Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Federal Government (serikali ya George W) ingependa sana kuchimba mafuta yaliyopo kwenye ANWR. Na hata serikali ya jimbo la Alaska. Na hata aliyekuwa seneta wa Alaska. Ni Congress ndiyo inayotia ngumu. Chama cha Republicans kimeshindwa kuwavuta watu wakutosha kupitisha sheria ya kuruhusu uchimbaji huo.
Mjadala kuhusu uchimbaji wa mafuta katika sehemu nyeti hauhusu mazingira tuu bali zaidi ni security issue. Security, in the sense ya kuondoa kuwa tegemezi kwa mafuta yatokayo nje. Wanao-support uchimbaji katika sehemu hizo wanadai kuwa kuwa na secure source ya mafuta ina trump mambo ya mazingira. Wanaopinga, wanadai kuwa hayo mafuta yatakayopatikana yatapunguza kwa kiasi kidogo sana utegemezi kwa mafuta kutoka nje. Wao wanasisitiza kuwa badala ya kuchimba huko ni kutafuta njia mbadala na kuongeza efficiency ya vyombo vinavyotumia mafuta.
Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nasisitiza kuwa taifa haliwezi kuachia maamuzi ya mwisho kuhusu mafuta yanayopatikana ndani ya mpaka wake yaamuliwe na sehemu moja tu ya Muungano. Maamuzi ni lazima yafanywe na bunge la muungano. Kudai kuwa mbona Zanzibar haifaidiki na gesi ni upuuzi maana hakuna serikali wala bunge la Tanzania Bara. Waziri kivuli wa wizara ya Nishati na Madini ni mbunge wa Mkanyageni (CUF) Mh. Mohamed Habib Juma Mayaa. Huyu ndiye anajukumu la kuangalia na kukosoa inapobidi jinsi serikali tawala ya JMT inavyoendesha shughuli zake katika sekta hii!
Sekta ya mafuta na gesi ni sekta sensitive mno na haziwezi kuwa nje ya Muungano. Au tuseme kwa vile sekta ya viwanda haimo katika masuala ya muungano basi Zanzibar wanaweza kujiamulia kujenga viwanda vya silaha kutosholeza soko la DRC bila kupata kibali cha Bunge la Muungano?
Tusijidanganye. Mafuta si Tanzanite au pamba.
Inabidi nicheke sana. Posti yangu moja umejibu mara mbili. Na unaanza kuleta mambo ya CUF. Fundi usitolee macho mafuta ya watu. Vya watu kuliwa kazi.
Nilishakwambia kwetu Morogoro. Na uungaji wangu mkono hauna maana mimi natoka Zanzibar. Ninachopendelea ni kuwa local governments au mamlaka za mikoa au majimbo ziwe ndizo zenye kuchukua sehemu kubwa ya mshiko.
Kwa juhudi zako za posti mbili nitajibu kwa kirefu katika posti hii. Kwanza nakuomba achana na kufuatilia Stump Speeches na maoni ya pundits. Na uliza wachumi sababu za kweli kuhusu ongezeko la bei la mafuta Marekani katika kipindi cha Summer 2008.
Wanasema sio technology au capital itakayokupa maendeleo bali who is behind it. Kama watanzania tuna vichwa vizuri, kwa vitu tulivyo navyo sasa tungefanya wonders. Mafuta hayatakubalisha Fundi Mchundo kuacha uroho wako wa kuwa na Lexus tatu na kuiba kutoka account ya EPA. Mafuta, hayatakufanya wewe umalize ujenzi wa makao makuu Dodoma au Makazi kule Michenzani au kuendesha shirika la reli.
Tukirudi mafuta ni commodity kama kahawa au sukari. Na thamani yake inafuata kanuni za kiuchumi kama commodities zingine. Hivyo ukielewa kanuni za kiuchumi za commodities mojawapo ikiwa hile ya supply and demand huwezi ukatolea mimacho kama mjusi aliyebanwa na mlango mali za asili iwe dhahabu au mafuta.
Nchi ulizozitaja kama vile Gabon, Botswana, Equatorial Guinea na nchi za Kiarabu zimefaidika sana na mafuta au madini. Lakini vile ukumbuke population za nchi hizo ni ndogo hivyo mapato yanayotokana na madini au mafuta yanachangia sana GDP.
Kwa mfano:
Equatorial Guinea inategemea uuzaji wa mafuta na GNI per capita: US $12,860 (source world bank). Population yake ni 500,000 (Nusu milion).
Hivyo Net Income ya Equatorial Guinea = US $12,860 x 500,000 = US $6430000000
Wakati huo huo Population ya Tanzania ni 40.4 million. Tukigawa Net Income ya Equatorial Guinea kwa population ya Tanzania $6,430,000,000/40,000,000 = US 160.
Nchi yetu ni kubwa na population yake ni kubwa. Hivyo tunatakiwa ku-diversify portfolio yetu. Hatutakiwi kuweka mayai kwenye kapu moja. Kama Zanzibar inaweza kuendelea kwa mafuta waachieni. Kama Mara wanaweza kutumia dhahabu waachieni. Na kama Mtwara wanaweza kutumia gesi waachieni. Hizi ni commodities tu. Nyerere aliwabana wazalishaji wa kahawa mpaka walishindwa kupeleka watoto shule. Lakini matumizi ya kahawa hayakulisaidia taifa zaidi ya kuwafanya wazalishaji wa zao hilo kuwa masikini.
Kwa ukubwa wa nchi yetu ni lazima tuonyeshe kila sehemu imeendelea kwa kutumia injini zipi. Huwezi kuendeleza nchi kama Tanzania kwa kukusanya mapato yote kwenye serikali kuu na baadaye kuyagawanya kwa kila mkoa. Ndio maana watu hamtaki kuondoka DSM.
Vilevile mafuta yakipatikana Zanzibar, Tanzania bara itafaidika vikubwa bila ya kumiliki rasimali yenyewe. Kwanza Mafuta ni commodity inayohitajika kila sehemu. Hivyo nchi kama Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi n.k Zitatumia bandari ya DSM. Vilevile refineries zitakuwepo. Na vilevile bei itakuwa stable.
Vilevile kutakuwepo na by products zinazotokana na mafuta. Na kama ilivyotokea Nigeria, uchimbaji wa mafuta utafanya watu kusahau kazi walizozijua kwa miaka mingi, itafanya Tanzania bara kupata soko la nguvu huko Zanzibar.
Kama ulivyosema kuwa nchi Asia zimeendelea kwa sababu ya location yao na Japan. Location ya Tanzania Bara kuwa karibu na Zanzibar itatusaidia kiuchumi kama mafuta yapo Zanzibar na hata kama mafuta hayo yanamilikiwa na waZanzibar kwa 100%. Lakini kwa uzembe na excuses zako Fundi, Mafuta yatapitia bandari ya Mombasa na wewe utasubiri ushuru wa TRA tu.
Hiyo achana na mambo ya securities unapoongea masuala ya uchumi. Masuala ya securities yamefanya nchi za kiafrika kutumia sana mapato yake katika masuala ya kijeshi.
My hair hurts now.