Kabla ya hatua hiyo/pendekezo lako kuchukuliwa hatua, hapana budi kulipia fidia kwa kuipunja Zenj kwa miaka 40 katika rasilimali za Tz
Mie naona hata sisi Watangayika twaonewa sana. Zanzibar ni kama kimkoa kimoja cha Tanganyika ila makelele utafikiri kuna alimasi kila kona huko. ...
Nyinyi Watanganyika mnaonewa na nani ? Ni nani aliwaunganisha na "kimkoa kimoja," wakoloni wa Kiingereza au United Nations ?
Nani anawazuieni kukata mzizi wa fitina ?
Tatizo la ka- inzi mwisho wake ni Chumbe..je, ka-inzi ka jamii forums kanaweza kunusu kilichomo kwenye ripoti??
Nyinyi Watanganyika mnaonewa na nani ? Ni nani aliwaunganisha na "kimkoa kimoja," wakoloni wa Kiingereza au United Nations ?
Nani anawazuieni kukata mzizi wa fitina ?
Mafuta hata Tanganyika yapo,kama mtu anaweza kupata data kutoka katika wizara ya Mali asili unaweza kuliona hilo ,tena yapo mengi sana kinachowasumbua ni kina cha mafuta hayo ukilinganisha na kina cha mafuta yaliopo katika bahari za Zenji ambayo yapo juu juu na ni rahisi kuyabukua.
Na mafuta yenyewe sasa yameanza kuanguka kibei japo wanasema ni mbinu za kurekebisha uchumi.
Ila iweje zaabu na almasi na mawe mingine yasiwepo katika Mali za Muungano au mambo ya Muungano la kujiuliza hapa hivi hizi ni mali za nani ?
Wazenji wanahoji mbona haya mawe hayamo kweny mali za Muungano iweje mafuta yapelekwe kwenye mambu ya Muungano ,suali linabakia haya mawe ni mali za kina nani ?
Kabla ya hatua hiyo/pendekezo lako kuchukuliwa hatua, hapana budi kulipia fidia kwa kuipunja Zenj kwa miaka 40 katika rasilimali za Tz
On what are u basing ur claim? Please quantify what mengi sana is.
FM,Thibitisha basi unayosema. Zenj imepunjwa vipi katika miaka 40 katika RASILIMALI za TZ? Mathlani, ni rasilimali zipi za Zenj ambazo JMT imenyang'anya na rasilimali zipi za JMT ambazo ziko bara lakini wazenj hawafaidiki! Au ndiyo mambo ya changu changu, chako chetu?
Thibitisha basi unayosema. Zenj imepunjwa vipi katika miaka 40 katika RASILIMALI za TZ? Mathlani, ni rasilimali zipi za Zenj ambazo JMT imenyang'anya na rasilimali zipi za JMT ambazo ziko bara lakini wazenj hawafaidiki! Au ndiyo mambo ya changu changu, chako chetu?
FM,
Wao wanadai kuwa TUMEKUWA TUKIPEWA MISAADA kama TANZANIA na misaada ikija basi tunaifanya kuwa ya Tanganyika. Tunaigawana sisi peke yetu bila wao kuwapa kitu. Madini tukiuza pia twagawana wenyewe bila wao kuwapa. Imekuja GAS pia tunafaidi wenyewe bila wao kuwapa (ingawa ninavyofahamu ni kuwa wanapata umeme wa dezo miaka kibao).
Sasa yamekuja mafuta tunataka yawe ya Muungano. Huu kwao ni WIZI wa waziwazi. Ila mie hapa nina swali moja. Nafahamu kwenye serikali ya Zanzibar hawana wizara nne. Ndani, Nje, Ulinzi na FEDHA. Ina maana kwenye hili tuna bajeti moja. Kama zinakuja hela za misaada na kuwekwa kwenye bajeti, si inamaana kuwa na wao ndiyo wanapatia humohumo? Au mie sielewi vizuri? Sasa huu wizi wa hela ya MISAADA uko wapi?
Ila nafikiri wenzetu vya DEZO wanavipenda. Wakishasikia MISAADA basi inakuwa shida. Hata wakijitenga, sidhani kama itaishia hapo. Miaka 40 wamejifunza kulilia Changu changu, chako changu. Wana uzoefu kwa hili na si ajabu imeshakuwa tabia. Sidhani kama wataishia hapo tu au kwena mbele.
Zaidi ya maelezo ya Sikonge katika paragrafu y kwanza, mgao kwa SMZ kwa muda mrefu umekuwa kwenye makabrasha tu, na ni asilimia kidogo tu... Tena hii inahusu misaada toka nje ya TZ na sio Maliasili ya TZ ambayo katika miaka ya karibuni imekuwa ikiendelezwa kibiashara zaidi tofauti na hapo zamani ilipokuwa ikiendesha na mtu mmoja mmoja.
Katika miaka ya tisini tatizo hili liliwekwa wazi na ni baada ya SMZ kuchoshwa kudai haki yao ambayo TZ Bara walikuwa wanaifanya kama kuisaidia Tz visiwani. Vikao vingi vilifanyika kurekebisha hilo tatizo ingawa sio kwa ufanisi wa kutosha, kutokana na baadhi ya wawakilishi wa Zenj kuburuzwa kwenye maafikiano.
Tz bara inachimba gasi kwa miaka kadhaa sasa lakini TZ visiwani wamekuwa hawapewi mgao wao kutokana na gesi hiyo zaidi ya kuinunua inapotumika kuzalishia umeme. Kama ripoti inavyosema kuwa ni shirika moja tu ambalo linahusika na uagizaji, ugawaji wa mafuta na uendelezaji wa gasi, shirika hilo lipo TZ bara na halina hata sura ya Muungano. Iweje kuwepo kwa fufunu ya mafuta huko Zenj wao wajitie ni ya muungano?
Yaani kweli mnataka tugawane gesi au mapato yake? Nijuavyo mimi gesi inayochimbwa haiuzwi nje bali inatumika kuzalisha umeme ambao hata wazenj wanafaidika! Huo umeme unaosema wazenj wananunua wanauziwa kwa bei ya chini kuliko gharama za uzalishaji wakati wenzao bara kila kukicha wanapandishiwa! Pamoja na bei nafuu, hawaishi kukopa. Sasa juu ya yote hayo unataka wapelekewe mitungi ya gesi!
Mapato yote haya (ya gesi, dhahabu, utalii n.k.) yanaenda chungu kimoja kuchangia bajeti ya serikali ya Muungano. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia wanajeshi wanaolinda uhuru wetu (pamoja na Zenj), balozi zetu zinazotuwakilisha wote n a kadhalika na kadhalika. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia madeni ambayo serikali ya muungano inadaiwa kutokana na miradi iliyofanyika kote. Mapato hayo ndiyo yanayoenda kuisaidia serikali ya Mapinduzi wanapokosa pesa za kulipia umeme na/au kuwalipa wafanyakazi wao. Leo mnataka tufanye biashara ya kishihiri kuanza kugawana mapato ya kila kitu kinachopatikana bara.
Serikali ya Mapinduzi je inatoa mchango gani katika serikali ya muungano ambayo yenyewe ni sehemu? Mbona siwasikii mkizungumzia kukatiwa sehemu ya mzigo wa madeni tunayodaiwa? Au mnaamini hiyo misaada yote ilikuwa ni grants? Hiyo misaada mara nyingi ilielekezwa kwenye maeneo ambao watoaji walipendelea. Leo ndugu zako waFinn wakiamua kutusaidia kwenye sekta ya maji Lindi unataka tuwaambie hapana lazima wawekeze na Pemba? Na waNorway wakiamua kuwekeza kwenye umeme Zanzibar tuwaambie hapana lazima wakaweke na Lindi? Kweli wenzetu hampendeki!