Inabidi nicheke sana. Posti yangu moja umejibu mara mbili. Na unaanza kuleta mambo ya CUF. Fundi usitolee macho mafuta ya watu. Vya watu kuliwa kazi.

Nilishakwambia kwetu Morogoro. Na uungaji wangu mkono hauna maana mimi natoka Zanzibar. Ninachopendelea ni kuwa local governments au mamlaka za mikoa au majimbo ziwe ndizo zenye kuchukua sehemu kubwa ya mshiko.

Kwa juhudi zako za posti mbili nitajibu kwa kirefu katika posti hii. Kwanza nakuomba achana na kufuatilia Stump Speeches na maoni ya pundits. Na uliza wachumi sababu za kweli kuhusu ongezeko la bei la mafuta Marekani katika kipindi cha Summer 2008.

Wanasema sio technology au capital itakayokupa maendeleo bali who is behind it. Kama watanzania tuna vichwa vizuri, kwa vitu tulivyo navyo sasa tungefanya wonders. Mafuta hayatakubalisha Fundi Mchundo kuacha uroho wako wa kuwa na Lexus tatu na kuiba kutoka account ya EPA. Mafuta, hayatakufanya wewe umalize ujenzi wa makao makuu Dodoma au Makazi kule Michenzani au kuendesha shirika la reli.

Tukirudi mafuta ni commodity kama kahawa au sukari. Na thamani yake inafuata kanuni za kiuchumi kama commodities zingine. Hivyo ukielewa kanuni za kiuchumi za commodities mojawapo ikiwa hile ya supply and demand huwezi ukatolea mimacho kama mjusi aliyebanwa na mlango mali za asili iwe dhahabu au mafuta.

Nchi ulizozitaja kama vile Gabon, Botswana, Equatorial Guinea na nchi za Kiarabu zimefaidika sana na mafuta au madini. Lakini vile ukumbuke population za nchi hizo ni ndogo hivyo mapato yanayotokana na madini au mafuta yanachangia sana GDP.

Kwa mfano:
Equatorial Guinea inategemea uuzaji wa mafuta na GNI per capita: US $12,860 (source world bank). Population yake ni 500,000 (Nusu milion).

Hivyo Net Income ya Equatorial Guinea = US $12,860 x 500,000 = US $6430000000

Wakati huo huo Population ya Tanzania ni 40.4 million. Tukigawa Net Income ya Equatorial Guinea kwa population ya Tanzania $6,430,000,000/40,000,000 = US 160.


Nchi yetu ni kubwa na population yake ni kubwa. Hivyo tunatakiwa ku-diversify portfolio yetu. Hatutakiwi kuweka mayai kwenye kapu moja. Kama Zanzibar inaweza kuendelea kwa mafuta waachieni. Kama Mara wanaweza kutumia dhahabu waachieni. Na kama Mtwara wanaweza kutumia gesi waachieni. Hizi ni commodities tu. Nyerere aliwabana wazalishaji wa kahawa mpaka walishindwa kupeleka watoto shule. Lakini matumizi ya kahawa hayakulisaidia taifa zaidi ya kuwafanya wazalishaji wa zao hilo kuwa masikini.

Kwa ukubwa wa nchi yetu ni lazima tuonyeshe kila sehemu imeendelea kwa kutumia injini zipi. Huwezi kuendeleza nchi kama Tanzania kwa kukusanya mapato yote kwenye serikali kuu na baadaye kuyagawanya kwa kila mkoa. Ndio maana watu hamtaki kuondoka DSM.

Vilevile mafuta yakipatikana Zanzibar, Tanzania bara itafaidika vikubwa bila ya kumiliki rasimali yenyewe. Kwanza Mafuta ni commodity inayohitajika kila sehemu. Hivyo nchi kama Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi n.k Zitatumia bandari ya DSM. Vilevile refineries zitakuwepo. Na vilevile bei itakuwa stable.

Vilevile kutakuwepo na by products zinazotokana na mafuta. Na kama ilivyotokea Nigeria, uchimbaji wa mafuta utafanya watu kusahau kazi walizozijua kwa miaka mingi, itafanya Tanzania bara kupata soko la nguvu huko Zanzibar.

Kama ulivyosema kuwa nchi Asia zimeendelea kwa sababu ya location yao na Japan. Location ya Tanzania Bara kuwa karibu na Zanzibar itatusaidia kiuchumi kama mafuta yapo Zanzibar na hata kama mafuta hayo yanamilikiwa na waZanzibar kwa 100%. Lakini kwa uzembe na excuses zako Fundi, Mafuta yatapitia bandari ya Mombasa na wewe utasubiri ushuru wa TRA tu.

Hiyo achana na mambo ya securities unapoongea masuala ya uchumi. Masuala ya securities yamefanya nchi za kiafrika kutumia sana mapato yake katika masuala ya kijeshi.

My hair hurts now.
 
Huwa sipendi kusema hili lakini, Mkuu Zakumi, inaelekea umesoma lakini haujaelimika.

Unasema kuwa ni mchumi lakini unalinganisha mapato ya Equatorial Guinea na JMT? Aliyekuambia nani kuwa mafuta (kama yapo) yatawiiana na yale ya Equatorial Guinea na sio ya Sudan?

Unadai kuwa impact ya mafuta au madini mengine ni kutokana na idadi ya watu. Sasa kwa nini nchi kama Botswana imeweza kupata maendeleo ya dhati wakati nchi kama Equatorial Guinea au Gabon pamoja na kuwa na GNP per capita kubwa maendeleo ya watu wake ni duni? Nchi zote hizi hazina watu wengi!

Halafu unalinganisha Mara na Zanzibar? Tangu lini watu wa Mara wakawa na bunge lao? Au serikali yao. Hapa tunazungumzia entities zilizo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo ni Zanzibar kwa upande mmoja na JMT kwa upande mwingine. Ninavyojua mimi hakuna serikali ya Tanzania Bara kama unavyo insinuate. Na ninavyojua mimi ni kuwa serikali ya Zanzibarna baraza la Mapinduzi la Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania, JMT ikiwa supreme.

Tofauti na unavyosema, kuweko kwa mafuta ndiko kutakakozidisha uroho wa Fundi Mchundo. Badala ya Lexus atataka Bentley. Badala ya nyumba Mbezi Beach atataka kuongeza nyingine Hampton Beach, Monaco n.k na kijibanda cha nyumba ndogo Dubai. Na ili kuhakikisha kuwa wadanganyika hawafurukuti ataenda Ukraine na Uchina kunua silaha kibao kuwashikisha adabu. Of course manunuzi haya hayatakosa vijisenti vitakavyoishia kwenye akaunti zake zilizoko Cayman Islands.

We Msomi mchumi uliyebobea, unalinganisha dhahabu na mafuta? Unadhani kama upatikanaji wa dhahabu kutoka Afrika ya Kusini utaanza kuwa na walakini Marekani itavamia Afrika ya Kusini? Kama commodity zote ni sawa mbona Cartel ya kahawa(ICO) haiyumbishi uchumi wa dunia kama Opec?

Sijali kama kwenu ni Morogoro, Mkuranga au Pemba. Nakupinga kwa sababu hoja yako kwangu mimi haina mantik.

Vile vile bei ya mafuta haina nafasi katika argument yangu ingawa unataka kuiingiza. Mimi sijali kama Zanzibar wanachukua asilimia mia ya kodi au mapato yeyote kutoka katika mafuta yatakayopatikana huko. Ninachosema mimi ni kuwa kama Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima Bunge la Muungano liwe na kauli ya mwisho kuhusu sera zinazohusu rasilimali hiyo. Sera zitahusu masuala ya mazingira, nani atakayeruhusiwa kuwekeza katika sekta hiyo, mchango wa mafuta hayo katika uchumi wa nchi ( kipesa au kwenye akiba ya tahadhari) n.k. Nchi ya Zanzibar haiwezi kuruhusiwa kukaribisha wawekezaji kutoka nchi ambazo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania una matatizo nzao (Kama zipo). Mathlan, Al Qaeda wachukue nchi ya Afghanistan, JMT haiwezi kuiruhusu Zanzibar kuiuzia mafuta nchi hiyo ati kwa vile mafuta yanapatikana kwake! Nchi ya Zanzibar haiwezi kuruhusiwa kuruhusu uchimbaji na usafirishaji wa mafuta utakaoathiri mazingira ya watu wake na wale wa Tanzania bara. Mgawanyo wa mapato ni sehemu ndogo katika sera.

Sikuingiza mambo ya CUF bali nimekufahamisha kuwa waziri kivuli wa wizara ya Nishati na Madini ya JMT ni Mh. Mohamed Habib Mnyaa ambaye anawakilisha jimbo la Mkanyageni lililoko Mkoani Kusini Pemba kupitia chama cha CUF. Wizara hii ndiyo inayosimamia sera za madini na nishati katika JMT na huyu mzanzibari ndiye mwenye dhamana ya kuangalia na kuikosoa. Sasa kwa vipi wazanzibari wadai kuwa hawashirikishwi katika masuala ya gesi, dhahabu n.k.?

Mwisho kabisa unalinganisha security na kuwa na jeshi! Kama kusoma kwenyewe ndiyo huku, nashukuru kuwa nilikwepa umande!

Ushauri mdogo. Ukitaka kuheshimika usipende kutumia maneno ya kejeli dhidi ya watu usiowajua!
 
Wapeni mafuta yaliyo ndani ya eneo lao. Rasilimali zote za asili na nishati mbalimbali ni bora zikafanywa ziwe aidha za visiwani au bara pekee. Natambua ya kwamba hakuna serikali ya Tanzania bara lakini Tanzania bara si ipo?


Mtaalamu kasema hakuna mafuta Zanzibar na walimparamia vibaya sana! Salama ya huu Muungano ni Zanzibar kutokuwa na Mafuta kama yapo Muungano uko kikaangoni!

Sijui huo uhakika wa mafuta Zanzibar wamepata wapi, kwa uelewa wangu mdogo kama Mafuta yapo Zanzibar hapa Tangantika lazima yatakuwepo and viceversa. Hivi karibuni nilisika kampuni moja ya Mafuta imeanza kuchimba au kutafiti mafuta Mwambao wa Tanga na wakaomba viongozi wa vijiji wawasaidie kutoa taarifa kwa wavuvi ili wavuvi wasije wakaogopa. Kuna feedback yoyote imepatikana?
 
Nakubaliana kabisa na mawazo yako Fundi. Ingawa siyo mawazo popular katika jamii yetu hasa kwa kule kwetu Zenj. Pengine hili linanatokana na wengi kutokuelewa nini kinajiri katika mafuta, na kufikiria sana ule mshiko tu unaotokana na mafuta. Ni kweli kabisa mafuta sio kama almasi wala siyo kama dhahabu, Mafuta ni zaidi ya hapo. Na Kwa vile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina-exist. lazima iwe na control ya mafuta hayo, ili iweze kudhibiti usalama, mazingira na kufanikisha foreign policy na International rerlations. Lakini Bwana wee huo mshiko lazima uwape faraja zaidi wa Zenj. Sisi wa Bara tuache kukodolea sana mshiko wao.
 
Nyinyi Watanganyika mnaonewa na nani ? Ni nani aliwaunganisha na "kimkoa kimoja," wakoloni wa Kiingereza ? Au United Nations ?

Nani anawazuieni kukata mzizi wa fitina ?

Teheee teheee, ukweli bwana sijui mkwanini huwa unauma.
 

Hilo la mshiko halina ubishi. Itakuwa ni aibu kwa serikali ya Muungano kudai sehemu kubwa kuliko Zanzibar.

Tatizo litakuja yakipatikana Pemba! Nani afaidike, Pemba au unguja?
 
Hilo la mshiko halina ubishi. Itakuwa ni aibu kwa serikali ya Muungano kudai sehemu kubwa kuliko Zanzibar.

Tatizo litakuja yakipatikana Pemba! Nani afaidike, Pemba au unguja?

Mafuta na Karafuu yapo Pemba na sio Unguja ,Unguja kuna mbata tu.Tatizo ni utawala kama Utawala utakuwa chini ya CUF mafuta yatachimbwa na kufaidika Tz nzima ,watawala waliopo Tz hawakubaliki katika jamii japo wanajitangazia ni washindi halali lakini si washindi wa maridhio ya wananchi kama wananchi wangeachiwa kuchagua wamtakae kwa ridhaa yao basi hata hizi kero za Muungano zingelikwisha tatuliwa zamani ,ila kwa hawa wanaoendesha Tz chini ya mafisadi ,hakutapatikana chochote kwa faida ya Mataifa haya mawili si dhahabu,si mafuta wa gesi.
Hii gesi iliyokuwepo Tz kama serikali ingekuwa makini basi Watanzania wote wangeliweza kutumia katika matumizi ya nyumbani na kusaidia kuhifadhi misitu kwani matrumizi ya mkaa na kuni yangelipungua kwa kiasi kikukbwa ,ila kila leo ytasikia wanatest visima vya gesi.
 

Naona mwenzetu Uko Pro na Against. Kwenu hasa ni wapi? Kwenu ni Zenji ila wewe ni wa BARA. Fundi Mchundo umeielezea hii tosha kabisa. Kichuguu katuwekea na hotuba ya JKN. Ile hotuba ya mwaka 95 ni kuwa tayari fununu ya kuwepo Mafuta Zenji ilianza. Hapo ndipo jamaa wakaanza kucharuka na Kisiwa chao. Tamaa mbele mauti nyuma.
Nakubaliana na mchangiaji kuwa, kila mkoa lazima uwe unafaidi na mali asili ya sehemu hiyo. Arusha wanafaidi sana na utalii. Vyakula vyao vinasoko kubwa. Nyumba zao za kulala wageni, kazi kwenye sekta ya utalii nk. Ukija kwenye migodi ni kuwa kwanza wanakuja wazungu na kusema "hapa Sikonge kuna madini". Hapo wanakuja wana siasa na kusema pesa hizi ondokeni. Hiyo ni balaa ya kwanza. Mnafukuzwa kwenye maeneo yenu. Baadaye mtaona mashine zikija na kuchimba shimo kubwaaaa. Wakimaliza wanaachia shimo kubwa na lundo la udongo. Mkitaka basi jengeni mji pembeni na hapo mfanye shimo la taka.
Nyie Wazenji, heri mlilie mpate mgao mkubwa kwenye KEKI ila mbaki kwenye Muungano. Mkijitenga basi Au Wapemba au Waugunja watataka pia kujitenga mara mafuta yakigundulika kuwa yako kwao. Nyerere anasema kuwa hii ni kama kula nyama ya mtu. Ukijitenga, basi milele utataka kujitenga tena. Waugunja waweza kujitenga bila matatizo, ila Pemba wakijathubutu fanya hivyo basi damu itamwagika. Hivi kwa nini Karume wawili waligombea Urais? Huku kweli ni kuelewana? Halafu naona huyu balozi kapotea, sijui kafichwa wapi. Haya kazi mnayo.
 


Fundi Mchundo:

Samahani sana kwa kukukejeli. Chonde mkuu, nisamehe nipo chini ya miguu yako. Baada ya kuomba msamaha ningependa kusema kuwa inamchukua msomi aliyeelimika kumtambua aliyesoma na kushindwa kuelimika.

Pamoja na kuelimika na kusoma kwako you are dead wrong. Una tatizo la kulazimisha view points zako. Inaonyesha kuwa upo kwenye mission ya kuelimisha umma.

Thread hii inazungumza mapato ya mafuta. Utangulizi uliowekwa na ripoti inazungumzia mshiko na sio masuala mengine.

waZenj wanataka kuchukua Lion Share. Na mimi nakubaliana nao. Sioni sababu ya mimi kuzua mzozo wa kitu kisicho changu.

Vilevile nitasimama katika jukwaa langu kuwa Mafuta na Kahawa ni commodities. Na ni principals za uchumi zinazo-apply katika commodities zote.

Na vilevile ni principle za uchumi zinazofanya nchi za OPEC kuwa na nguvu kuliko nchi ICO.

Kahawa ina alternative. Ukipandisha bei ya kahawa walaji wana-alternatives nyingi. Watakunywa chai, gongo, soda, chimpum na vitu vingine. Watu wanaweza kuacha kutumia kahawa na wasipate matatizo yoyote.

Kwa upande mwingine Mafuta hayajapata alternatives ambayo itaondoa matumizi yake. Kwa mtaji huu wazalishaji wanauwezo wa ku-control supply na kuongeza bei. Lakini technologia inavyoendelea kukua, kuna uwezekano mkubwa wa Mafuta kuwa kama Mkonge na kuondoa muhimu wa OPEC.

Na kuhusu Gabon na Equatorial Guinea kushindwa kutumia ongezeko la GNI lao nitakwambia kitu kimoja tu. Inachukua muda kwa nchi ambayo ina rasimali lakini haina watu wenye elimu ku-master matumizi ya mapato yao ili kufikia maisha ya kisasa. Imewachukua waarabu zaidi ya miaka 50 kuweza ku-master matumizi ya mapato ya mafuta. Na bado kuna nchi za kiarabu zinashindwa kutumia mapato yake vizuri.

Mwisho: Mada ni mapato naomba turudi huko.
 

Bila samahani,Zakumi. Nashukuru kwa kunipa sifa ya usomi isiyo yangu.

Quote ya hapo juu nimeitoa kutoka kwenye bandiko la kwanza kwenye thread hii.

Suala hapa (kama alivyosema Waziri Mansour) ni kuingia kwa suala la mafuta ya Zanzibar katika orodha ya mambo ya Muungano. Mgawanyo wa mapato ni sehemu tu ya ishu bali hoja ya msingi ni kuwa wazanzibari hawataki serikali ya Muungano ihusike kwa njia yeyote na suala la mafuta yao. Mimi hili ndilo ninalopinga. Kwa mtazamo wangu suala la mafuta katika sehemu yeyote ya Jamhuri ya Muungano ni suala la Muungano. Mambo ya mgao wa mapato, uendeshaji wa kila siku yatatokana na sera zitakazoandaliwa na Bunge la Muungano. Bunge hilo linaweza kuagiza kuwa serikali ya mapinduzi isimamie uendeshaji na mapato kutoka mafuta hayo. Bunge hilo linaweza kusema kuwa mapato yote yanayopatikana huko yaende kwenye bajeti ya serikali ya Mapinduzi. Lakini Zanzibar kama sehemu ya Muungano ni lazima itambue authority ya Bunge la Muungano juu ya suala hili.

Vile vile sijapinga kuwa mafuta ni commodity kama kahawa au pamba. Ninachosema ni kuwa kutokana na huko kukosa alternative na umuhimu wake katika uchumi wa sasa ndiko kunakofanya mafuta kuwa suala la usalama wa taifa. Kwa sababu hiyo tu, ndiyo inanifanya niseme kuwa mafuta ni lazima liwe suala la Muungano. Karafuu, ambayo ni commodity pia, haina sifa za kufanya iwe ya Muungano kwa hiyo inaweza kusimamiwa na Baraza la Mapinduzi. Uranium,commodity nyingine, kutokana na sifa zake, nayo ni lazima iwe suala la Muungano bila kujali imepatikana wapi. Kahawa si lazima iwe ya Muungano. Na kadhalika na kadhalika.

Nadhani tumeijadili ishu hii vya kutosha na pengine ni bora tukubaliane kutofautiana.

Amandla....
 

Fundi Mchundo:

Masuala mengi nakubaliana na wewe kimsingi. Lakini mfumo wa uendeshaji wa serikali yetu haukuundwa kuwafanya watu wanaotoka katika maeneo yenye rasimali hizo wanafaidika na kile kilichopo katika mazingira yao.

Kwa ndugu zangu wasukuma serikali inaweza kufanya chochote kuhusu dhahabu na watu wakanyamaza. Lakini kwa Zanzibar hicho kitu hakitatokea.

Mambo yanayotokea Niger Delta Region, yatatokea Tanzania iwapo tutaacha kutumia akili.

Machimbo ya Tanzanite yalivumbuliwa na wananchi bila msaada wa serikali. Na kwa pretext ya national interest serikali imechukua na kuwapa wawekezaji. Wananchi wali-fight back lakini serikali ilishinda.

Investment katika mafuta inahitaji infrastucture kubwa: pipes, ports, refineries na mambo mengine. Bila kuwa na amani hizi installations itakuwa tatizo kuzilinda.
 
Mkuu Zakumi,
Haki haiji bure. Wananchi ndiyo wanaowachagua hao wanaounda serikali. Pale wanapoona hawatendewi haki ni lazima waseme bila kuogopa. Kama vile wanavyofanya wenzao waZanzibari. Wamweleze huyo mwakilishi wao wanaompeleka bungeni kuwa asipofanya juhudi kuwatetea watamtema. Na wamteme kweli. Ni kwa kufanya hivyo tu ndio serikali yao itaacha kuwa-take for granted. Hamuwezi kulalamika kutokufaidi rasilimali yenu na kila mara mnamchagua mbunge huyo huyo kuwawakilisha. Hata baada ya kumshuhudia kuwa katika wakati wote huo hajawahi kutetea hoja zinazomhusu!

Ni haki ya waZanzibari kudai wanachodai lakini ni wajibu wa serikali ya JMT kuwakatalia. Ndiyo demokrasi.

Wananchi wanatakiwa kuwa creative wanapopigania haki zao. Inabidi waungani na wajitahidi kuwavuta wenzao wawaunge mkono. Kama wale wachimbaji wa tanzanite wangefanya umoja na wananchi wa eneo lile pengine hadithi ingekuwa nyingine. Badala ya kwenda kutupa hela kutoka maghorofani, wangejenga shule, zahanati n.k. na kuboresha usalama kwenye machimbo yao, pengine wangepata sympathy zaidi. Labda wangeungana na kuhakikisha kuwa eneo lao haliwi wild west ya Tanzania ambapo kila uovu unavumiliwa, pengine wangepata sympathy. Na hii hadithi inajirudia sehemu zote walipo hao wanaojiita wachimbaji wadogo wadogo.

Amandla.......
 
Mafuta ya Zanzibar ni ya wazanzibar au ya Watanganyika au ni ya Watanzania?

Kwanza kabisa nikiwa ni mzanzibar napenda kuwapa hongera wabunge wetu wa Baraza la bunge na la wawakilishi kwa kuonesha msimamo wao kujali hali na maslahi ya wazanzibar wenyewe. Haya yote yanathibitika katika vikavyo vya Bunge vilivyotokea hivi karibuni ndani ya Bunge Mjini Zanzibar. Pata video hapa chini uone wachangiaji hao na mchango wao akiwemo mshauri alietumwa kutoka Tanganyika:


http://www.motionbox.com/videos/ee9bd3bd181ce764


MSIMAMO NDIO HUU HUU tumechoka na kero za Muungano bandia
 
naona unasema uongo vedio gani iliopo unatudanganya tu

well nimesikiliza na kuona hizi videi za maongezi ya wazanzibari kuhusiana na mafuta kule kwao Binafsi nitawaeleza wale wote walikuwapo katika kongamano lile la mafuta kule zenji ni sawa na povu la soda kwa Tarifa yao mafuta yatachimbwa kama mafuta ya TANZANIA na sio mafuta ya ZANZIBAR kama vile wanavyodai kuwa ni yao peke yao , wale ambao hawataki kuamini maneno yangu weka kumbukumbu hii itakuja kukumbusha maneno yangu ikiwa leo ni 1/12/08 .
 
Duh.. toka lini Zenj kukawa na Bunge?
 
Kwani mafuta yamepatikana kweli? ama tunatafuta soko la maziwa kabla ngombe hajashika mimba?
 
Imegundulika sio mafuta bali ni lami kama kule katika milima ya Alberta Canada na gharama ya kuyakamua mafuta ni kubwa na ndefu sana ,hivyo majeshi ya uchimbaji mafuta yamehamishiwa mtwara katika bonde la mto rufiji huko wanasema yapo mengi sana na hata siku za mvua kali michirizi flani flani inakuwa kama iliyomwagiwa dizeli ,hivyo mafuta sasa yatachimbwa huko na mgawo kugaiwa sawasawa kwa Zanzibar.
 
I have heard this talk of oil in tz for so long and nothing has come of it. I doubt its there at all otherwise the chinese would have been all over the place and production would have been underway by now.
 

Slowly ur coming to ur sense now.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…