sasa kama hawakubali ushauri na wanaamini mafuta yapo, si wachukue majembe wayachimbe? kama waliweza kumwaondoa sultan kwa silaha za jadi dhidi ya za moto, kinawashinda nini kuchimba mafuta kwa dhana za jadi? MAPINDUZI DAIMA!!!!
 
Mambo yataiva watakapoambiwa kuna mafuta kibao PEMBA! Je CUF watakubali kugawana na Unguja?
 
Tatizo la Muungano linakuwa linafichwa. Kinachoendelea huko Zanzibar kwa hao wawakilishi na hasa viongozi wa CCM Zanzibar (Afro Shiraz) ni kuutafuta umaarufu tu wa kisiasa. CCM Zanzibar wanajua kabisa hawawezi kubakia madarakani bila ya sapoti ya serikali ya JMT. Hivi nani ambaye hajui matokeo ya uchaguzi Zanzibar yamekuwa yakipikwa kwa kutumia nguvu za Bara? Hao Mawaziri wa Karume wanaopiga kelele kwamba Zanzibar ni Nchi, wana malengo makubwa ya kutafuta umarufu wa kisiasa.

Nina imani ukimuuliza mwananchi wa kawaida wa Zanzibar khs Muungano atakwambia hautaki. Hautaki sio kwa 'vijisababu' wanavyotoa akina Shamhuna. Nani ambaye hajui ubabe unaofanywa na Serikali ya JMT kwa wananchi wa Zanzibar ambao ambao haiungi mkono Afro Shiraz? Wanawake wangapi wamebakwa na Polisi waliotoka Bara kwenda kumlinda Karume na wenzake? Wanaume wangapi wamekimbia familia zao kwa sababu ya undava wa Mahita na wenzake? Wapemba wangapi waliuwawa na Serikali ya Mkapa? Wazanzibari wangapi wamekosa ajira kwa kutomshabikia Karume tu. Sasa nani atataka Muungano au ataupenda huo Muungano kwa matlaba niliyoyataja hapo juu. Karume na wenzake wanapiga kelele ili kuonesha kwa wazanzibari kuwa nao wamechoka na Muungano wakati wanajua ndio kwanza wanauhitaji kuliko wakati mwingine wowote.

Tatizo lililopo ni kwamba Karume na wenzake WAMEDEKEZWA na CCM Bara. Na hili linatokana na namna Karume alivyompa sapoti kubwa JK kuingia madarakani. Angalia Karume na wenzake walivyomchafua SAS kwa lengo la kumfanya asiingie madarakani. Karume mdogo alipandikizwa ili avuruge kura za SAS.

kihistoria Wazazibari ndio wamekuwa wakipandikiza Marais wa JMT. Mkatae msikatae marais wote wa Tanzania wamepatikana kutokana na nguvu za Wazanzibar. Kuanzia Nyerere. Karume alipokubali kuwa Makamu wa Rais ina maana aliamua kwa makusudi kumpa Nyerere Urais. Karume hakuwa na ubavu wa kuongoza Zanzibar kwa sababu yeye alikaribishwa tu kwenye serikali ya mapinduzi kwa kuwa yeye hakushiriki. Mwalimu alipeleka wanajeshi kumlinda na alipomwambia mwanzoni kuhusu kuunganisha nchi Karume alikataa. Mwalimu kwa kusaidiwa na Marekani walitishia kuyaondoa majeshi ya Tanganyika na Karume akajua kuwa hana ujanja ila kusalimu amri na kumuuzia Mwalimu nchi kwa bei poa.

Mwinyi hakuwa chaguo la Nyerere. Chaguo la Nyerere alikuwa ni SAS. Kwa msingi huo Mwalimu kumchagua SAS alikuwa anawakilisha mawazo ya watanganyika wengi lakini tunakumbuka akina Natepe walivyokuja kumzima Mwalimu na kuteletea Mwinyi JMT. Wazanzibari tena wakatuchagulia Rais.

Wazanzibari tena wakatuletea Mkapa. Kumbuka Salmini mwanzoni hakuwataka Mkapa na JK hivyo kura zake na wenzake walimpa Msuya. Walipokuja kugombanishwa Ben na JK kura za 'kujazia' za Salmini na wenzake akapewa Ben. Salmini hawakuwa na mahusiano mazuri na JK hasa pale walipokuwa watumishi wa CCM. Wazanzibar tena wakatutafutia Rais.

Akaja JK. Naye akaletwa na Wazanzibari. JK akijua namna Karume alivyokuwa hawaivi na Salmini aliamua kumpiga tafu kubwa kwenye vikao vya juu vya CCM. Kumbuka kwenye uchaguzi wa Rais wa Zanzibar Karume alikuwa ni wa tatu kwenye mapendekezo ya Kamati Maalum ya CCM Zanzibar akitanguliwa na Bilal na Amina Salum Ali. Kwenye vikao vya Dodoma Karume aliibuka kidedea kwa nguvu za kina JK. Hapo ndipo sasa uswahiba wa JK na Karume ukakolea na ndio kama mlivyoona walivyoamua kummaliza SAS.

Kwa mtizamo huo hapo juu. CCM Zanzibar haina ubavu wa kuongoza Zanzibar bila kuwa na nguvu za Bara. Kelele za kina Karume kama nilivyosema awali ni KUDEKA tu. Sasa hivi CUF na CCM Zanzibar wameungana kupiga kelele kwamba Zanzibar ni nchi na ina Rais. Nataka nimuulize Seif Hamad Rais wa Zanzibar ni nani? Na amechaguliwa lini? Na yeye Hamad na CUF wametambua lini kwamba Karume ni Rais wa Zanzibar?

Kama nilivyosema hapo awali, wananchi wa kawaida wa Zanzibar hawautaki Muungano kwa madhila waliyofanyiwa na wenzao wa Bara, kuanzia kupelekewa Polisi na Wanajeshi kuwapa kibano, kuongezewa wapiga kura kutoka Bara ili wapandikiziwe utawala wasioutaka, Kwa upande wa wananchi wa wa kawaida wa Bara, Muungano ndio hata hawauelewi. Kimsingi huku Bara Rais wa TFF Leodgar Tenga ni maarufu sana kuliko Rais wa Zanzibar Karume. Huku Bara Laila Odinga ni maarufu sana kuliko Rais wa Zanzibar Karume. Huku Bara Zanzibar ni 'kamkoa kadogo sana' kuliko Wilaya ya Kahama. Huku Bara Nadir Haroub Kanavaro ni maarufu sana kuliko kiongozi yoyote yule wa Zanzibar. Kwa maana hiyo kwa wananchi wa kawaida wa Bara kuvunja Muungano hakuna tofauti yoyote na kutovunja Muungano.

Tunapozungumzia Muungano wa Tanzania huwa tunamsahau Mdau mmoja muhimu sana katika Muungano huu. Serikali ya Marekani. Kwa sasa ni wazi kabisa Marekani ilihusika kwa kiwango kikubwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar. Nadhani kwa sasa makabrasha ya namna Marekani ilivyohusika na Muungano yako wazi kwenye tovuti za serikali ya Marekani. Siku 10 kabla ya Muungano Mwalimu Nyerere alimtuma Kambona kwenda Kenya kuongea na Jommo Kenyata namna ya kuziunganisha Nchi za Afrka Mashariki. Siku 10 kabla ya Muungano hakuna aliyekuwa ametamka hadharani kwamba kulikuwa na maongezi ya kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar. Marekani ambao walikuwa wakimhofia Mohamed Abdulrahman Babu kama mkomunisti hatari na mwenye nguvu kubwa na ushawishi angeweza kuifanya Zanzibar kuwa Cuba ya Afrika. Mwalimu ambaye alikuwa anaogopa kukaribishwa Zanzibar maadui zake na kwa maneno yake mwenyewe aliwahi kutamka kuwa angeweza angevisukumia Visiwa hivyo mbali zaidi baharini. Ilikuwa ni Rais kwa Marekani kumtumia Mwalumu kumlazimisha Karume akubali kuunanisha Nchi ukizingatia Wanajeshi waliokuwa wakimlinda walitoka Bara na Mwalimu akatishia kuwaondoa.

Nimelisema hili la Marekani. Je Marekani kwa sasa iko tayari kuruhusu Muungano wa Tanzania uvunjike. Kwa dunia ya sasa ya Marekani adui yake mkubwa ni Al Qaeda. Je hatuoni kwamba bado Marekani anautaka Muungano kwa gharama yeyote kwa hili la Zanzibar kuwa kituo cha Al Qaeda? Hivi Marekani hajui mchezo mchafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na JMT katika kucheza faulo kwa uchaguzi wa Zanzibar? Nina imani Marekani yu radhi Afro Shiraza iendelee kutawala Zenji kuliko CUF. Ukijumlisha na hayo Mafuta kiduchu na Migodi ile ya Buzwagi ambayo naambiwa familia ya Bush ina nasaba nayo ukiachilia mbali na Marekani yenyewe kuna kuvunjwa Muungano hapa kweli? AU TUNAZUGANA na VIJIKELELE vya kitoto vya kina SHAMHUNA?
 
hivi huyu mtaalamu wa mafuta au wa siasa? wapi kapata data? TIPER hawakutowa yeye kapata wapi au ndio aliyeletwa kupanga shares
 
hivi huyu mtaalamu wa mafuta au wa siasa? wapi kapata data? TIPER hawakutowa yeye kapata wapi au ndio aliyeletwa kupanga shares

Kwani walomleta walisema ni mtaalamu wa ushauri nasaha akawapa za mafuta. Usituulize masuali ya kipupu.

Kama waligungua mafuta toka 1950 mbona hawajayachimba hadi leo?
Hatutaki mafuta yao feki wala karafuu yao. Wachape mwendo .Period!!!!!!!!!
 
Hii ni hadithi ya Ali Nacha. Tunagombea mafuta ambayo hayajapatikana.
 
wameonyesha upeo wao mdogo wa kuelewa.. sasa wanataka wadanganywe? wapumbavu kweli
 
Wengi wao hapa wanabishana kama nani zaidi, bara au visiwani

Mmeshindwa kujadili kitu cha msingi.
Cha kujadili Ndugu yangu ni kuwa Zanzibaris want the control of their destiny.
Hali ilivyo hivi sasa ni kuwa hawana control hiyo. Vile walivyoambiwa wana-surrender kwa United Republic of Tanzania wana-loose control navyo. Lakini la kushangaza kuwa control inakwenda kwa Tanzania Bara (Tanganyika) na siyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kama inavyopaswa iwe). Kwa hivyo na hata hayo mafuta kama yapo, control ya mafuta hayo (rasilmali ambayo kama ipo ni ya Wazanzibari) itakuwa chini ya control ya Tanganyika kwahiyo ndiyo maana nakueleza kuwa la muhimu hivi sasa ni kuupitia Muungano ili kuweka utaratibu ambao utaifanya Zanzibar isi-loose control ya mambo yake ambayo tutayaainisha kuwa ni masusala ya Muungano. Experience imeonyesha kwamba Zanzibar ime-loose control ya maslahi yake katika mambo yote yaliyo katika himaya ya Muungano. Angalia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. angalia JWTZ, Angalia Polisi, Angalia Ushuru Forodha na makorokoro yake (Vyote viko katika control ya Tanzania Bara-Tanganyika).
 
Nimesema kila mara kwamba tatizo sio mafuta bali muungano wenyewe ulivyokua.

Ukitaka kula na kipofu usimshike mikono

Usemi huu unaendana na wenzetu wa visiwani kwa sasa.

Swali tujiulize sisi watu wa bara kama kweli tunataka kudumisha muungano kwanini vilivyoko bara hatugawani nao?

Huwezi ukasema ng'ombe huyu anatoa maziwa mengi kwahio wale ambao hawatoi maziwa mengi niwape majani kidogo.

Na ingekua hivyo basi zile wilaya au mikoa ambayo haina kipato zaidi wangepewa kidogo kwasababu hawazalishi sana.
 
Tatizo hapa ni hao wawakilishi kujua zaidi ya mtaalamu,tabia hii ndio kikwazo hata katika mahusiano yetu na hawa wa visiwani wanakua na degree hata kabla hajaenda shule.
 
Hivi wewe una upeo gani wa kuelewa? Na nini unachokielewa. Weka hapa tukuone.

kama watalaamu wanawambia hakuna mafuta wanang'ang'ania yapo hicho ni kipimo kizuri tu cha uelewa wao. na kwa vile na wewe ni mzanzibar kiwango chako ni hicho hicho. ueledi sifuri
 
Hivi mafuta zanizbra yapo au hayapo?

Yapo hayapo lakini wengi wenu hapa,
Narudia MMESHINDWA KUELEWA KWAMBA TATIZO NI MUUNGANO NA MASLAHI YAKE NA SIO SUALA LA MAFUTA.

Kama huu muungano ungekua na baraka kwa pande zote basi sisi watu wa bara tusingeona kwamba ni issue kubwa kuona wavisiwani wanang'ang'ania mafuta yao.
 
..hivi ni kwanini Baraza la Wawakilishi halitangazi kuvunja Muungano?

..mimi nadhani ni rahisi zaidi kwa Wazanzibari kutumia vyombo[baraza la wawakilishi,SMZ,baraza la mapinduzi] vyao kuvunjilia mbali Muungano kuliko sisi Watanganyika.

..Wazanzibari wamshinikize Karume na serikali yake kutangaza kujitoa ktk muungano. Zanzibar pia has every thing in place kuanza kujiendesha ikiwa watavunja muungano.
 
kama watalaamu wanawambia hakuna mafuta wanang'ang'ania yapo hicho ni kipimo kizuri tu cha uelewa wao. na kwa vile na wewe ni mzanzibar kiwango chako ni hicho hicho. ueledi sifuri
suali liliopo sio uelewa, suali liliopo ni kuchoshwa kwa wazanzibari na utawala wa tanganyika uliobeba jina hewa la tanzania ,ndio maana katika hiyo habari wanasema hata ikiwa ni kidogo kiasi gani tutajipaka wenyewe mwilini. siifagilii sana hii hali lakini nadhani umefika wakati wazanzibari kutamka maneno kama haya ili kuweka msisitizo.
 
Kilichowapa wasiwasi wenzetu wazanzibari ni muda ulioteuliwa kufanya mapendekezo ya mabadiliko katika yale masuala ya muungano na yasiyo ya muungano. Kabla ya tetesi za kuwapo mafuta Zanzibar, hiyo oil and gas resources halikuwa suala la muungano. Baada ya tetesi kuashiria kuwa mafuta huenda yapo Zanzibar na tena kwa wingi, zikaanza juhudi za kufanya kuwa mafuta liwe suala la muungano. Ndio wale wanaokuwa suspicious haraka wakahisi kuna jambo hapa! Wakaanza kupinga. Sasa leo hii mtaalamu anadai mafuta yale yaliyosemwa yapo, kumbe ni kama hayapo maana hata kazi ya kuyatafiti tu kuona ni kiasi gani inaonekana ni ya hasara, ni kidogo sana hayo mafuta. Wengine wanaona hapana, kwa nini hili la kukosekana mafuta lisemwe leo tunapokataa yasiwe ya muungano? Pengine bado kuna tusilolijua! Ndio wasiwasi ulioko hapo wakuu, lakini ripoti ya wataalamu ndio kama hivyo, hakuna mafuta ya kutosha kuendesha uchimbaji hata wa matumizi tu ya kawaida, acha wa kibiashara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…