Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mzee Mkandara,
Mimi naamini hakuna kitu kitachotutengenisha kati yenu na Zanzibar kijamii, sisi ni wamoja na tunashirikiana vizuri sana kijamii. Muungano wa kiuchumi na kisiasa unaturudisha nyuma sana kimaendeleo. Ni kitu ambacho hakiingii akilini kwa nini Zanzibar iwe na serikali yake ndani yamuungano wakati Dar es Salaam ambayo wakati wake ni mara mbili ya wakazi wa visiwani na bado wanataka wachukua 40% for what. Kama hawataki Zanzibar uwe mkoa basi muungano wa kisisa na uchumi ufe, ni gharama kubwa kwa serikali ya Muungano.

My take: Mfumo wa kiutawala zanziba ubadirishwe ili tupate mikoa miwili yaani mkoa wa kwanza uwe unguja na wa pili uwe pemba. Vinginevo tuvunje muungano!
 
My take: Mfumo wa kiutawala zanziba ubadirishwe ili tupate mikoa miwili yaani mkoa wa kwanza uwe unguja na wa pili uwe pemba. Vinginevo tuvunje muungano!
Unaona mnavyokwenda kombo na kujichanganya, nani alisema Muungano Uvunjwe ,tatizo mnaogopa kusawazisha mambo ili yaendane na MKATABA wa Muungano,mnalazimisha mambo ambayo hayamo na yameingizwa kinguvunguvu tu.Mkataba wa Muungano ni Sheria mama ambayo haitaki kuchezewa hata kidogo,na kubadilishwa badilishwa mambo ambayo hayakuafikiwa wala kujadiliwa na pande zinazohusika na pia kama mlikuwa mnakubaliana ,tuchukulie hivyo hivyo kinyemela basi mlikuwa muwakilishe mabadiliko hayo kwenye Umoja wa Mataifa ambako ndiko kwenye kukubaliwa,tunaambiwa kwamba baada ya makubaliano ambayo ni hayo yajulikanayo kama Mkataba wa Muungano kulipigwa kura huko umoja wa Mataifa kama kuna pingamizi lakini bahati ilikuwa nzuri hakuna pingamizi ila kuna nchi moja haikupiga kura au tunaweza kusema kura moja iliharibika.
Sasa haya yote mliyoyachomekea hayajulikani ndani ya Mkataba wa awali na ndio tatizo lilipo jikita.
Na kwa asili hiyo hata atakaezaliwa baada ya miaka 100 basi atakuwa na haki ya kuchambua na kuhakiki na kuzusha madai ya Muungano huu.kusema Wazanzibari hawautaki Muungano kwa kweli sio sahihi kabisa ,nchi mbili zimeungana sawasawa ,mambo ya kusema sisi wengi tuchukue kikubwa hilo halimo,tumeungana with equal rights no one is above the other side,sasa inapotokea mmoja kutaka au kuchota ziada sio kosa ikiwa tu makubaliano yanafuatwa na kwa mchujo huo hayo yatakuwa maridhiano na yanaweza kubadilika kutokana na hali ya kila msimu,nimesema ni maridhiano lakini linaloonekana leo sio maridhiano bali ni magube au mabavu au wizi.
Nani atakubali upumbavu huo ? Tanganyika lazima irudi kama mnaoona aibu ni hiari yenu lakini Zanzibar inahitaji haki na rights zake zote kuheshimiwa kama Nchi husika katika muungano.
Kinachofanywa na Serikali ya Tanganyika ambayo imejivisha koti la Muungano ni ucowboy mnapanga kuiba pamoja mkishafanikiwa unamuua mwenzio.
Tokea Muungano huu ulipoundwa haijawahi kutokea Mzanzibari kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hapa ndipo pia inapoongezeka ile dhana ya kuwepo Tanganyika ndani ya koti la Muungano na sasa ndio kabisa WaZanzibari wameshapoteza hata ile nafasi ya Raisi wao awe ni Makamo wa Kwanza wa Raisi ,yaani ukiangalia japo haitaleta maana sana lakini ile status ya umoja itapatikana,eti wameondoa kwa kusema kama Chama kimoja kitashinda nafasi ya Jamhuri na Upinzani utashinda Zanzibar itakuwaje ? Mnasahau kuwa unapokuwa Raisi unapoteza nafasi ya kushughulikia Chama na mambo yako yanatakiwa yawe ya Kitaifa japo ni mwenyekiti wa Chama fulani,unatakiwa ufiche sura ya Chama na kuvaa sura ya Utaifa kwa wananchi wote ,ila bado CCM wanaona wao ndio wenye hati miliki ya Nchi mbili hizi ,Napiga mbiu ya mgambo Tanganyika lazima irudi.
 
Unaona mnavyokwenda kombo na kujichanganya, nani alisema Muungano Uvunjwe ,tatizo mnaogopa kusawazisha mambo ili yaendane na MKATABA wa Muungano,mnalazimisha mambo ambayo hayamo na yameingizwa kinguvunguvu tu.Mkataba wa Muungano ni Sheria mama ambayo haitaki kuchezewa hata kidogo,na kubadilishwa badilishwa mambo ambayo hayakuafikiwa wala kujadiliwa na pande zinazohusika...

Bila kuingia sana katika maswala ya contract law, unavyojua wewe, Mkataba baina ya Juma na Roza unaweza kubadilishwa na Juma na Roza?
 
Bila kuingia sana katika maswala ya contract law, unavyojua wewe, Mkataba baina ya Juma na Roza unaweza kubadilishwa na Juma na Roza?
Unaweza kubadilishwa na Juma na Roza ,any question ?
 
Unaweza kubadilishwa na Juma na Roza ,any question ?

Ahsante.

Kwa hiyo, bila ya kwenda kwenye undani wa ulivyobadilishwa au nani aliubadilisha, unakubali kwamba Mkataba wa Muungano unaweza kubalishwa.

Sawa ?
 
Mwiba,

Kwa hiyo, bila ya kwenda kwenye undani wa ulivyobadilishwa au nani aliubadilisha, unakubali kwamba Mkataba wa Muungano unaweza kubalishwa.
Sawa ?
Sio sawa ,umekusudia mfano wa Roza na Juma ,naomba kigezo na ukifafanue ili nifunge kazi ?
 
Sio sawa ,umekusudia mfano wa Roza na Juma ,naomba kigezo na ukifafanue ili nifunge kazi ?

Ahsante kunipa nafasi ya kufafanua.

Juma na Roza wamekubaliana kuchanganya umiliki na maamuzi ya utawala wa ng'ombe zao. Sasa wanataka kuubadilisha mkataba wa awali, waongeze na mbuzi pia.

Jibu lako la awali linabadilika au linabaki pale pale kwamba wanaweza kuubalisha Mkataba ?
 
Niko pale pale Juma na Roza wanaweza kubadilisha .
 
Kwa nini Mkataba wa Muungano hauwezi kubadilishwa, lakini wa Juma na Roza unaweza ?
 
Kwa nini Mkataba wa Muungano hauwezi kubadilishwa, lakini wa Juma na Roza unaweza ?
Mkataba wa Juma na Roza sijauona na isitoshe kuna tofauti kati ya makubaliano na Mkataba na hapo natumai ndipo hupatikana Hati ya Mkataba ambayo inajulikana kama Treaty na kama itatosha Makubaliano ya Tanganyika na Zanzibar yalizaa Mkataba wa Tanganyika na Zanzibar na kusajiliwa katika Umoja wa Mataifa ambao ulitoa Hati ya Makubaliano na kwa kukuongezea ulipigiwa kura na kupitishwa, nikirudi kwa Roza na Juma sina uhakika kama katika makubaliano yao walipata Hati inayothibitisha Makubaliano hayo na pia sijui kama katika makubaliano yao kuliwa na masharti wakati Hati ya Muungano ina masharti.Na ndipo inapopatikana tofauti ya kuweza au kutoweza kubadilishwa.
Hivyo hapa hakuna unyemela wa kuongeza bata wala kuku,chochote kitakachofanyika ni lazima itazamwe Hati inasemaje ,kwa maana hiyo chochote kitakachofanywa ni lazima kikubaliane na Hati ya Muungano inasemaje ? Kama unataka kuongeza kuku au Mbuzi Je hati inakuruhusu moja kwa moja kufanya hivyo ? Na ikiwa mtafanya wakati Hati hairuhusu mtakuwa mnatenda kosa ,nini kifanywe kwanza ni kuitafuta Hati ya Muungano na kuisoma vizuri ili kuepuka migongano baadae , ili mujitosheleze ni lazima Juma na Roza wabadilishe Hati kwanza ili iruhusu makubaliano mengine yanayotaka kuingizwa.
Na kutokana na hati iliyohifadhiwa Umoja wa Mataifa juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (sio huu wa Juma na Roza) haya yote ya kuongeza mbuzi na kuku yatakuwa hayana mshiko kwa sababu hayatambuliki na hayana nafasi kwenye Hati ya Muungano maana yakichambuliwa na kutafutiwa nafasi ndani ya Hati ya Muungano basi yote yataonekana ni mizengwe iliyo wazi ni utapeli.
Hivyo hata mafisadi wanapojichukulia migodi na wakasema ni yao wanaweza japo inaonekana ni mali ya Tanzania lakini ndani ya makubaliano na Hati ya Muungano hayo mambo hayamo.Sasa mkiwashitaki na kusema wameiba mali ya au uchumi wa Tanzania mtakwenda mchomo kwani wamechukua mali ya Tanganyika tu.
Si umesikia UVVCCM sijui ka ndivyo wanavyokabana koo wengine wanasema makubaliano tayari ila Hati ndio haijatiwa saini sijui umefahamu matatizo yaliopo ? Hapo kuna feza ishatafunwa na wajenxi washaanza kazi ila mkuu hajaweka saini.
Makubaliano - Mkataba - Hati.
Hivyo ikiwa matatizo yatatokea cha kwanza kitakachotazamwa ni Hati halafu Mkataba halafu makubaliano ndio ukaona kunapoandikwa mwisho kunaandikwa any alteration kutavuruga kila kitu.
WAZANZIBARI WANASEMA ONYESHENI HATI YA MUUNGANO tuone kama hamjavuruga ? Hapo ndio kindende mara utaambiwa na kuitwa Mhaini na makada wa mafisadi.
 
Polisi waruhusu maandamano ya kudai Zanzibar ni nchi

karume.jpg

Rais Amani Karume wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Na Salma Said, Zanzibar

JESHI la Polisi Zanzibar, limetoa kibali cha kufanyika maandamano ya kutetea Zanzibar kuwa ni nchi yaliyoandaliwa na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), visiwani hapa.
Taarifa ya polisi iliyotolewa visiwani hapa jana ilisema kwamba, maandamano hayo yameruhusiwa kufanyika keshokutwa na yataanza saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Kombawapya hadi Kibanda Maiti Uwanja wa Demokrasia.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa masharti kwa wahusika, ikiwa ni pamoja na wahusika kutochukua silaha ya aina yoyote wala kubeba mabango katika maandamano hayo.
Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kumbukumbu No. W/MJN/SO.7/2A/106, pia Polisi imewataka waandaaji kuhakikisha wanawadhibiti wanachama wao wasiharibu mali za raia na wananchi katika maeneo ambayo yatapitia.
"Kusiwepo na lugha ya matusi kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa kwa nia ya kuleta jazba, ugomvi na kupelekea kuhatarisha amani na utulivu," inaeleza barua hiyo ambayo Mwananchi imeiona ikiwa imeandikwa Agosti 7, mwaka huu na kusainiwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam.
Aidha, viongozi wa NRA wametakiwa kuhakikisha vyombo vya habari vinaruhusiwa katika maandamano hayo vikiendelea kufanya kazi zao bila ya kuwepo vikwazo vyovyote.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa NRA Zanzibar, Suleiman Gaddafi, alisema matayarisho ya maandamano hayo yamekwishakamilika ikiwemo kuwaalika viongozi wa vyama vingine ili kuongeza nguvu ya mahudhurio.
Alisema takriban vyama vyote vilivyopata usajili wa kudumu nchini vimekaribishwa katika maandamano hayo isipokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamesema hao hawatashiriki kwa vile wanaunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba suala hilo waachiwe wanasheria wa pande mbili kulishughulikia.
"Naibu Katibu Mkuu wa CCM nilipokutana naye ili kumkaribisha katika maandamano hayo amenijibu chama chake hakiko tayari kwa vile kinaamini suala hilo linashughulikiwa kama ilivyoagizwa na serikali," alisema Gaddafi. Alisema pamoja na msharti magumu yaliyowekwa na polisi, wanashukuru kwa kuruhusiwa kufanya maandamano hayo kwa vile yatatoa fursa kwa wananchi wa Zanzibar kuonyesha ni jinsi gani walivyokerwa na kauli ya Pinda kwamba Zanzibar sio nchi. Gaddafi alisema, maandamano hayo si ya itikadi ya chama na kwamba wananchi wote wa Zanzibar wanaruhusiwa kushiriki bila kujali tofauti zao za kisiasa kwa vile suala hilo linahusu nchi na sio chama.Awali, maandamano kama hayo yalikuwa yafanyike Zanzibar, lakini yalishindikana baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kugoma kuyapokea.
Alikataa kupokea maandamano hayo yaliyokuwa yamalizikie katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa maelezo kwamba, katika kipindi hicho Viwanja vya Baraza vilihitaji mazingira ya utulivu kutokana na wajumbe kuendelea kujadili bajeti ya serikali, kwa hiyo haikuwa jambo la busara kuruhusu mikutano ya watu katika viwanja hivyo.
Maandamano hayo yalikuwa yameandaliwa na Wazanzibari wanne kwa niaba ya wenzao 10,000 wanaotetea kuwa Zanzibar ni nchi licha ya kufikiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Tangu Pinda atoe kauli kwamba Zanzibar si nchi akiwa bungeni akinukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumekuwa na mjadala mkali kutoka kwa watu mbalimbali, baadhi wakimuunga mkono ilhali wengine wakimpinga.
Pinda hadi sasa amekwishapingwa na viongozi waandamizi ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwamo Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Juma Shamhuna, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Iddi Pandu Hassan na wawakilishi kadhaa.
 
Mkataba wa Juma na Roza sijauona na isitoshe kuna tofauti kati ya makubaliano na Mkataba na hapo natumai ndipo hupatikana Hati ya Mkataba ambayo inajulikana kama Treaty na kama itatosha Makubaliano ya Tanganyika na Zanzibar yalizaa Mkataba wa Tanganyika na Zanzibar na kusajiliwa katika Umoja wa Mataifa ambao ulitoa Hati ya Makubaliano na kwa kukuongezea ulipigiwa kura na kupitishwa, nikirudi kwa Roza na Juma sina uhakika kama katika makubaliano yao walipata Hati inayothibitisha Makubaliano hayo na pia sijui kama katika makubaliano yao kuliwa na masharti wakati Hati ya Muungano ina masharti.Na ndipo inapopatikana tofauti ya kuweza au kutoweza kubadilishwa.
Hivyo hapa hakuna unyemela wa kuongeza bata wala kuku,chochote kitakachofanyika ni lazima itazamwe Hati inasemaje ,kwa maana hiyo chochote kitakachofanywa ni lazima kikubaliane na Hati ya Muungano inasemaje ? Kama unataka kuongeza kuku au Mbuzi Je hati inakuruhusu moja kwa moja kufanya hivyo ? Na ikiwa mtafanya wakati Hati hairuhusu mtakuwa mnatenda kosa ,nini kifanywe kwanza ni kuitafuta Hati ya Muungano na kuisoma vizuri ili kuepuka migongano baadae , ili mujitosheleze ni lazima Juma na Roza wabadilishe Hati kwanza ili iruhusu makubaliano mengine yanayotaka kuingizwa.
Na kutokana na hati iliyohifadhiwa Umoja wa Mataifa juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (sio huu wa Juma na Roza) haya yote ya kuongeza mbuzi na kuku yatakuwa hayana mshiko kwa sababu hayatambuliki na hayana nafasi kwenye Hati ya Muungano maana yakichambuliwa na kutafutiwa nafasi ndani ya Hati ya Muungano basi yote yataonekana ni mizengwe iliyo wazi ni utapeli.

Ahsante.

Kwa hiyo unasema inategemea Mkataba wa Muungano ulisema nini kuhusu kubadisha huo Mkataba.

Basi mwanzoni kabisa, kabla sijaleta mifano ya Mkataba wa ku share utawala ya ngo'ombe za Juma na Roza, ulisema na kueleweka kwamba (at least mimi nilikuelewa hivi) kwamba Mkataba wa Muungano haubadilishiki zaidi ya yale yaliyokuwemo awali. Post yako namba 611:
Mkataba wa Muungano ni Sheria mama ambayo haitaki kuchezewa hata kidogo,na kubadilishwa badilishwa mambo ambayo hayakuafikiwa wala kujadiliwa na pande zinazohusika...

Kumbe una maana Mkataba wa Muungano unaweza kubadilishika kutegemeana na Mkataba wenyewe ulivyosema kuhusu kuubadilisha.

Kwa hiyo usirudie kutumia lugha inayoweza ku imply kwamba mkataba haubadilishiki.

Let's move along.

Mkataba wa Muungano unasema nini kuhusu mabadiliko ya Mkataba wa Muungano ?

By the way, Hati ya Muungano haihifadhiwi Umoja wa Mataifa. Attorney General wa Zanzibar, do you hear me, Attorney General wa Zanzibar alisema yeye mwenyewe hajawahi kuuona! Mahakama ilim subpoena alete nakala ya Articles of Union Mahakamani kwenye kesi ya Muungano ya 2003. Akasema hana. Ikasemekana haupo!

Mkataba wa Muungano unasema nini kuhusu mabadiliko ya Mkataba ?
 
Gadafi ni wa Zanzibar?
Basi MAKUBWA!
Haya...Wapewe nchi yao wasipewe?
Maana hapo ndio kwenye mzizi wa FITINA...JAMANI WANA JF..WAPEWE NCHI YAO WASIPEWE?!
 
Date::8/7/2008
Polisi waruhusu maandamano ya kudai Zanzibar ni nchi

Rais Amani Karume wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Na Salma Said, Zanzibar
Mwananchi

JESHI la Polisi Zanzibar, limetoa kibali cha kufanyika maandamano ya kutetea Zanzibar kuwa ni nchi yaliyoandaliwa na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), visiwani hapa.

Taarifa ya polisi iliyotolewa visiwani hapa jana ilisema kwamba, maandamano hayo yameruhusiwa kufanyika keshokutwa na yataanza saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Kombawapya hadi Kibanda Maiti Uwanja wa Demokrasia.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa masharti kwa wahusika, ikiwa ni pamoja na wahusika kutochukua silaha ya aina yoyote wala kubeba mabango katika maandamano hayo.

Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kumbukumbu No. W/MJN/SO.7/2A/106, pia Polisi imewataka waandaaji kuhakikisha wanawadhibiti wanachama wao wasiharibu mali za raia na wananchi katika maeneo ambayo yatapitia.

“Kusiwepo na lugha ya matusi kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa kwa nia ya kuleta jazba, ugomvi na kupelekea kuhatarisha amani na utulivu,” inaeleza barua hiyo ambayo Mwananchi imeiona ikiwa imeandikwa Agosti 7, mwaka huu na kusainiwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam.

Aidha, viongozi wa NRA wametakiwa kuhakikisha vyombo vya habari vinaruhusiwa katika maandamano hayo vikiendelea kufanya kazi zao bila ya kuwepo vikwazo vyovyote.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa NRA Zanzibar, Suleiman Gaddafi, alisema matayarisho ya maandamano hayo yamekwishakamilika ikiwemo kuwaalika viongozi wa vyama vingine ili kuongeza nguvu ya mahudhurio.

Alisema takriban vyama vyote vilivyopata usajili wa kudumu nchini vimekaribishwa katika maandamano hayo isipokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamesema hao hawatashiriki kwa vile wanaunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba suala hilo waachiwe wanasheria wa pande mbili kulishughulikia.

“Naibu Katibu Mkuu wa CCM nilipokutana naye ili kumkaribisha katika maandamano hayo amenijibu chama chake hakiko tayari kwa vile kinaamini suala hilo linashughulikiwa kama ilivyoagizwa na serikali,” alisema Gaddafi.

Alisema pamoja na msharti magumu yaliyowekwa na polisi, wanashukuru kwa
kuruhusiwa kufanya maandamano hayo kwa vile yatatoa fursa kwa wananchi wa Zanzibar kuonyesha ni jinsi gani walivyokerwa na kauli ya Pinda kwamba Zanzibar sio nchi.

Gaddafi alisema, maandamano hayo si ya itikadi ya chama na kwamba wananchi wote wa Zanzibar wanaruhusiwa kushiriki bila kujali tofauti zao za kisiasa kwa vile suala hilo linahusu nchi na sio chama.

Awali, maandamano kama hayo yalikuwa yafanyike Zanzibar, lakini yalishindikana baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kugoma kuyapokea.

Alikataa kupokea maandamano hayo yaliyokuwa yamalizikie katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa maelezo kwamba, katika kipindi hicho Viwanja vya Baraza vilihitaji mazingira ya utulivu kutokana na wajumbe kuendelea kujadili bajeti ya serikali, kwa hiyo haikuwa jambo la busara kuruhusu mikutano ya watu katika viwanja hivyo.

Maandamano hayo yalikuwa yameandaliwa na Wazanzibari wanne kwa niaba ya wenzao 10,000 wanaotetea kuwa Zanzibar ni nchi licha ya kufikiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Tangu Pinda atoe kauli kwamba Zanzibar si nchi akiwa bungeni akinukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumekuwa na mjadala mkali kutoka kwa watu mbalimbali, baadhi wakimuunga mkono ilhali wengine wakimpinga.

Pinda hadi sasa amekwishapingwa na viongozi waandamizi ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwamo Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Juma Shamhuna, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Iddi Pandu Hassan na wawakilishi kadhaa.
 
Wapewe nchi yao wasipewe?
Hapo ndio kwenye swali...Kama wao wanataka nchi yao....Sioni kwa nini wanyimwe.
 
Halafu kwasababu wana ccm wa zanzibar nao wanakubaliana na wale wa cuf pamoja na baadhi wa bara...Basi Zenji itakuwa nchi na mafisadi wakivuka mpaka huko kisiwani wakiwaachia bara yenu wakiwapa Tanganyika mtafanya nini?

Maana kama wakisaini pacts na nchi ya Zanzibar ambayo itakuwa Taifa la kiarabu..BASI WAKIVUKA MPAKA WAKIINGIA HAPO ZANZIBAR HAUWAGUSI WALA NINI...Say wakikubaliana na cuf na wahafidhina wengineo wa ccm kuwa wapewe zenji kwa masharti ya kuwaminya Tanganyika wasiwashitaki...Kwa hiyo ni bora mkae mzungumze ama muwape chao.

Maana ikiwa collaboration ya NRA-CUF-CCM....Basi ngoma ntolee.
 
Back
Top Bottom