Gottee
R I P
- Sep 7, 2008
- 174
- 2
Umeolewa au umeoa. Mwenzako humpendi. Anakunyanyasa. Hataki kukushirikisha katika maamuzi ya nyumba yenu. Hapendi ndugu zako (OIC). Badala ya kuchukua chako ujiondokee, unangoja akupe talaka? Kama ni yeye anafaidika na ndoa hiyo unadhani kweli atakuachia?
Zanzibar kila siku tunaambiwa jinsi wananchi wake WOTE wasivyopenda Muungano. Jinsi wanavyonyimwa haki yao hata ya kujiamulia wenyewe. Jinsi hata mambo yenye manufaa kwao yanavyozibwa na serikali ya Muungano. Jinsi ambavyo muungano mzima usivyo na faida kwao. Kitu gani kinachowazuia kutangaza rasmi kuwa wanajitoa katika hii ndoa isiyo na maslahi kwao? Si CUF wala CCM/Zanzibar walio na ujasiri wa kusema enough is enough, sisi tunajiendea zetu. Wanachodai ni kuweka plasta kwenye kidonda ambacho wenyewe wameishasema ni kidonda ndugu! Kama hawana ubavu wa kusema hivyo wanyamaze kwani ubavu huo hata siku moja hawawezi kupewa na serikali ya Muungano. Kama ni true patriots wa nchi ya Zanzibar, wasimame watamke hadharani kuwa hii ndoa haina maslahi basi ivunjwe. Nje ya hiyo ni unafik!
Hakuna Federation ( kuanzia US, Canada, Great Britain, Spain, Belgium, Switzerland, Nigeria etc) yenye Nchi tofauti ndani yake. Ukikubali muungano(kama ilivyo katika ndoa) ni lazima ukubali kuachia baadhi ya haki zako. Hauwezi ukataka muungano na serikali sovereign ya Zanzibar. Haiwezekani. Ni ndoto za Alinacha. Ukitaka kumiliki kikamilifu rasilimali zote zilizo ndani ya nchi yako, jawabu ni kujitoa. Si vinginevyo.
Wajitoe waende wapi? Hao wanaopiga kelele wanataka kupata umaarufu wa kisiasa tu! Aboud Jumbe aliyetaka kuhoji Muungano leo anaishi wapi? Kwa mwaka anakwenda Zenj mara ngapi? Seif Sharif Hamad ndiye 'mwizi' wa 'dokyumenti' za Jumbe alizohoji na kuzipeleka kwa Nyerere. Hakuona wakati huo umuhimu wa yeye kuungana na Jumbe kudai 'uhuru' wao' leo ndio aone! Hao wakiachwa peke yao hata wiki haitaisha Pemba itajitangazia uhuru wake.