Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Zenj si chochote.
Wanajikanyaga tuuuuuuuuuu
O.K jitoeni haraka kwenye MUUNGANO muone matunda yake.
Hata ivo hakuna M-Tanganyika anaewahitaji.
Mwambie na huyo presido wenu atangaze kujitoa,la sivo fungeni midomo yenu,tumechoka na Vijineno venu.
una uhakika na unachokisema.? wakati zanzibar ilipoendelea tanganyika lilikuwa pori tu bwamdogo kama hujui . na mpaka leo hii ni tabu sana duniani nje ya east africa kumfahamisha mtu tanganyika akaifahamu ila zanzibar una uwezo wa kuitaja popote na ikajulikana.. ni vyema ukafunga domo lako wewe ambae hujui unachokiongea,maendeleo ya zanzibar yanadumazwa na tanganyika. kuwa mstaarabu uongee lugha njema na tutatue matatizo huwezi hilo basi usiongee usilolijua.
 
Mapenzi yamepungua katika ndoa hii. Mheshimiwa aliyepita alibwabwaja vitu pasi na kuviweka sawa ila na wewe kubwabwaja majibu pia si suluhisho. Umemshutumu aliyepita kwa kuongea asichokijua, je na wewe una uhakika na hili?

maendeleo ya zanzibar yanadumazwa na tanganyika.
 
Bila kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo iko juu ya katiba zote nchini, inasema nini
source; Tanzania Daima.
Sasa tutatoa maoni yetu binafsi yasiyo na rejea!!!
Makala yako ni matamanio ya watu wa Zanzibar. Lakini kisheria hiyo usiyotaka kujali inasema nini ndiyo ilyopo kisheria na kutambulika mengine yote uliyoyataja ni internal matters. Bendera, wimbo wa taifa pekee si alama ya soverignity ya nchi. Nenda nchi kama Belgium yenye mataifa matatu , Waflemish, Wawalonia na Wadachi. Wote hawa wana hayo yoye uliyoyaandika lakini bado si soverign na ni Belgium ndiyo inayotambulika kimataifa. Vivyo hivyo kwenye miungano mingine duniani kama Uingereza(UK), Ujerumani, USA na kadhalika.
Kwa hiyo yote yaliyofanywa na yanyofanywa na SMZ ni matayarisho, halali pengine, ya kujitenga na tunayaombea yaishie kwa heri kama Slovakia na Czech na si Serbia na Kosovo.
Itakuwa vema mwandishi kuandika ukweli, rais wa Zanzibar huwakilisha mapendekezo ya uteuzi wa wateuliwa mbalimbali katika vyombo vya muungano kuhusiana na Zanzibar, lakini ukweli uteuzi hutangazwa na rais wa jamhuri ya Muungano. Kulemba ni jambo zuri, lakini malembo yapendeze.
 
Mwiba , Umeula na Chuwa. Naona sasa unataka kukumbatia wana CCM kwa nguvu kwa kisingizio cha Muungano. Wao na ,wewe na wenzako, ni tofauti kabisa. Elewa kuwa wao (CCM -Zenj) hawatakiokuvunja Muungano wala kubadilisha Muundo wake- wanachogombania wao (CCM- Zenj) ni fair deal (ambayo ilianza kugombewa na mwenyewe muasisi Marehemu Mzee Karume). Mwiba na watu wako mnataka kuvunja Muungano. Usidanganyike hakuna CCM hata mmoja Zanzibar ambaye yuko pamoja na nyinyi CUF. CUF kaeni chonjo. CCM -Bara wanatuelewa CCM -Zanzibar - Nyie CUF mlie tu.
hapa ndugu naona unazungunza lugha ya ajabu ajabu ,maana kati ya waliotaka kuwasilisha hoja binafsi mmoja ni kutoka CCM na mwanasheria wa Baraza amezikubali zote na amewashauri kuwa ataifanyia kazi na kuifanya moja na tayari alikwisha fanyisha muhtasari wa hoja hizo na kuifanya moja ,siku ya pili ilikuwa iwakilishwe barazani na Mwanasheria huyo ,Serikali ya bara kwa kumtumia Kificho wakaingia mitini na kutoa muda hadi October,hili si suala la CCM au CUF hili ni suala la kila Mzanzibari, so far CUF walitoka nje ila CCM walibakia kwani CCM inajulikana kuwa ni woga katika kutake action ,sikuwashangaa ! Hivyo watakuwa na masuala ya kuwajibu wananchi wao huko mitaani ,wakati CUF wamesema sasa sio kupitia hapo tena ni moja kwa moja kwa wananchi kwani suala hili wakulijadili na kuamua ni wananchi na sio watu wawili (Mwanasheria Mkuu wa Bara na Visiwani),hao wamekuwa na miaka arubaini hakuna walilokuja nalo na kwa hivyo watakuwa hawana jipya zaidi ya kununua mida.
 
WANASHERIA wakuu wa serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanashughulikia tafsiri sahihi ya kisheria kuhusu utata ulioibuka nchini wa kama Zanzibar ni nchi. Hii inafuatia tamko la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilotoa bungeni wakati akijibu swali.
Itakuaje wanasheria wakishindwa kuafikiana? Suluhisho pekee litapatikana suala hili likipelekwa Mahakama Maalumu ya Katiba.
Kwa mujibu wa Ibara ya 126(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, mahakama hii inaundwa ili "kusikiliza shauri lililotolewa mbele yake na kutoa uamuzi wa usuluhishi, juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar".
Katiba ya Zanzibar, Ibara ya pili inatamka: "Zanzibar is a State." Maana yake Zanzibar ni nchi. Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiingereza – Kiswahili, Toleo la Tatu, iliyoandikwa na kutolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (TUKI), neno "state" limetafsiriwa ni "dola"; "Serikali"; "jimbo".
Ibara ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, inaitaja Tanzania kuwa ni "Jamhuri ya Muungano"; kwa lugha ya Kiingereza, ni: "Tanzania is a United Sovereign Republic." Neno "State" halipo hapo. Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI, neno "Sovereign" lina maana "kuu", "enye enzi", na "Sovereignty" ni "mamlaka" au "utawala", wakati neno "Republic" linamaanisha "Jamhuri".
Kwa hivyo basi, Tanzania ni "Mamlaka au utawala wa Jamhuri ya Muungano". Je, Mamlaka au Jamhuri ni dola au Serikali kwa maana ya "state"? Je, ni nchi? Ni ipi "nchi, kati ya "state" na "sovereign Republic"? Nini kilichokusudiwa chini ya Muungano huu, na utata uko wapi?
Msingi mkuu wa muungano na wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar ni "Mkataba wa Muungano" uliotiwa saini na waasisi wake, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Abeid Amani Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hii inaitwa "Hati ya Muungano au "Articles of Union."
Chini ya mkataba huo, nchi hizi zilikubaliana kuunda "Jamhuri ya Muungano" kwa hiari kwa kuachia baadhi tu ya madaraka/mamlaka yake ili yaingie na kushughulikiwa na Muungano na kubakiza mengine yote.
Yafuatayo ni mambo 11 yaliyoingizwa kwenye Muungano: Katiba ya Muungano; Mambo ya Nje; Ulinzi na Usalama; Polisi; Uraia na Uhamiaji.
Mengine ni Mikopo na Biashara ya Nje; Utumishi katika Serikali ya Muungano; Kodi ya Mapato na Ushuru wa Forodha; na Bandari na Usafiri wa Anga.
Kwa kuwa Muungano ulifikiwa kidharura au "zima moto", ilikubaliwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika irekebishwe kwa kuingiza masuala hayo 11 ya Muungano na kutumika pia kama Katiba ya muda ya Muungano hadi Muungano huo utakapopata Katiba yake katika mwaka mmoja.
Ibara hii inaonyesha: Jamhuri ya Tanganyika haikufa kufuatia Muungano huo, hoja inayopewa nguvu na Ibara 5 ya Mkataba huo isemayo: "Sheria za Tanganyika zilizopo na zile za Zanzibar zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi hizo" (Hapa Mh.Pinda aulize ni nchi zipi hizo ili apatiwe jibu)wakati wote wa uhai wa Muungano huu.
Mkataba huo unatambua kuwapo kwa Makamu wa Rais wawili wa Jamhuri ya Muungano, mmoja kutoka Zanzibar ambaye pia ndiye Rais wa Zanzibar, na mwingine kutoka Tanganyika. Kazi zao zimefafanuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na ya Muungano kuwa ni "mmoja atakuwa msaidizi Mkuu wa Rais kwa shughuli za Muungano Zanzibar na ndiye pia Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Serikali ya Zanzibar; na mwingine atakuwa msaidizi mkuu wa Rais kwa shughuli za Muungano upande wa Tanganyika na ndiye pia kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni."
Kama ilivyo mikataba yote ya kimataifa, Mkataba wa Muungano ulitakiwa kuridhiwa na Mabunge ya nchi hizo mbili ili uwe na nguvu za kisheria na kuweza kutumika. Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Zanzibar yaliridhia Mkataba huo 25 Aprili1964 na kuupa Muungano huu jina la "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" (kif .4) ambapo, pamoja na mambo mengine, Mabunge hayo yalimpa Rais uwezo wa kuifanyia marekebisho Katiba ya Tanganyika kwa njia ya AMRI za Rais (Decrees) ili iweze kukidhi mambo ya Muungano (kif. 5(2). Hapo ndipo utata wa Muungano ulipoanzia.
Marekebisho ya kwanza kwa njia ya AMRI ya Rais (The Transitional Provision Decree, 1964) yaliyochapishwa kama Taarifa ya Serikali (GN) Na 245 ya 1/5/1964, yaliwahamishia watumishi wote wa Jamhuri ya Tanganyika kwenye utumishi wa Jamhuri ya Muungano kana kwamba shughuli zote za Tanganyika zilikuwa za Muungano, na ikaagizwa "sheria za ajira za Jamhuri ya Tanganyika zilizopo zitatumika pia katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano", na Mahakama Kuu ya Tanganyika ikawa ndiyo Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano.
Amri hiyo ilielekeza pia kutumika kwa mhuri wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kama pia mhuri wa Jamhuri ya Muungano, hadi hapo Bunge la Muungano litakapopitisha mhuri wake. Amri ilielekeza kuwa "mali zote na haki kwa mali za Jamhuri ya Tanganyika za aina yote, na mali zote na haki kwa mali za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zinazomilikiwa au kutumika kuhusiana na mambo ya Muungano zitamilikiwa na Jamhuri ya Muungano".
Tatizo hapa ni kuwa wakati Tanganyika ilikabidhi kila kitu kilichokuwa chake kwenye Serikali ya Muungano, Zanzibar ilichangia zile tu zinazohusiana na taasisi za muungano na kuruhusiwa kumiliki mali zote nyingine. Ni bahati iliyoje kwa Zanzibar kurithi utajiri wote wa Tanganyika ndani ya Muungano, wakati ikiendelea kumiliki mali zake zote bila ya kuingiliwa?
Amri ya pili ya Rais iliyochapishwa kama Taarifa ya Serikali Nam. 246 ya 1/5/1964 ilifanya marekebisho yenye utata zaidi unaoendelea hadi leo. Chini ya kifungu 4(2) ilielekezwa, "Mamlaka kuhusiana na mambo yote ya Muungano ndani na kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano, na kwa mambo mengine yote ndani na kwa ajili ya Tanganyika, yatakuwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano".
Ndiyo kusema utawala kuhusiana na mambo ya Muungano, na mamlaka kuhusiana na mambo yote ndani na kwa ajili ya Jamhuri ya Tanganyika, yameunganishwa na kuwa chini ya rais wa Jamhuri ya Muungano, na hapo hadhi ya Tanganyika ikafutika kinyemela.
Na kwa kuwa sasa kila kitu cha Jamhuri ya Tanganyika kilikuwa mali ya Muungano, ndiyo kusema Tanganyika ndiyo iliyogeuka kuwa Muungano, na Muungano kuwa ndiyo Tanganyika; Bunge la Jamhuri ya Tanganyika likawa Bunge la Muungano, Rais wa Jamhuri ya Muungano akawa Rais pia wa Tanganyika, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika akawa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano asiye na nchi, wakati Zanzibar iliruhusiwa kuendesha mambo yake kama nchi huru, isipokuwa kwa mambo ya Muungano tu.
Na kupitia Amri nyingine (the Transitional Provision No 2 Decree, 1964) ya 1/5/1964, iliagizwa jina "Tanganyika" lisomeke na kumaanisha "Jamhuri ya Muungano", katika vitabu vyote vya sheria", na neno "Serikali ya Tanganyika na mambo yote yanayohusiana na Jamhuri ya Tanganyika" nayo yasomeke kumaanisha "Serikali ya Jamhuri ya Muungano".
Hapa ndipo dhana ya serikali mbili ndani ya Muungano ilipoanza kujitokeza. Kwamba Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, badala ya mtazamo wa awali wa kuwapo Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano.
Pamoja na Zanzibar kuanza kuhofu kumezwa na Tanganyika, kimisingi nchi hiyo ilionekana kama mgeni ndani ya Muungano aliyealikwa kuja kufaidi na kufurahia "vinono" vya mwenyeji wake Tanganyika bila ya kuvitolea jasho.
Pengine ni hofu hii iliyomfanya Karume atofautiane na Nyerere juu ya muundo sahihi wa Muungano na hiyo ikaua uteuzi wa Tume ya kuandika Katiba ya Muungano. Pia Bunge la kupitisha Katiba hiyo halikuitishwa Aprili 1965 kama ulivyoelekeza mkataba hadi mwaka 1977.
Juhudi za kufifisha au kufuta kabisa nafasi ya Tanganyika kwa maamuzi ya mtu mmoja kupitia Amri za Rais (Decrees), zilifanikiwa kwa kiasi fulani, lakini "Mkataba wa Muungano" na Sheria ya Muungano kama zilivyo, zilikuwa na zinaendelea kugoma kwa muundo wa sasa.
Hata Katiba Mpya (Act No. 43) ya 1965 iliyotungwa kwa mujibu ya matakwa ya serikali ya kuanzisha serikali ya kidemokrasia ya chama kimoja, iliendelea kutambua muundo wa Serikali Tatu na kuwapo Tanganyika.
Ushahidi ni Ibara ya 20, iliyosema "Rais atateua Mkuu wa Mkoa kwa kila Mkoa ndani ya "Tanganyika" na Ibara ya 25 iliyosema "Tanganyika itagawanywa katika majimbo mengi ya uchaguzi kwa kuzingatia idadi ya watu kwa kila jimbo…."
Na kuhusu utumishi wa Mahakama, Katiba ilisema, "Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ndani na kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano ndani ya Tanganyika…." Ndiyo kusema muundo wa Shirikisho ulitambuliwa kisheria tangu 1964 hadi ulipofutwa kinyemela na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, lakini Mkataba na Sheria ya Muungano zinagoma.
Tatizo hili si la kisiasa kama wengi tunavyodhani, bali ni la kikatiba na hivyo lazima litatuliwe kikatiba kwa kuangalia chimbuko, madhumuni na muundo wa Muungano uliokusudiwa. Je, ulilenga kuunda Serikali moja, mbili au tatu?
Halafu mtu aje hapa aseme huku kabana pua Zanzibar si nchi , ukweli ndio huo na kila siku unazidi kufanya chemchem.hapa hakuna cha mwanasheria mkuu wala mpya.
Ukweli siku zote utaishinda zuluma na ndio tuonavyo ukisoma utaona Zanzibar ilibakia kuwa Nchi na Tanganyika ilijizamisha wakati makubaliano hayakubali kujizamisha huko.
 
Tunakushukuru Mwiba kwa hili chapisho. Nafikiri ukilisoma kwa undani unaweza kupata jibu la Zanzibar ni Nchi au La. Na nini kinajiri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nini hatima ya Zanzibar, na nini hatima ya iliyokuwa Tanganyika (ingawa bado naamini ipo-and is very strong)
 
Last edited:
Nakupongeza Mwiba kwa hoja zako za kikatiba na kwa upande wangu nahisi kuwaZanzibar imeshaamuwa kuwa mshiriki sawa wa Muungano na si vyenginevyo.
 
Nakupongeza Mwiba kwa hoja zako za kikatiba na kwa upande wangu nahisi kuwaZanzibar imeshaamuwa kuwa mshiriki sawa wa Muungano na si vyenginevyo.
Zanzibar ipo pembeni na ni Nchi kamili tatizo ni kuipapatua Tanganyika ndani ya Muungano ili nayo iwe pembeni ,si umeona hiyo kesi hapo juu ,Tanganyika ndio imejigeuza na kujiita Tanzania , Tanganyika ipo ila Tanzania ndio haipo ila Tanganyika wamejivalisha ugozi wa kondoo.
lazima Tanganyika ipapatuliwe ndani ya Muungano ili kuwafichua mafisadi na kuwahukumu hukumu ya paka mwizi.
 
Khee! Bwan Mwiba. Bahati yako Mwalimu Kambarage hayupo Ungekiona kilichomtoa kanga manyoya. Tanganyika ndiyo hiyo inayojibadilisha kuwa mara-sijui- Tanzania. Upo hapo. Lakini sisi wana- Zanzibar tunashikilia mawili tu sasa. Moja Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili Zanzibar yetu. Hatuna habari na hii Tanzania nyengine ya Mheshimiwa Pinda.
 
Itabidi mkazane la mkitembea huku mnapunga mikono basi mjue na miguu nayo itabidi ifanye matege au matendegu.
 
Katiba ya Zanzibar, Ibara ya pili inatamka....

Mwiba, kama hujali, naomba nakala ya Katiba ya Zanzibar. Haipatikani kwa urahisi, sijui kwa nini. Una PDF au DOC au link yake ?
 
Zanzibar ipo pembeni na ni Nchi kamili tatizo ni kuipapatua Tanganyika ndani ya Muungano ili nayo iwe pembeni ,si umeona hiyo kesi hapo juu ,Tanganyika ndio imejigeuza na kujiita Tanzania , Tanganyika ipo ila Tanzania ndio haipo ila Tanganyika wamejivalisha ugozi wa kondoo.
lazima Tanganyika ipapatuliwe ndani ya Muungano ili kuwafichua mafisadi na kuwahukumu hukumu ya paka mwizi.
mwiba.
nimependa hii post yako, na hii post yako ni reality tupu hamna uongo hata chembe. kwangu mimi hakuna serikali ya muungano kuna tanganyika iliyojivisha utanzania huku ikimlaghai zanzibar kwa kumpa kijiserikali ambacho hata hapo kwa jirani zetu kenya hakitambuliwi, mawaziri wao ndio wanawakilisha tanzania ,mawaziri wa zanzibar mwisho wao chumbe. ila nadhani ipo siku ,tutanasuka, bi idhni llahi tabaraka wata'ala
 
Kilichomtoa kanga manyoya kitajulikana karibuni,kila wakichochea Zanzibar si Nchi ndivyo kunakoifanyisha Zanzibar Kuchanua tena.
Kuna msemaji wa Ikulu nae karukia eti Katiba ya Muungano nayo inasema Zanzibar ilipoteza hadhi ya kuwa Nchi pale ilipokabidhi mamlaka yake 1964.Sasa na atazame Katiba ya Zanzibar nayo inasemaje ,wakati Tanzania katika kubungua bungua sijaona kuwa imeitwa State wakati Zanzibar inajulikana kuwa ni State au Nchi ,wakati Tanganyika Inajulikana kuwa ni State ,ila narudia tena hakuna sehemu ambayo inasema kuwa Tanzania ni State kwa maana ya Nchi na hivyo kupatikana kitu kimoja.
Sa ingine ndio nikaona kuwa watu wana mashahada makubwa makubwa lakini ukiwapeleka kwenye mambo ya kusoma na kufahamu unakuta ni sifuri,ndipo ikapatikana hesabu ya watu wanaisabu nazi wao wanaisabu makumbi na ndio ukaona hatua iliyofikishwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasomi wa aina hii.
Hivi huyu hafahamu kama kuna Mkataba wa Muungano je ameupitia nadhani hata sijui kama anajua kitu kama hicho kipo.
Na pia atuonyeshe Kama Tanganyika ilipoteza kuwepo kwake kimaandiko.Ni bora mkanyamasa kimya iri haya mambu yapite bila kupingwa ,yaani yapotee tu on the thin air.
Lakini kila mkijidai kuchokonoa basi ndio mnapozidi kuhatarisha kupatikana kwa marekebisho makubwaambayo mafisadi hawataki yatokee.Hao wanasheria mnaojivunia kuwa watarekebisha wameshaanza kupigwa kumbo na kuambiwa hawana uwezo kisheria kutokana na makubaliano ya Muungano,sasa sijui watajifichia wapi na kutoka na pendekezo lao.
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kama ilivyo Tanzania kuwa ni sehemu ya Afrika lakini huwezi kusema Zanzibar si nchi.Mwinyi aliwaona watu hawa waliosoma lakini hawakufahamu.
 
Mkubwa Mwiba hongera kwa kuzidi kufunguwa macho ya wengi na matokeo ni kuzidi kuwapukutisha wale wanaolonga kuwa zanzibar si nchi. Walikimbilia kwenye maamuzi ya kesi ya uhaini wakaona kuwa kilichotolewa hukumu ilikuwa ni kuwa iwapo hilo jambo la uhaini ni suala la Muungano au la na ikasabahi kuwa ni jambo la muungano kwa hivyo lisingeweza kufanyika Zanzibar pekee.
Wakangangania katiba lakini nayo inawagomba hivyo wakatumia nguvu za chama na Bunge lakini harakati haijazimika sasa kilichobaki ni kutumia nguvu kunyamazisha lakini sijui kiasi gani hilo linaweza likaleta ufumbuzi wa kudumu.
Kwanini hatutandiki jamvi na kuujadili Muungano kwa uwazi na kuutibu madonda ndugu yanayoukabili.
 
Na pia atuonyeshe Kama Tanganyika ilipoteza kuwepo kwake kimaandiko.

Kwa mujibu wa maandiko yaliyopo, Tanganyika pekee ndiyo ilipitisha sheria ya Muungano wa Zanzibar na tanganyika (rejea kitabu cha prof Issa Shivji- Pan-Africanism or Pragmatism? uk 69-99). Zipo documents, ikiwemo na sheria hiyo, ambazo zinaonyesha kuwa Zanzibar haikuwahi kukaa na kupitisha sheria hiyo. Muungano kwa upande wa zaniz bra ulikubaliwa kwa ubabe wa Karume tu na alifanya hivyo kama his only polisical survival mean.
 
MWIBA:
Umejitahidi sana kueleza maoni yako kuhusu Zanzibar kuwa nchi au vinginevyo. Wakati ukiendeleza hoja zako naomba ufahamu kitu kimoja. Huwezi kuwa na nchi kama huna sovereignty! Sovereignty ndicho kitu muhimu katika kufafanua kuwepo kwa nchi au la. Sovereignty inakupa uwezo wa kujiamulia mambo yako mwenyewe bila kuingiliwa na mamlaka nyingine yoyote. Niirudi kwenye tafsiri yako ya katiba ya Zanzibar, naomba ufahamu kuwa Katiba inayotawala ni ile ya mwaka 1984 ambayo ni ya Kiswahili. Katika katiba hiyo, Zanzibar haitafsiriwi kama nchi huru (correct me if I am wrong). Pili, neno "state" halina maana ya nchi kama ambavyo unataka wasomaji wako wakubali. Chukulia nchi zenye mamlaka ya majimbo kama vile Nigeria au hata marekani. Ukisema State of California, Yoruba au Igbo hauna maana ya nchi. California is a state but it is not a soverign state. The USA is noot a state but a unification of many individual states. Do you wish to reconsider your interpretation? My take, Zanzibar siyo nchi. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mpita Njia,
Ukisema hivyo unakuwa unapotosha ukweli. Hata Issa Shivji mwenyewe anajua kuwa anachokisema siyo 'ukweli" ila ni tafsiri yake ya nini kilipaswa kufanywa. Baada ya Mapinduzi ya umwagaji damu ya mwaka 1964, Mzee karume alitawala Zanzibar kwa kutumia decrees! baraza la mapinduzi lilikuwa nothing but a sham. Kulipitishwa decree iliyoridhia Muungano iliyoitwa "the Union Decree" sawa na Acts of the Union iliyopitishwa na bunge la Muungano.
 
kwa kweli nimeeangali POLL hapo juu nimesikitika sana kuona watu wengi wame vote kuvunja muungano
Lakini niseme tu naheshimu vote hizo.Kikubwa kwa mtazamo wamngu ni kurejelea kila kitu husuhu muungano A to Z na kufanya tathimi ya kina kwa kuhusisha wananchi wa pande zote zote kwa 100% ili kuboresha muungano kwa misingi ya kimaendeleo kwa faida ya kila Mtanzania
lakini swala la kuvunja muungano sizania kama ni jema Tunafahamu sikuzote neno au tendo kuvunja halina matunda bora
 
MWIBA:
Umejitahidi sana kueleza maoni yako kuhusu Zanzibar kuwa nchi au vinginevyo. Wakati ukiendeleza hoja zako naomba ufahamu kitu kimoja. Huwezi kuwa na nchi kama huna sovereignty! Sovereignty ndicho kitu muhimu katika kufafanua kuwepo kwa nchi au la. Sovereignty inakupa uwezo wa kujiamulia mambo yako mwenyewe bila kuingiliwa na mamlaka nyingine yoyote. Niirudi kwenye tafsiri yako ya katiba ya Zanzibar, naomba ufahamu kuwa Katiba inayotawala ni ile ya mwaka 1984 ambayo ni ya Kiswahili. Katika katiba hiyo, Zanzibar haitafsiriwi kama nchi huru (correct me if I am wrong). Pili, neno "state" halina maana ya nchi kama ambavyo unataka wasomaji wako wakubali. Chukulia nchi zenye mamlaka ya majimbo kama vile Nigeria au hata marekani. Ukisema State of California, Yoruba au Igbo hauna maana ya nchi. California is a state but it is not a soverign state. The USA is noot a state but a unification of many individual states. Do you wish to reconsider your interpretation? My take, Zanzibar siyo nchi. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Yakhe watu hawataki kuzungulushwa zungulushwa na mafisadi , maana hayo unayoyasema na kuyadai yote yameshapitiwa na hayana mshiko katika Mkataba wa Muungano ,yaani kwa hivyo unavyotaka basi mambo yasingekuwa yanachemka halafu yananywea ,mnapoulizwa ni lini Zanzibar ilifutwa mnakuja na story nyingi ,tunataka straight jawabu .
1 ) Ni lini Tanganyika ilifutwa.
2 ) Ni lini Zanzibar ilifutwa.
3 ) Ikiwa zilifutwa ni kipengele gani cha Mkataba (Treaty) kimetoa nguvu hiyo kisheria kuweza kuzifuta Nchi hizo. Au ndio kinyemela.
Usiniletee mambo ya Katiba hapa ,maana Katiba unayoizungumzia inatokana na Muungano uliovurugwa ambao haukuzingatia matakwa ya Mkataba ,na ndicho ambacho kama kesi hii itapelekwa kwenye mahakama za Kimataifa basi mafisadi watarudi vibudu.
 
Zanzibar at present is politically united with the mainland territory of Tanganyika, but it has had its own institutions and laws. From unity in 1965 it has retained its own government. The president of Zanzibar has been one of the two Vice-Presidents of Tanzania.The territory consists of the two main islands of Zanzibar and Pemba.
Yaani kila ukichungua ndipo kuku atakapokushinda kumla , wachunguzi wa mambo ndio kama walivyosema tumeungana kisiasa tu si kiroho ,sasa napata akili kwa nini mafisadi wameng'ang'ania.
Kitu kimoja hadi sasa naona walioshika bango ni wajamaa kutoka kanisani :-
Mizengo Peter Pinda huyu mambu yamemshinda kakiachia Chama.
Tambwe Hiza..Huyu hajui kuzungumza amegonganisha wenziwe sasa ameufyata.
Sengondo Mvungi ..anajipendekeza ili asionekane kama ni fisadi
Peter Kisumo... Kachanganyikiwa
Kadinali Pengo...anafanya kazi ya kanisa
Sylvesto Rweyemam ...kasoma lakini hakufahamu.
John Nchimbi
 
Back
Top Bottom