on the other hand , hautusaidii lolote wazanzibari zaidi ya kuturudisha nyuma.Muungano ni mzigo kwa tanganyika bora uvunjike wabaki na Zanzibar yao
ah rev. hivi wazanzibari hawajajaribu kujitoa lakini nyinyi mkawang'ang'ania au ushasahau sakata la aboud jumbe na nyerere?, na badili ya yote si mmetunyang'anya mpaka sauti bwana, linaloamuliwa dodoma ndilo linalotendeka au ushasahau wazanzibari tulipomchagua dk bilal lakini dodoma wakamchagua karume?Ngekewa,
Usitafune mawe hapa! Kama Wazanzibari wameuchoka Muungano kwa nini wasijitoe? mbona mwanyoosha vidole ati?
Kama mmedhulumiwa na kudhalilishwa, kinaashinda nini kuamka sikumja na kusema Muungano sasa basi na kutoa talaka? kwa nini ubabaishaji wa maneno?
well said bro rev. huyu ccm kujiunganisha bara na visiwani na akatawala nchi nzima na akazilazimisha sera zake za kichama ndani ya serikali ya muungano bila kujali wananchi basi pia ni mmoja kati ya wachawi wa muungano tunaowatafutaUnajua kwa mfumo wa sasa na jinsi CCM ilivyo, Uraisi wa Zanzibar hauna maana yeyote kama NEC na CC zitakaa na kumshurtisha unless aamue kuvunja Muungano.
Huku kudinda kwa Karume, Shamhuna na wengine wafanyie kelele Serikalini wakifika katika chama, kende zitasinyaa. Sasa hapo ndipo mujiulize ni nani mwenye nguvu!
Mheshimiwa Kichuguu nakuomba uweke mbali unazi wako na utafakari kilichozungumzwa.
Kimuundo Tanzania ina Serikali mbili ile ya Muungano ambayo itashughulikia masuala ya muungano na masuala ya jamhuri ya iliyokuwa Tanganyika na Serikali ya pili ni SMZ ambayo itashughulikia mambo ya Zanzibar.
Katika Serikali ya Muungano kutakuwa na Waziri Mkuu ambaye ataongoza mambo ya Muungano na yale ya Tanganyika. Huyu Bwana Bosi wake ni Rais wa Muungano ambaye ndie kiongozi wa Muungano. Kimakubaliano ni kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa Kiongozi Mkubwa kwa Tanzania namba mbili akizidiwa na Rais pekee.
Rais wa Zanzibar atakuwa na mamlaka kamili juuu ya Zanzibar na Rais wa Muungano hatoweza kufanya kitu chochote kwa Zanzibar bila kumshauri huyu Rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar ana Baraza lakw la Mawaziri na Serikali yenyewe ina Baraza lake la Kutunga Sheria ambalo Kiongozi wake ni Waziri Kiongozi. Sasa ukubwa wa Waziri Mku kwaZanzibar uko wapi?
Mkorogeko wa mambo upo kwa ile hatuwa ya kuunganisha vyama na wakati wa hatamu za chama mkorogo ulikuwa mkubwa na ndio maana mambo mengi ya kuimaliza Zanzibar yalifanywa kwa jina la CCM.
Wakati umeshabadilika na Wazanzibari wameamuwa kutaka muungano kama ulivyokubaliwa awali sasa tatizo nini wenzetu kututukana na kutuona maaduwi badala ya kufurahia kuwa tunataka Muungano utakaoondowa migogoro ya kila siku? KUWENI FAIR sisi ni nchi mbili tulioamuwa kuungana basi matakwa ya kila upande yatapatikana kwa mijadala na mashauriano.
Mkuu haya maneno mazito sana na lazima hawa viongozi waliodandia Muungano wapate kujua hivyo...Sina ushabiki wowote, ila nadhani tumeshakomaa kitaifa kutambua kuwa tunatawaliwa kwa sheria za nchi, na Katiba ya nchi ndiyo sheria kuu ya nchi. Niliyoongea ni kufuata Katiba ya nchi na siyo swala la makubaliano ya watu wawili. Nchi hii ina katiba moja tu ambayo ndiyo inayofanya kazi Zanazibar na Bara. Katiba hiyo inamuweka rais wa zanzibar kuwa mtu wa nne kwenye baraza la mawaziri baada ya Rais wa Jamhuri, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kama ambavyo Rais, na makamu wake wanavyofanya kazi Zanzibar na Bara, vile vile Waziri Mkuu ni wa jamhuri ya Muungano wote kutokea bara hadi Zanzibar. Ni kweli kuwa kuna mambo kadhaa ya Zanzibar hawezi kuyaingilia kwa vile siyo ya Muungano. Swala la kutetea katiba ni la Muungano na ni jukumu la viongozi wote wawe wa Zanzibar au wa bara kwa vile wako madarakani chini ya Katiba hiyo. Wakati Pinda alipokuwa akitetea Katiba alikuwa akifanya hivyo kama Kiongozi wa Muungano na hivyo Shamhuna alitakiwa kumtii Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano.
Waislamu Z'bar kuandamana kutetea 'nchi'
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
WANAHARAKATI wa Kupigania na Kuendeleza Uislamu visiwani hapa wamekasirishwa na kile walichodai kauli za baadhi ya viongozi wa Tanganyika kudai Zanzibar si nchi na kueleza kuwa kauli hizo zinahatarisha Muungano, kuidhalilisha Zanzibar na Waislamu kwa ujumla .
Hayo yalisemwa na Amiri Faridi wakati akitoa waadhi kwa maelfu ya Waislamu waliohudhuria katika Ijitimai ya Kimataifa iliyofanyika katika Viwanja vya Tabligh Fuoni, Migombani mjini hapa.
Alisema wale wote wanaosema kuwa Zanzibar si nchi wana kijicho na nchi hiyo kwani ilikuwa inatambulika ulimwenguni kote, hivyo lengo lao ni kuifuta katika ramani ya dunia.
Alisema sababu nyingine ya kutolewa kauli hizo ni kwamba asilimia 99.99 ya Wazanzibari ni Waislamu ikilinganishwa na Tanganyika, hivyo wale wote ambao si Waislamu hawapendelei kuona Uislamu unaimarika visiwani ndio maana wanafanya hila kuwadhalilisha Waislamu visiwani humo.
Amiri Faridi, alidai kuwa tangu kuasisiwa Muungano wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hajamsikia kiongozi yeyote wa ngazi za juu akiikashifu Zanzibar wazi wazi kama alivyofanya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Mbunge wa Kyela, Dkt. Harson Mwakyembe , Kadinali Pengo na Mwenyekiti wa CEGODETA, Bw.Thomas Ngawaiya na kuwataka Waislamu kukataa kile alichodai, kutukaniwa nchi yao.
Amiri huyo aliongeza kuwa hata Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere hakudiriki hata siku moja kusimama bungeni au sehemu yeyote ile na kuitukana Zanzibar kwa kusema kuwa si nchi.
Aidha alisema licha ya viongozi wa kidini kutakiwa kutozungumzia, siasa alisema kwa vitendo vya kuidhalilisha Zanzibar hawawezi kukaa kimya daima na wako tayari kujitoa muhanga kwa lolote .
"Takbiri ,Takbiri! Watukufu wa Kiislamu Zanzibar inahitaji kutolewa muhanga tena wa vitendo na si wa kauli vinginevyo hawa jamaa zetu wa Tanganyika wataendelea kuwatukana Wazanzibar, ambao ni Waislamu, Bora watuue sote ila Zanzibar ibakie kuwa nchi ...Waislamu muko tayari kujitoa muhanga kwa nchi yenu Inshaalah," alihamasisha Amiri Faridi.
Amiri huyo amemtaka Waziri Mkuu na wenzake waache mara moja kuingilia kati mambo ya Zanzibar kwani Zanzibar ni nchi kamili ina Rais wake na Waziri Kiongozi wake ambaye amesema ni sawa sawa na Waziri Mkuu wa Tanzania.
Alimhakikishia Rais Amani Karume na serikali yake kuwa Waislamu wako tayari kutetea nchi yao mpaka kieleweke kwani jambo hilo si tusi kwa chama, serikali au kundi fulani la watu bali ni la Wazanzibari wote.
Alisema kama Watanganyika wako tayari kuendelea na Muungano, basi uasisiwe upya ili pasiwepo manung'uniko ya upande mmoja unaonewa.
Hata hivyo amemuomba Rais Karume kukaa pamoja na Rais Jakaya Kikwete ili kulipatia ufumbuzi suala hilo pamoja na kuitaka serikali na Jeshi la Polisi nchini kuwakubalia Waislamu wa Zanzibar kufanya maandamano makubwa ya amani ya kutetea nchi yao.
Wakati Amiri Faridi akiyasema hayo, tayari jana yake Serikali ya Mapinduzi (SMZ) ilitoa msimamo wake wa kumtaka Dkt. Mwakyembe kuacha mara moja tabia ya kuwatukana Viongozi wa Zanzibar kwa kuwa hakuna sheria yeyote inayoonesha kuwa Serikali ya Muungano iko juu SMZ.
Bora ufe kwakweli hata mie sioni faida ya kiuchumi wa muungano
Aliyeapa na kupewa dhamana bado amelala akiamka hataikuta Tanzania. Hivi pamoja na system yetu ambayo ilijengeka ilikuwaje tukampata huyu SI?
Kichuguu,
Mkuu sasa hivi nchi imekoa mwelekeo kabisaaaaa! utasikia swala hili ni la Wakurya mara Waislaam yaani sasa hvi nchi yetu imefikia mahala tunaanza kujitazama kwa rangi zetu. Nimeyaona hata hapa JF watu wanaandika vitu kwa rangi zao ni hatari kubwa sana na Kikwete atakuwa na wakati mgumu sana kuzima moto kama huu.
Hayo maandamano ya Zanzibar kama yatapewa kibali basi mkuu wa Polisi na yeyote yule aliyetoa kibali wafukuzwe kazi haraka sana...
Tumeisha sema kama wanataka kujitenga dawa ni kuwasilisha muswada wa referendum tena basi watapata kura nyingi kutoka bara wala wasiwe na wasiwasi na kamba za CCM.. wananchi wa bara wamemchoka mke huyu...
Leo hii mimi ukiniuliza status yangu badala ya kuuliza kama niko single ukauliza kama niko independent (kunitega) naweza kabisa kujibu No... I'm married kwa kuelewa kwamba hoja yako ilikuwa inalenga kujua nafasi yangu ktk ndoa!..
Mimi nachotaka kuelewa hawa Wazanzibar kina Shamhuna kama wanakubaliana na maelezo ya mbunge mmoja wa Visiwani aliyesema kwamba Waziri mkuu kateleza tu lakini Zanzibar ni nchi isipokuwa sio Taifa akiwa na maana Taifa ni eneo la Jamhuri ya Muungano!..
Kama wanakubaliana na hilo basi Zanzibar ni nchi na tuone kama itabadilisha kitu zaidi ya ku amend katiba kutoa maandishi ya nchi na kuweka Taifa, haitawaongezea kitu.
mwakanjuki ni mmoja wa wanasiasa wa zanzibar waliowahi kukanwa kwa madai kuwa yeye si mzenj halali bali ni mnyakyusa wa bara; iko kazi kweli kweli.