Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mkijiji sijakupata hapo wamaanisha nini mkuu?

Inabidi uwe mpenzi wa Star Trek.. kuna madubwasha ambayo ni mashine zenye conscience zimefungamana pamoja na wote wanafanya kazi kama pamoja hata wakiwa mbali; chochote mmoja anajua mwingine naye anajua kufungamana kwao si kutokana na mitambo bali a conscience of one.

sasa hawa wana uwezo wa kumchukua mwanadamu yeyote na kumfanyia kile kinachoitwa assimiliation. Na kumgeuza kuwa mtu-mashine.

Maarufu ya hao ma cyborgs (maborgu kwa Kiswakinge) ni yule Seven of Nine..(she is my favourity mwana CCM)

Voyager_Seven_of_Nine.jpg

Hapa maborgu wakiwa kwenye process ya assimilation na kujazwa itikadii za ki CCM za kibogu ili wawe na conscience of one.

3_borgs.jpg
 
NChi zinapoamua kuungana kama USA, zile nchi hugeuka na kuwa States, au mikoa ya nchi, sasa mnaosema kuwa Zanzibar sio State, au mkoa mna maana muungano wetu una tofauti na ya wenzetu?

Msijifanye politically sensitive, wakati neno lenu ni lile lile tu kuwa Zanzibar ni State au mkoa wa Tanzania, hilo halina ubishi, hayo maneno yenu ya politically kujaribu kuwa sensitive ndio yametufikisha hapa tulipo sasa hatuelewani wakati ukweli upo wazi na very clear,

Semeni ukweli kwamba Zainzibar ni state au mkoa wa Tanzania, kama kubadilisha waanze sasa ili tujua kwenye huu muungano bado nchi zilizomo zinaendelea kuwa nchi, what a muungano!

Stop kidding yourself, Zanzibar ni state ndani ya Tanzania yaani mkoa, au? Maana maneno ya Seleli yako very clear kama yangu hebu someni kule tena wakuu!
 
Mkuu labda usome maneno ya Seleli kule maana hayatofautiani na yangu mkuu! kama ni ualimu labda ujisaidie wewe mkuu, Seleli ameweka wazi nenda ujisomee mkuu elimu yabure kwua Zanibar ni mkoa ndani ya muungano, FULL STOP!
 
NChi zinapoamua kuungana kama USA, zile nchi hugeuka na kuwa States, au mikoa ya nchi, sasa mnaosema kuwa Zanzibar sio State, au mkoa mna maana muungano wetu una tofauti na ya wenzetu?

Stop kidding yourself, Zanzibar ni state ndani ya Tanzania yaani mkoa, au? Maana maneno ya Seleli yako very clear kama yangu hebu someni kule tena wakuu!

Kwani malumbano hapa yapo wapi? Nakubaliana nawe kuwa Tanzania ina states mbili. State of Zanzibar na State of Tanganyika. State of Tanganyika ina vijisehemu vyake huko kama Mwanza, Iringa, Rukwa etc. na state ya Zanzibar ina visehemu vyake kama Mkoa Mjini /Magharibi, na Kaskazini Pemba etc. Sikubaliani nawe hata siku-moja kuwa Zanzibar state ni sawa na kijisehemu kinachoitwa Mwanza. Abadan.
 
Wazenj acheni pumba

Kila kiumbe kinafahamu fika m-mewamiss waume zenu waarabu.Yakiwashinda hatuwapi John Okello mwingine.

JK vunja muungano,uwape nafasi.

Bahati yako kuwa wenye hii forum hawataki matusi. Kwani ilikuwa ni busara kukwambia kuwa na wewe umewamiss............ Pole sana Ndugu
 
Ala. Na ukianzisha Tanganyika yako kuwa tayari kuanzisha na nchi za Ziwa Victoria Republic. Nyanda za Juu Republic, Unyanyem,be Republic, bilam ya kusahau Machinga Republic. Sawa.

Tanzania Bara hawana mkwara kama hiyo umeshasikia unyanyembe inataka kujitenga?

Na je? kama BUZWAG ingekua Ungunja ,Ugunja ndio Geita harafu mwadui ndio wilaya moja unguja na Nyamongo wilaya nyingine Pemba si mngekua balaa.

Tuambiane Ukweli tu Nyerere na Karume walifahamu vizuri watu karibia wote wenye asili nyeusi wametoka KIGOMA na TABORA.harafu wengi wenye asili ya kiasia wengi wametoka OMANI Nyerere na Karume walitumia tu busara ya kawaida kuwakutanisha pamoja wana KIGOMA na wana TABORA walioporezana siku nyingi,sasa kuanza kulazimisha kujitenga ni tamaa tu ama wenye asili za OMAN hawataki .

Kama umeshafuatilia vizuri watu wa kigoma ,tabora na zanzibar wana common kitu fulani kwanza ni wajanja fulani pili wao hua wanaona kiswahili ndio kwao kimeishi.

Zanzibar na Tanzania bara watu ni wale wale tu ila walikuja wahuni tu hao waarabu akina sultani wakijikita zenji na hawa wazungu wakijikita bara.
 
Seleli ana mawazo mgando ya kuimeza Zanzibar ndani ya Muungano. Waasisi walikemea sana mawazo kama hayo. Kupiga mbiu kuimeza Zanzibar ndani ya Muungano ni kitendo cha uhaini kama vile ulivyo uasi wa kutaka kujitenga. Mheshimiwa Seleli upo?

Hivi Muungano ukivunjika who is the bigger loser????????????
 
Muungano huu una matatizo yake na mazuri yake. Sasa ifike mahala viongozi wakubali marekebisho yanayolalamikiwa kama yapo. Kwani katiba ni biblia au qurani isirekebishwe? Mbona kuna mambo mengi tu yalishatokea yaliyohitaji marekebisho yaliwezekana? Hili la muungano lina ugumu gani? Hebu ifikie mahali watanzania tuwe wawazi, wakweli na tuache siasa za kubishana, kutishana kwa mambo ambayn yanawezekana kutatuliwa.
 
Safi sana muungano ukifa. Jinsi mlivyo wavivu lazima mtakufa njaa tu!
sometime nakuwa siwaelewi ndugu zangu watanganyika, mara mnapiga kelele wapemba ndio wachapa kazi huko bongo na waliomiliki maduka makubwa2, na huyu sasa anasema wazanzibari ni wavivu. tushike lipi tuache lipi?
 
NChi zinapoamua kuungana kama USA, zile nchi hugeuka na kuwa States, au mikoa ya nchi, sasa mnaosema kuwa Zanzibar sio State, au mkoa mna maana muungano wetu una tofauti na ya wenzetu?

Msijifanye politically sensitive, wakati neno lenu ni lile lile tu kuwa Zanzibar ni State au mkoa wa Tanzania, hilo halina ubishi, hayo maneno yenu ya politically kujaribu kuwa sensitive ndio yametufikisha hapa tulipo sasa hatuelewani wakati ukweli upo wazi na very clear,

Semeni ukweli kwamba Zainzibar ni state au mkoa wa Tanzania, kama kubadilisha waanze sasa ili tujua kwenye huu muungano bado nchi zilizomo zinaendelea kuwa nchi, what a muungano!

Stop kidding yourself, Zanzibar ni state ndani ya Tanzania yaani mkoa, au? Maana maneno ya Seleli yako very clear kama yangu hebu someni kule tena wakuu!
.
ni vigumu sana muungano wa tanzania kuufananisha na muungano wa u.s.a . ili kukutaka uniweke wazi basi nakupa suali dogo sana na naomba jibu.
je zanzibar kama unaiita state basi naomba unifafanulie kitu hiki -: je hadhi ya zanzibar ni sawa na tanganyika nzima au ni sawa na mkoa mmoja tu wa tanganyika (e.g kigoma)?.
 
Mzee nipe sababu kubwa tatu kwanini Unguja na pemba sio mikoa, sio za kikatiba nataka.

Angalia idadi ya watu
Uchumi
Eneo

Asante
mimi sijaenda shule , lakini je wewe mwenzangu angalau umekwenda shule walau madarasa matano? mlipoungana na zanzibar mliungana na idadi ya watu au mliungana na nchi ya zanzibar?
 
Kwani malumbano hapa yapo wapi? Nakubaliana nawe kuwa Tanzania ina states mbili. State of Zanzibar na State of Tanganyika. State of Tanganyika ina vijisehemu vyake huko kama Mwanza, Iringa, Rukwa etc. na state ya Zanzibar ina visehemu vyake kama Mkoa Mjini /Magharibi, na Kaskazini Pemba etc. Sikubaliani nawe hata siku-moja kuwa Zanzibar state ni sawa na kijisehemu kinachoitwa Mwanza. Abadan.

Ni kweli sana Mwanza ni kubwa ki eneo kuliko zanzibar na ina watu wengi kuliko zanzibar.

Zanzibar inafanywa kama mtoto na Tanzania bara nao bila aibu wanakubali....we watu laki moja mbunge hamuoni kama ni mbinu za bara kuwafanya kama mtoto akililia pipi unampa?

Na wewe Under_age Aliyesema maduka ni ujasiri au uhodari ni nani? maduka yanayofungwa saa saba mpaka saa tisa mchana? wanaenda kulala kama sio uvivu ni nini?
 
Muda mfupi Seleli kamaliza yote,

Kwa ufupi amesema kuwa Zanzibar tukivunja muungano nao watajiingiza kwenye VITA na kuuwana wenyewe kwa wenyewe.

Au tuvunje serikali ya Zanzibar ibakie serikali moja tu!

Mi nakubaliana na hili la pili, TUWE NA SERIKALI YA MUUNGANO TU
siasa za propaganda again!
 
We Ami waziri mkuu wa Tanganyika ndo nani tena? Nchi gani hiyo inaitwa Tanganyika? Au ulikuwa na maana ya mkoa wa Tanga?. Na hakuna aliyesema Pinda ni waziri mkuu wa Zanzibar.

Duh kaazi kweli kweli ami

Sijakuelewa ami
ikisemwa waziri mkuu wa muungano ina maana waziri mkuu wa tanganyika , ni lugha ya kisiasa tu wala isikushtue. sie wazanzibari tunakuwa tunazugwa kwa kuambiwa tuna waziri kiongozi wetu, lakini mamlaka yake yanaishia chumbe hata bahari hayavuki.
 
Muungano huu una matatizo yake na mazuri yake. Sasa ifike mahala viongozi wakubali marekebisho yanayolalamikiwa kama yapo. Kwani katiba ni biblia au qurani isirekebishwe? Mbona kuna mambo mengi tu yalishatokea yaliyohitaji marekebisho yaliwezekana? Hili la muungano lina ugumu gani? Hebu ifikie mahali watanzania tuwe wawazi, wakweli na tuache siasa za kubishana, kutishana kwa mambo ambayn yanawezekana kutatuliwa.

Hata wakikubali kurekebisha watu wataendelea kudai vitu vingine.

Ni kweli Ktk muungano kuna matatizo na tatizo kubwa ni ZANZIBAR kua na serikali ndani ya SERIKALI,hili ndilo tatizo kubwa maana serikali iliyo ndani ya serikali wanataka kua serikali juu ya serikali ,hapo ndipo mimi naona ni tatizo.

Kama muungano unatakiwa kuundwa basi hiyo serikali iliyo ndani ya serikali ivunjwe tuwe na serikali moja.
Ama tuwe na serikali za majimbo mfano serikali ya jimbo la pemba,ugunja,kanda za juu kusini, kanda ya kati,kaskazini ,mashariki,kanda ya ziwa na magharibi. Harafu hizi ziwe zinaitumikia serikali kuu.Vinginevyo mimi naona hakuna muundo mwingine utakaokubarika.
 
Na wewe Under_age Aliyesema maduka ni ujasiri au uhodari ni nani? maduka yanayofungwa saa saba mpaka saa tisa mchana? wanaenda kulala kama sio uvivu ni nini?
Nasikia mzee wa kizenji anakwenda na nazi zake 10 anauza 3 ukitaka kununua zoote anasema yakhe, za kesho hizi.......Besides Zenji naona tuwape nchi yao bana kwani Bara wanafaidkika nini zaidi ya kuumia tu......
 
ikisemwa waziri mkuu wa muungano ina maana waziri mkuu wa tanganyika , ni lugha ya kisiasa tu wala isikushtue. sie wazanzibari tunakuwa tunazugwa kwa kuambiwa tuna waziri kiongozi wetu, lakini mamlaka yake yanaishia chumbe hata bahari hayavuki.

Wewe wasema!
 
Mshkaji ni reality. Zenji mmezidi kulalamika sana. Mbona sisi bara hatuna serikali lakini hatulalamiki?
ah ha ah ha , kijana unafurahisha sana . bara hamna serikali? hebu leo inamisha kichwa chako dakika kumi kisha fikiri na kisha njoo tena na urudie haya maneno kwamba bara hamna serikali.
 
Back
Top Bottom