Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wee Kibunago,
Toka lini Wanyamwezi wakawa Wakwezi? Wa miembe sawa ila siyo Minazi. Jambo moja labda tu kukubali ni kuwa kuna Wanyamwezi wengi walilowea mikoa ya Pwani na Zanzibar. Wengine walibakia wakati wa biashara ya utumwa na leo hii ndugu zangu hao wanajiita Waarabu.
Wengine hata Zanzibar hawakufika, wakaishia mkoa wa Pwani/maeneo ya Bagamoyo na wakabadili jina la kabila na kujiita Wakwere. Ndiyo maana hawa ni watu pekee wa Pwani hatuna utani nao, maana ni WANETU.
Wazaramo ni Wagogo walioZARAMIA Pwani. Kwa maana hiyo, sijui hadi leo wenyeji hasa wa Dar es Salaam.

Sio Muda mrefu uliobaki kutoka sasa utawajuwa ni nani wenyeji wa DAR
 
Ndugu Mkwegi,
Nasikitika kuwa hukufanya "homework" yako vizuri. Swali la kujiuliza ni moja, Zanzbar wanauwezo (institutional and human capacity) wa kunufaika na mafuta waliyonayo (kama wanayo)? Do they even have people to monitor production? (Refer Mzalendo halisi above). Au ndiyo yale mambo ya elimu=madrasa, kazi = mkwezi.

Kama wakigundua wana mafuta, ni vyema wakatumia muda usiopungua miaka 10 (estimates) kujiandaa kunufaika na mafuta hayo. Otherwise, mafuta yatachimbwa na watabaki kukwea minazi.

I stand to be corrected.

Ndugu inaonyesha una habari za kuokotea okotea,historia ya mafuta ya Zanzibar imeanzia mbali sana saana pengine mimi na wewe bado hata hatujazaliwa seuze wazee wetu.
Historia ya Mafuta inaonyesha na kusema kuwa mafuta ya Zanzibar yaligunduliwa Pemba tokea enzi za Masultani wa mwanzomwanzo,na visima vilichimbwa na baada ya kuthibitisha vikazibwa kwa amri ya Sultan ambae alisema kwa sasa hatuna shida ya mafuta fedha tuliyokuwa nayo inatosha kuagiza mafuta kwa kuendeshea gari zilizopo ambazo kwa wakati huo zikihesebika pengine ilikuwa moja au tatu na nyengine ya mzungu.
Historia ya Zanzibar inasema kuwa ,Zanzibar iliwahi kuzisaidia nchi za Norway,Denmark kifedha wakati huo wa zamani hivyo utaona ni kiasi gani cha fedha walikuwa nazo watawala wake,Zanzibar ilikuwa kituo cha Watumwa ,machifu wa bara wakiwakamata wenzao na kuja kuwapiga bei Zanzibar,Zanzibar ilikuwa kituo cha biashara za spice za vyakula aidha vikilimwa bara na kuja kupata soko la uhakika Zanzibar ,fahamu kuwa Zanzibar ya wakati huo ilikuwa imetapakaa mpaka mikoani yote hiyo ikijulikana kama ni Zanzibar ,sijui kwa nini wananchi au watoto wa shule za KiTanzania hawafundishwi jambo hili naona lingeondoa msuguano kwa kiasi fulani.
Point ni kuwa Sultani alikataa mafuta yasichimbwe na zaidi alisema ni kwa vizazi vijavyo kwani wao hawana shida kwa wakati huo.
Sasa kama unajua visima vinaweza kuchimbwa na kuzibwa waulize wenye elimu ya uchimbaji watakueleza kwa kina vipi na chemical gani zinatumika kuziba miamba ya mafuta au gesi. Na kama haitoshi wapo wazee wakawaida tu ambao bado wapo hai na wanakumbukumbu ya sehemu ambazo kuliwahi kuchimbwa visima na kuzibwa. Tatizo jingine ambalo lilikuwa kero ya uchimbaji kwa wakati huu tulionao ni uharibifu wa mazingira na jamaa wa UN unajuwa wametenga maeneo ya visiwa hivi ukichanganya na Kilwa kuwa ni za hifadhiya kimataifa hivyo maeneo haya yapo chini ya uangalizi wa UN na kampuni yeyote itabeba lawama ikiwa kutatokea uharibifu kuhusu kama mafuta ni ya waPemba tu hayo si yenu yawacheni kama yalivyo mbona Almasi na dhahabu haziwanufaishi wanyamwezi na wasukuma pamoja na wakuriya.
Zanzibar inao wataalamu wa Nuklia wacha mafuta ,nyie kaeni mkiibiana tu, mpaka wengine wanatoa machozi ya mamba.Ikiwa janadume linalia wale akina mama pale bungeni wafanye nini?
Wizmtup
 
Wasemaje wewe?

Kwamba Rais Kikwete ni mnyamwezi na kwamba ndio maana wazaramo wengine ni omba omba?

Hivi wakina Mwakanjuki wa Zanzibar asili yao ni wapi?

........ndiyohiyo

Kumbe ulikuwa hujui? Muulize Mkwere yeyote kama ana utani na Mnyamwezi. Hiyo milele haitakuja kutokea. Ni kama useme utani wa Mnyamwezi/msukuma. Mtusi na Mchaga.
Hii ya Wagogo na Wazaramo kweli inaleta utata. Wagogo wao husema kuwa jamaa walizamia Dar na ndiyo maana wakaitwa Wazaramo. Wazaramo wao husema kuwa waliwatuma wenzao kwenda kkununua mbuzi wa Matanga huko Dodoma. Jamaa wakala hela na kuishia mbele. Huku Wazaramo wakakaa na kufanya SALA ya laana. Wagogo wakaanza KUPOFUKA!!!
Mwakanjuki,mhhhh labda ni Mshamba fulani wa Kyela. Ila ile Zenji, kuna mchanyato pale wacha tu. Wengine hukiri wazi kuwa Wana asili ya Unyamwezi. Ila wengine huona Choo. Sijui yakipatikana mafuta Pemba watatukumbuka sisi ndugu zao wa Tabora? Au itakuwa ile ya PAKA. Chako, changu, changu changu........
 
Naona hapo umnifulahisha sana na hako kakisa cha Wagogo na Wazalamo ,afu hao si ndio haohao wandengeleko.
Msitie wasi juu ya mafuta hatutawatupa kabisa kwani roho zetu ni za imani sana,Pemba hukatishi nyumba au mitaa saa za mchana ,lazima utalazimishwa kula na lazima ule.
 
Hawa ndugu zetu nadhani wanasumbuliwa na ule ugonjwa wa inferiority complex.They don believe on themselves thats why lugha zao na response zao zinatia shaka. Nafikiri its better serikali ikijipanga zaidi katika kujiletea maendeleo kuliko kuingia katika mazozano yasiyo ya msingi sana.
 
Wewe unaona hayana msingi lakini mafisadi wanawamaliza maalbino kutafuta utajiri.
 
wandugu,

..mtaalamu toka Scotland aliyetafutwa ili atoe ushauri kuhusu suluhu ya mgogoro wa mgawanyo wa mafuta kati ya Bara na Zanzibar alishamaliza kazi yake mwaka jana.

..mtaalamu huyo alikabidhi ripoti yake kwa serikali ya Muungano, na serikali ya Mapinduzi. sasa sijui ni kwanini serikali zote zimekaa kimya kuhusu mapendekezo ya ripoti hiyo ya kitaalamu.

NB:

..wenzetu Uganda wamegundua mafuta na tayari wako ktk mchakato wa kuyachimba.
 
Taib sheikh,

Hapo umenena..😀..!!
Endeleeni kuzarau maana zarau ndizo zilizofanya T/Bara kuzaa viongozi mafisadi na bado. Zanzibar wanaondoka na na kuhakikishieni kuwa tutawawacha nyuma sana ili muzidi kuilea CCM Baba ,maana bado wananchi wa huko hawawezi kupambana ni magoigoi ,Pemba kwa vyovyote vile wamepambana kiume ndio wakafanikiwa kuitokomeza CCM ,sasa wamebaki akina Kikwete kuanza na mapema kupeleka vitisho lakini Nyerere alitoka kamasi, na siri ya yote ni kuwa wananchi wameamua kikweli kweli liwalo na liwe sasa hata ukipeleka batalion nzima haitowezekana kubadilisha masimamo wao na ndio watazidi maana kwanza ni watu wasiokubali jambo kwa maneno matamu hivyo ni wakaidi wa kupindukia na mnaweza mkabishana mpaka asubuhi na ndio hivyo wanabishana na serikali,serikali inataka waichague CCM wao wanasema mpaka mwisho wa dunia CCM haipati kura.
Watanganyika bado mpo nyuma sana mpaka kufika kuikataa CCM jamaa watakuwa wanaogelea katika mafuta na kunusa gesi,na msizani kama mambo yatakuwa kama ilivyo hivi sasa,sijui kama mnatambua kuwa Mzanzibari ana ID Nationality.
Wakisema tu anaeingia na kutoka Zanzibar lazima awe na Zanzibar ID basi mjue kumekucha. Nyie mtabakia wenzetu Uganda basi inakuja wenzetu Pemba !!
 
???????????????????????????????????????????????????
 
mafuta yapo tena ya commercial katika ukanda huu wa afrika mashariki, kwa sababu formation ya mafuta inayopatika arabia is the same kama hii ya hapa Tanzania ni ina same age kwa sababu zote ziliform wakati wa split ya Gondwana land,
kwa sababu kulikua hakuna upungufu sana wa mafuta duniani na kuzisaidia nchi za jangwani ziwe na njia ya kujikimu ilibidi wawekezaji wajikite sana Middle east, lakini sasa politics ya dunia imebadilika wawekezaji wanataka kutafuta source nyingine ya mafuta ambayo ni cheap na ikaonekana east afrika ndio kwa kuanzia,
na sasa haya mambo ya zamnzibar sio mambo madogo, hao jamaa wana data za uhakika kutoka kwa watafiti na mafuta yapo mengi especially pemba, tusubiri tuone.
Nafikiri analysis yako ina changamoto ya 60 ni kweli yapo na Kijisima kile cha utafiti kikafunikwa (sealed) hadi leo. Yale ya Tundauwa ni kweli yapo. Na kisa cha kutafitiwa katika miaka ya 80 huko ni udadisi wa watafiti wenyewe. Wale waliokuwa wakiruka na videge vyao katika mwambao wa Tanzania-ndio waliosema kuwa mishale yao inaashiria kuwepo kwa dalili za mafuta katika maeneo kama ya Tundauwa Kisiwani Pemba. Mambo ya kafanywa hapo haraka haraka na Pemba ikaingizwa katika utafiti uliokuwa ukiendeshwa katika mwambao wa Tanzania wakati huo (haikuwemo katika mpango wa awali) Wale watafiti wanaeleza kabisa na walionesha bashasha ya kufurahia kazi yao nzuri ya kugundua kiwango kikubwa cha mafuta- nakumbuka pale tulipokuwa tukizungumza nao wakati wa kupata kahawa ndani ya hema lao[ hema lao kuleTundauwa. Lakini masuala ya Kuthibitisha na kutoa data hilo ni jambo lenye utaratibu mwengine. Ukweli ni kuwa huko Zenj mafuta yapo. Ukanda wa Zanzibar Kusini ambako sasa kunaimarika Utalii ni eneo pia mishale ya vile videge vya utafiti imeonyesha kuwa jambo lipo huko.
 
wandugu,

..mtaalamu toka Scotland aliyetafutwa ili atoe ushauri kuhusu suluhu ya mgogoro wa mgawanyo wa mafuta kati ya Bara na Zanzibar alishamaliza kazi yake mwaka jana.

..mtaalamu huyo alikabidhi ripoti yake kwa serikali ya Muungano, na serikali ya Mapinduzi. sasa sijui ni kwanini serikali zote zimekaa kimya kuhusu mapendekezo ya ripoti hiyo ya kitaalamu.

NB:

Unahitaji kuyafuatilia mambo kwa undani na umakini. Serikali hazijakaa kimya kwani Ngeleja akinguruma pale Bungeni ni SMT. na Mansoor akinguruma naye pale BLW ni SMZ hiyo. Ripoti yas Mscotish ndiyo hiyo inatolewa kidogo kidogo kwa utaratibu maalum usioyumbisha wadau. Angalia picha inavyokwenda. Kwa ufupi tu Mafuta ni suala la Muungano, na TPDC itabadilishwa kisheria ili kiwe chombo cha Muungano kuendelea na kuratibu utafiti na uchimbaji wa mafuta kwa niaba ya JMT na SMZ. JMT itachukua kodi na mirahaba kama inavyofanya katika masuala mengine ya Muungano. Lakini suala la mgao wa raslmali hiyo hakuna. Ikiwa mafuta yatachimbwa Zanzibar , SMZ ndiyo itakayochukua pato na kulitumia kwa ajili ya kunufaisha wenye rasilmali hiyo. Na mafuta yakichimbwa Mkuranga JMT itakusanya na kutumia pato hilo kwa ajili ya Watanganyika (Wazanzibari hawamo humo). Hili si suala la kuleta mzozo hata kidogo. Ni la matumizi ya rasilmali kwa wenyewe wahusika. lakini kwa mujibu wa taratibu zetu (Ndani ya JMT) kwenye neema hatujawahi kutupana hata siku moja. Unakumbuka katika miaka ya Sitini na mapema sabini huko Bara walipokuwa wakipatiwa foreign currency na Zanzibar ili wakidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ndugu zetu wa Bara.
 
???????????????????????????????????????????????????

Vipi mbona maandishi hayaonekani,kila mtu na chake dhahabu,almasi,ruby,Tanzanite yote hayo yanachimbwa T/Bara na yana bei kali na faida kali lakini si ya Muungano unafikiri mwenye akili atakubali ndio hapo penye kero,sasa na haya mafuta jamaa washasema ni kwa ajili ya vizazi vyao.
T/bara na Uranium kila siku inaondoshwa kwa vipolo kwa ajili ya uchunguzi ,mnaambiwa itoeni watu watumie kwa umeme mnakuja na mashairi ndio kwanza kuna fizibiliti stadi,study hiyo miaka mingapi ? mbona ukanda wa dhahabu wa Greenbelt kule Mwanza unagawiwa vitalu wakati haujafika hata miaka mitano ?Na watu wanauziana na bei mbaya maana hata Stock Exchanges za Marekani zinasheya na watu wananunua.
WaZanzibari wameshaona kuwa wenzao waTanganyika hawana maslahi na raia zao hivyo kujikubalisha mafuta yawe ya Muungano ni kuuwa vizazi vya Zanzibar jambo ambalo wawakilishi wake wameshaungana na kukataa katakata kuwa mafuta ya Zanzibar yasipelekwe kwenye Muungano ule umeme mmeleta unanunuliwa kwa gharama za fedha za kigeni sasa mnajidai kujisogeza Pemba .

Mimi nashangaa sana ikiwa hapo DSM mabarabara hayana taa za barabarani mtaenda kuwekesha Pemba,Dar umeme na maji ni shida jamaa anaenda kufungua tangi la maji Pemba haimuhusu shikio wala pua,hivi mnawafanya watu mapunguani? Anakwenda kwa nguvu za vyombo vya dola lakini kwa nguvu za raia kwamba wanahamu nae sana wamuone,hilo halipo amejipeleka amepokewa kistaarabu.
 
Pakacha said:
Unahitaji kuyafuatilia mambo kwa undani na umakini. Serikali hazijakaa kimya kwani Ngeleja akinguruma pale Bungeni ni SMT. na Mansoor akinguruma naye pale BLW ni SMZ hiyo. Ripoti yas Mscotish ndiyo hiyo inatolewa kidogo kidogo kwa utaratibu maalum usioyumbisha wadau. Angalia picha inavyokwenda. Kwa ufupi tu Mafuta ni suala la Muungano, na TPDC itabadilishwa kisheria ili kiwe chombo cha Muungano kuendelea na kuratibu utafiti na uchimbaji wa mafuta kwa niaba ya JMT na SMZ. JMT itachukua kodi na mirahaba kama inavyofanya katika masuala mengine ya Muungano. Lakini suala la mgao wa raslmali hiyo hakuna. Ikiwa mafuta yatachimbwa Zanzibar , SMZ ndiyo itakayochukua pato na kulitumia kwa ajili ya kunufaisha wenye rasilmali hiyo. Na mafuta yakichimbwa Mkuranga JMT itakusanya na kutumia pato hilo kwa ajili ya Watanganyika (Wazanzibari hawamo humo). Hili si suala la kuleta mzozo hata kidogo. Ni la matumizi ya rasilmali kwa wenyewe wahusika. lakini kwa mujibu wa taratibu zetu (Ndani ya JMT) kwenye neema hatujawahi kutupana hata siku moja. Unakumbuka katika miaka ya Sitini na mapema sabini huko Bara walipokuwa wakipatiwa foreign currency na Zanzibar ili wakidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ndugu zetu wa Bara.

Pakacha,

..umeniacha hoi ndugu yangu.

..nilitegemea ripoti hiyo ingewekwa wazi kwa wananchi kupitia wabunge na vyombo vya habari.

..sijui kwanini ripoti nyingi zinazohusu masuala ya Muungano zinafanywa siri.
 
1. Kweli- mafuta nchi zingine imekuwa laana (Nigaria, Equatorial Guinea)...hope mafuta Vioswani (kama yapo) yasiwe laana pia!

2. Better invest in human resouces kwanza ktk elimu, IT, na good health care hii ni nzuri zaidi kuliko kutegemea mafuta!Human resouces we can even export na kupata foreign currency!

Mwenzangu hilo linataka Fedhwa na Zanzibar kwa hilo Nhh111. Wacha tupate fedhwa kwani waarabu sasa wanawafukuza wale waliowaajiri zamani baada ya kusomesha wao sababu ya Fedhwa.
 
Ndugu Mkwegi,
Nasikitika kuwa hukufanya "homework" yako vizuri. Swali la kujiuliza ni moja, Zanzbar wanauwezo (institutional and human capacity) wa kunufaika na mafuta waliyonayo (kama wanayo)? Do they even have people to monitor production? (Refer Mzalendo halisi above). Au ndiyo yale mambo ya elimu=madrasa, kazi = mkwezi.

Kama wakigundua wana mafuta, ni vyema wakatumia muda usiopungua miaka 10 (estimates) kujiandaa kunufaika na mafuta hayo. Otherwise, mafuta yatachimbwa na watabaki kukwea minazi.

I stand to be corrected.

Tatizo wewe ukijana na unadanganyika na majigambo. Si kweli kuwa Wazanzibari hawakusoma au hawana wataalamu. Si tabia ya Wazanzibari kujisifu na ndiyo unafikiri kuwa hakuna wasomi. Hata hivyo kwa huku bara tukijidai kuwa ni wasomi hebu nieleze kuna kitu gani cha utaalamu kilichowasaidia Watanzania na hiyo elimu "Shule".
Si vizyri kuwabeza watu eti tu kwa vile hawajilabu kama wengi wetu.
 
Hawa ndugu zetu nadhani wanasumbuliwa na ule ugonjwa wa inferiority complex.They don believe on themselves thats why lugha zao na response zao zinatia shaka. Nafikiri its better serikali ikijipanga zaidi katika kujiletea maendeleo kuliko kuingia katika mazozano yasiyo ya msingi sana.

Iwapo nyie mlio na 'superior complex" mnazozana na hao "inferior complex" tutashindwa kujua tofauti. Kwenu nyie chenu ni chenu na cha wenzenu ni chenu pamoja. Hivyo mtu kudai chake ni inferior complex.? Ach matusi ya reja reja.
 
Wee Kibunago,
Toka lini Wanyamwezi wakawa Wakwezi? Wa miembe sawa ila siyo Minazi. Jambo moja labda tu kukubali ni kuwa kuna Wanyamwezi wengi walilowea mikoa ya Pwani na Zanzibar. Wengine walibakia wakati wa biashara ya utumwa na leo hii ndugu zangu hao wanajiita Waarabu.
Wengine hata Zanzibar hawakufika, wakaishia mkoa wa Pwani/maeneo ya Bagamoyo na wakabadili jina la kabila na kujiita Wakwere. Ndiyo maana hawa ni watu pekee wa Pwani hatuna utani nao, maana ni WANETU.
Wazaramo ni Wagogo walioZARAMIA Pwani. Kwa maana hiyo, sijui hadi leo wenyeji hasa wa Dar es Salaam.
Habari ndiyo hiyo Kamanda, zaidi ya ukwezi Wanyamwezi na wenzao Wamakonde ndio vibarua kwenye konde za Wazenj. Aidha kwa wakati wao wa ziada, wamakonde hupenda kutengeneza Tende, huku Wanyamwezi wakijifunza kufanya biashara.
 
wandugu,

..mtaalamu toka Scotland aliyetafutwa ili atoe ushauri kuhusu suluhu ya mgogoro wa mgawanyo wa mafuta kati ya Bara na Zanzibar alishamaliza kazi yake mwaka jana.

..mtaalamu huyo alikabidhi ripoti yake kwa serikali ya Muungano, na serikali ya Mapinduzi. sasa sijui ni kwanini serikali zote zimekaa kimya kuhusu mapendekezo ya ripoti hiyo ya kitaalamu.

NB:

Unahitaji kuyafuatilia mambo kwa undani na umakini. Serikali hazijakaa kimya kwani Ngeleja akinguruma pale Bungeni ni SMT. na Mansoor akinguruma naye pale BLW ni SMZ hiyo. Ripoti yas Mscotish ndiyo hiyo inatolewa kidogo kidogo kwa utaratibu maalum usioyumbisha wadau. Angalia picha inavyokwenda. Kwa ufupi tu Mafuta ni suala la Muungano, na TPDC itabadilishwa kisheria ili kiwe chombo cha Muungano kuendelea na kuratibu utafiti na uchimbaji wa mafuta kwa niaba ya JMT na SMZ. JMT itachukua kodi na mirahaba kama inavyofanya katika masuala mengine ya Muungano. Lakini suala la mgao wa raslmali hiyo hakuna. Ikiwa mafuta yatachimbwa Zanzibar , SMZ ndiyo itakayochukua pato na kulitumia kwa ajili ya kunufaisha wenye rasilmali hiyo. Na mafuta yakichimbwa Mkuranga JMT itakusanya na kutumia pato hilo kwa ajili ya Watanganyika (Wazanzibari hawamo humo). Hili si suala la kuleta mzozo hata kidogo. Ni la matumizi ya rasilmali kwa wenyewe wahusika. lakini kwa mujibu wa taratibu zetu (Ndani ya JMT) kwenye neema hatujawahi kutupana hata siku moja. Unakumbuka katika miaka ya Sitini na mapema sabini huko Bara walipokuwa wakipatiwa foreign currency na Zanzibar ili wakidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ndugu zetu wa Bara.

PAKACHA BWANA!!! unaota ndoto ,tangu lini nyinyi mkawa na msemo kwa chochote? Tumeshasema Rasilimali mafuta ni ya muungano na Rasilimali MADINI huo mpango unaosema ndio unaoapply.
 
" Hao wanaosema hakuna mie nasema hakuna technology ya 100% lakini ninachoweza kusema ni kuwa uwezekano wa kuwepo mafuta Zanzibar upo na hilo tutalijua zaidi tukianza kuchimba sasa ikiwa tutapata kinibu, geloni au pipa hayo yatakuwa ni maumuzi ya wazanzibari kama mafuta kidogo tutajipaka na kama gesi kidogo basi tutanusa, kule Tundauwa Pemba mafuta yanakuja yenyewe " alisema Waziri Himid.

...hapa nilipo sina mbavu na lugha ya huyo mheshimiwa...eti kama gesi ni kidogo watanusa na mafuta kama ni kidogo watajipaka!
 
Back
Top Bottom