tu ila tusiruhusu Wakimbizi wataoikimbia Zanzibar baada ya Muungano kuvunjika; mimi naona Tanganyinka hatuna cha kupoteza kabisa.
 

Ingawa si kijana, sina cha kuongeza. Umesema yote yaliyo muhimu.
 
Pull out of Parliament, Raza tells Isles MPs

By Salma Said, Zanzibar
THE CITIZEN

A prominent Isles businessman and former adviser to the Zanzibar president on sports matters, Mr Mohammed Raza, has advised all members of Parliament representing Zanzibar in the National Assembly to return home since they do not represent a country.

Speaking in Zanzibar yesterday Mr Raza also wanted all civil servants in Union institutions representing Zanzibar on the Mainland to return home since the Isles are not a country.

"All members of Parliament from Zanzibar and workers from the Isles in the Union Government should return home since they do not represent any country, until it is established otherwise by the relevant authorities," said Mr Raza, a CCM cadre from the Isles.

He said that those who claimed that describing Zanzibar as a country was tantamount to committing treason were suggesting that all Zanzibaris have committed such an offense since all of them were defending that political status.

'We are told that Zanzibar is not a country, so does that mean that Zanzibaris were sold to Mainlanders (Tanganyikans) in 1964�during unification?' inquired Mr Raza.

He asserted that threats would not stop Zanzibaris from defending their country's political status, saying Zanzibaris had suffered much from the union, which he claimed was signed by two people over 44 years ago.

'All Zanzibaris,including myself, have committed a treasonous offence and we shall continue committing that offence 'It has also been stated in the House of Representatives that Zanzibar is a country and nothing will change that fact,� said the Isles political troubleshooter.

He said any meetings that had endorsed that Zanzibar was not a country were not legal since they did not have the mandate of Zanzibaris.

"Those meetings did not get a two thirds majority of Zanzibaris, yet our constitution stipulates that this is a requirement to change the status of the country," he further stated.

He said the constitution was breached while approving some changes in the document, which removed the Zanzibar president from becoming the vice president of the Union. Those changes have not yet been agreed upon by Zanzibaris as the constitution requires, he affirmed.
 
...Raza naye ana historia ya kukurupuka, huenda bado anaweweseka na 'aura' aliyojiwekea sababu ya uswahiba wake na 'Komandoo' Salmin, enzi za utawala wake.
 
Ibrah.Fundi Mchundo,Congo,WildCard,

..SIASA ndiyo zinawachanganya na kuwasukuma wananchi mbalimbali kutoa kauli za ajabu-ajabu.

..natokea Tanzania Bara, na kwa kweli sioni faida wala hasara za waziwazi za Muungano huu.

..kama imeshindikana basi uvunjwe tu. ila katika kufanya hivyo, naomba uungwana utumike ktk kuhakikisha kwamba wale Wazanzibari[wafanya biashara, waalimu,mafundi,wauguzi,...] walioko Bara ambao watapenda kuhamia huku wasibugudhiwe kwa namna yoyote ile.
 

Nyinyi akina Ngekewa na Mwiba hamna mpya. Mko extremist sana. zipo kasoro katika Muungano ambazo inabidi zirekebishwe haraka ili Zanzibar iwe na fair deal. Lakini hizo hadithi zenu ni potofu na hazifai kufikia masikio
ya wenetu. Yarabi Mola awalaani nyinyi.
 
Ninajitahidi Kutafakari Yote Haya Na Sasa Nimsomavyo Raza Inanijia Hisia Ya Hasira Ya Wazanzibar Wenye Mahusiano Na Dola Tangulizi Huko Na Jamhurini Sasa Wanajiuliza Kwanini Walishiriki Kumtenga Ndg. Yao Salim Ktk Uchaguzi Wa Jamhuri 2005, Huenda Kuna Wanaojutia Kwa Dhati Kwa Maana Walijikuta Wameingizwa Mkumboni Na Sasa Majuto Ni Mjukuu, Kuna Wengine Wanaonekana Kusukumwa Na Ubinafsi Wao Lakini Wanajifanya Wazalendo Na Pia Wapo Wale Ambao Tangu Ujio Wa Dkt Karume 2000 Na Yaliyojiri 2005 Wamekuwa Yao Macho Tu Ila Rohoni Wana Sononeka Sana.

Wakuu Nikiwaangalia Hawa Jamaa Zetu Ni Kama Wanamjengea Mazingira Magumu Jk Na Ccm Yetu Ktk Kupata Clean Candidate 2010 Kwa Kutishia Nyau Kwa Mtu Mzima Jk.

Saa Zaenda Na Dakika Zayoyoma Kwa Kasi Kuelekea 2010, Siasa Nazo Zinaashiria Hilo Kuwa Idadi Ya Wapenda Mamlaka Inaongezeka Na Kwa Kasi Iliyopo Sidhani Kama Tutakuwa Na Kifua Cha Kuhimili Ubovu Wa Maneno Yajayo Aili Muradi Wapenda Madaraka Wajiimarishe Na Kuwapora Wenzi Wao Nguvu Za Dola.

Wazanzibar Kama Watakumbuka Wasia Wa Mwisho Mwisho Wa Marhum Ahmed Hassan Diria, Hawatapata Taabu Sana Kuwatambua Wabaya Wao Na Aina Ya Siasa Wanayoipasa Kuifuata.

Binafsi Mimi Ni Mwana Ccm Ambaye Ninaamini Sana Muungano Wa Serikali Moja Ambao Utazalisha Mikoa Yenye Nguvu Za Kisiasa Na Mwenendo Wa Kichumi.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Jk Na Ccm Hawatakubali Kuwa Chanzo Cha Kuvunja Muungano Ila Misuguano Hii Ni Hamu Tu Mamlaka
 
Pakacha,Ngekewa,Fundi Mchundo,Mwiba,

..mimi naomba kuelekezwa hizo kasoro au kero za Muungano ni zipi.

..naomba pia mtueleze njia ya kuzitatua.

..wako wanao-suggest tuunde tuwe na serikali tatu.

..sidhani kama mazingira ya serikali 3 yataipa madaraka na nguvu zaidi SMZ. zaidi nafikiri madaraka ya serikali ya TGK yatakuwa kama ya serikali ya SMZ sasa hivi.

..pia nadhani serikali 3 zitaongeza gharama na matumizi ya serikali. mzigo huo itabidi ubebwe na wananchi wa Tanganyika kwasababu wao ndiyo wanaowakilisha majority ya population ya Muungano.

..kitendawili kikubwa ktk Muungano huu nadhani ni udogo wa Zanzibar, kieneo, idadi ya watu, na kiuchumu. katika mazingira kama hayo kila upande hauishi kulalamika kwamba haupati a fair deal.
 
hicho unachokiongelea ambacho nimeki highlight kimetokezea baada ya mfumo huu wa muungano kuilazimisha zanzibar lazima iwe dependent kwa tanganyika in other way unaweza ukasema system ya muungano inamfanya tanganyika awe mtawala wa kiuchumi wa zanzibar. same thing imetokezea kwa kila nchi iliotawaliwa aidha kisiasa ,kimabavu,kiuchumi au hata kiutamaduni.mfano mzuri ni wa irish wengi walioivamia uingereza na kuwekeza wakati wakitawaliwa na muingereza na walipokubali kujipapatua nadhani unaiona ireland sasa inavyojiimarisha kiuchumi. hivyo kwa hilo usiwalaumu wazanzibari ulaumu mfumo tegemezi wa muungano wetu. itakumbukwa pia kwamba zanzibar ilipokuwa ikizitawala sehemu kadhaa za afrika mashariki basi makabila mengi ya kiafrika na ya kigeni yaliwekeza ndani ya zanzibar na hii haikuwa sababu ya kuporomoka kwao wakati zanzibar walipoporomoka.
 
kwangu mimi hii ni siasa ya propaganda, karume hakuamua kuungana kwa hilo unalolielezea , jaribu kuisoma tena historia ya zanzibar,. wazanzibari ni watu wa amani sana kama hawajatiwa vijiti vya maskio. ni mzanzibari ambae nimeishi zanzibar na kuiona hali halisi ya zanzibar na sio kuisoma magazetini.
 
udugu wetu utazidi mapenzi na nguvu kama muungano huu utatenda haki sawa kwa nchi hizi 2 zilizoungana.
 
under_age,

..tufafanulie kuhusu hii hoja yako ya Tanganyika kuitawala Zanzibar kiuchumi.

..kuna Wazanzibari wengi tu wametajirika/wanatajirika huku Tanganyika bila kubugudhiwa.

..Wazanzibari hao wanaweza kurudi kwao na kuwekeza kiuchumi.

..vilevile Zanzibar ina wizara yake ya fedha, mamlaka yake ya mapato na kodi, wizara ya utalii, viwanda, etc etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…