No, tatizo la Zenji sio Karume. Tatizo la Zenji ni Maalim Seif Shariff Hamad. Itakumbukwa kuwa kipindi Jumbe na Mwl (in the mid-60s) walipokuwa na tofauti za waziwazi kuhusu hili suala zima la muungano (Jumbe akitaka kuwepo serikali 3, na Mchonga aking'ang'ania zibaki 2), the same guy, Seif, alikuwa wa kwanza kumtuhumu/sell-out Jumbe-kuwa anataka kuvunja muungano. This Shariff guy is a sole looser! Mroho wa madaraka, pia! Leo anataka kujitenga na bara, kesho atataka kujitenga na unguja.
Sasa unataka tukuone umezungumza ukweli ,tatizo la Zanzibar kama ulivyosema sio Karume na vilevile sio Seif ,hayo ya Jumbe yanaingia katika politics au political game na propaganda zinaweza kuwa zina ukweli au zimejaa majungu ,wanasiasa wanafahamiana si inasemwa siasa ni mchezo mchafu au ni rafu tupu ,sasa mchezo huu umeingia kikamilifu kwenye Muungano na ndio unachezwa. yaani mechi ipo uwanjani.
Umemtaja Nyerere ,ngoja nami nikueleze alivyosema Nyerere Muasisi wa Tanganyika,alisema siku moja mashoka yalikwenda msituni kutaka kuiingilia miti na kuikata kufika huko msituni miti ilichachamaa na haikuweza kukatwa ,Mashoka wakakutana wakapata shauri kuwa ili wafanikiwe kuikata miti ni lazima wapate mipini itokanayo na miti ambayo inapatikana hukohuko msituni,hivyo wakaingia kazini na kupata mipini mizuri sana,na kuanza kuingia msituni kuikata miti.
CCM wamekuwa wakiitawala Zanzibar kutokana na mipini hiyo ambayo ni Wazanzibari,Sisemi Tanganyika wameikalia Zanzibar kwani hivi sasa kuna vyama vingi matatizo haya yalianza tokea mfumo wa Chama kimoja ambacho kinaendelea kuikalia Tanganyika na Zanzibar kwa mabavu,sijui kwanza kama unakubalianza na hilo,Upinzani uliokuwepo Tanzania hauwezi kufanikiwa kama hawakuipapatua CCM katika umiliki wa nchi mbili hizi,ni lazima kwa hali yeyote ile CCM ipapatuliwe katika kuzikalia nchi mbili hizi kimabavu,na utajua kama nchi hizi zinakaliwa kimabavu na kikundi kikubwa kutokana na aina ya matatizo yanayo au yaliyomo ndani ya Tanzania ,ndani ya CCM kwa muda huu tulionao kuna matatizo kuna makundi kuna mitandao ukiangalia yote hayo na kuyapima utaona TANZANIA inaongozwa na makundi ya CCM wakati kila kundi likitaka kumkomoa mwenziwe ,usitegemee kuondokana na hali ya maisha duni na kupelekwa kwenye maisha bora,hiyo ni ndoto,Jakaya aliahidi kupambana na matatizo lakini sasa ni miaka mitatu hakuna mafanikio ambayo ameyapata na kila siku tunasikia wanakurupushana na vidole machoni , wanaogopana wanatishana na wanauwana, watu hawa CCM hawajali maisha ya Mtanganyika wala Mzanzibari ,hivyo kuendelea na Muungano au kuulinda Muungano ni kudanganyana na ni kuwapa nafasi mafisadi kuzidi kuzinyonya nchi mbili hizi kwa manufaa yao binafsi na kwa manufaa ya makundi yao.
Ikiwa maanadamano ya Zanzibar yatafanyika na kufanikiwa basi sehemu ya pili ya Maandamano itabidi yafanyike upande wa Tanganyika na ili kuwahi ni lazima vyama vya upinzani viandae maandamano makubwa kwa Tanganyika yote mara tu baada ya kumalizika yale ya Zanzibar kuidai Tanganyika ijivue ndani ya koti la Muungano ,na hata Mataifa ya nje hayatashangaa yataona ni ukweli ambao ulikuwa umejificha au umefichwa ,Tanganyika haikufa ipo ila serikali yake imetekwa na kundi ndani ya makundi ya CCM na kuifanya ionekane ya Muungano.
Ni lazima serikali hii ya Tanganyika ipapatuliwe na kuvuliwa ndani ya serikali ya Muungano na huo ndio utakuwa mwisho wa ukiritimba wa CCM dhidi ya nchi mbili hizi.
Nimekuwa nikijaribu kuonyesha kuwa Muungano hauna tatizo ila matatizo yapo katika uendeshaji na waendeshaji ambao ni CCM,hawa hawana wanalolifanya kwa faida ya nchi mbili hizi,hawa ni makundi yanaozimaliza nchi mbili hizi kwa faida yao binafsi na makundi yao,makundi haya yanapatikana ndani ya CCM ,kuipapatua Tanganyika ni kuyaanika makundi haya na kuyaweka pakavu ,sheria zitakuwa msumeno ,sheria zitafuatwa ,amri zitafuatwa na ukweli utakuwa sio siri tena, sasa hivi hakuna cha makubaliano ya mkataba,wala hati ya mkataba wala nani na nani walisaini mambo ni mbele kwa mbele lazima ziwepo serikali tatu.
Na sasa tupo kwenye wakati mzuri kwani vyama vyetu vya siasa vinaruhusika kufanya siasa katika Nchi zote mbili Tanganyika na Zanzibar ,Zanzibar ambayo inaendesha Uchaguzi wake tokea ipate uhuru haina kazi kubwa kukaa sawa ila Tanganyika kidogo itakuwa na kazi kwani haina Raisi wala waziri hawa mafisadi waliojikita ndani ya serikali ya Muungano wote watapoteza ulaji na kurudi katika Chama chao ambacho kitawapa wakati mgumu kutokana na makundi yaliomo ,makundi ambayo itabidi yasambaratike.
Muungano hauvunjwi hilo sina wasi wasi nalo ,ila Tanganyika ndio itakayorudishwa kama Nchi,kwani karibu vyama vyote vya upinzani vinakubaliana na serikali Tatu na vimeona hilo ni jambo muhimu,sasa ukiritimba wa Chama kimoja tu kutaka serikali mbili au moja ni jambo la kulitilia shaka.
CCM kama utawasikia siku hizi wamekazania anaetaka kuvunja Muungano ni haini ,anaesema Zanzibar ni Nchi nae pia ni haini ,naamini anaesema Tanganyika nayo ni Nchi huyo pia atachanganywa na kutiwa ndani ya kapu la uhaini ,hawa mafisadi wanatafuta pa kushika (
Samahanini CCM mliokuwa si mafisadi ,tunamsemo wa kiswahili usemao akioza samaki mmoja basi wote watakuwa wameoza) ,CCM wanatafuta pa kushika ili kuendelea kuzikalia nchi mbili hizi na kuzitapeli.
Ni lazima vyama vya upinzani kushirikiana ili kuidaia Tanganyika hadhi yake kama nchi yenye serikali msiwaachie WaZanzibari peke yao kwa kuogopa kuitwa wahaini.
Tanganyika na Zanzibar zimetekwa na CCM ,hivyo vyama vilivyobakia ambavyo vina imani na kuwepo kwa serikali tatu ni lazima visimame kidete kupambana na CCM naamini kabisa vita hii tutashinda ,na hapo ndipo kutapatikana Katiba mpya itakuwepo kwa upande wa Tanganyika na vilevile kwa upande wa Zanzibar na vilevile kwa upande wa Muungano.
Lakini hivi vitisho vya CCM kuwaita watu wahaini wanapoulizia Nchi yao visikubalike ,na kama utachunguza kwa kina wanaolipinga suala hili na kulivalia njuga na kuwaita watu wahaini ni maneno kutoka Chama kimoja tu cha CCM , na Zanzibar wameshaanza kupigwa ngwara kwani wale woga waliomo ndani ya CCM huko Zanzibar sasa woga umeshawaondoka na kuona ukweli wa kuwa wanatawaliwa kimakundi na mafisadi waliojikita ndani ya CCM.
Mtanganyika unasubiri nini ungana na WaZanzibari kuipapatua Tanganyika ili tushinde vita dhidi ya mafisadi.