'Anger is a condition whereby the mounth works faster than the brain'

Inaelekea ulikwa unaandika kama vile unvyoongea upupu huko Bungeni. Rekebisha hiyo text tuweze kuisoma .Otherwise semi iliteracy may just mean it.
 
Kuna mchangiaji humu anajibu hoja ki-mdebwedo. When it comes to worse, the Constitution prevails. Not hearsay, not opinion. Ukisoma jinsi Jaji A Ramadhani na wenzake walivyochambua vifungu hadi kufikia maamuzi kwamba hakukuwa na uhaini Zanzibar, ndio mfumo huo huo utakaotumika kuamua nani mkubwa: Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zenj, au Waziri Mkuu..

Kama hoja ni kuvunja muungano... basi hoja na iwe kuvunja muungano. Tatizo, wanaotaka kuvunja muungano hawana ujasiri, wanatumia vi-hoja vyepesi vyepesi, typical Zanzibari. Muda wa kupiga Kiswahili umekwisha, ndiyo maana Waziri Pinda mpaka leo hajabadili kauli kwamba Zanzibar si nchi, that's how the books say.

My vote: Let Zanzibar Go, Its Been a Pain all Along. Tanganyika has enough problems to focus on, Umaskini, Mafisadi n.k
 

You are a real MTANZANIA. Hongera sana. Nakubaliana nawe moja kwa moja. Tuna shida nyingi zinahitaji kutatuliwa. Na tuchangiane mawazo katika hili.
 
Sekenke,

Ni vizuri ukamtaja tu kama ni Mwiba au huyu Ngekewa. Kwa kweli wanachoandika ni purely kutoka kichwani mwao na si katika maandiko ya katiba na uamuzi wa mahakama.

Ukiwauliza maswali madogo kama Pinda ni waziri mkuu wa wapi, Hawana majibu.

Ngoja nijadiliane na wengine, ndio maana nimesema kuwa hii ni kama Palestine na Israel.
 

Pengine hukutaka kuwafungulia lakini mimi nitajaribu kuwafungulia. Tatizo la wenzetu huwa hawayaelewi mambo ya Zenji na kukurupuka kwa habari za waandishi uchwara wasioijuwa Zenji.
Umaarufu na nafasi aliyonayo Mwakyembe unatokana na nguvu za Zanzibar na sasa ameshawakanyaga basi na tuangalie kama atarejea tena Bungeni. Mwakyembe aliwashinda Mtandao ka backing ya Zanzibar, katika kinyanganyiro cha ubunge. Backing ya Zanzibar kwa Mwakyembe ilianzia na midahalo iliyokuwa ikifanywa ndani ya TVZ (TV ya serikali ya Zamzibar). idahalo hiyo ikifanywa kati yake na waasheria wengine wa Bara akiwemo DR Mvungi wa NCCR na Dr. Kabodi (kama nimelipatia vizuri jina). Kwenye midahalo hii Mwakyembe alionekana moja kwa moja kuipigia debe Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hivyo SMZ ikamzawadia kuwa mjumbe wa Kamati ya Mwafaka wa CCM na CUF(yeye alikuwa mjumbe pekee kutoka Bara)/

Uhusiano huo ndio uliompa umaarufu na kumfanya awe na Gutts za kuomba ubunge na akaweza kuvuka wikwazo vya Mtandao kwa backing ya Zanzibar. Fadhila zake ni hizi na hivyo tungojee.
 

Ubavu Anao Au Hataki Kurejea 2010?
 

Mseto si lazima uwe wa chakula fulani na unaweza ukachanganya mtiririko wa vyakula na ukabaki kuwa mseto . Muungano unavyouona wewe sio ulivyo bali ni mchanganyiko usioeleweka hivyo tunahitaji recipe iliyo wazi na hili ndilo wanalogombania Wazanzibari. Huu mtindo wa mkubwa ndie sahihi na mkubwa achukuwe chake na cha mwenziwe ndio unaokupeni tabu ndugu zetu.

TANBIHI: Mwwerevu kuelimishwa na Mjinga ndiko huku.
 

MAMBO sivyo yalivyo BABA, MATAKWA YAKO YAWEKE KWAKO.
 
Tunachopinga wengi ni hypocrisy ya hawa wenzetu. Utadaije sovereignty ndani ya muungano? Si watamke wazi kuwa Muungano kama ulivyo haukidhi mahitaji yao kwa hiyo uvunjwe ili tubaki na ushirikiano wa nchi mbili zilizo na full sovereignty! Kigugumizi cha nini?
 

Mkuu najisi ya mmoja si najisi kwa mwengine. Hiyo najisi unayoiona wewe si najisi kwa Viongozi wa Zanzibar na wa Muungano hata Nyerere wakati wa uhai wake. Kama ulikuwa hujui kama wana vikosi viongozi wanajuwa na wao wangekuwa na uwezo wa kuchukua hatuwa kwa vitendo na si kuropoka tu kama wewe. Kwa nini hawajachukua hatuwa labda najisi hii kwao ni halali.
 
mwakyembe yuko sahihi. kumbuka tena huyu ni mtaalamu ya constitutional law. someni kitabu chake.

Hata awe na vitabu Mia. Tunampima sasa kwa utumbo wake anaoeleza Bungeni. Upo hapo.
 
Tunafanya kosa kufikiri kwamba tutaendelea kuwang'ang'aniza wazanzibar wabaki kwenye muungano huku tukiwatukana. Ipo siku CCM na CUF huko Zanzibar watatufanyia kitu mbaya na ndio utakuwa mwisho wa huu muungano.

Haya ni maneno ya busara.
 
Ngekewa,

Ukisha ruka ruka weeeeeeeee, naomba ujibu maswali yangu ukitulia.

Asante
 

Kwa nini wangoje ruhusa au kuachiwa na hao watanganyika? Wao wanaoona wanaonewa na hawapendwi si waseme tu wazi kuwa huu Muungano sell-by date yake imeishapita! Si kujificha nyuma ya vijineno visivyo na maana. Watamke, na kama kweli wanawazungumzia wazanzibari walio wengi, sioni sababu hoja yao ishindwe. Sidhani kama watanganyika wana ubavu wa kuwang'ang'ania wazanzibari walioamua kuondoka. Si zama hizi!
 
Reverend na wenzio (wakiwemo Dr. Mwakiyembe na waheshimiwa wengine) na nyinyi mnaonyesha dhahiri kuwa hamuelewi Katiba ya Zanzibar. Hamuelewi Nini wajibu wa Baraza la Wawakilishi na majumbe wa Baraza la Wawakilishi, Hamuelewi nini wajibu na majukumu ya Rais wa Zanzibar na Baraza lake la Mawaziri kwa wananchi wa Zanzibar. Jifunzeni hayo kabla ya kushupalia kupayuka tu na kusisitiza misimamo yenu. Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania ina madaraka yake nba mipaka yake, Na Zanz\ibar ina mipaka yake na madaraka yake. Sijui Tanganyika (Tanzania Bara) ambayo hamuelewi kama ipo ama imezimia.
 

Mkuu wa Medani! Shamhuna VP?!!!!!!!!! Was it planned by JK and his Team or?

Tunashukuru kusikia haya ila bado hilo halimnyimi nguvu ya kupiga kelele , mind u mtaalam ana machungu ya kutoswa NEC hivyo the only way ya yeye ku survive ktk siasa za Zenj ni kugusa area zote sensitive kila anapopata mwanya.

Tuipende nchi yetu kwa hoja za kujenga na si kutishana.
 
Mkuu Field Marshall ES.

Nakuongezea... President wa Zanzibar... ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Muungano.

Mkuu Kasheshe,

Hivi ndivyo nijuavyo siku zote, na ndio maana Salimin alipokuwa rais wa Zanzibar kwa kushauriwa na Raza, hakuhudhuria kikao hata kimoja cha Baraza la Mawaziri kwa kutokubaliana na hiki kipengere cha kwenda cabinet kama waziri, lakini hakujaribu hata mara moja kuibadili hii sheria,

Wa-Zanzibari wasitutingishie kibiriti sisi wananchi wa bara on this ishu ya Muungano, kwa sababu we have absolutely nothing to do na hiyo misery yao na Muungano, sisi wananchi sio viongozi kwamba watatu-bully kama walivyowafanyia viongozi wa CCM Butiama,

Nyinyi wananchi wa Visiwani, get this straight kwamba Zanzibari ni mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama mnataka kuibadili hiyo inabidi mtumie sheria sio kupiga piga makelele kwenye migahawa na kashata, sisi huku forum hatuwezi kuwasaidia anything, kwa sababu hapa tuna mawe tu na fimbo hatuna peremende, wala tende, nendeni mkapigie kelele viongozi wa juu huko CCM.

Ahsanteni Sana.
 
MAMBO sivyo yalivyo BABA, MATAKWA YAKO YAWEKE KWAKO.

Mkuu it not about matakwa yangu au yako, ni about sheria kupiga kelele zako hapa forum ni the wrong place, sisi wananchi wa Bara pia tumechoshwa na never ending nonesense, matakwa yako kwenye muungano hayawezi kutatuliwa hapa forum hata urushe maneno kiasi gani, hapa utapewa facts tu za muungano kama zilivyo,

Nazo ni kwamba nchi yako ni mkoa ndani ya muungano, FULL STOP!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…