Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Muungano ukivunjika waTanganyika watauana mpaka kila mmoja arudi mkoani kwake na ukabila utafumka ,unajua Zanzibar hakuna ukabila kwa maana ya ukabila isipokuwa kuna lahaja tu nazo zinaeleweka ikiwa utatega sikio makini lakini huku upande wa pili kuna makabila kibao na vita vya chini kwa chini vipo yupo mtu anaweibisha kuhusu vita vya makabila japo vinapakwa rangi ya wakulima na wafugaji lakini ukweli ni vita haswa.
Yaani Watanganyika washukuru sana huu Muungano ndio ukasikia lazima waulinde siju wataulinda mpaka lini maana ni kama Active volcano one day yes itafumka tu.

Wacha jazba mwana wa kwetu, si unajuwa ule msemo wa kwetu bundi................!
 
Mkuu Mwiba hebu tufafanunulie Fomula ya Muungano inayozuia WATANGANYIKA wasiwe na VITA vya Makabila hivi sasa au Fomula hiyo inavyosaidia ukabila usifumke sasa hivi. UKABILA ulikuwepo na utaendelea kuwepo usimsadiki yeyote atakaekwambia Nyerere aliondoa UKABILA yawezekana aliupalilia na pia kupandikiza mbegu za UDINI ambazo Matunda yake leo hii yanatafuta mwanya wa kupenya yalete Madhara kwa Taifa. Pia akaiwacha Tanganyika na Raia wa aina mbili wale wa ukanda wa Pwani ambao wengi wao ni Waislamu chini ya himaya yake(Nyerere) wakawa hawana haki ya Elimu ya juu. na ukanda wa Bara ambako wengi wake ni Wakrito akawapa haki ya Elimu ya juu na Ajira pia. Pamoja na yote hayo WATANGANIKA wamevumiliana na wamekua wenye Subira. Pamoja na kuigawa TANZANIA (Nyerere) baada ya so called Muungano kwa shinikizo la TZ Bara na TZ Visiwani Hakuchoche UPEMBA na UZANZIBARI au USHIRAZI au UARABU na NK mvutano ambao uko waziwazi dakika hii popote walipo Wazanzibari zaidi waliopo nje ya TZ kwa hiyo mkuu Mwiba hizo LAHAJA ulizozitaja zinaweza kabisa kugeuka zikawa HAJA. Tuombe salama.

Hoja zako nzuri lakini kawaida yetu tunaposhindwa kutatua matatizo yetu au tunapopatwa matatatizo hukimbilia kuangalia vizingizio vya nje ili kuhalalisha hayo lakini ukweli ni kuwa matatizo yetu au umasikini wetu sababu ni sisi wenyewe si Nyerere au Bush.

Naamini kabisa na huo ni ukweli kama Nyerere asingeleta Muungano Zanzibar ingeweza kuwa kama Comoro tu (Wangazija si wapo huko pia?) na pengine hata huo umasikini unaosemwa kuwepo Pemba ungekuwepo mwingi zaidi.

Tena, kama Nyerere asingetaifisha hizo shule za Wakristo hivyo visingizio vya uduni wa Waislamu unaosmemekana kuwepo ungekuwepo zaidi, hata huo udini unaojiingiza kila siku kuleta kubaguana miongoni mwetu ungekuwa umeshageuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hayo maendeleo ya watu wa Bara kuliko watu wa Bara yameletwa na Nyerere au Wamissionari? Nijuavyo mimi Wamisionari ndiyo waliojenga shule huko Bara na sababu kuu ni kuwa watu wa Bara waliupokea Ukristo wakati watu wa Pwani wakati huo walikuwa na dini -Uislamu kwa hiyo Wamisionari wakaelekea bara na kuwaacha watu wa Pwani na Ustaarabu wa Kiislamu, sasa lawama hiyo inatoka wapi?

Ni vema tujichunguze ni wapi tuliposhindwana kuanguka kwanza kabla ya kuwanyooshea vidole watu wengine.
 
Mkuu Mwiba hebu tufafanunulie Fomula ya Muungano inayozuia WATANGANYIKA wasiwe na VITA vya Makabila hivi sasa au Fomula hiyo inavyosaidia ukabila usifumke sasa hivi.

Napenda ufahamu kuwa huu Muungano ndio unaoiweka CCM madarakani pia ukiangalia wabunge wa T/Bara wengi wao wanatoka katika mikoa ambayo imechanganya makabila .

Kitakachotokea ikiwa Muungano utakufa au utavunjika ni lazima Raisi Kikwete na mawaziri wake wote wapoteze kazi ,kitakachofuata ni Uchaguzi Mkuu wa Kwanza kwa Tanganyika kuchagua raisi wao ,sidhani kama umewahi kufanyika Uchaguzi Mkuu hapa Tanganyika.Ila Zanzibar ndio ambao wamewahi tokea wapate Uhuru ndipo yakafuatia Machafuzi.

CCM itabidi ipokonywe hatamu za Uongozi na za dola hilo si jambo rahisi ,Tanganyika itaingia katika mvutano wa ndani.Watakaoipitisha Tanganyika katika kipindi cha mpito itabidi waitishe uchaguzi pengine ndani ya miezi mitatu au sita au mwaka,hivyo katika mbinde hiyo Mikoani hakutakuwa salama wapigania ubunge itabidi wajikombe makwao na kishindo chake tunakielewa ikiwa Kiteto tumeona,Tarime tumeona hivyo kishindo hiki kitaendelea kwa sehemu nyingine na hakitasimama kwa nguvu za polisi ,na mapigano ndipo yatakapoanza au tuwache kuita mapigano tuite machafuko.Hivyo ndivyo ukaona akina Kikwete wanaapa kuyalinda Mapinduzi kinachoendelea itafika wakati hayalindiki tena ,kwani WaZanzibari sasa lao ni moja.Na ikifikia hapo itabidi WaTanganyika wafuate yale ambayo WaZanzibari wanayataka ,kama tulivyoona Tanesco walipoikatia Umeme kwa ajili ya kodi,siku zile ilitolewa tahadhari kuwa umeme kama haukurudi basi Muungano basi siku ya tatu umeme ukarudishwa.
 
"On mainland, it is not true that we do not benefit from minerals, we do but the problem is few of us , for our own reasons we have decided to collaborate with those who cheat us with our minerals."

I am sorry, this is not clear to me. What are you referring to by "We"? We benefit but few of us and we collaborate with those who cheat us??? In other words, you are saying you are among the few who benefit from the on-going looting of mineral resources in Tanzania. Good for you!

This reminds me of one of my Professor who used to say, "in life, there's no we."
 
Anachosema Ngekewa, kwa uelewa wangu, ni kwamba wajanja wachache wameamua kushirikiana na wazungu kuyafaidi hayo madini na kwa hiyo siyo Watanzania wote wanayoyafaidi hayo madini.
 
Narudia jamani mafuta yakipatikana na jamhuri ya pemba ndo hiyooo inanukia
 
Anachosema Ngekewa, kwa uelewa wangu, ni kwamba wajanja wachache wameamua kushirikiana na wazungu kuyafaidi hayo madini na kwa hiyo siyo Watanzania wote wanayoyafaidi hayo madini.

Japo wacheche wanakwapua lakini japo kidogo kinaingia na kinaendeleza bara maana hakimo kwenye Muungano iweje mafuta yawemo ,naona Kikwete atawauwa wengi wanaoitetea Zanzibar ,Kuna aliemvaa Pinda mwanzoni Zanzibar ni Nchi Bilali CCM,kuna wa Mafuta ni mali ya Zanzibar pekee Mansour CCM, Kuna Seif makamo wa kwanza wa Tanzania lazima awe ni Rais wa Zanzibar yaani hao na wafuasi wao nyuma ambao ni WaZanzibar wenye upendo na nchi yao hivyo akina Kikwete au serikali ya Kikwete ni fisadi wanao faa kufunguliwa mashtaka kimataifa kama atakavyofunguliwa mkapa na mauaji ya Januari.
 
mafuta hayajaanza kuchimbwa huko visiwan lakin waache wapemba au waunguja au wazanzibar watishike. siku zote unatumia ulichonacho kutoka (kuendelea/kufanikiwa). hapa bara tuna vivutio vya utalii, madin, ardhi nzur na nk. lakin hatuvitumii ipasavyo kutusogeza mbele kimaendeleo. badala yake tunasikia mikataba mibovu inayowaneemesha wachache na makampun ya nje. kwamfano, kuna dhahabu inachimbwa mwanza lakin atakaye ingia 'dili' ya uchimbaj na kampun ya nje ni suppose daniel yona wa huko kilimanjaro. wao, na akiambiwa atafute wawakilishi wengine kwa niaba ya tz atachukua watu wengine wa mbali na huko mwanza. Mpaka hapo si kitu. shida hasa iko hiv, dili linakuwa dili hasa. kias cha dhahab kinachochimbwa hakuna ajuae, kias wanachopewa wananch wa sehem ile kinakuwa kidogo kwa vipimo vyovyote vile, serikalin nako kinaingia kiduchu na wakat huohuo dalili zote zinaonyesha kuwa huyo mchimbaj anapata zaid. mpemba au mzanzibar anaona yote haya. leo umwambie mafuta eti yawe ya muungano au kitu kama hicho anaona yatakuwa yaleyale.
huenda wao wenyew huko mbelen wasinufaike nayo sana kwa ujumla wao, lakin kwa hali ilivyosasa hiv, machale yanawacheza. na mim naona wana haki wacha machale yawacheze.
wanaona ubinafs na ufisad mkubwa huku bara. huku bara wanaiba, wakienda zanzibar kitawazuia nin?
Laiti kama watu wa visiwan wangeona tuna manage vizur resources huku bara wasingekuwa na waswas sana kama mafuta yawe ya muungano au la. Zaid zaid wangeomba bara ihusike sana katka kuyachimba mpaka kuyauza. Lakin wanachokiona sicho. Wanaona huku kumejaa wez tu. Ufisad kila pahala. Wanaona bora waibiane wao kwa wao kama nako huko kuna virus vya ufisad kama huku bara
Kunapokuwa na ufisad mkubwa wa ajab ajab kunakuwa hakuna kuaminiana ndan ya taifa. Zaid zaid ni chuki na kutengana
 
Okay, ni kweli siijui "society ya wazanzibari". Lakini hao wataalamu unaozungumzia wako wapi? Wanaisaidiaje Zanzibar? Zanzibar is very potential for tourism, fishery and spices production. Ni nini tofauti ya utalii na mafuta katika kuiletea maendeleo Zanzibar? Hao wataalamu wanafanya nini? Tena ni bora utalii kwa sababu mafuta yatawaingiza kwenye mgogoro, hususani kama mafuta hayo yanapatikana Pemba.

"Society ya Wazanzibari" imepiga hatua? Umetumia vigezo gani kusema hivi? Issue hapa si kwamba Zanzibar kuna mafuta au la. Swali hapa ni je Zanzibar imejiandaa vipi kunufaika na raslimali hiyo?

Ukweli ni kwamba kuna wazanzibar wako Oman na wako tayari. Usipuuzie wazanzibari.
 
Zanzibar ikitaka kuendelea inatakiwa kuimarisha elimu ambayo ni ya hali ya chini sana. Zanzibar wakifikiria kwamba mafuta yatakuwa ya kwao ni kichekesho kwani hata UN hawaitambui Zanzibar kama nchi, haina jeshi, pesa, elimu, wafanyakazi, umeme. Hakuna kampuni ambayo ita sign na Zanzibar mkataba wa uchimbaji bila signature ya bara.
 
....shida yenu nini nyie ati? ambao hata mikataba yenu ya dhahabu hampati kitu,kama gas ikiwa kidogo tutanusa tuu na mafuta yakiwa kidogo basi tutajipaka ati na hili jambo ni la wazanzibar na tutalimaliza wenyewe,hamna aibu wachonganishi wakubwa nyie!
 
umeniua mbavu zangu, yaani kusema wabara ndio wenye vichogo na counterpart ni flat head??!! Kiukweli, huu muungano umeshakufa ni mazishi tu ndio yanasubiriwa.

Wenzetu wanatuita sisi tunaotoka bara "machogo"! Bado wanatuona watwana. Hawatupendi, na hawasiti kutuambia hivyo. Sisi ndiyo tunajifanya viziwi na kuendelea kujipendekeza.
 
Wenzetu wanatuita sisi tunaotoka bara "machogo"! Bado wanatuona watwana. Hawatupendi, na hawasiti kutuambia hivyo. Sisi ndiyo tunajifanya viziwi na kuendelea kujipendekeza.

Hayo ni ya kawaida yakhe! Na sio nasi twawaita mdebwedo?
 
Haya! Na wale wapemba wa Namanga na Sharif Shamba watakuwa na vitambulisho vya wapi?

Ukweli ni kuwa hakuna nchi ya kiafrika iliyo kusini mwa Sahara iliyofaidika na mafuta. Kuanzia Nigeria, Gabon, Angola, Chad, Sudan, Equatorial Guinea n.k), mafuta yamewafaidisha wachache na sehemu kubwa ya wananchi kubaki masikini. Tukiangalia historia ya Zanzibar na jinsi ilivyotepenya mafweza waliyorithi ya karafuu ( viwanja vya watoto, tv stesheni ya rangi, nyumba Hampton n.k.), ndiyo maana watu wanatoa caution. Sasa hamjaanza kuyachimba, tayari mnatugeleshea vitambulisho vyenu. Mkianza kuchimba si itakuwa balaa?

Si kweli kuwa hakuna nchi iliyofaidika na mafuta Afrika kusini ya Sahara. Ivyo utatufananisha Tanzania na Nigeria au Angola? Watanzania wa sasa hatuna ile tabia ya Zamani eti bora umasikini wetu kuliko utajiri wa wenzetu. Hii haijatufikisha pahala na ndio maana hata vijinchi vilivyo kwenye migogoro ya kila siku kama Burundi na Rwanda vinatupita kimaendeleo.
Waache Wazanzibar wachimbe mafuta kama yapo na ile tabia ya kuwafumbia macho mafisadi sidhani kama itakubalika katika kizazi cha sasa.
 
Hoja zako nzuri lakini kawaida yetu tunaposhindwa kutatua matatizo yetu au tunapopatwa matatatizo hukimbilia kuangalia vizingizio vya nje ili kuhalalisha hayo lakini ukweli ni kuwa matatizo yetu au umasikini wetu sababu ni sisi wenyewe si Nyerere au Bush.

Naamini kabisa na huo ni ukweli kama Nyerere asingeleta Muungano Zanzibar ingeweza kuwa kama Comoro tu (Wangazija si wapo huko pia?) na pengine hata huo umasikini unaosemwa kuwepo Pemba ungekuwepo mwingi zaidi.

Tena, kama Nyerere asingetaifisha hizo shule za Wakristo hivyo visingizio vya uduni wa Waislamu unaosmemekana kuwepo ungekuwepo zaidi, hata huo udini unaojiingiza kila siku kuleta kubaguana miongoni mwetu ungekuwa umeshageuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hayo maendeleo ya watu wa Bara kuliko watu wa Bara yameletwa na Nyerere au Wamissionari? Nijuavyo mimi Wamisionari ndiyo waliojenga shule huko Bara na sababu kuu ni kuwa watu wa Bara waliupokea Ukristo wakati watu wa Pwani wakati huo walikuwa na dini -Uislamu kwa hiyo Wamisionari wakaelekea bara na kuwaacha watu wa Pwani na Ustaarabu wa Kiislamu, sasa lawama hiyo inatoka wapi?

Ni vema tujichunguze ni wapi tuliposhindwana kuanguka kwanza kabla ya kuwanyooshea vidole watu wengine.

Nimeshakutana na huyu bwana kwenye forum fulani (kama sie basi wanashabihiana kuupotofu) na nimebaini kuwa ni mtu anaependa kueleza mambo kwa kutumia utashi.
Ni kupotosha ukweli kusema kuwa kama si Nyerere basi umasikini wa Zanzibar ungezidi.Inafaa aelewe kuwa Zanzibar haijawahi kuwa masikini hadi pale palipounganishwa ASP na TANU 1977. Tangu enzi za ukoloni Zanzibar ilikuwa nchi tajiri na iliyokuwa ikitowa misaada kwa nchi nyingi hata za Ulaya. Shughuli kubwa iliyoipatia utajiri Zanzibar ni Biashara na Karafuu. Baada ya Mapinduzi na kuja kwa Muungano Zanzibar iliendelea kuwa nchi tajiri hadi kufikia kwa Mzee Karume kukataa misaada ya nje kwani hakukuwa na haja hiyo(Sasa Tanzania na utajiri wake tunategemea misaada). Endelea kufahamu bwana mdogo kuwa kwa kipindi chote cha uhai wa Mzee Karume Nyerere hakuwa na usemi wala mamlaka yoyote kwa Zanzibar na hata Azimio la Arusha lilipokuja Karume alisema kuwa Azimio hilo mwisho wake Chumbe (akimaanisha visiwa vidogo kati ya Tanganyika na Zanzibar). Kabla ya kufa kwa Karume aliacha miradi chungu nzima ambayo hata majirani wa Zanzibar hawakuwa nayo, na Karume aliwahi kutowa msaada wa pesa hata kwa Kenya sasa utajiuliza mwenyewe kwa ndugu yake (Bara) angefanya kiasi gani.
Kufa kwa Mzee Karume na kuunganishwa kwa ASP na TANU ndiko kulikoleta balaa kwa Zanzibar. Hawana uhuru wa kuamuwa wafanye nini kwa maendeleo yao bila kupewa idhini na aidha Serikali ya Muungano (Tanganyika) au ikishindikana kwa kelele za Wazanzibari basi inatumika CCM.
Hebu jiulize Bwana Mdogo iwapo hapo zamani utajiri wa Zanzibar ulikuwa kwa Karafuu iliyoshuka bei na uzalishaji na Biashara kwa kuwa na Bandari stahiki kwa nchi za Afrika Mashariki lakini Serikali ya Muungano inaweka vikwazo vya Biashara kwa Zanzibar nini unategemea itatokea? Ukweli utabaki ukweli hata kama uongo utaurembesha.
 
Zanzibar ikitaka kuendelea inatakiwa kuimarisha elimu ambayo ni ya hali ya chini sana. Zanzibar wakifikiria kwamba mafuta yatakuwa ya kwao ni kichekesho kwani hata UN hawaitambui Zanzibar kama nchi, haina jeshi, pesa, elimu, wafanyakazi, umeme. Hakuna kampuni ambayo ita sign na Zanzibar mkataba wa uchimbaji bila signature ya bara.

Tafadhali acha dharau yako. Ivyo umepata wapi hiyo notion kuwa Wazanzibari wana shida ya Elimu na sio wana shida ya kuondowa umasikini. Hebu jaribuni leo kuwaachia Wazanzibari wafanye mambo yao uone kuwa watashindwa eti hawana elimu. Tatizo la Wazanzibari ni watu kama nyinyi msotambuwa kuwa binaadamu anatakiwa kuwa huru katika maamuzi yake. Una maana gani kufikiria kuwa Wazanzibari hawastahiki kuishi wakiwa nchi, kwa kigezo gani? Kiutawala Zanzibar ilikuwa mwanachama wa UNO hivyo kutambuliwa ilikwishakutambuliwa, kwa uchache? mbona kuna nchi zenye population mdogo zaidi ya Zanzibar nazo ni nchi huru. Nafikiri hicho kajielimu pengine ndio tatizo kwani kwenda shule au kuwa na cheti si kuelimika.
 
I am sorry, this is not clear to me. What are you referring to by "We"? We benefit but few of us and we collaborate with those who cheat us??? In other words, you are saying you are among the few who benefit from the on-going looting of mineral resources in Tanzania. Good for you!

This reminds me of one of my Professor who used to say, "in life, there's no we."

When I say "we" I mean I and you who had through priviledge, acquirred the knowledge of discussing issue regarding matters that concern more than 32 million people who can not afford to use the language we use in our discussion. Perhaps if we count ourselves priviledged through peoples sweat and tears then may be you will agree that there are few who benefit. For me I take that ,that money which come out of minning ang be included into budget is what is our share we had agreed to share with mining investors.
 
Ndugu Mkwegi,
Nasikitika kuwa hukufanya "homework" yako vizuri. Swali la kujiuliza ni moja, Zanzbar wanauwezo (institutional and human capacity) wa kunufaika na mafuta waliyonayo (kama wanayo)? Do they even have people to monitor production? (Refer Mzalendo halisi above). Au ndiyo yale mambo ya elimu=madrasa, kazi = mkwezi.

Kama wakigundua wana mafuta, ni vyema wakatumia muda usiopungua miaka 10 (estimates) kujiandaa kunufaika na mafuta hayo. Otherwise, mafuta yatachimbwa na watabaki kukwea minazi.

I stand to be corrected.

Zundu pule una point ktk maelezo yako.
Kitu kimoja tu ni kwamba hukuelewa ujumbe na argument yangu bado;
point ya msingi hapa ni kwamba hatuna ushahidi wa kitaalam iwapo kuna mafuta Zanzibar au la na kwa kiasi gani,lakini kwa hii move yao waliyonayo kwa sasa ni ishara tosha kuwa jamaa walishaanza muda mrefu kuwa independent bila muungano kujua na hivyo wanajua wanachokisema.
Tazama mifano ya kuwa na vitambulisho vyao vya kitaifa(ambavyo ni vya kisasa),ubadilishaji wa usajili na namba mpya za magari,kujiunga na OIC,...n.k.
Ni reasoning hii hii inayofanya tusibeze matamshi ya waziri.
Pia tusiwe na notion na mawazo ya kizamani juu ya wazanzibar kuwa hawajasoma, hili ni kosa kubwa kuwa under estimate maana kuna wataalam wengi tu tunawaona ktk database zao na siyo habari ya "ukwezi" tena.
Hawajasema ni kampuni ya kizanzibar ndo itakodishwa kuchimba hivyo mwanzoni siyo lazima kuwe na 100% wataalam wa nyumbani.
Ni lini na kwa muda gani watanufaika na uchimbaji huo itategemea kiasi cha mafuta kilichopo.
So my take is, badala ya kuwabeza kwa fikra za kizamani, tuwape necessary support and inputs ktk kufanikisha hili maana litanufaisha eneo letu lote.
 
Back
Top Bottom