You have hammered it all.......🙂 ......walifikia mpaka hatua ya kuwekeana vinyesi kwenye visima vya maji, kutokwenda kuzikana, n.k ....
 
Watanganyika tunaung'ang'ania na kuuenzi kwasababu kuna tunayotaka kule, kama hakuna basi muungano huu ungevunjika toka wakati wa Abdu Jumbe.

Wazanzibari hawautaki na wameshachoka nao kwani hawaoni faida ya muungano.

Kama ni kweli Tanganyika wanapata hasara sana kwenye muungano wala wasingeukumbatia kila leo. Kinyume na hicho upande wa pili [visiwani] ndio hawautaki kabisa.

Aliyesema meli zinazoenda visiwani ni za watu wa bara na wazisimamishe basi hana analojua.
 
Jee, unaweza kuyasasambua!!. Ni Mzanzibari?
 
Samahani, naona niliteleza. Tuliongozwa na m-Zanzibari kwa miaka kumi na si minne kama nilivyoandika. Mawazo yote yako kwa Obama sasa hivi! Miaka kumi ambapo the colonized ameshika usukani! Bado mnatuambia ati tunawafanya koloni letu! Chama cha upinzani chenye wabunge wengi katika bunge la muungano ni CUF. Chama ambacho kilishinda viti vyake karibu vyote kutoka Pemba!

Angalia baraza la mawaziri vivuli lilivyo, likiongozwa na mbunge wa wawi, Mheshimiwa Bw. Hamad Rashid Mohammed!



Katika bunge la mtawala wenu, kiongozi wa upinzani mpemba. Ukiendelea, utaona mawaziri vivuli wote wa wizara ya Afya ambayo si ya Muungano ni wapemba! Waziri kivuli wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana ni Abdul Khalfani; wa Mifugo na Uvuvi ni Mwadini Abbas Jecha; Nishati na Madini ni Mohamed Habib Juma Mnyaa; Kilimo, Chakula na Ushirika ni Salim Hemed Khamis; Habari, Utamaduni na michezo ni Mwanawetu Said Zarafi akisaidiwa na Mohamed Ali Said n.k.

Waziri kivuli Zitto Kabwe msaidizi wake ni Kabar Shamis Faki; John Cheyo msaidizi wake ni Ali Said Salim; Susan Lyimo msaidizi wake ni Nuru Awadh Bafadhil n.k

Hawa mawaziri vivuli wote wanahudumiwa na serikali ya Muungano. Hawa ndio wanaotakiwa kuisimamia kidete serikali iliyo madarakani, kila mmoja aki-focus katika wizara yake. Hawa ndio wanaojibu na kukosoa mapendekezo ya bajeti ya wizara za serikali iliyo madarakani. Sasa kama hawa niliowataja kutoka kwa wenzetu hawautambui Muungano, kweli mbunge wa Konde atakuwa na uchungu gani na mkulima wa Kibondo ili ahakikishe anapata huduma bora katika zahanati zake?

Leo, hamna hata aibu, mnasema tunawatawala? Au hamjui maana, uzito na majukumu ya Official Opposition?
 
Kumlazimisha mwanamke asiyekupenda kuwa mkeo atakusumbua hadi talaka tatu zitakutoka. Haya ndo Tanganyika inakutana nayo kwenye ndoa yake ya mkeka na ZNZ.

ukweli unarudi pale pale kuwa Muungano huu hauna maana hata kidogo.

Muungano ni wa CCM wala si wa Watanzania. CCM haiwezi kukubali muungano uvunjike maana ina mali zake nyingi tu imewekeza huko Zanzibar. Muungano ukivunjika CCM Zanzibar nayo inakufa rasmi. kama hamuamini tuchague chama kingine kisicho na umaarufu zanzibar ifikapo 2010.

Ukitaka kuharakisha huu mvunjiko basi Serikali kuu iseme ok, waZanzibari wote wachukuliwe kama ni wageni upande wa bara na wanapokuja lazima nao wawe na passport na hawaruhususiwi kumiliki ardhi na majengo. Hayo tu yanatosha kuvunja Muungano ndani ya masaa 24 tu.
 
Kwenda Zanzibar kwa passport

Hebu niwaulize kina Yakhe ambao GDP per capita yao ni dola za kimarekani 100 hivi, yaani, kila Mzanzibari hapati dola 1 kwa siku. Yaani, kwa maneno mengine thamani ya Mzanzibari ni shilingi kama 900 bongos shillings!

Sasa hivyo vitambulisho ndugu zangu, wandani wetu, wenzetu, kaka zetu na dada zetu zitawasaidia kupunguza makali ya njaa yenu?

Kuna mwandishi katoa matakwimu hapa kuna vinchi vina watu chini ya laki 5 lakini Zanzibar yenye watu milioni 1 haioni na itachukua miaka mia kuona indiketa,yaani, zile taa za nyuma za nchi hizo .....

Tatizo lenu nyie mnadhani mtaweza kuishi kwa kugombana gombana tu kila saa na bara. Huo mkate wa siasa hautawafikisha popote. Na watu wenu sijui wana gundi nyeusi machoni mwao na pamba nzito masikioni mwao-kiasi cha kushindwa kuwawajibisha ipasavyo au hii ndio laana inayokumba waibaji kura kila mahala duniani-uongozi mbovu na umasikini wa mawazo?

Kisiwa ambacho kingeweza kuwa Dubai kubwa ya Afrika kinaongozwa kama shule ya chekechea?

Hizi ndio baadhi ya sifa za Zanzibar sasa:

1. Zanzibar International Airport (ZIA): One of the world's worst airports
2. Wazushi na wabishi
3. Wababaishaji
4. Masultani weusi kwa rangi ya udongo waliomuondoa sultani Mwarabu,
5. Njaa kali, mtu ananunuliwa kwa kandambili-yebo yebo ghali, au kanga au pilau au juisi na akakupigia kura,
6. Roho mbaya,
7. Waliojaa husuda na wivu,
8. Warushi na matapeli.

Imekuwaje jamani, na njaa ndio kwanza sasa inaanza sasa itakuwaje?


ZINGATIO: Inasikitisha kuona viongozi wanaostahili kuwa na busara na hekima na waandishi wa habari mamluki nao wanashabikia utoto na upuuzi huu wa kisiasa badala ya kuwachambua hoja za watu fulani walioshiwa mawazo na fikira za kuwaendeleza Wazanzibar na kuwakosoa ipasavyo!
 
AU kwa kuwa jamaa wanamuona mheshimiwa kama vile anashindwa kuwadhibiti wabara basi ndio wanaanza kumchezea wakijua hawezi kuwafanya lolote kwa upole wake?
 
AU kwa kuwa jamaa wanamuona mheshimiwa kama vile anashindwa kuwadhibiti wabara basi ndio wanaanza kumchezea wakijua hawezi kuwafanya lolote kwa upole wake?

sijui kwa nini tunawang'ang'ania utadhani bila wao hakuna maisha..tuwaachie nchi yao na sisi tubaki na tanganyika yetu...kwanza nashangaa sisi tunajipendekeza eti tunajiita tanzania bara...wakati wao wakiwa huku ughaibuni wala hawataki kusikia hilo neno tanzania zaidi ya kwenye passport ..wanajitambulisha kama wanzibar...
hao jamaa wamezoea ulalamishi sana...kwanza ni mzigo kwetu tuwaache waende zao..maana hata bili ya umeme wa tanesco hawalipi ....wanatutia hasara ya bure...
 

Fundi Mchundo na Enderea inaonekana hamtaki kufahamu dhana ya Serikali mbili (lakini la hatuelekei kwenye moja-asilan). Halafu rejeeni kwa Bwan JK- anasema Zanzibar ni nchi ndani ya Muungano (Tanzania), lakini nje ya Muungano nchi ni Tanzania. Sasa unaona hapo Tanzania ni yetu (Mzanzibari ya nini Paspoti akienda Sumbawanga), lakini Mchaga wa Marangu anaweza kuambiwa alete paspoti akienda Zanzibar (ni nchi ndani ya Muungano)
 

Hapa ndipo kwenye tatizo...kuna watu wanaona kuwa seriakali ya muungano ni serikali ya Tanganyika na wanzanzibari kuwa humo ni kama kuwasaidia ili wajione kuwa nao ni wadau...fikra kama hizi na zile za mmoja kujiona mume na mwingine kuonekana mke "aliyeolewa" na "mume mwema" huyo ni moja ya mizizi ya fitina za kimuono zinazoathiri vibaya hali ya muungano wetu ama Taifa letu....

Siamini kama muono wa aina hii kuwa Tanzania ni ya Watanganyika waliowakaribisha ama kuwahifadhi Wazanzibari ni muono ulio sawa. Na kuendelea kuchukulia hali ya muungano katika muono huo ni moja ya sababu zinazokuza challenges za muungano wetu kwa muda mrefu sasa.

Kumbukeni kuwa dhima ya muungano ni USHIRIKIANO na sio USHINDANI wa nani mkubwa nani mdogo, nani mzuri nani mbaya, nani mbabe nani mnyonge, nani mwerevu nani mpuuzi, nani anamuhitaji mwenzake na nani mzigo...

Arguments za aina hii zinatufanya wote kuwa WAPUUZI...

Tanzanianjema
 
Mimi sijawahi kusikia mtanzania bara akilalamika kuwa Salim Ahmed Salim hakustahili kuwa Waziri Mkuu, Waziri au balozi wetu. Sijawahi kumsikia mtanzania bara akilalamika kuwa Ali Hassan Mwinyi hakustahili kuwa rais wetu kwa vile ametokea Zanzibar. Sijawahi kumsikia mtanzania bara akikataa kuitwa mtanzania na kukazania kuwa yeye ni mtanzania bara au mtanganyika. Sijawahi kumsikia mtanzania bara akilalama kuhusu wapemba walivyojaa Namanga na Sharif Shamba. Sijamsikia mtanzania bara akihoji kwa nini bajeti ya serikali ya Muungano inachangiwa kwa kiasi kikubwa mno na Tanzania bara. Sijasikia hawa machogo wakilalamika wakati walipoambiwa serikali yao imefuta sehemu ya deni la wananchi wa zanzibar kwa tanesco. Sijawasikia hawa machogo wakilalamika kuhusu serikali ya muungano kuipatia fedha serikali ya mapinduzi kulipa mishahara. Hata tulipoambiwa kuwa tubebe pasi kuingia Zanzibar tulifanya hivyo. Sisi haya yote tuliyakubali kwa vile tuliona wale ni wenzetu. Lakini inaonekana ukimya huo umeeleweka kama ubwege na kujipendekeza. Imefika mahali viongozi wa serikali ya Mapinduzi wanatoa maneno ya kichochezi dhidi ya Muungano na kutubeza kuwa ati tu wakoloni bila hata kuogopa. imefika mahali hata kabla mafuta kupatikana, tunaonywa kwa sauti kubwa kwamba safari hii tusidhani kama tutawadhulumu maana hayo ni ya kwao! lini tumewadhulumu? Hiyo kodi wanayolalamikia hivi ni hiyo ya biashara ya kimachinga ya kuingiza sidiria kutoka darajani? Kuna mheshimiwa mmoja alifikia hata hatua ya kudai kuwa wao ndio wanaoibeba Tanesco!

Hapana,Tanzanianjema. Imefika mahali tuulizane wote kama kweli huu Muungano tunautaka. Hao wanaosema wanawasemea wazanzibari waliokuwa wengi watuthibitishie hivyo. Na wale wanaodaiwa kuwa wanawang'ang'ania wenzao nao wapate nafasi watuthibitishie hilo. Imefika mahali ambapo wananchi wa hii nchi, na sio wanasiasa, waseme wazi kama kweli huu Muungano wanautaka au hapana. Wao ndio wenye nchi. Waulizwe basi!

Tunaelewa sana maana ya serikali mbili. Lakini hii haiwapi haki upande mmoja kila kukicha kumtukana mwenzie ati kwa vile yeye ni nchi. Hapana. Hii hatukubali. Hata kama tumeoleana na tumesoma pamoja. Enough is enough.
 

Ungekua wewe ndio mkubwa wa nchi unayesema hivi basi Wazanzibari wangekimbia mitaani kwa shangwe na vigelegele.

Watanganyika tunaziba viraka nguo ambayo imeshaoza, kwanini tunafanya hivyo?
Kwasababu tunaipenda sana Zanzibar.
 
Ungekua wewe ndio mkubwa wa nchi unayesema hivi basi Wazanzibari wangekimbia mitaani kwa shangwe na vigelegele.

Watanganyika tunaziba viraka nguo ambayo imeshaoza, kwanini tunafanya hivyo?
Kwasababu tunaipenda sana Zanzibar.

Darwin.
Siamini kuwa wazanzibari wote hawaupendi Muungano. Naamini kuwa kama watajua kuwa sasa si masihara tena wako watakaowarudi hao wanaojifanya kuwaongelea. Viongozi wa Quebec waliamini kabisa kuwa wananchi wao wengi wangependa kujitenga na Canada. Kwa muda mrefu walitumia hiyo kudai upendeleo katika kila nyanja kwa vile wote waliamini kuwa bila hivyo wananchi wa Quebec wangekitoa. Lakini madai yalipofika kikomo na majimbo mengine ya Canada wakawaeleza bayana kuwa kama wanataka kwenda waende, waligwaya. Referendum ilifanyika na ikashindwa. Hawa wenzetu watakapojua kuwa tuko serious na tumechoka, watajirudi. Wengi wao wanaamini kabisa kuwa hatuko tayari kuwaachia ndio kiburi chao. Lakini itafika wakati ambapo wanachokiombea kitatokea. Kama wachina wanavyosema, chunga sana unayomuomba Mwenyezi Mungu maana anaweza akakupatia!Hakuna anayejua kwa dhati raia wa pande zote mbili wanataka nini maana hawajawahi kuulizwa. tuwaulize basi!
 
Hizi ndio baadhi ya sifa za Zanzibar sasa:

1. Zanzibar International Airport (ZIA): One of the world's worst airports
Kwasababu iko kwenye SMZ CCM
2. Wazushi na wabishi

Kama mtu kazusha jambo siunamshitaki ili sheria ijulikane nani mwenye hatia. mara ngapi watanganyika tumefanya hivyo?
3. Wababaishaji
4. Masultani weusi kwa rangi ya udongo waliomuondoa sultani Mwarabu,

Umesahau ndio alikotoka Alhaji Hassan Mwinyi.
5. Njaa kali, mtu ananunuliwa kwa kandambili-yebo yebo ghali, au kanga au pilau au juisi na akakupigia kura,

Labda hii umeigeuza waulize CCM wanavyomaliza pesa visiwani lakini watu wanachukua hivyo vitu lakini kwenye uchaguzi wanampa kura wanayemtaka. Kama ni Pemba ndio hawaambulii hata udiwani.
6. Roho mbaya,


7. Waliojaa husuda na wivu,
8. Warushi na matapeli.
Wivu tumejaza sisi watu wa bara, Zanzibar inachosema tu basi hatulali vitandani tunaogopa kwamba watatutenga.

Matapeli!!! hivi unajua unachoongea
 

Nitangojea hio siku kwa hamu Tanganyika itakaposema imechoka na Muungano.

Kinyume chake wenzetu ndio wanaosema kila siku.

Watu wengi wanaona Umeme ndio utawakomesha wazanzibari.

Kama wazanzibari wanajali maendeleo yao basi umeme wanaweza kununua hata kutoka Kenya au msumbiji tena wenye uhakika.

Kumbuka pia hawa watu ndio wa kwanza afrika mashariki kutumia umeme, kwahio umeme kwao sio big issue.

CCM inaogopa kisiwa kitakua sio chao tena Zanzibar itang'aa zaidi.
 


,,,,,,,Ndugu yangu tatizo la UMEME ni kubwa sana,na kama unakumbuka wakati ule tuliolala gizani kwa mwezi mmoja tu ilikuaje,naogopa sana kujipiga kifua katika hili suala la nishati,Umeme wa generator za diesel ni balaa,kwa mapato yetu haya kiduchu zenji hapa,sidhani kama tutaweza kuhimili kukimbiza vinu hivyo kwa saa 24/7 kwa wiki,labda tununue toka KENYA au Msumbiji???,mzee unazungumzia $ hapo na sio TSHS,na ujue ikifikia stage hiyo,basi mpaka mbatata, nyanya, kitunguu toka Tabora kule na mchele wa Mbeya itabidi uwe imported kwa $ pia,Haya mambo hayapo rahisi kama mnavyofikiria wazee,tusijidai tupo tayari kufa wakati hata KUZIMIA tu hatuwezi.
 
Wewe King Zenji kama unakumbuka ni miaka ya juzi tu wafanyabiashara wengi wa bara wanafungashia Zanzibar, Sasa iweje tanganyika yenye bandari ya tanga, mtwara, bagamoyo na DAR wafanyabiashara wake wavuke bahari? huoni kwamba hapo kwamba kitu ni uongozi tu.
Halafu nasema kwanini kama bara tunaiona zanzibar ni mzigo tukaichia ikajishughulikia yenyewe?

Gari ikiwa inaleta hasara kwanini usiiuze?
Bara bado tunainyenyekea Zanzibar
 

Biashara gani unayoizungumzia? Hiyo ya kwenda darajani kununua sidiria kuja kukopesha wakina mama wa maofisini Dar? Watu walikuwa wakienda Zanzibar kwa sababu kodi Zanzibar ni chini kuliko Tanganyika kwa hiyo vitu vilikuwa vikipatikana kwa bei poa maana walikuwa wakiviingiza bila kulipa ushuru. Moja ya malalamiko ya wenzetu kuhusu TRA kuwaharibia biashara ni hili. TRA walipoanza kutoza tofauti ya ushuru wa Tanganyika na Zanzibar biashara ikadoda! Ilikuwa ni biashara ya kimachinga tu.

Unaposema tuiachie iende unadhani ni rahisi kama kutoa talaka rejea? Hakuna kiongozi wa Zanzibar aliyedai kuwa Muungano uvunjwe. Hata Maalim anapata kigugumizi. Wanachodai wao ni kurekebishwa kwa yale wanayoyaona ni kero kwao. Wengine tunasema ( sisi si wanasiasa) ili kukata mzizi wa fitna ni muhimu wananchi waulizwe maoni yao juu ya huu Muungano wetu. Ingawa hatukuulizwa tulipoungana, tutasutwa na vizazi vijayo kama tutauvunja bila kuwashirikisha raia wa nchi yetu. Baada ya kupata maoni yao ndio tuamue nini cha kufanya. Kama wataridhia (pande zote mbili, Tanganyika na Zanzibar) basi tuangalie namna ya kuurekebisha maana wenye chao wameishazungumza. Kama mmoja wao akikataa huu Muungano basi tuanze hatua za kutengana kwa amani.

Wanaoinyenyekea Zanzibar ni wanasiasa wala si wananchi.
 
ONE DAY YES ZANZIBAR WILL BE FREE FROM MKOLONI MWEUSI ,WACHENI TULANE WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HATUMALIZANI ,ILA NAOGOPA USALAMA WA WATANGANYIKA UMO MIKONONI MWA HUU MUUNGANO SIKU UKISAMBARATIKA NDIPO SIKU TANGANYOKA ITAKAPOTOA WAKIMBIZI ,JAPO HIVI SASA WAPO WANAOKIMBIA Mapigano ya kikabila ila watapatikana wa kitaifa.
GOD BLESS ZANZIBAR , Halafu Muungano mbona ulikwisha kufa zamani imebaki mazishi tu maana bado maiti hajapatikana.
HAPPY X-MASS to everyone out there , Dont panic still the time gap is high .
Hata kama CUF hawatotaka kuuvuruga muungano bado wenye siasa zenye msimamo mkali wataendeleza mapambano ya kuidai Zanzibar ---as marehemu Mtakatifu BOB MARLEY alipoiambia jamii ya kimasikini GET UP STAND UP & STAND UP FOR YOUR RIGHT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…