Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Umeolewa au umeoa. Mwenzako humpendi. Anakunyanyasa. Hataki kukushirikisha katika maamuzi ya nyumba yenu. Hapendi ndugu zako (OIC). Badala ya kuchukua chako ujiondokee, unangoja akupe talaka? Kama ni yeye anafaidika na ndoa hiyo unadhani kweli atakuachia?

Zanzibar kila siku tunaambiwa jinsi wananchi wake WOTE wasivyopenda Muungano. Jinsi wanavyonyimwa haki yao hata ya kujiamulia wenyewe. Jinsi hata mambo yenye manufaa kwao yanavyozibwa na serikali ya Muungano. Jinsi ambavyo muungano mzima usivyo na faida kwao. Kitu gani kinachowazuia kutangaza rasmi kuwa wanajitoa katika hii ndoa isiyo na maslahi kwao? Si CUF wala CCM/Zanzibar walio na ujasiri wa kusema enough is enough, sisi tunajiendea zetu. Wanachodai ni kuweka plasta kwenye kidonda ambacho wenyewe wameishasema ni kidonda ndugu! Kama hawana ubavu wa kusema hivyo wanyamaze kwani ubavu huo hata siku moja hawawezi kupewa na serikali ya Muungano. Kama ni true patriots wa nchi ya Zanzibar, wasimame watamke hadharani kuwa hii ndoa haina maslahi basi ivunjwe. Nje ya hiyo ni unafik!

Hakuna Federation ( kuanzia US, Canada, Great Britain, Spain, Belgium, Switzerland, Nigeria etc) yenye Nchi tofauti ndani yake. Ukikubali muungano(kama ilivyo katika ndoa) ni lazima ukubali kuachia baadhi ya haki zako. Hauwezi ukataka muungano na serikali sovereign ya Zanzibar. Haiwezekani. Ni ndoto za Alinacha. Ukitaka kumiliki kikamilifu rasilimali zote zilizo ndani ya nchi yako, jawabu ni kujitoa. Si vinginevyo.

Wajitoe waende wapi? Hao wanaopiga kelele wanataka kupata umaarufu wa kisiasa tu! Aboud Jumbe aliyetaka kuhoji Muungano leo anaishi wapi? Kwa mwaka anakwenda Zenj mara ngapi? Seif Sharif Hamad ndiye 'mwizi' wa 'dokyumenti' za Jumbe alizohoji na kuzipeleka kwa Nyerere. Hakuona wakati huo umuhimu wa yeye kuungana na Jumbe kudai 'uhuru' wao' leo ndio aone! Hao wakiachwa peke yao hata wiki haitaisha Pemba itajitangazia uhuru wake.
 
Bwana H. Yusufu,
Umeandika vizuri saana, lakini kama alivyoandika na kuuliza "gottee" hebu tueleze kama nyhinyi mnaipenda nchi yenu sasa mnatafuta nini kwetu? wapemba wamejaa sharifu shamba, Jumbe huyo anafanya nini? si muanze kuondoka basi kwani tuliwatumia meli kuwaleta bara? Nilishawahi kusema wazanzibar ni wavivu wakufikiri na hamjui mnachokitaka, hawa wanaowadanganya kuwa mtakuwa na maisha bora mkibaki wenyewe wanawadanganyeni, shida yao ni kutawala milele. mtaanza kubakana tuuuuuuuuuuu
 
Wazee wa JF
Kisa cha kugombana ni nini? Huko Unguja na Pemba si kuna wasomi, tena wasomi maridhawa? Tena kuna vijana shadidi hasa wa elimu! Kwa nini kama hawa wawakilishi wametobolewa macho na mtaalam, wasitumie wasomi wao kufanya kazi hiyo? Nijuavyo mie tafiti hujibiwa kwa tafiti, si ngumi ati!
 
Kumbe Msambaa mwenzangu! Angalia na wewe posting yangu. Utaona nimewatoa waZanzibari milioni 3 kwenye hesabu ya hao waTanzania ndipo nikachukua asilimia kumi ya milioni 36.4 ( sio milioni 39.4 kama unavyodai). Bado asilimia 10 ya watanganyika ni zaidi ya asilimia 100 ya wazanzibari! na Pemba nimefika. Najua si wote wenye umeme. Na ukienda nje ya mji wa Zanzibar ( nahani wenyewe wanaita mashamba) wengi tu wanaotumia vibatali. Nimewasamee wote hao na kusema kwa vile Zanzibar wametuzidi maendeleao wote wanatumia umeme wa Tanesco! Au unataka tuseme kila mZanzibari ana mashine ya unga ili hesabu zako zitimie? Haya ni matumizi ya nyumbani wakati tunajua matumizi makubwa ni kwenye viwanda migodi na kadhalika. Haya, msambaa mwenzangu, Zanzibar kuna viwanda vingapi?

Nilikimbia umande lakini wakati wetu hauvuki darasani bila kujua multiplication table!
Nikusaidie kidogo

Ni juzi tu mashindano ya olympic yalimalizika kule China na China walishika nafasi ya kwanza katika dunia.

Sasa basi ukilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zilipeleka wanariadha wachache kutokana na udogo wa nchi zao lakini wameshika nafafi ya tano au ya sita basi utajua kwamba China haiko nafasi ya kwanza, hapa unajirudia yale mahesabu niliyotoa mwanzo.

Unasema umefika Zanzibar na vijijini.

Kitu kilichokushinda hata kuangalia country profile kwenye net ya jamhuri ya muungano.

Asilimia kubwa ya wazanzibari wanaishi mjini ukilinganisha na sisi watu wa bara, kwahio hapa pia umeshindwa kuainisha.

Kusema kwamba watumiaji wakubwa wa umeme sio kwamba kila mzanzibari anatumia mashine ya kusaga.

Baadhi ya viwanda.
Sukari
Mafuta ya nazi
Sabuni
Marashi

Sina haja yakuvisema vyote kwani hii pia hatufananishi sisi watanganyika idadi tunayotumia umeme tunaotumia majumbani na kiwanda cha saruji Tanga.

Zanzibar wanatumia umeme mwingi kutokana na wale watu wanaoutumia majumbani ukilinganisha na sisi wa bara ambao asilimia yetu ni ndogo.

Mwisho kabisa kama nilivyosema kwenye post yangu kwa kisambaa

Wazanzibari ni watu wa kwanza kutumia umeme afrika nzima ya mashariki
 
Bwana H. Yusufu,
Umeandika vizuri saana, lakini kama alivyoandika na kuuliza "gottee" hebu tueleze kama nyhinyi mnaipenda nchi yenu sasa mnatafuta nini kwetu? wapemba wamejaa sharifu shamba, Jumbe huyo anafanya nini? si muanze kuondoka basi kwani tuliwatumia meli kuwaleta bara? Nilishawahi kusema wazanzibar ni wavivu wakufikiri na hamjui mnachokitaka, hawa wanaowadanganya kuwa mtakuwa na maisha bora mkibaki wenyewe wanawadanganyeni, shida yao ni kutawala milele. mtaanza kubakana tuuuuuuuuuuu

Swali hili pia waulizie wakubwa wetu kwanini wanang'ang'ania Zanzibar na huku wanajua inawatia hasara kwenye muungano?

Post yako imekaa kiushindani tu, NANI ZAIDI

Kama wapemba ni wavivu iweje ndio wenye kumiliki majumba mazuri, biashara nyingi huku kwetu bara?

Sisisi hatuna uvivu?

Kwanini tusiwashinde wao?
 
Ndugu Kipunguni,
Huyu bwana Reading hizi siasa za Tanzania atakuwa kazitoa wapi wakati yeye kaja kwa ajili ya utafiti wa mafuta? Au hili suala la siasa lilikuwepo katika hadidu za rejea za kazi aliyotumwa kuifanya Bw Reading?
Naomba kueleweshwa

Idimi,
Bw Reading "aliletwa" na "taasisi" fulani kuja kutoa huo "utaalamu" wake ... sasa wewe niambie alifiakiaje conclusion ya kwamba hakuna mafuta wakati TPDC hawakumpa geological reports zozote??!! ... go figure!
 
Msambaa kweli mbishi.

Kwa kujua wazanzibari wametuzidi kwa kila kitu ndiyo maana katika hesabu zangu nikasema zanzibar asilimia 100 wanatumia umeme na bara asilimia 10. Bado bara ni wengi zaidi. Ukitumia statistics za kutoka census ya mwaka 2002, Tanzania bara ina watu 33,461,849 na Zanzibar wako 981,754 ( angalia hapa 2002 POPULATION AND HOUSING CENSUS. Hata wakizaana kama pimbi hawatafikia hao milioni 3 niliotumia mimi katika hesabu zangu. Ukitaka labda useme kila mzanzibari ana kiyoyozi, jiko la umeme, jokofu na mashine ya kusaga ndiyo wataweza kufikia matumizi ya umeme ya hao asilimia 10 ya watu wa bara.

Hilo la viwanda sina la kukuambia. Naona unawatania shemeji zako. Viwanda vya mafuta ya nazi ( nazi zenyewe zinakaushwa juani) unalinganisha na Tanga cement!

Haya. Siendelei.
 
Hahaaaa
Sensa ya nini?

Unachukua watu kumi kutoka bara, na kumi kutoka visiwani

7 wa visiwani wanatumia umeme na 3 wa bara wanatumia umeme
Nani ni mteja mkuu wa Tanesco? Tanganyika au wa bara.

Mahesabu ya msingi haya
 
,,,,,Siku moja hivi katika pita pita zangu mitaa ya kati hapa na pale ,,,,KISONGE,wakati uleee wa GIZA totoro la mwezi mzima,nikakutana na stori za wanasiasa na watu wa ZECO,jamaa wa ZECO anawaambia wale wazee pale kwenye benchi la zege KISONGE hapo kwamba,,,watu wanaoongoza kwa kulipa bill kubwa ya umeme kwa ZENJI ni ZAMANI KEMPISKI HOTEL,ikifuatiwa na Bank of Tanzania tower,,,,daah nikajiuliza hivi matumizi ya taasisi za kawaida kabisa ndo yanachangia kuendesha hii ZECO???,,,Hakika hakuna kiwanda kikubwa cha kutumia umeme kwa kiasi kikubwa hata kidogo,na hata hivyo viwanda ambavyo unaweza kuhisi labda huwa vinatumia umeme zaidi,vyote ngoma yake huwa HAIKESHI,mwisho ni saa 11 jioni ndio mpaka kesho.
 
Zanzibar ni nchi yetu, sisi hatuna pengine yawepo mafuta yasiwepo hapa ndiyo nyumbani, ndio tulipozaliwa na hatuna shangazi wala mjomba nje ya Zanzibar, huo ndio ukweli hata kama hamuupendi.

,,,Huwa najiuliza sana,hivi kwani wazanzibari ni watu gani,,,,,manake mimi kwa mfano ni MTANZANIA wa zanzibar,,,na nina ndugu zangu wanaoshi NZEGA huko TABORA,,,nina watoto zangu wanaoishi KAHAMA huko SHY,najiona ni MTANZANIA zaidi ya Mzanzibari,hizi siasa kwa kweli zitatuharibia nchi,na sijui mwisho wake utakuwa ni nini,Manake kwa level hii tuliofikia,i can't see the REVERSE gear..
 
Hahaaaa
Sensa ya nini?

Unachukua watu kumi kutoka bara, na kumi kutoka visiwani

7 wa visiwani wanatumia umeme na 3 wa bara wanatumia umeme
Nani ni mteja mkuu wa Tanesco? Tanganyika au wa bara.

Mahesabu ya msingi haya

Sasa kama statistics zinasema kuwa katika kila watanzania 10, wawili wana ukimwi basi ukichukua kundi la watu kumi na ukikuta wanane hawana ukimwi basi hao waliobaki ni lazima wawe wamekanyaga miwaya?

Ulifeli hesabu, Mkuu! Au ulikuwa unatazamia!
 
,,,Huwa najiuliza sana,hivi kwani wazanzibari ni watu gani,,,,,manake mimi kwa mfano ni MTANZANIA wa zanzibar,,,na nina ndugu zangu wanaoshi NZEGA huko TABORA,,,nina watoto zangu wanaoishi KAHAMA huko SHY,najiona ni MTANZANIA zaidi ya Mzanzibari,hizi siasa kwa kweli zitatuharibia nchi,na sijui mwisho wake utakuwa ni nini,Manake kwa level hii tuliofikia,i can't see the REVERSE gear..

Waambie, Mkuu! Waambie!
 
Mahesabu yako na mehesabu yangu
Hata kipofu anaona kwamba umefeli.

Mgeni na asiyeijua Tanzania akija ukimuambia kwamba watu saba kati ya kumi wanatumia umeme zanzibar keshejua jawabu lake.

Mgeni huyo huyo akiambiwa watu watatu kati ya kumi Tanganyika wanatumia umeme keshajua jawabu tayari.

Kama bado huyaoni makosa yako endelea na mahesabu yako lakini mwalimu wako aliyekufundisha hesabu akiona haya ataona aibu.

Haahaahaaaa
 
,,,Huwa najiuliza sana,hivi kwani wazanzibari ni watu gani,,,,,manake mimi kwa mfano ni MTANZANIA wa zanzibar,,,na nina ndugu zangu wanaoshi NZEGA huko TABORA,,,nina watoto zangu wanaoishi KAHAMA huko SHY,najiona ni MTANZANIA zaidi ya Mzanzibari,hizi siasa kwa kweli zitatuharibia nchi,na sijui mwisho wake utakuwa ni nini,Manake kwa level hii tuliofikia,i can't see the REVERSE gear..
Sijui!!!. Lakini unahitaji duruso katika somo la sociology na mada ya evolution.Hivyo uelewe kuwa pia wapo Watanzania waliopo Nzega ambao hawana kabisa jamaa yoyote Zanzibar au Pemba au popote pale nje ya Nzega.. Hivyo huyo mwenzio aliyedaI kuwa kwao ni Zanzibar na hana jamaa yoyote nje ya Zanzibar ni sahihi kabisa-na lazima aringie pake na apalilie pake, na ajione nkuwa Mzanzibari zaidi kuliko Mtanzania.
 
Mgeni huyo huyo akikuambia asilimia 10 ya watu China wanatumia umeme na aslimia 50 Tanzania bado utasema watu wengi zaidi Tanzania wanatumia umeme kuliko China?

Hesabu, ndugu yangu, hesabu!

Basi yaishe, Mkuu. Wazanzibari wengi zaidi watumia umeme kuliko bara!!!!
 
,,,Huwa najiuliza sana,hivi kwani wazanzibari ni watu gani,,,,,QUOTE]
Kwani Wa-Tanganyika ni watu gani. Tatizo lako kuwa wewe unafuta U-Tanganyika- huo haufutiki, na wala haukufutika kwa kuja U-Tanzania. hivyo heshimu Uzanzibari. Kama una bahati ya kuwa na asili ya Tanganyika na pia asili ya Zanzibar- basi hongera, Wewe ni Mtanzania halisi. Lakini usikatae kamwe Utanganyika wako wala Uzanzibari wako.
 
Ubinafsi, Umimi, na urohombaya unatumaliza Waafrika.

Vita vinavyopiganwa sehemu yeyote Afrika ni kwa ajili ya ubinafsi; watu wengi Afrika wanateseka kwa ajili ya ubinafsi na kutokana na baadhi ya Waafrika wasiopenda wenzao wapate.

Mungu atusaidie Waafrika.
 
,,,Huwa najiuliza sana,hivi kwani wazanzibari ni watu gani,,,,,QUOTE]
Kwani Wa-Tanganyika ni watu gani. Tatizo lako kuwa wewe unafuta U-Tanganyika- huo haufutiki, na wala haukufutika kwa kuja U-Tanzania. hivyo heshimu Uzanzibari. Kama una bahati ya kuwa na asili ya Tanganyika na pia asili ya Zanzibar- basi hongera, Wewe ni Mtanzania halisi. Lakini usikatae kamwe Utanganyika wako wala Uzanzibari wako.

Ndugu yangu, huu uhafidhina na kutotaka mabadiliko ndio umetufikisha mahali leo tunahofia kila kitu kipya. kwa nini tsikubali kubadilika katika mambo ambayo yatatufanya tusigee mbele?
Ni vema tukaendelea kushikilia Utanganyika na Uzanzibari wetu kwa sababu huo ni utambulisho wetu. lakini hili lifanyike kwa namna ambayo haitaathiri Utanzania kwa sababu huo ndio utambulisho mpya yulioamua kujipa. Tukikumbatia uhafidhina katika hili na mambo mengine, kamwe hatutaendelea, tutakuwa tunawaza nyuma tu
 
Wenzetu wana usemi "trying to have our cake and eat it also." Hatuwezi kuwa na utanganyika na uzanzibari kama utaifa wetu na hapo hapo tukawa na utanzania! Kama tunataka utanganyika na uzanzibari ni lazima tubali utanzania ufe. La sivyo hizo Tanganyika na Zanzibar zibaki kuwa majimbo katika Tanzania, majimbo yasiyo na utaifa. Tunakuwa disingenuous kudai kuwa hatutaki Tanzania ife lakini tunataka tutambulika kama watanganyika na wazanzibari! Tuwe wazi, tuseme Muungano tumeuchoka, tugawane vilivyopo na kila mmoja aende kivyake. kama walivyofanya Czechoslovakia. Kama walivyofanya USSR. Lakini tuwe waangalifu tunapodai hili waana kuna wakina King Zenji wengi miongoni mwetu na hawatakuja kutusamehe kwa kuwavunjia undugu wao!
 
Back
Top Bottom