Huyo waziri wa Zenj lazima ashikishwe adabu, Na huyo Mbunge kasema kweli, na kitu ambacho kwa miaka mingi viongozi wa SMT na SMZ wameshindwa kukikemea...
 
Last edited:
Mwiba,
In a Government administration yule Waziri wa Zanzibar ni "bomu" kweli kweli; hajui miiko yake ya kazi! Harrison kama mbunge kaongea ukweli mtupu! It is time for presidents to appoint people who are capable as learders than such a crap like this Zanzibar fellow!

Sielewi kipi kimekufanya upelekee attack kwa Harrison! Different stories!
 
Sasa utovu wa Mwakiembe uko wapi hapa? Ni roho gani imekuongoza kubandika haya hapa? unajua maslahi yakikuongoza wewe, usitake na sisi tuamini unachokiamini.
 

Nashindwa kukusoma mkuu, unaonekana bado una mengi ya kusema kuhusu Mwakyembe, maliza yote tuendelee na mjadala.Kufananisha kamati ya bunge kumsema Lowasa na huyo kiongozi wa Zanzibar ni vitu viwili tofauti kabisa!

Tena jamaa inaonekana hamuogopi mtu yeyote yule anazungumza ukweli kabisa.anazungumzia kanuni za baraza la mawaziri.umechanganya vitu tofauti kabisa kaka.Are you senior???

Big up Dr.; mwiba ukuchome wenyewe!!!!!

Waberoya
''Dot let school interfere with your education''
 

Of course, this Shamuhuna guy anastahili kuadhibiwa. Hili ni suala la kikatiba ndugu Mwiba na halina uhusiano kabisa na makosa ya kiutendaji yaliyofanywa na Lowassa.

Nadhani unachuki binafasi na Mwakyembe mkuu. Otherwise, it looks like you must be experiencing some serious pyschological problems; and I strongly suggest that you find some good professional counseling before things get even worse.
 
Nahisi mkuu mwiba amekurupuka......... heading na story tofauti kabisaaaa au ni mwandishi wa yale magazeti yaleeeeee.........
 
Mwakyembe is very right. I would expect these strong words to have been uttered by the president and the issue of Zanzibar would have come into the end. Leaving this issue of whether Zanzibar is a sovereign state or not into the hands of Sitta and people like Shamhuna it gives much worries if proper answer/solution can be obtained.
 
Nadhani unachuki binafasi na Mwakyembe mkuu. Otherwise, it looks like you must be experiencing some serious pyschological problems; and I strongly suggest that you find some good professional counseling before things get even worse.

Hapohapo, umegusa mahali pake. Au ndio Kalokiro ipo kazini?
 

Mhe Mwiba

Naomba uwe kama Isayamwita uwe unadhubuti, usikimbie ila naomba ujibu hoja plz!
 

Mwiba unashangaza sana hivi wewe na Lowassa ni ndugu? Tofautisha sana kati ya aliyoyafanya Lowassa na haya aliyoyatamka Pinda. Hatuwezi kukuunga mkono kwa kumtetea Lowassa kwa yale aliyoyafanya hujuma ile haitaweza kutibika kwa miaka mingi. Lakini baya zaidi utengano wa Wazanzibar kwa kujiita Zanzibar ni nchi wakati ilishaungana siku nyingi 26.4.1964 ikawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii mnaibuka na miiba yenu na kusifia utengano huo nadhani hakuna nafasi hiyo. Tanzania is one. Hakuna nchi inayoitwa Zanzibar hapa Duniani.
 
MWIBA,sasa umenunuliwa na mafisadi! Ukimshambulia Mwakyembe aibu itakurudia mwenyewe. Mwakyembe ni msema kweli daima na yuko makini sana wakati wa kuongea. ORATORY yake ni ya hali ya juu sana kama unabisha, kawaulize aliowafundisha pale faculty of law udsm.

Alichokisema Mwakyembe ni wazi kuwa mawaziri wengine hawaijui katiba na hivyo hawana adabu kikatiba mbele ya waziri mkuu. Huo ndio utovu wa nidhamu kikatiba mbele ya waziri mkuu.

Sasa nagundua wewe siyo MWIBA ila ni kipande cha uyoga ambacho hakiwezi kuchoma hata karatasi! POLE sana ndugu yetu RUDI KUNDINI!
 
Kwa maoni yangu Mwakyembe yuko sahihi ndivyo inavystahili. hata kama waziri mkuu alikosea Shamhuna hakustahili kutoa kauli yake.Isitoshe hakutoa kauli ya kungwana ni kauli ya kihuni ambayo yeye kama waziri hakustahili nchi hii haiendeshwi na kauli za kuhuni kama za shamhuna mbona pandu kuficho hajalaumiwa.
 


Mkuu Mwiba UMETOKOTA, Lowassa alifanya ufisadi hivyo alikuwa na tuhuma za wizi na akaambia yeye ni "MWIZI".

PINDA alikuwa anatoa UFAFANUZI wa nafasi ya Zanzabar kama ni nchi au la katika MUUNGANO kulingana na KATIBA ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania baada ya kuulizwa swali.

Hivi Mwiba umeshindwa kutumia akili ndogo tu kutofautisha vitu hivyo viwili ambavyo ni tofauti kabisa. Next time, fikiri kabla ya kuandika maana wewe ni MWIBA UNAOCHOMA
 

mwiba Kweli Unachomaaaa... Mpaka Unajichoma Mwenyewe, Kwa Hili Ndugu Mwiba Umenishangaza Mtanzania... Kweli Tanzania Bado Sana
 
Hayo ya Mwakyembe na Lowassa hayaendani kabisa nadhani ndio yale yale ya Mwnakjj ya BEING OFF POINT!
Vilevile sijaona la Mwakyembe la kuadhibiwa ni lipi?
 
Si staili yangu kunyoosha kidole kwa mwanaJF yoyote,lakini hili la Mwiba limenifanya niamini kwamba kuna watu wakitumiwa wanaweza kubadili rangi nyekundu kuwa nyeusi na nyeupe ikawa kijani ili mradi tu.Unapotaka kumkosoa mzalendo Dr.Harrison Mwakyembe au mwingine yeyote unapaswa kuja na hoja siyo hoja zisizo na msingi zinazonyesha ni namna gani umelalia huo upande wako.Nafikiri ingekuwa vyema kama ungemzungumzia Mwakyembe na issue ya kamati yake bila kuihusisha na hoja aliyoitoa jana bungeni kuhusiana na suala la katiba (muungano). Dr.Harrison aliyazungumza yale ambayo nilifikiri yalitakiwa kukemewa angalau chini kwa chini na Mh.JK ili yasiendelee kuanzisha mpasuko mwingine katika nchi yetu.
 
Tena, Kamati ya Mwakyembe ilimheshimu sana Lowassa. Haikutaka hata kumwita ili imhoji. Lowassa alipopewa nafasi ya kuongea BUNGENI, akaitumia alivyoona yeye inafaa.
Shamhuna atamharibia sana KARUME. Au ndio kampeni za URAIS wa Zanzibar zimeanza?
Kwa nini Karume hajalikemea hili?
 
Mwiba uzalendo umetushinda wa JF ukizingatia wewe ni mwanachama. Tumekuwa tukipambana na ufisadi na mambo mengine mengi ya kijamii. Tumekushangaa sana wewe kumkandia Dr. Harrison Mwakyembe kwa kutoa report ya tume iliyochunguza mkataba wa Richmond. Mateso yote tunayoyapata hapa Tanzania kuhusiana na umeme ni kwa ajili ya matumizi mabaya aliyoyafanya Lowassa akiwa Waziri Mkuu. Pinda ametetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba Zanzibar si nchi. Na sisi Watanzania waelewa tunaamini Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo Tanganyika si nchi.

Mimi binafsi japo SLOGAN yetu ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY" Lakini huo uwazi nao una mipaka. Ushauri wangu nakupa tena bure OMBA RADHI KWA KAULI ZAKO ZISIZO LINGANA NA HADHI YAKO, UMETELEZA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…