Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Nin kweli huielewi Zanzibar na society ya Wazanzibari. Na ndiyo maana una munkar wa kusema hayo. TPDC Na Wizara yenu ya Nishati huko haina utalaamu wa mafuta na ndiyo maana wanatoa kauli kuwa Zanzibar sijui hakuna mafuta. Ni kweli Tiper na Mashirika kama hayo makubwa ndiyo yana utaalamu na ndiyo yaliyofanya utafiti. Society ya Wazanzibar imefika mbali Ndugu yangu na huko waliko wana access za data za utafiti uliofanywa Zanzibar, Hao wanauwezo wa kuprocess data hizo na ndiyo maana katika pembe za chaki ndiyo hueleza kuwa kwetu (Zanzibar) kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa mafuta yapo. Jitahidi uielewe society ya Wazanzibari. Ni wengi tu wanafanya kazi katika sekta ya mafuta tena huko kwa wenye mafuta na Makampuni yanayosifika yenye access za data hata za Mkuranga na Songosongo.

Okay, ni kweli siijui "society ya wazanzibari". Lakini hao wataalamu unaozungumzia wako wapi? Wanaisaidiaje Zanzibar? Zanzibar is very potential for tourism, fishery and spices production. Ni nini tofauti ya utalii na mafuta katika kuiletea maendeleo Zanzibar? Hao wataalamu wanafanya nini? Tena ni bora utalii kwa sababu mafuta yatawaingiza kwenye mgogoro, hususani kama mafuta hayo yanapatikana Pemba.

"Society ya Wazanzibari" imepiga hatua? Umetumia vigezo gani kusema hivi? Issue hapa si kwamba Zanzibar kuna mafuta au la. Swali hapa ni je Zanzibar imejiandaa vipi kunufaika na raslimali hiyo?
 
Well, kama TPDC kuna wataalamu wa kutafiti mafuta, kwa nini tunatumia wageni kufanya kazi hiyo? Utaniambia kuwa hawana vifaa, I guess! Sasa uwezo wao uko wapi? Then, utasema nina dharau. Lakini kwa nini kukisifia kitu wakati hakistahili sifa? Unajua bila kulitambua tatizo huwezi kulipatia jawabu la uhakika. Just be objective, TPDC wanachokifanya ni nini? Kukusanya sampuli za mafuta au kuhifadhi sampuli za mafuta?

Hao Wazanzibar laki sita unaozungumzia, ni vyema wakawepo na wakajiendeleza kama unavyodai. Na wanahitajika sana Zanzibar sasa kuliko wakati mwingine wowote. Ningewashauri warejee nyumbani wasaidie kuijenga Zanzibar. Zanzibar inahitaji madaktari, wataalamu wa kilimo, wataalamu wa utalii, engineers, wataalamu wa uvuvi, just name it. Wasisubiri mpaka mafuta yaanze kuchimbwa ndio warudi. Zanzibar inaweza kupata maendeleo makubwa sana bila kuwa na mafuta.

Ni muhimu kuzingatia kuwa Zanzibar (kama ilivyo Tanzania bara) haina upungufu wa wanasiasa. Ina upungufu wa "human resources".

Hawawezi kurudi kwa sababu hawana imani na serikali iliyokuwepo madarakani au zilizokuwepo na siku serikali itakayochaguliwa kwa ridhaa za wananchi itakapoingia madarakani,unaweza kusema ni maajabu lakini watarudi watu na hata kama hawakurudi wataweza kuisaidia Zanzibar kutoka huko waliko ,hata hiyo CCM kama ingepata madaraka kwa njia za amani na uchaguzi kwenda bila ya aibu basi wangeliweza kusaidia ,kuna watu wanathamini elimu zao na hawawezi kuwasadia wezi wa kura ni aibu kwao. Ndivyo mtu mwenye elimu aliesoma kisha akafahamu.
 
Zanzibar suspends oil search

2009-02-01 11:22:15
By Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Zanzibar has halted implementation of oil search contract by Canada`s Petroleum Exploration and Production in Zanzibari waters, pending determination on sharing arrangement ``to ensure costs and benefits are rationally carved up by the two sides of the Union.``

The Isles Minister for Water, Construction, Energy Resources and Lands, Mansour Yussuf Himid, made the announcement in the House of Representatives here on Friday.

``The intervention is necessary until we reach a solution on sharing the costs and benefits in the exploration and production of petroleum,`` the minister told the House.

In 1997, the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), on behalf of the Union government, and the Canadian firm signed the agreement.

The minister said the foreign firm would not be allowed to conduct any form of research on petroleum exploration and production in Zanzibar waters, stating the government`s official position when replying to a supplementary question by the Deputy Minister for Information, Culture and Sports, Mahmoud Thabit Kombo.

Mahmoud asked whether there were any signs of oil being found in the isles.

The deputy minister`s question follows a statement by the Tanzania Mainland Deputy Minister for Energy Resources Adam Malima who said water depths in Zanzibar block were lower or non existent, and thus not viable for a commercial venture.

He claimed that previous searches indicated that there was enough petroleum, especially at Tandaua area in Pemba.

He said the matter would be discussed in the cabinet and later in the Isles legislature for deliberation and decision.

Answering the original question by Ali Suleiman Ali (Kwahani-CCM), the minister said oil exploration would take into account environmental aspects.

Petroleum and gas are included in the Union List in 1984 at a time when Seif Shariff Hamad was the Zanzibar Chief Minister.
 
Waziri azidi kutonesha
Akijibu swali la kuwaandaa vijana kupata ajira katika uchimbaji wa mafuta Waziri huyo alisema wizara imeandaa mikakati madhubuti ya kusomesha vijana kwa kuwapeleka katika vyuo mbali mbali ndani na nje ya Tanzania hasa kwa kuwa makampuni yote ya utafutaji wa mafuta katika mikataba yao kipo kipengele cha mafunzo.

Alisema mkataba wa antrim wa mwaka wa 1997 ulikubali kutoa dola za kimarekani 50,000 kwa mwaka na kuna baadhi ya makampuni amabyo yamepewa lesini Tanzania Bara yamefikia hadi dola za kimarekani 100,000 kwa mwaka ambapo uchimbaji ukianza fedha kama hizo zitasaidia kuwapatia mafunzo vijana.
 
Habari ndiyo hiyo Kamanda, zaidi ya ukwezi Wanyamwezi na wenzao Wamakonde ndio vibarua kwenye konde za Wazenj. Aidha kwa wakati wao wa ziada, wamakonde hupenda kutengeneza Tende, huku Wanyamwezi wakijifunza kufanya biashara.

Kibunago,
Hii imekaa zaidi kama ya kila kijana muuza vitu mkononi pale Dar basi kawa Machinga. Machinga ni wale watu wanaotoka kijiji cha Mchinga. Sasa kama Dar wako wengi namna ile, hicho kijiji kweli kikubwa. Au ile ya madada wa kwenye Madangulo eti Wahaya!! Minziro akicheza mpira aitwa SHEMEJI. Jamani kweli madanguro yote ni Wahaya tu?
Nafikiri huko Zenji, kila kibarua anajiita/mnamwita Mnyamwezi. Naona ambavyo ANADHARAULIWA na kutupiwa kila aina ya dharau. Siku moja itabidi tuje turudishe heshima ya Mirambo/Isike/Fundikira.
Wewe hapo Kibunago pia waweza kukuta ni Mnyamwezi. Ila naona Zenji watu hawataki kabisaa kukubali. Nilishakutana na watu wanaokubali Unyamwezi wao. Cha jabu ni kuwa wote walikuwa na damu ya Kiarabu. Sasa najiuliza, kwa nini MIPINGO hukataa kabisa Unyamwezi wao? Mmanga wa kwanza nilitana naye ilikuwa Kariakoo kwenye duka lake, na akaniita brother. Mwingine ni Salim Ahmed Sallim.
Wee Kibunago ni KIYUNGI kuanzia leo.
 
Mafuta yakipatikana Pemba, nyie Waunguja msitufuatefuate. Tena mtuk*** kabisaaa. Lazima mjue mafuta ni ya wenyeji wa sehemu hiyo. Ugunja mbaki na CCM yenu. Na lazima mjue kuwa tutakesha tukiimba "we are getting good in missing you " - By Don Williams. Kwani kuna raha gani ya kufaidi mafuta na Waunguja? Si heri yakipatikana basi tufaidi wenyewe tu? Hata kama ardhi haitoshi, basi tutaanza kujenga baharini na kununua udongo kutoka Tanga/Mombasa.
Ninaposema Waunguja msitufuate fuate, nyie Wabara nafikiri mnajua mnatakiwa mkae sehemu gani wakati Neema ya mafuta ikiifunika Pemba. Msichukie sana, ndiyo biashara hiyo. Tutakuwa tunawauzia na mkijifanya wajanja, basi tunafunga bomba la mafuta. Hadi na nyie muanze kulialia kama Ukraine kwa GASPROM (Mrusi), ndiyo tukifikiria tunaweza warudishia tena mgao. Yes, nothing personal. Biashara ni biashara tu wandugu. Wee Mwiba kwenu wapi? Kama kwenue Ugunja, basi heri ulilie muungano udumu. Kibunago aka KIYUNGI je? Hiii, tutaona mengi mwaka huu. Tuombe uzima.
 
Ajabu na kweli..yote haya ya nini wakati hata ushahidi wa mafuta bado?

Mafuta yenyewe yako wapi?

Invest in human resouces man!
 
Mheshimiwa Spika mimi nataka kujua maana juzi nimemsikia Waziri Mheshimiwa Malima akisema Zanzibar hakuna mafuta huku mheshimiwa waziri Mansoor anatakwambia mafuta yapo na sasa nataka kujua ukweli upo wapi" aliuliza Kombo ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

" Hao wanaosema hakuna mie nasema hakuna technology ya 100% lakini ninachoweza kusema ni kuwa uwezekano wa kuwepo mafuta Zanzibar upo na hilo tutalijua zaidi tukianza kuchimba sasa ikiwa tutapata kinibu, geloni au pipa hayo yatakuwa ni maumuzi ya wazanzibari kama mafuta kidogo tutajipaka na kama gesi kidogo basi tutanusa, kule Tundauwa Pemba mafuta yanakuja yenyewe " alisema Waziri Himid.

"Ninachoomba kwa sasa wajumbe mjiandae kuipokea ripoti ya mshauri mwelekezi na kumshauri mwelekezi atakapotoa ripoti yake ninaamini wajumbe wana ushauri mzuri na wa hoja nzuri sana tuna wataalamu wengi hapa tafiti zinaonesha kwamba upo uwezekano wa kupatikana kwa mafuta kwa mujibu wa mazingira ya jiografia ya bahari yetu" alisisitiza Waziri huyo aliekua akisema kwa kujiamini.

Aliwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kujiandaa na majadiliano hayo kwa kujenga misingi ya hoja katika suala hilo muhimu kwa maslahi ya taifa la Zanzibar na kizazi kijacho.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wa pande mbili za CCM na CUF walilingana kwa pamoja na kutaka suala la mafuta na gesi kuondoshwa katika orodha ya mambo ya muungano.

Haya "mafuta" ya Zanzibari yana mambo! Tutashangilia kama mafuta yatapatikana, hata kama tutanunua kwa bei ya sokoni bado tutafaidika kwa kuokoa gharama za usafiri ambazo huchangia ughali wa mafuta nchini.

Hata hivyo kauli za viongozi wa Zanzibar kuhusu mafuta hayo ni za maringo mno na ni kama vile Zanzibar iko jinsi ilivyo (hali mbaya kwa sababu ya ukosefu wa raslimali na Muungano wake nza Zanzibar) kwa sababu ya Tanganyika, hofu yangu ni kuwa kama vile Zanzibar kama Taifa wanailaumu Serikali ya Muungano vilevile Pemba nao wanalalmikia uduni wao kuwa unasababishwa na Unguja!

Mungu apishie mbali mafua hayo yasije kuugharimu Muungano; kama ikiiwa hivyo basi ni wazi mafuta hayohayo yataigharimu Zanzibar kwa maana ya kuwa Mafuta ya Pemba yanaweza kuunda Jamhuri nyingine na kukawa na Jamhuri ya Tanganyika, JAmhuri ya Unguja, na Jamhuri ya Pemba. God forbid. Viongozi wa Zanzabar na Muungano wanahitaji hekima ya kipekee ya kuhandle suala hilo.
 
Mimi ndiyo maana nafikiri kuna haja ya kuungalia huu Muungano wetu kwa undani wakati bado sote tu masikini wa kutupwa. Tuungalia na tuulegitimise kwa kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili. Muungano uendelee tu pale ambapo majority ya wananchi kutoka kila upande wakiukubali. Kama upande mmoja, Zanzibar au Tanganyika, wakiukataa, tuuvunje na tugawane tulicho nacho. Wakiukubali, bila masharti, basi ndiyo tuangalie tutatatua vipi haya matatizo ya ugawanyaji wa rasilimali. Hatuwezi kuwa na Muungano endelezi wakati upande mmoja kila siku unamwona mwenzake kuwa ni mgeni aliye na nia mbaya kwake.
 
Hayo uliyoyasema kwa kutilia mashaka si mashaka bali ni kweli tupu. Maendeleo ya Zanzibar yanadumazwa na namna muundo wa Muungano wa Tanzania ulivyo na ni kweli kuwa hicho kidogo kinachopatikana bado hakijagawiwa sawa kati ya Unguja na Pemba. Hata hivyo haya yote ni masuala ya kutengenezwa kwa kutilia maanani maslahi ya wananchi na si maslaha ya wachache hasa wanasiasa kwani si CCM si CUF viongozi wao hawana matatizo ya maisha.
Wanasiasa siku zote huutumia umasikini wa wananchi kwa maslaha yao huku wananchi wakiamini kuwa tabu zote zipo kwa sababu ya umasikini. Wazanzibari wanafikiri kuwa uokozi uko kwenyemafuta huku wakisahau kuwa wanasiasa nao wanategemea manufaa zaidi kutokana na mafuta hayo hivyo ugomvi kati ya wale wa Bara na wale wa Visiwani unaletwa na hiyo fikira ya kujinufaisha zaidi kuliko manufaa ya wananchi.
 
My apologies. I am just telling the facts. Bahati mbaya wengi wetu tunapenda kuambiwa kile tunachotaka kusikia. The world is not that fair. What does the history of Zanzibar has to do with their capacity to monitor oil production and allocate resources wisely? Kwa nini unafikiri mafuta ndiyo yatakayowatoa kwenye umaskini na si utalii au uvuvi, kwa mfano? Na kama ni kweli mafuta yanapatikana Pemba, ninachokiona huo ndio utakuwa mwisho wa Zanzibar!

And do you think the mainland Tanzania is benefitting from the mineral resources they have? They have never been ready to benefit either. Na bahati mbaya ni kuwa madini ni "exhaustible resource". Hii ina maana kuwa, it will come a day when the reserve we have will last. Although, it's difficult to estimate the remaining stock with certainty, it makes a big difference at least to be able to monitor production with certainty. If you don't know the production level/rate (or you are relying on mining companies to report their production), how can you pretend that we are benefiting? [note: mining companies have strong incentive to cheat!]. And the whole game lies on the careful balance between output consumption and investment. If we are consuming everything we accrue from mineral production, then both the current and future generations are being made worse-off.

Tatizo sio kusema ukweli tatizo ni kuwa kuna watu kila siku watalaumu kitu lakini hawana mchango wa kutatuwa tatizo. Kwa nilivyokufahamu kuwa Zanzibar kwa namna unavyoona wewe kuwa hawana wataalamu wa kuchimba mafuta hivyo wasichimbe mafuta. Mpaka lini?

Nilikupa mfano wa Waarabu na namna walivyotumia wageni katika hatuwa ya mwanzo nawe hukuwa tayari kulijadili hili. Kauli yako ya kuwa historia ya Zanzibar itawasaidia nini na uchimbaji wa mafuta ni muendelezo wa kudharau wenzio, kwani Zanzibar ina wataalamu wengi wanaotumika nchi za nje ambao daima wako tayari kurudi kwao kuitumikia nchi yao. Ninapotaja nje naamanisha pia hata hapa Bara wako Wazanzibari wasomi wengi tu.

On mainland, it is not true that we do not benefit from minerals, we do but the problem is few of us , for our own reasons we have decided to collaborate with those who cheat us with our minerals. For instance Kabwe Zitto and others who take effort at revealing the theft do theyhave degrees on minning?
It is unfortunate that minning and petroleum technology are possesed by foreigners and it is the normal trend in our life that we share what we have with those who can develop it,then let it be. I wonder when those developed nationals will let us have all of our cakes without sharing with them. They have their grips on us if not through technology then it wili be on financial . I remember your say that some people are not ready to be told facts, there are still some who do not want to accept facts however bare they are,let the Zanzibaris share iwth those will help them.
 
Mimi ndiyo maana nafikiri kuna haja ya kuungalia huu Muungano wetu kwa undani wakati bado sote tu masikini wa kutupwa. Tuungalia na tuulegitimise kwa kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili. Muungano uendelee tu pale ambapo majority ya wananchi kutoka kila upande wakiukubali. Kama upande mmoja, Zanzibar au Tanganyika, wakiukataa, tuuvunje na tugawane tulicho nacho. Wakiukubali, bila masharti, basi ndiyo tuangalie tutatatua vipi haya matatizo ya ugawanyaji wa rasilimali. Hatuwezi kuwa na Muungano endelezi wakati upande mmoja kila siku unamwona mwenzake kuwa ni mgeni aliye na nia mbaya kwake.

Tanzania si wa masikini wa kutupwa,hizo ni kasumba za CCM wanazowalisha wananchi ili wapate nafasi ya kukwapua na nyie mnakondeana mkiamini nchi zetu ni masikini na ukienda kwenye data za Kimataifa utaona tunakaribia kushika mkia kwa grade za umasikini ,hawa viongozi ndio wamefanya ionekane hivyo.

Ikiwa nchi ina ZOO tu inajijengea umaarufu na kuweka fedha za kigeni na kuendesha mambo kwa furaha kabisa ,sisi hapa tuna mimbuga kibao na madege kwa madege yanaleta watalii ,na hapa wanatumia dola au fedha za kigeni.Kuanzia dola 3000 kwa mtu mmoja na hiyo ni kuangalia masokwe tu.Yaani ndugu haina haja ya kusema iyo kitu inatilisha imani kabisa kwa jinsi tunavyoburuzwa hapa Tanganyika,si unaona magari ya bei mbaya ya viongozi na wateja wao ,hivyo hiyo fedha inaliwa hovyohovyo na wajanja hao wakitumia kwa kumwaga ,mlala hoi hana chake ni kupigwa maneno ya CCM ndie baba nae kura yake anaitoa huku anacheka kuwa amefanya maamuzi yatakayomkwamua ,hivyo kwa wananchi wa Zanzibar wanazikataa sera hizo za CCM Chama Cha Maangamizi na ndio maana wanapigia makelele kujitenga kwani hakuwanufaisihi kuendelea na Muungano ambao wananchi wa upande wa pili hawaoni wala hawasikii na wanabadilishwa msimamo wao kwa kopo la ulevi na upande wa kanga,akiambiwa CCM ndo imekusomesha ndo itakuletea mbolea na mambo kibao nyimbo ambazo WaZanzibari hawazihitaji tena wala hawazisikilizi ,na huyo alieandika hapo juu kuwa Zanzibar kuna makundi matatu hajakosea wanaokazania Muungano ambao ni kundi la Wezi ,wasioutaka Muungano ambao ni wakombozi na hao anaowajua yeye kuwa hawako upande wowote ni ambao ni wananchi hewa..!

Tanzania masikini wakutupwa !!!,we vipi salama lakini ? Hebu nenda kabukue na kupiga ronyo hapa kwenye link:-
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23773-yu-wapi-anayesema-tanzania-ni-maskini.html
 
Wakuu hebu tuweke karata mezani zikiwa wazi, Hivi TANGANYIKA itapungua nini ikiiwacha ZANZIBAR ijikate kivyake????? Mbona WANASIASA mnatubabaisha na USANII wenu??? Au kwa vile WATANGANYIKA wamekaa kimnya hawaidai au kuitaja TANGANYIKA??? Na ZANZIBAR itakosa nini au kupungua nini ikiwa nje ya MUUNGANO???? Pamoja na RASILIMALI zinazotajwa, kuwe na MAFUTA au kusiwe na MAFUTA bado tutategemea MISAADA na RUZUKU toka nje AIBU iliyoje at the age of 47. Hakuna mwenye SERA za MAENDELEO, Kila siku USANII mpya WIZI wa kupindukia na UBADHIRIFU wa mali ya TAIFA umevuka mipaka. VIONGOZI waliopo madarakni hawatambui NGUVU na DHAMANA walizopewa wanashindwa na wanafumbia macho MAHARAMIA kwa vizingizio vya KATIBA au vinginevyo WHAT A NONSENSE!!!!!!! LETS SPLIT THE SOONER THE BETTER.
 
Muungano ukivunjika waTanganyika watauana mpaka kila mmoja arudi mkoani kwake na ukabila utafumka ,unajua Zanzibar hakuna ukabila kwa maana ya ukabila isipokuwa kuna lahaja tu nazo zinaeleweka ikiwa utatega sikio makini lakini huku upande wa pili kuna makabila kibao na vita vya chini kwa chini vipo yupo mtu anaweibisha kuhusu vita vya makabila japo vinapakwa rangi ya wakulima na wafugaji lakini ukweli ni vita haswa.
Yaani Watanganyika washukuru sana huu Muungano ndio ukasikia lazima waulinde siju wataulinda mpaka lini maana ni kama Active volcano one day yes itafumka tu.
 
Kibunago,
Wee Kibunago ni KIYUNGI kuanzia leo.
Kiyungi ina maana gani? Well naona umejaribu tu kuwatetea Wanyamwezi, vipi kuhusu Wamakonde...Tena hawa na fujo sana na ngoma zao za usiku usiku.
 
Muungano ukivunjika waTanganyika watauana mpaka kila mmoja arudi mkoani kwake na ukabila utafumka ,unajua Zanzibar hakuna ukabila kwa maana ya ukabila isipokuwa kuna lahaja tu nazo zinaeleweka ikiwa utatega sikio makini lakini huku upande wa pili kuna makabila kibao na vita vya chini kwa chini vipo yupo mtu anaweibisha kuhusu vita vya makabila japo vinapakwa rangi ya wakulima na wafugaji lakini ukweli ni vita haswa.
Yaani Watanganyika washukuru sana huu Muungano ndio ukasikia lazima waulinde siju wataulinda mpaka lini maana ni kama Active volcano one day yes itafumka tu.

Nadhani hapo unapindisha ukweli. Isingekuwa Mwungano Zanzibar isingekuwa tafauti sana na Comoro.
 
Katika kitabu cha hadithi za Abunuwasi, kuna ile hadithi ya Alinacha. Kwa kifupi alinacha aliamua kufanya biashara ya vikombe, birika, visahani vyote vya udongo, china. Akavijaza kwenye kikapo chake kwenda sokoni kuviuza. Njiani akaamua kupumzika chini ya mti kupumzika. Wakati akipumzika akawa anapiga "alinacha" (anawaza). "Nikisha viuza vyombo hivi, nitakuwa tajiri. Nikiwa tajiri nitamwoa binti Mfalme. Kwa kuwa yeye ni binti Mfalme, atakuwa jeuri. Akinifanyia jeuri, nitampiga teke." Katika kupiga teke, alilipiga teke kapu lake na vyombo vyote vikavunjika. Utajiri na binti Mfalme, vyote akavikosa.

Sasa na sisi hivi tulivyo tunakuwa hatuna tofauti na Alinacha. Sisi sote Tanzania Bara na
Tanzania Visiwani hatuna mafuta. Na kama yapo hatupajui hata pale yalipo. Na hata tukijua yalipo hatuna zana wala jinsi ya kuyapata. Tunagombea nini?

Uchumi tumeukalia miaka nenda miaka rudi. Kazi yetu kujisifu tu, tuna madini na mali ghafi ya kutumia na kusaza. Miaka karibu 50 ya uhuru. Tunafanya mikakati gani ya kutuwezesha kuchimba, kusafisha na kuuza wenyewe?

Tuna mito, maziwa na ardhi safi bwelele. Tunazitumiaje mali asili hizi kuboresha maisha yetu? Mpaka waje wawekezaji na wawekezaji wenyewe sharti wawe wageni. Tuna kazi.
 
Tanzania si wa masikini wa kutupwa,hizo ni kasumba za CCM wanazowalisha wananchi ili wapate nafasi ya kukwapua na nyie mnakondeana mkiamini nchi zetu ni masikini na ukienda kwenye data za Kimataifa utaona tunakaribia kushika mkia kwa grade za umasikini ,hawa viongozi ndio wamefanya ionekane hivyo.

Ikiwa nchi ina ZOO tu inajijengea umaarufu na kuweka fedha za kigeni na kuendesha mambo kwa furaha kabisa ,sisi hapa tuna mimbuga kibao na madege kwa madege yanaleta watalii ,na hapa wanatumia dola au fedha za kigeni.Kuanzia dola 3000 kwa mtu mmoja na hiyo ni kuangalia masokwe tu.Yaani ndugu haina haja ya kusema iyo kitu inatilisha imani kabisa kwa jinsi tunavyoburuzwa hapa Tanganyika,si unaona magari ya bei mbaya ya viongozi na wateja wao ,hivyo hiyo fedha inaliwa hovyohovyo na wajanja hao wakitumia kwa kumwaga ,mlala hoi hana chake ni kupigwa maneno ya CCM ndie baba nae kura yake anaitoa huku anacheka kuwa amefanya maamuzi yatakayomkwamua ,hivyo kwa wananchi wa Zanzibar wanazikataa sera hizo za CCM Chama Cha Maangamizi na ndio maana wanapigia makelele kujitenga kwani hakuwanufaisihi kuendelea na Muungano ambao wananchi wa upande wa pili hawaoni wala hawasikii na wanabadilishwa msimamo wao kwa kopo la ulevi na upande wa kanga,akiambiwa CCM ndo imekusomesha ndo itakuletea mbolea na mambo kibao nyimbo ambazo WaZanzibari hawazihitaji tena wala hawazisikilizi ,na huyo alieandika hapo juu kuwa Zanzibar kuna makundi matatu hajakosea wanaokazania Muungano ambao ni kundi la Wezi ,wasioutaka Muungano ambao ni wakombozi na hao anaowajua yeye kuwa hawako upande wowote ni ambao ni wananchi hewa..!

Tanzania masikini wakutupwa !!!,we vipi salama lakini ? Hebu nenda kabukue na kupiga ronyo hapa kwenye link:-
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23773-yu-wapi-anayesema-tanzania-ni-maskini.html

Mwiba. Kwa vigezo vyote Tanzania ni nchi masikini mno. Hapa tunazungumzia hali ilivyo na si potentialities. Umasikini huo unajitokeza katika picha ya huko Pemba uliyoibandika mwenyewe ( kuanzia nyumba hadi infrastructure), imani za kishirikina zinazotupeleka kuamini kuwa viungo vya albino vinaweza kutuletea mafanikio katika uchimbaji wa madini, kuwa bibi mwenye macho mekundu ( kutokana na kupikia kuni mahali pasipo na ventilation) ni mchawi na anastahili kufa, bibi mwenye alzheimer anayetembea uchi kuwa ni mwanga na anastahili kuuawa n.k. n.k. Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni moja ya nchi masikini duniani na kusema vingine ni kujidanganya!
 
Muungano ukivunjika waTanganyika watauana mpaka kila mmoja arudi mkoani kwake na ukabila utafumka ,unajua Zanzibar hakuna ukabila kwa maana ya ukabila isipokuwa kuna lahaja tu nazo zinaeleweka ikiwa utatega sikio makini lakini huku upande wa pili kuna makabila kibao na vita vya chini kwa chini vipo yupo mtu anaweibisha kuhusu vita vya makabila japo vinapakwa rangi ya wakulima na wafugaji lakini ukweli ni vita haswa.
Yaani Watanganyika washukuru sana huu Muungano ndio ukasikia lazima waulinde siju wataulinda mpaka lini maana ni kama Active volcano one day yes itafumka tu.

Mkuu Mwiba hebu tufafanunulie Fomula ya Muungano inayozuia WATANGANYIKA wasiwe na VITA vya Makabila hivi sasa au Fomula hiyo inavyosaidia ukabila usifumke sasa hivi. UKABILA ulikuwepo na utaendelea kuwepo usimsadiki yeyote atakaekwambia Nyerere aliondoa UKABILA yawezekana aliupalilia na pia kupandikiza mbegu za UDINI ambazo Matunda yake leo hii yanatafuta mwanya wa kupenya yalete Madhara kwa Taifa. Pia akaiwacha Tanganyika na Raia wa aina mbili wale wa ukanda wa Pwani ambao wengi wao ni Waislamu chini ya himaya yake(Nyerere) wakawa hawana haki ya Elimu ya juu. na ukanda wa Bara ambako wengi wake ni Wakrito akawapa haki ya Elimu ya juu na Ajira pia. Pamoja na yote hayo WATANGANIKA wamevumiliana na wamekua wenye Subira. Pamoja na kuigawa TANZANIA (Nyerere) baada ya so called Muungano kwa shinikizo la TZ Bara na TZ Visiwani Hakuchoche UPEMBA na UZANZIBARI au USHIRAZI au UARABU na NK mvutano ambao uko waziwazi dakika hii popote walipo Wazanzibari zaidi waliopo nje ya TZ kwa hiyo mkuu Mwiba hizo LAHAJA ulizozitaja zinaweza kabisa kugeuka zikawa HAJA. Tuombe salama.
 
Back
Top Bottom