Mfamaji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 6,630
- 1,945
Acheni jazba ,inaonekana hata humu mumepoteza muelekeo na sasa ni wazi uzalendo wa Utanganyika unawaandama japo wengine mnaota kuwa Tanganyika ilikwisha kufa,hao siwezi kuwaelewesha ni sawa na kumtambua mwendawazimu aliepona na kumpa uhuru.
Hizi serikali mbili ni tofauti ,na kila serikali ina mamlaka yake na mipaka yake ,sasa inapohojiwa kuwa Je serikali ya Muungano ina mamlaka juu ya serikali ya Zanzibar ,msiwe na pupa na kukurupuka na kujijibu wenyewe ,maana mnajiuliza halafu mnajijibu ,kwa nini msitazame mipaka ya serikali hizi ? Mimi sitaki kuweko upande wenu kwa mnayoyaona mambo haya ni mepesi na hivyo mnajibu vile mnavyojiuliza wenyewe ,very interesting !
Sijui Mwakiyembe ni Mwanasheria atulie na hawezi kujibu hoja hizi za viongozi wa Zanzibar maana ni za kipumbavu, nilisema katika ile topik ya Mwakiyembe ndie aliekuwa hana adabu ,maana amevunja hata amri ya Spika ,mnakuja na kuhoji eti nikatazame nukuu za Bunge , mimi si mwana siasa wala mwanasheria ni mlala hoi tu,lakini kauli ya Mwakiyembe at the first hearingi niliiona amekwisha kosea kwa maneno aliyotumia ,haihitaji misamiati mingi kuielezea na nilisema Mwakiyembe akibanwa basi atakuwa matatani kwa kauli aliyotumia hasa maneno au lugha chafu ,nikatoa Chalenge ,yatazamwe maneno aliyosema Shamhuna na aliyosema Mwakiyembe ,mnaposikia kila ngoma ikivuma ndipo inapokaribia kupasuka ,Mwakiyembe amepasuka na sasa hafai na ametoa mtihani mwengine kwa Bunge na Raisi Kikwete ,japo kwa mtazamo wenu mnaona hana kosa ,lakini sivyo Mwakiyembe ametenda kosa tena baya zaidi hata kuliko wale wanaosema Zanzibar si nchi.
Ninachowataka msiingie katika kujigawa mkaona labda Mwiba niMpemba Mzanzibari anatetea WaZanzibari na Mwakiyembe ni mwenzetu Chogo basi tumlinde ,mtakuwa mnakosea , mimi ninaweza kuwa bora kwa Mwakiyembe kuliko nyinyi mnaojidai kumlinda na kumkazania ashike na kusimamia msimamo wake ,hamumtakii mwema Mwakiembe , mmesikia mmoja alipohojiwa kuhusu madai ya Zanzibar na kauli ya Mwakiyembe na taratibu za Bunge ,jamaa alijibu waandishi nendeni katafuteni ,soma hiki kipande :-
...Naye Naibu Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda alipoulizwa kuhusu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu shinikizo anazopewa Dkt. Mwakyembe, alimtaka mwandishi azitafute ili ajionee mwenyewe... Umeona ustadi wa kukwepa suala ,huyu Bibi Anne ameshaona tatizo linalomnyemelea Mwakiyembe.
Ushauri wa bure kwa Mwakiyembe ,awaombe radhi ikiwa anajiona ana kosa au hana kosa na atakuwa amefunga mjadala kiustaarabu kabisa.Mwakiyembe afahamu kuwa yeye ni mbunge na natumai anaifahamu CCM vilivyo ,Mwakiyembe amegusa sega ,sega ambalo linawanufaisha magogo wa CCM bara , natumai mtaiona factor na hatari inayoplay kwa Mwakiyembe.
'Anger is a condition whereby the mounth works faster than the brain'
Inaelekea ulikwa unaandika kama vile unvyoongea upupu huko Bungeni. Rekebisha hiyo text tuweze kuisoma .Otherwise semi iliteracy may just mean it.