Wandugu Masanja
JF-Expert Member
- Apr 26, 2008
- 1,574
- 522
yule sio mtaalamu wa mafuta na ninabisha kwa yeyote aliyetayari kwani aliletwa kufanya uchmbuzi yakinifu juu ya mgao, na tusubiri tuone kama kuna mtu alete CV za huyo mtaalamu
Nafikiri aliye mpumbavu ni wewe. La msingi ni kuwa kwa nini nyinyi wa Bara mshikilie hili la mafuta tu. Kama kweli ni watu mnaojali haki na usawa.-Na ujadiliwe Muungano sasa na kurekebisha mapungufu yote (tena mengi tu yaliyopo) Siyo kugawana mafuta tu. Tafadhali Bwana msiwafanye Wazanzibari ni mazuzu sikuzote. Hao waliotoa maoni ni Wawakilishi waliochaguliwa na Wazanzibari majimboni mwao. Hayo ni maoni ya Wazanzibari. Kama unayabeza, nafikiri ni wewe wa kubezwa na kuambiwa zuzu. Fahantum?
Zanzibar ni Nchi bibie...Pakacha,
We naona unatakiwa uchukue maji na kuweka kwenye pakacha upeleke home.
Kama huelewi kuwa Mkoa wa Zanzibar ni mdogo kuliko Wilaya ya Ilala ambao una wabunge watatu wakati mkoa wako una wabunge sijui wangapi na mawaziri na makatibu wakuu etc. Gharama za uendeshaji ni kubwa na hamlioni hilo na bado UNAWAITA KUWA SIO WAJINGA!
Basi hata Pangani tunaweza kuiita nchi. Kwa taarifa yako tu Wilaya ya Handeni Tanga ina ardhi kubwa kuliko Kata ya Zanzibar na Pemba!.
Una miss a big picture hapo mzee. Ninachoongelea ni kuwa angalia IDADI ya viongozi Zanzibar, linganisha na eneo, idadi yake ya watu, uchumi wake etc, Kweli wana justify kuwepo?. Kisha linganisha hivyo nilivyovitaja na Wilaya ya TARIME au KAHAMA.
Usiangalie mambo kama hao "viongozi" wanaopingana na Mtaalamu....
..hivi ni kwanini Baraza la Wawakilishi halitangazi kuvunja Muungano?
..mimi nadhani ni rahisi zaidi kwa Wazanzibari kutumia vyombo[baraza la wawakilishi,SMZ,baraza la mapinduzi] vyao kuvunjilia mbali Muungano kuliko sisi Watanganyika.
..Wazanzibari wamshinikize Karume na serikali yake kutangaza kujitoa ktk muungano. Zanzibar pia has every thing in place kuanza kujiendesha ikiwa watavunja muungano.
Nenda TANESCO na cheki mteja namba moja ni nchi gani... Na nchi gani unaingiza mapato kwa wingi kwa mwezi katika Shirika hilo..wametumia umeme bure toka bara miaka nenda rudi sasa wanatuletea sera za "chako ni chetu na changu ni changu" Ama kweli shukrani za punda........
its wrong ,its not fair pia its painful kuifananisha zanzibar na wilaya ya ilala. kama tatizo ni ukubwa wa eneo au population .why did u bother urself kuungana na kajisehemu ambako kanaonekana kama wilaya tu. kasome historia kisha njoo tena na naamini utarekebisha bandiko lako. kama ukubwa wa eneo ni big deal nadhani japan lisingekuwa taifa la pili kwa uchumi duniani.Pakacha,
We naona unatakiwa uchukue maji na kuweka kwenye pakacha upeleke home.
Kama huelewi kuwa Mkoa wa Zanzibar ni mdogo kuliko Wilaya ya Ilala ambao una wabunge watatu wakati mkoa wako una wabunge sijui wangapi na mawaziri na makatibu wakuu etc. Gharama za uendeshaji ni kubwa na hamlioni hilo na bado UNAWAITA KUWA SIO WAJINGA!
Na wewe nawe! umekuwa kama yule "Geologist" wa Baba kutoka Reading....
ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi... Zanzibar ni nchi
Naona unakaribia kulielewa tatizo lilipo. Hivyo vyombo vyote unavyotaja, kwa mfumo wa sasa na mazingira ya sasa havina ubavu wa kuvunja huo Muungano. Vinaambiwa kuwa ndio mamlaka ya Zanzibar na Wazanzibari, lakini kwa kweli havina mamlaka hayo (kwa maana yake kamili). Hivyo ni kurekebisha Muungano na kuwa na vyombo ambayo kweli vitakuwa na Mamlaka kwa kutetea maslahi ya Wazanzibari. Siyo vyombo ambavyo vimekunyatwa katika himaya ya Tanganyika.Unaweza kuwa na Serikali moja ukipenda. Au hata tatu ukipenda. Lakini la muhimu ni kuwa na vyombo na utaratibu utakaolinda (Nchi) ya Zanzibar na watu wake na himaya yake ndani ya Muungano. Hakuna atakaye kuuvunja Muungano. Waliozaliwa 64 wama wajukuu sasa. Wacheni wakue ndani ya United Republic of Tanzania.(Lakini usanii La.)
Nenda TANESCO na cheki mteja namba moja ni nchi gani... Na nchi gani unaingiza mapato kwa wingi kwa mwezi katika Shirika hilo..
Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi... Zanzibar ni nchi
Zanzibar wanaingiza kuliko Tanganyika? Hard to believe. Au unalinganisha Zanzibar na Wazo hill?
Tanganyika sio nchi...Zanzibar wanaingiza kuliko Tanganyika? Hard to believe. Au unalinganisha Zanzibar na Wazo hill?
Umeolewa au umeoa. Mwenzako humpendi. Anakunyanyasa. Hataki kukushirikisha katika maamuzi ya nyumba yenu. Hapendi ndugu zako (OIC). Badala ya kuchukua chako ujiondokee, unangoja akupe talaka? Kama ni yeye anafaidika na ndoa hiyo unadhani kweli atakuachia?
Zanzibar kila siku tunaambiwa jinsi wananchi wake WOTE wasivyopenda Muungano. Jinsi wanavyonyimwa haki yao hata ya kujiamulia wenyewe. Jinsi hata mambo yenye manufaa kwao yanavyozibwa na serikali ya Muungano. Jinsi ambavyo muungano mzima usivyo na faida kwao. Kitu gani kinachowazuia kutangaza rasmi kuwa wanajitoa katika hii ndoa isiyo na maslahi kwao? Si CUF wala CCM/Zanzibar walio na ujasiri wa kusema enough is enough, sisi tunajiendea zetu. Wanachodai ni kuweka plasta kwenye kidonda ambacho wenyewe wameishasema ni kidonda ndugu! Kama hawana ubavu wa kusema hivyo wanyamaze kwani ubavu huo hata siku moja hawawezi kupewa na serikali ya Muungano. Kama ni true patriots wa nchi ya Zanzibar, wasimame watamke hadharani kuwa hii ndoa haina maslahi basi ivunjwe. Nje ya hiyo ni unafik!
Hakuna Federation ( kuanzia US, Canada, Great Britain, Spain, Belgium, Switzerland, Nigeria etc) yenye Nchi tofauti ndani yake. Ukikubali muungano(kama ilivyo katika ndoa) ni lazima ukubali kuachia baadhi ya haki zako. Hauwezi ukataka muungano na serikali sovereign ya Zanzibar. Haiwezekani. Ni ndoto za Alinacha. Ukitaka kumiliki kikamilifu rasilimali zote zilizo ndani ya nchi yako, jawabu ni kujitoa. Si vinginevyo.
Tanganyika sio nchi...
Kwa sababu tumewaambia, kupitia Mkuu wetu wa Jeshi la polisi, kwamba Mzanzibar atakaethubutu kufanya hivyo ni mhaini.