Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Kabla ya hatua hiyo/pendekezo lako kuchukuliwa hatua, hapana budi kulipia fidia kwa kuipunja Zenj kwa miaka 40 katika rasilimali za Tz
 
Kweli wajinga ndio waliwao! tunatafuta formula ya kugawana kabla kuthibitika kwa uwepo wa mafuta yenyewe talk abt kufanya baby shower kabla mtoto kuzaliwa!

Mr Reading atakuwa kushachukua mchuzi wake na he must be laughing all the way to the bank!
 
Mie naona hata sisi Watangayika twaonewa sana. Zanzibar ni kama kimkoa kimoja cha Tanganyika ila makelele utafikiri kuna alimasi kila kona huko. ...

Nyinyi Watanganyika mnaonewa na nani ? Ni nani aliwaunganisha na "kimkoa kimoja," wakoloni wa Kiingereza ? Au United Nations ?

Nani anawazuieni kukata mzizi wa fitina ?
 
Nyinyi Watanganyika mnaonewa na nani ? Ni nani aliwaunganisha na "kimkoa kimoja," wakoloni wa Kiingereza au United Nations ?

Nani anawazuieni kukata mzizi wa fitina ?

Kuhani,
Nafikiri Nyani kanisaida. Na kwa lengo moja au jingine nilifuta ujumbe. CCM ndiyo wenye Tanzania, Tanganyika na Zanzibar. Hapa hakuna Waislaam wala Wakristo au wapagani. Hakuna Wabara au Wapwani. CCM wamejitengenezea kajumuia kao. Ni au umo ndani unafaidi na au uko nje. Ka jumuia ka ubabe sana na kukaa ndani ni kazi kweli kwani kila mtu ni kama mbegu ya kiume, yuko busy kwenda kwenye YAI ili yeye awe baba wa nchi Tanzania. Hawa jamaa kwa kutumia jeshi na Polisi ukiongeza na Usalama wa Taifa, wanaweza kumshughulikia kila kenge atayejifanya kuwafundisha kazi au kuwaondolea mnofu wao. Hawa jamaa maisha yao ni kama Mbwa mwitu. Wanashirikiana kushambulia ila nyama ikishapatikana, kila mtu anawahi pande lake. Wazenji wanafanya makosa kusema hayo mapande hata sisi tunafaidi.
Nyani kauliza, "Vipi Dokta Masau...?"
 
.....yaani CCM na CUF waliungana kwenye hili na kusema ni mali ya WaZanzibari? na kwa kupitia post hapo juu utajua tuu wazanzibari ni kina nani? maana wakali kweli kweli na wameshaanza kusema wameonewa kwa miaka 40...mafuta kweli yakipatikana sitashangaa wabara wote wakitimuliwa zanzibar na wazanzibar kwa asilimia 100 watapiga kura kujitoa kwenye muungano,huu muungano ni very delicate na hata sioni future yake na kinachowaweka wazanzibar kwenye muungano ni utemi na vitisho vya CCM na umaskini wa Zanzibar...hawa watu waachieni nchi yao kwa asilimia 100 wafaidi samaki wao,karafuu na mafuta yao kama kweli yapo,halafu ndoto yao ya Islamic state itimie...hizo bilioni 100 tunazopeleka huko kila mwaka bora zijenge highway zetu mkoa mpaka mkoa.
 
Mafuta hata Tanganyika yapo,kama mtu anaweza kupata data kutoka katika wizara ya Mali asili unaweza kuliona hilo ,tena yapo mengi sana kinachowasumbua ni kina cha mafuta hayo ukilinganisha na kina cha mafuta yaliopo katika bahari za Zenji ambayo yapo juu juu na ni rahisi kuyabukua.
Na mafuta yenyewe sasa yameanza kuanguka kibei japo wanasema ni mbinu za kurekebisha uchumi.
Ila iweje zaabu na almasi na mawe mingine yasiwepo katika Mali za Muungano au mambo ya Muungano la kujiuliza hapa hivi hizi ni mali za nani ?
Wazenji wanahoji mbona haya mawe hayamo kweny mali za Muungano iweje mafuta yapelekwe kwenye mambu ya Muungano ,suali linabakia haya mawe ni mali za kina nani ?
 
On what are u basing ur claim? Please quantify what mengi sana is.
 
Kabla ya hatua hiyo/pendekezo lako kuchukuliwa hatua, hapana budi kulipia fidia kwa kuipunja Zenj kwa miaka 40 katika rasilimali za Tz

Thibitisha basi unayosema. Zenj imepunjwa vipi katika miaka 40 katika RASILIMALI za TZ? Mathlani, ni rasilimali zipi za Zenj ambazo JMT imenyang'anya na rasilimali zipi za JMT ambazo ziko bara lakini wazenj hawafaidiki! Au ndiyo mambo ya changu changu, chako chetu?
 
On what are u basing ur claim? Please quantify what mengi sana is.

The Company will have to negotiate the terms of a Production Sharing Agreement (PSA) before any work can commence.
Oil seeps and surface slicks are well known on the surface of Lake Tanganyika whose South Block covers approximately 5,400 square kilometres. It forms part of the western arm of the 6,400-kilometre long East African Rift system as does Lake Albert
 
Thibitisha basi unayosema. Zenj imepunjwa vipi katika miaka 40 katika RASILIMALI za TZ? Mathlani, ni rasilimali zipi za Zenj ambazo JMT imenyang'anya na rasilimali zipi za JMT ambazo ziko bara lakini wazenj hawafaidiki! Au ndiyo mambo ya changu changu, chako chetu?
FM,
Wao wanadai kuwa TUMEKUWA TUKIPEWA MISAADA kama TANZANIA na misaada ikija basi tunaifanya kuwa ya Tanganyika. Tunaigawana sisi peke yetu bila wao kuwapa kitu. Madini tukiuza pia twagawana wenyewe bila wao kuwapa. Imekuja GAS pia tunafaidi wenyewe bila wao kuwapa (ingawa ninavyofahamu ni kuwa wanapata umeme wa dezo miaka kibao).
Sasa yamekuja mafuta tunataka yawe ya Muungano. Huu kwao ni WIZI wa waziwazi. Ila mie hapa nina swali moja. Nafahamu kwenye serikali ya Zanzibar hawana wizara nne. Ndani, Nje, Ulinzi na FEDHA. Ina maana kwenye hili tuna bajeti moja. Kama zinakuja hela za misaada na kuwekwa kwenye bajeti, si inamaana kuwa na wao ndiyo wanapatia humohumo? Au mie sielewi vizuri? Sasa huu wizi wa hela ya MISAADA uko wapi?
Ila nafikiri wenzetu vya DEZO wanavipenda. Wakishasikia MISAADA basi inakuwa shida. Hata wakijitenga, sidhani kama itaishia hapo. Miaka 40 wamejifunza kulilia Changu changu, chako changu. Wana uzoefu kwa hili na si ajabu imeshakuwa tabia. Sidhani kama wataishia hapo tu au kwena mbele.
 
Zaidi ya maelezo ya Sikonge katika paragrafu y kwanza, mgao kwa SMZ kwa muda mrefu umekuwa kwenye makabrasha tu, na ni asilimia kidogo tu... Tena hii inahusu misaada toka nje ya TZ na sio Maliasili ya TZ ambayo katika miaka ya karibuni imekuwa ikiendelezwa kibiashara zaidi tofauti na hapo zamani ilipokuwa ikiendesha na mtu mmoja mmoja.

Katika miaka ya tisini tatizo hili liliwekwa wazi na ni baada ya SMZ kuchoshwa kudai haki yao ambayo TZ Bara walikuwa wanaifanya kama kuisaidia Tz visiwani. Vikao vingi vilifanyika kurekebisha hilo tatizo ingawa sio kwa ufanisi wa kutosha, kutokana na baadhi ya wawakilishi wa Zenj kuburuzwa kwenye maafikiano.

Tz bara inachimba gasi kwa miaka kadhaa sasa lakini TZ visiwani wamekuwa hawapewi mgao wao kutokana na gesi hiyo zaidi ya kuinunua inapotumika kuzalishia umeme. Kama ripoti inavyosema kuwa ni shirika moja tu ambalo linahusika na uagizaji, ugawaji wa mafuta na uendelezaji wa gasi, shirika hilo lipo TZ bara na halina hata sura ya Muungano. Iweje kuwepo kwa fufunu ya mafuta huko Zenj wao wajitie ni ya muungano?
 
Salaam Wakubwa humu jamvini

jamani kuna swala linanisumbua, hivyo naomba michango yenu kimawazo....

eti ni kwa nini baadhi ya shule binafsi nchini zinaendeshwa kama miradi ya kuku, kwani wamiliki wake wanashindwa kuwa na mipango endelevu na taratibu nzuri za kiuendeshaji. taratibu hizo zinaweza kuwa za kifedha, uongozi na utawala ikiwa ni pamoja na utoaji wa maamuzi mbalimbali mazito juu ya hatma ya wanafunzi bila kujali utu.

Mfano hai ni huyu Mrs. Bayi mbaye ni Mke wa Bw. Bayi nani Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari ya Filbert Bayi. Jamani huyu mama amekuwa na mtindo wa kujichukulia mamlaka makubwa mikono mwake kiasi cha kufukuza wanafunzi bila kuzingatia sheria na taratibu mbalimbali.

tafadhali mawazo (ideas) needed
 
Kamanda karibu sana, ila hapa sio mwake kwa tatizo lako...Jaribu kufungua bandiko jipya ili uweze kuchangiwa kwa kina..
 
Zaidi ya maelezo ya Sikonge katika paragrafu y kwanza, mgao kwa SMZ kwa muda mrefu umekuwa kwenye makabrasha tu, na ni asilimia kidogo tu... Tena hii inahusu misaada toka nje ya TZ na sio Maliasili ya TZ ambayo katika miaka ya karibuni imekuwa ikiendelezwa kibiashara zaidi tofauti na hapo zamani ilipokuwa ikiendesha na mtu mmoja mmoja.

Katika miaka ya tisini tatizo hili liliwekwa wazi na ni baada ya SMZ kuchoshwa kudai haki yao ambayo TZ Bara walikuwa wanaifanya kama kuisaidia Tz visiwani. Vikao vingi vilifanyika kurekebisha hilo tatizo ingawa sio kwa ufanisi wa kutosha, kutokana na baadhi ya wawakilishi wa Zenj kuburuzwa kwenye maafikiano.

Tz bara inachimba gasi kwa miaka kadhaa sasa lakini TZ visiwani wamekuwa hawapewi mgao wao kutokana na gesi hiyo zaidi ya kuinunua inapotumika kuzalishia umeme. Kama ripoti inavyosema kuwa ni shirika moja tu ambalo linahusika na uagizaji, ugawaji wa mafuta na uendelezaji wa gasi, shirika hilo lipo TZ bara na halina hata sura ya Muungano. Iweje kuwepo kwa fufunu ya mafuta huko Zenj wao wajitie ni ya muungano?

Yaani kweli mnataka tugawane gesi au mapato yake? Nijuavyo mimi gesi inayochimbwa haiuzwi nje bali inatumika kuzalisha umeme ambao hata wazenj wanafaidika! Huo umeme unaosema wazenj wananunua wanauziwa kwa bei ya chini kuliko gharama za uzalishaji wakati wenzao bara kila kukicha wanapandishiwa! Pamoja na bei nafuu, hawaishi kukopa. Sasa juu ya yote hayo unataka wapelekewe mitungi ya gesi!

Mapato yote haya (ya gesi, dhahabu, utalii n.k.) yanaenda chungu kimoja kuchangia bajeti ya serikali ya Muungano. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia wanajeshi wanaolinda uhuru wetu (pamoja na Zenj), balozi zetu zinazotuwakilisha wote n a kadhalika na kadhalika. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia madeni ambayo serikali ya muungano inadaiwa kutokana na miradi iliyofanyika kote. Mapato hayo ndiyo yanayoenda kuisaidia serikali ya Mapinduzi wanapokosa pesa za kulipia umeme na/au kuwalipa wafanyakazi wao. Leo mnataka tufanye biashara ya kishihiri kuanza kugawana mapato ya kila kitu kinachopatikana bara.

Serikali ya Mapinduzi je inatoa mchango gani katika serikali ya muungano ambayo yenyewe ni sehemu? Mbona siwasikii mkizungumzia kukatiwa sehemu ya mzigo wa madeni tunayodaiwa? Au mnaamini hiyo misaada yote ilikuwa ni grants? Hiyo misaada mara nyingi ilielekezwa kwenye maeneo ambao watoaji walipendelea. Leo ndugu zako waFinn wakiamua kutusaidia kwenye sekta ya maji Lindi unataka tuwaambie hapana lazima wawekeze na Pemba? Na waNorway wakiamua kuwekeza kwenye umeme Zanzibar tuwaambie hapana lazima wakaweke na Lindi? Kweli wenzetu hampendeki!
 
Fm na Kibunago,
Hapa ndiyo lilikuwa swali langu. Acha nilifungulie thread mpya ili lionekane na wachangiaji wengi na ikibidi baadaye lichanganywe na hili. Swala hasa ni ukusanyaji wa mapato ya ZENJI na TRA.
 
Fundi Mchundo,

..waZanzibari wamezoea vya bure hao na wanatunyonya.

..Prof.Teddy Malyamkono, pamoja na wanazuoni wenzake, wameandika kitabu kinachochambua jinsi Zanzibar inavyoishi kwa kuomba-omba Tanzania Bara.

Sikonge,

..ZNZ wana wizara yao ya fedha na kila mwaka wana bajeti ya Serikali yao.

..jaribu kutafuta hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha ZNZ utaona kwamba wanapata misaada toka nje. labda hapa tuangalie misaada inayokwenda ZNZ, tulinganishe na idadi ya watu, tuone kama wanapunjwa.

..ZNZ ina mamlaka yake ya mapato, lakini sielewi ina kazi gani tofauti na TRA.
 
Yaani kweli mnataka tugawane gesi au mapato yake? Nijuavyo mimi gesi inayochimbwa haiuzwi nje bali inatumika kuzalisha umeme ambao hata wazenj wanafaidika! Huo umeme unaosema wazenj wananunua wanauziwa kwa bei ya chini kuliko gharama za uzalishaji wakati wenzao bara kila kukicha wanapandishiwa! Pamoja na bei nafuu, hawaishi kukopa. Sasa juu ya yote hayo unataka wapelekewe mitungi ya gesi!

Mapato yote haya (ya gesi, dhahabu, utalii n.k.) yanaenda chungu kimoja kuchangia bajeti ya serikali ya Muungano. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia wanajeshi wanaolinda uhuru wetu (pamoja na Zenj), balozi zetu zinazotuwakilisha wote n a kadhalika na kadhalika. Bajeti hiyo ndiyo inayolipia madeni ambayo serikali ya muungano inadaiwa kutokana na miradi iliyofanyika kote. Mapato hayo ndiyo yanayoenda kuisaidia serikali ya Mapinduzi wanapokosa pesa za kulipia umeme na/au kuwalipa wafanyakazi wao. Leo mnataka tufanye biashara ya kishihiri kuanza kugawana mapato ya kila kitu kinachopatikana bara.

Serikali ya Mapinduzi je inatoa mchango gani katika serikali ya muungano ambayo yenyewe ni sehemu? Mbona siwasikii mkizungumzia kukatiwa sehemu ya mzigo wa madeni tunayodaiwa? Au mnaamini hiyo misaada yote ilikuwa ni grants? Hiyo misaada mara nyingi ilielekezwa kwenye maeneo ambao watoaji walipendelea. Leo ndugu zako waFinn wakiamua kutusaidia kwenye sekta ya maji Lindi unataka tuwaambie hapana lazima wawekeze na Pemba? Na waNorway wakiamua kuwekeza kwenye umeme Zanzibar tuwaambie hapana lazima wakaweke na Lindi? Kweli wenzetu hampendeki!

Fundi:

Umezungumza jambo la maana kuhusu umeme. Cha muhimu tuwachie mafuta na wao watuuzie kwa bei nafuu kama vile tunavyowauzia umeme.

Mi sioni sababu wa kulalamika hapa. Kama mkulima wa Kagera anaweza kumiliki shamba na kuzuia mapato yake mwenyewe. Kwanini waZanzibar wasifanye hivyo au wasukuma wasifanye hivyo kwenye migodi ya dhahabu?

Hata hiyo gesi inayotoka Songosongo, mapato yabaki hukohuko. Hii falsafa ya spread the wealth inafanya nchi kuwa masikini tu.

Mapato yabaki yalikotoka. Tuache kuombaomba wahisani na shughuli za maendeleo zitokane na mapato ya sehemu hizo. Tuone kama tunakuwa na migogoro.
 
Back
Top Bottom