Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Ngekewa,

Usitafune mawe hapa! Kama Wazanzibari wameuchoka Muungano kwa nini wasijitoe? mbona mwanyoosha vidole ati?

Kama mmedhulumiwa na kudhalilishwa, kinaashinda nini kuamka sikumja na kusema Muungano sasa basi na kutoa talaka? kwa nini ubabaishaji wa maneno?
ah rev. hivi wazanzibari hawajajaribu kujitoa lakini nyinyi mkawang'ang'ania au ushasahau sakata la aboud jumbe na nyerere?, na badili ya yote si mmetunyang'anya mpaka sauti bwana, linaloamuliwa dodoma ndilo linalotendeka au ushasahau wazanzibari tulipomchagua dk bilal lakini dodoma wakamchagua karume?
 
Unajua kwa mfumo wa sasa na jinsi CCM ilivyo, Uraisi wa Zanzibar hauna maana yeyote kama NEC na CC zitakaa na kumshurtisha unless aamue kuvunja Muungano.

Huku kudinda kwa Karume, Shamhuna na wengine wafanyie kelele Serikalini wakifika katika chama, kende zitasinyaa. Sasa hapo ndipo mujiulize ni nani mwenye nguvu!
well said bro rev. huyu ccm kujiunganisha bara na visiwani na akatawala nchi nzima na akazilazimisha sera zake za kichama ndani ya serikali ya muungano bila kujali wananchi basi pia ni mmoja kati ya wachawi wa muungano tunaowatafuta
 
Mheshimiwa Kichuguu nakuomba uweke mbali unazi wako na utafakari kilichozungumzwa.

Kimuundo Tanzania ina Serikali mbili ile ya Muungano ambayo itashughulikia masuala ya muungano na masuala ya jamhuri ya iliyokuwa Tanganyika na Serikali ya pili ni SMZ ambayo itashughulikia mambo ya Zanzibar.

Katika Serikali ya Muungano kutakuwa na Waziri Mkuu ambaye ataongoza mambo ya Muungano na yale ya Tanganyika. Huyu Bwana Bosi wake ni Rais wa Muungano ambaye ndie kiongozi wa Muungano. Kimakubaliano ni kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa Kiongozi Mkubwa kwa Tanzania namba mbili akizidiwa na Rais pekee.
Rais wa Zanzibar atakuwa na mamlaka kamili juuu ya Zanzibar na Rais wa Muungano hatoweza kufanya kitu chochote kwa Zanzibar bila kumshauri huyu Rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar ana Baraza lakw la Mawaziri na Serikali yenyewe ina Baraza lake la Kutunga Sheria ambalo Kiongozi wake ni Waziri Kiongozi. Sasa ukubwa wa Waziri Mku kwaZanzibar uko wapi?
Mkorogeko wa mambo upo kwa ile hatuwa ya kuunganisha vyama na wakati wa hatamu za chama mkorogo ulikuwa mkubwa na ndio maana mambo mengi ya kuimaliza Zanzibar yalifanywa kwa jina la CCM.
Wakati umeshabadilika na Wazanzibari wameamuwa kutaka muungano kama ulivyokubaliwa awali sasa tatizo nini wenzetu kututukana na kutuona maaduwi badala ya kufurahia kuwa tunataka Muungano utakaoondowa migogoro ya kila siku? KUWENI FAIR sisi ni nchi mbili tulioamuwa kuungana basi matakwa ya kila upande yatapatikana kwa mijadala na mashauriano.


Sina ushabiki wowote, ila nadhani tumeshakomaa kitaifa kutambua kuwa tunatawaliwa kwa sheria za nchi, na Katiba ya nchi ndiyo sheria kuu ya nchi. Niliyoongea ni kufuata Katiba ya nchi na siyo swala la makubaliano ya watu wawili. Nchi hii ina katiba moja tu ambayo ndiyo inayofanya kazi Zanazibar na Bara. Katiba hiyo inamuweka rais wa zanzibar kuwa mtu wa nne kwenye baraza la mawaziri baada ya Rais wa Jamhuri, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kama ambavyo Rais, na makamu wake wanavyofanya kazi Zanzibar na Bara, vile vile Waziri Mkuu ni wa jamhuri ya Muungano wote kutokea bara hadi Zanzibar. Ni kweli kuwa kuna mambo kadhaa ya Zanzibar hawezi kuyaingilia kwa vile siyo ya Muungano. Swala la kutetea katiba ni la Muungano na ni jukumu la viongozi wote wawe wa Zanzibar au wa bara kwa vile wako madarakani chini ya Katiba hiyo. Wakati Pinda alipokuwa akitetea Katiba alikuwa akifanya hivyo kama Kiongozi wa Muungano na hivyo Shamhuna alitakiwa kumtii Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano.

Katiba ya kwanza ya mwaka 1964 ilikuwa inampa madaraka ya pili kiongozi wa Zanzibar wakati huo akiwa anajulikana kama Makamu wa Kwanza wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, hakuwa akiitwa Rais wa Zanzibar wakati huo. Mabadiliko ya katiba yaliyofanyika baada Sheikh Karume kufariki ndiyo yaliyoleta Baraza la Wawakilishi na kuweka cheo cha Rais wa Zanzibar, ambaye eliendelea kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, akiwa na madaraka ya pili baada ya Rais. Mabadiliko ya kikatiba yaliyotokea baada ya kuanza kwa mafumo wa vyama vingi yalipunguza sana madaraka ya Rais wa zanzibar na kumfanya mtu wa nne. Kilichotokea hapa ni kuwa endapo Rais akiwa wa bara basi makamu wake lazima awe ni mzanzibari, na endapo rais atatoka zanzibar basi makamu wake atakuwa ni mbara, Rais wa Zanzibar siyo Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano tena. Mfumo huu unaipendelea sana zanzibar kwa vile rais wa jamhuri anaweza kumteua Waziri mkuu kutoka sehemu yoyote ya Muungano. Na Hivyo endapo Rais atatoka zanzibar, na makamu wake kutoka Bara, bado rais anaweza kumteua waziri Mkuu kutoka zanzibar na hivyo kufanya nafasi tatu kubwa kwenye kabineti kuwa zimechukuliwa na wazanzibar, wakiacha nafasi moja tu kwa watu wa bara. Najua watu wa bara hawajawahi kulalamikia muundo huo ambao uko unaipendelea Zanzibar, ni dhahiri ungelalamikiwa sana na wazanzibar kama ungekuwa unaipendelea Bara.

Makosa anayofanya Shamhuna kama kiongozi wa nchi ni kukiuka katiba ile ile iliyomuweka madarakani, hilo ni kosa kubwa sana. Kama wanataka kuindoa Zanzibar kutoka kwenye Muungano na hivyo kutotumia Katiba hii iliyopo, ni lazima watafute utaratibu wa kusimamisha matumizi ya katiba hii kisheria ndipo taratibu za kujiondoa zifuatwe. Lakini kuendesha maneno ya uchochezi kama anavyofanya Shamhuna huku akiwa bado yuko chini ya katiba hiyo hiyo anayokiuka ni kuvunja sheria kuu ya nchi na unaweza kuwa uhaini pale anapokana madaraka ya viongozi halali wa kikatiba na kutaka ajitwike madaraka yao.
 
Kichuguu,
Sina ushabiki wowote, ila nadhani tumeshakomaa kitaifa kutambua kuwa tunatawaliwa kwa sheria za nchi, na Katiba ya nchi ndiyo sheria kuu ya nchi. Niliyoongea ni kufuata Katiba ya nchi na siyo swala la makubaliano ya watu wawili. Nchi hii ina katiba moja tu ambayo ndiyo inayofanya kazi Zanazibar na Bara. Katiba hiyo inamuweka rais wa zanzibar kuwa mtu wa nne kwenye baraza la mawaziri baada ya Rais wa Jamhuri, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kama ambavyo Rais, na makamu wake wanavyofanya kazi Zanzibar na Bara, vile vile Waziri Mkuu ni wa jamhuri ya Muungano wote kutokea bara hadi Zanzibar. Ni kweli kuwa kuna mambo kadhaa ya Zanzibar hawezi kuyaingilia kwa vile siyo ya Muungano. Swala la kutetea katiba ni la Muungano na ni jukumu la viongozi wote wawe wa Zanzibar au wa bara kwa vile wako madarakani chini ya Katiba hiyo. Wakati Pinda alipokuwa akitetea Katiba alikuwa akifanya hivyo kama Kiongozi wa Muungano na hivyo Shamhuna alitakiwa kumtii Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano.
Mkuu haya maneno mazito sana na lazima hawa viongozi waliodandia Muungano wapate kujua hivyo...
Hivi kweli wanashindwa kujiuliza kwa nini Wabunge wao wapo Bungeni Dodoma na swali la Zanzibar limeulizwa Dodoma na sio Bunge la Unguja?..mbona majibu yao yanazidi kuonyesha jinsi walivyo finyu kufikiria..
Hapa wanachoshindwa kuelewa kuwa sio hoja nani ni nani na anaingilia mambo gani. Majibu ya Waziri mkuu yalikuwa kuhusiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano na huyo Shamhuna hakuwepo wala swali halikuwakilishwa kwake kwa sababu yeye hana madaraka ya kujibu isipokuwa Waziri mkuu, Hilo kwanza na kinachotakiwa yeye Shemhuna aombe msamaha ni kutokana na utovu wa adabu kutoheshimu Muungano na katiba ya Muungano huo...
Unajua inanipa picha ya Zitto, akijibu swala lolote linalohusiana na Buzwagi, mbunge mmoja asimame na kusema wewe ni mbunge wa Kigoma haya maswala ya Buzwagi yanakuhusu nini wakati huna hata mamlaka wizara ya madini..
Hii issue ya Zanzibar haina wizara ya Zanzibar wala bara! na wala haina mkubwa nani hata kama angejibu Malecela kwa kutumia katiba hainge badilisha ukweli.. Ni wakati watu kama hawa wawajibishwe tuone kama kweli serikali ya Muungano haina nguvu visiwani.. Wamuulize Jumbe! si alikuwa rais? yuko wapi...
 
Brigedia Mwakanjuki: Zanzibar ni nchi

na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

ALIYEKUWA Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Brigedia Jenerali (mstaafu) Adam Mwakanjuki, ameibuka na kusema Zanzibar ni nchi na anakerwa na wanaopinga ukweli huo.

Mwakanjuki, mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za visiwani Zanzibar, alisema hatua ya baadhi ya watu na viongozi kusema Zanzibar si nchi haina maana, kwani ina kila kitu kinachofanya ijitawale yenyewe.

Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalumu Dar es Salaam, jana, Mwakanjuki alisema Zanzibar ni nchi kamili ambayo haipaswa kujadiliwa kwa vile haoni sababu ya kuanzisha malumbano yasiyo na tija.

“Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi kamili ambayo imejitosheleza kwa kila kitu. Sasa hawa wanaosema si nchi hawana jipya…hii ni dola ukizingatia tuna Rais anayechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na wananchi,” alisema Mwakanjuki.

Alisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi kwa sababu mawaziri wake huteuliwa na Rais wa SMZ na kuwaapisha kwa kutumia katiba ya Zanzibar.

“Hapa tuna mawaziri wanaoteuliwa na Rais wa SMZ, ambao wametokana na Wazanzibari kuwapigia kura na kuwaapisha kwa kutumia katiba yetu, sasa hapa tatizo liko wapi …hii ni nchi ambayo pia ina Waziri Kiongozi aliye mtendaji mkuu wa shughuli za SMZ,” alisema.

Alisema amekuwa kiongozi wa SMZ kwa muda mrefu, anaielewa vyema historia yake tangu mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zilipoungana, hivyo hatua ya kuhoji hadhi ya Zanzibar kwa sasa si jambo la busara.

“Napenda kusisitiza tena kwamba hii ni nchi, nimekuwa muda mrefu kwenye SMZ, mimi ni mmoja wa watu tunaoielewa vyema historia yake tangu mwaka 1964, sasa nashangaa kuona mambo kama haya yanaibuka, hayasaidii kuleta maendeleo,” alisema Mwakanjuki.

“Nina uchungu sana na watu wanaosema Zanzibar si nchi, mimi hadi sasa ni waziri lakini niko kwenye mapumziko kutokana na matatizo yaliyonipata…sisi tunaendelea na mipango yetu ya kuijenga nchi yetu,” Mwakanjuki alisema.

Alisema pamoja na mzozo huo, bado kuna matatizo ya Muungano ambayo alisema yanapaswa kushughulikiwa haraka.

“Hili si tatizo kubwa, bado kuna matatizo mengi ya Muungano ambayo tunaamini yako pale pale yanahitaji kumalizwa haraka kwa manufaa ya pande mbili,” alimalizia.

Mwakanjuki ni mmoja wa wanasiasa wanaheshimika sana na amekuwa na mchango mkubwa ndani ya SMZ.
 
Hebu Ona Uchochezi mwingine huu hapa. waislamu wanahusikaje na Muungano? Kwani Bara hakuna waislamu?

Waislamu Z'bar kuandamana kutetea 'nchi'
Na Mwandishi wetu, Zanzibar

WANAHARAKATI wa Kupigania na Kuendeleza Uislamu visiwani hapa wamekasirishwa na kile walichodai kauli za baadhi ya viongozi wa Tanganyika kudai Zanzibar si nchi na kueleza kuwa kauli hizo zinahatarisha Muungano, kuidhalilisha Zanzibar na Waislamu kwa ujumla .

Hayo yalisemwa na Amiri Faridi wakati akitoa waadhi kwa maelfu ya Waislamu waliohudhuria katika Ijitimai ya Kimataifa iliyofanyika katika Viwanja vya Tabligh Fuoni, Migombani mjini hapa.

Alisema wale wote wanaosema kuwa Zanzibar si nchi wana kijicho na nchi hiyo kwani ilikuwa inatambulika ulimwenguni kote, hivyo lengo lao ni kuifuta katika ramani ya dunia.

Alisema sababu nyingine ya kutolewa kauli hizo ni kwamba asilimia 99.99 ya Wazanzibari ni Waislamu ikilinganishwa na Tanganyika, hivyo wale wote ambao si Waislamu hawapendelei kuona Uislamu unaimarika visiwani ndio maana wanafanya hila kuwadhalilisha Waislamu visiwani humo.

Amiri Faridi, alidai kuwa tangu kuasisiwa Muungano wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hajamsikia kiongozi yeyote wa ngazi za juu akiikashifu Zanzibar wazi wazi kama alivyofanya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Mbunge wa Kyela, Dkt. Harson Mwakyembe , Kadinali Pengo na Mwenyekiti wa CEGODETA, Bw.Thomas Ngawaiya na kuwataka Waislamu kukataa kile alichodai, kutukaniwa nchi yao.

Amiri huyo aliongeza kuwa hata Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere hakudiriki hata siku moja kusimama bungeni au sehemu yeyote ile na kuitukana Zanzibar kwa kusema kuwa si nchi.

Aidha alisema licha ya viongozi wa kidini kutakiwa kutozungumzia, siasa alisema kwa vitendo vya kuidhalilisha Zanzibar hawawezi kukaa kimya daima na wako tayari kujitoa muhanga kwa lolote .


"Takbiri ,Takbiri! Watukufu wa Kiislamu Zanzibar inahitaji kutolewa muhanga tena wa vitendo na si wa kauli vinginevyo hawa jamaa zetu wa Tanganyika wataendelea kuwatukana Wazanzibar, ambao ni Waislamu, Bora watuue sote ila Zanzibar ibakie kuwa nchi ...Waislamu muko tayari kujitoa muhanga kwa nchi yenu Inshaalah," alihamasisha Amiri Faridi.

Amiri huyo amemtaka Waziri Mkuu na wenzake waache mara moja kuingilia kati mambo ya Zanzibar kwani Zanzibar ni nchi kamili ina Rais wake na Waziri Kiongozi wake ambaye amesema ni sawa sawa na Waziri Mkuu wa Tanzania.

Alimhakikishia Rais Amani Karume na serikali yake kuwa Waislamu wako tayari kutetea nchi yao mpaka kieleweke kwani jambo hilo si tusi kwa chama, serikali au kundi fulani la watu bali ni la Wazanzibari wote.

Alisema kama Watanganyika wako tayari kuendelea na Muungano, basi uasisiwe upya ili pasiwepo manung'uniko ya upande mmoja unaonewa.

Hata hivyo amemuomba Rais Karume kukaa pamoja na Rais Jakaya Kikwete ili kulipatia ufumbuzi suala hilo pamoja na kuitaka serikali na Jeshi la Polisi nchini kuwakubalia Waislamu wa Zanzibar kufanya maandamano makubwa ya amani ya kutetea nchi yao.

Wakati Amiri Faridi akiyasema hayo, tayari jana yake Serikali ya Mapinduzi (SMZ) ilitoa msimamo wake wa kumtaka Dkt. Mwakyembe kuacha mara moja tabia ya kuwatukana Viongozi wa Zanzibar kwa kuwa hakuna sheria yeyote inayoonesha kuwa Serikali ya Muungano iko juu SMZ.
 
eacart180808.jpg
 
Kichuguu,
Mkuu sasa hivi nchi imekoa mwelekeo kabisaaaaa! utasikia swala hili ni la Wakurya mara Waislaam yaani sasa hvi nchi yetu imefikia mahala tunaanza kujitazama kwa rangi zetu. Nimeyaona hata hapa JF watu wanaandika vitu kwa rangi zao ni hatari kubwa sana na Kikwete atakuwa na wakati mgumu sana kuzima moto kama huu.
Hayo maandamano ya Zanzibar kama yatapewa kibali basi mkuu wa Polisi na yeyote yule aliyetoa kibali wafukuzwe kazi haraka sana...
Tumeisha sema kama wanataka kujitenga dawa ni kuwasilisha muswada wa referendum tena basi watapata kura nyingi kutoka bara wala wasiwe na wasiwasi na kamba za CCM.. wananchi wa bara wamemchoka mke huyu...

Leo hii mimi ukiniuliza status yangu badala ya kuuliza kama niko single ukauliza kama niko independent (kunitega) naweza kabisa kujibu No... I'm married kwa kuelewa kwamba hoja yako ilikuwa inalenga kujua nafasi yangu ktk ndoa!..

Mimi nachotaka kuelewa hawa Wazanzibar kina Shamhuna kama wanakubaliana na maelezo ya mbunge mmoja wa Visiwani aliyesema kwamba Waziri mkuu kateleza tu lakini Zanzibar ni nchi isipokuwa sio Taifa akiwa na maana Taifa ni eneo la Jamhuri ya Muungano!..
Kama wanakubaliana na hilo basi Zanzibar ni nchi na tuone kama itabadilisha kitu zaidi ya ku amend katiba kutoa maandishi ya nchi na kuweka Taifa, haitawaongezea kitu.
 
Kwa swala la Muungano nashauri tusitumie jazba, busara zetu zinahitajika hapa. Nakubali kwamba kuna matatizo mengi kwenye muungano wetu ila nionavyo huu ni wakati mzuri wa kutafakari ni yapi tulikosea wapi turekebishe.

Tukubali kimsingi kwamba hatutapata faida yeyote kwa bara na visiwani kuachana, wote tutapata hasara maana kwanza tutakosa haya tuliyonayo kwa sasa. Wengi watasema kwani tunafaidi nini...?tuna faida kubwa ila tatizo faida zilizopo zinafukiwa kwa kiasi kikubwa na shida zilizopo, sawa kuna matatizo kutokana na mengi ambayo tumeyazembea kwa muda, lakini suluhu sio kumtimua nyumbani mtoto uliyemzembea akabwia unga. Shurti umfanyie tiba ingawa itakugharimu.
 
Aliyeapa na kupewa dhamana bado amelala akiamka hataikuta Tanzania. Hivi pamoja na system yetu ambayo ilijengeka ilikuwaje tukampata huyu SI?
 
Aliyeapa na kupewa dhamana bado amelala akiamka hataikuta Tanzania. Hivi pamoja na system yetu ambayo ilijengeka ilikuwaje tukampata huyu SI?

Du, kali hii: Rais wa Tanzania amelala, na akiamka atakuta hakuna Tanzania tena bali Tanganyika na Zanzibar kwa hiyo hatakuwa na nchi ya kutawala tena kwani alichaguliwa kutawala Tanzania wals siyo Tanganyika au Zanzibar .
 
Kichuguu,
Mkuu sasa hivi nchi imekoa mwelekeo kabisaaaaa! utasikia swala hili ni la Wakurya mara Waislaam yaani sasa hvi nchi yetu imefikia mahala tunaanza kujitazama kwa rangi zetu. Nimeyaona hata hapa JF watu wanaandika vitu kwa rangi zao ni hatari kubwa sana na Kikwete atakuwa na wakati mgumu sana kuzima moto kama huu.
Hayo maandamano ya Zanzibar kama yatapewa kibali basi mkuu wa Polisi na yeyote yule aliyetoa kibali wafukuzwe kazi haraka sana...
Tumeisha sema kama wanataka kujitenga dawa ni kuwasilisha muswada wa referendum tena basi watapata kura nyingi kutoka bara wala wasiwe na wasiwasi na kamba za CCM.. wananchi wa bara wamemchoka mke huyu...

Leo hii mimi ukiniuliza status yangu badala ya kuuliza kama niko single ukauliza kama niko independent (kunitega) naweza kabisa kujibu No... I'm married kwa kuelewa kwamba hoja yako ilikuwa inalenga kujua nafasi yangu ktk ndoa!..

Mimi nachotaka kuelewa hawa Wazanzibar kina Shamhuna kama wanakubaliana na maelezo ya mbunge mmoja wa Visiwani aliyesema kwamba Waziri mkuu kateleza tu lakini Zanzibar ni nchi isipokuwa sio Taifa akiwa na maana Taifa ni eneo la Jamhuri ya Muungano!..
Kama wanakubaliana na hilo basi Zanzibar ni nchi na tuone kama itabadilisha kitu zaidi ya ku amend katiba kutoa maandishi ya nchi na kuweka Taifa, haitawaongezea kitu.

Nyuma huko niliwahi kuandika kuwa Zanzibar ni nchi kwa maana ya pande la ardhi linalokaliwa na watu, wala siyo bahari isyokuwa na watu. Ila dai kuwa Zanzibar ni nchi yenye mamlaka yake binafsi ndilo linaloleta utata hapa. Hata mkoa wetu wa Tabora ni nchi kwa vile ni pande la ardhi linalokaliwa na watu, lakini ni nchi iliyo ndani ya mamlaka ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania. Ubishi unaoendelea hapa ni kuhusu mamlaka wala siyo mgawanyo wa ardhi.
 
mwakanjuki ni mmoja wa wanasiasa wa zanzibar waliowahi kukanwa kwa madai kuwa yeye si mzenj halali bali ni mnyakyusa wa bara; iko kazi kweli kweli.
 
mwakanjuki ni mmoja wa wanasiasa wa zanzibar waliowahi kukanwa kwa madai kuwa yeye si mzenj halali bali ni mnyakyusa wa bara; iko kazi kweli kweli.

So is he kissing up to the Zanzibaris or proving this issue is post Bara-Tanganyika.
 
There is only one country called United Republic Of Tanzania. Zanzibar and Tanganyika ceased to exist in 1964 April 26th. Zanzibar maintains some Autonomy; but is not a country. All countries are recognized by United Nations; Zanzibar is part of United Republic of Tanzania. Therefore Zanzibar is NOT a country.
 
I.O,
I wish you had the last word on this debate, because you have summed it up brilliantly.
 
Tatizo la CCM wanadhani WaTZ bado Bongo lala, thubutu, kwa kweli kiama kinakuja tena kwa kasi kubwa. Hili ni anguko lingine kwa chama hiki kisichokuwa makini kilichojaa ubabaishaji na wababaishaji. Hili la Zanzibar kuwa nchi nalo waliltee usanii basi tuone au walifanye ni vikao vya ndani vya chama as if CCM ina hati miliki ya nchi hii
 
Mkandara,

POLISI ipo responsible Mainland (jamhuri). Zanzibar hawana POLISI!

Hawa jamaa hata siwaelewi kabisa!
 
Back
Top Bottom