Kukaa upya mezani na kuujadili muungano ndiyo suluhisho la kudumu litakalo toa haki sawa na kumaliza shida zote. Kwa sasa kuna nyufa ukutani, serikali ya CCM imeamua kutia viraka, dawa ya ufa sio kiraka bali kubomoa na kuziba ufa. Kuiondoa CCM haiwezekani, ni kusubiri tuu mpaka ukuta ubomoke ndipo ujenzi mpya uanze.Pasco, nimekusoma vizuri. Kwamaneno mengine as long as CCM iko madarakani no way CUF itashinda. Suruhisho, Piga chini CCM ruhusu ushindi kwa CUF, funua muungano weka mezani tafuta suruhisho la kudumu.
Wacha kasumba hiyo eti kuiondoa CCM haiwezekani nani kasema KANU itaondolewa nani alijua kuwa Kaunda ataondolewa nani alifikiria kuwa Soviet unio itaparaganyika na mifani mingi tu ,hivyo kusema CCM haitaondoka naona unakuwa mganga wa kienyeji sasa, mfano mdogo tu CCM imeangushwa Pemba tena imeangushwa kifudifudi ,sio CUF walioiangusha CCM bali ni wananchi ndio walioiangusha CCM ,hivyo basi wananchi hawahawa wa sehemu nyengine wanaweza kabisa kuiangusha CCM kama wenzao wa Pemba ,kule Pemba CCM ipo kwenye magwanda ya kuvaa tu ,utawaona watu siku ya sherehe wamekutilia magwanda ya kijani na manjano utafikiri ni wapenzi wa Yanga kumbe wana lao rohoni.Kukaa upya mezani na kuujadili muungano ndiyo suluhisho la kudumu litakalo toa haki sawa na kumaliza shida zote. Kwa sasa kuna nyufa ukutani, serikali ya CCM imeamua kutia viraka, dawa ya ufa sio kiraka bali kubomoa na kuziba ufa. Kuiondoa CCM haiwezekani, ni kusubiri tuu mpaka ukuta ubomoke ndipo ujenzi mpya uanze.
Tiba ya Muungano ni kidonge kigumu sana kumeza kwa serikali ya CCM na CUF wanaonyesha kila dalili ya kutoimeza dose ya CCC kwa tiba ya muungano na ndio maana kila siku wanapokwa ushindi na mwakani ni vivyo hivyo, labda 2015, zamu ya Hamad Rashid au Juma Duni, lakini Mzee wa Sharubu anafafana sana wajihi na Sultan Jamsid hadi kuna mashaka ya nasaba.
Kwa 2010, tutake tusitake, ni yale yale.
Halafu mtu kama wewe eti ndiyo uje uwe kiongozi. Naona Wazenji wataruka ,,,,, na kukanyaga........ Kila la kheri.
Bye bye the end of the Rooooooooooooooooooad
Wewe kama kungekuwa na uwezo zaidi ningekwambia mfufue Mwalimu Nyerere (Kumradhi hapa) halafu akueleze kwanini Tanganyika iin'gan'ganie Zanzibar. Mpaka kati ya Zanzibar na Tanganyika kama unakuwepo? Tanganyika haina amani , haina uchumi, haina ustawi wa jamii. Ni Tanganyika ambayo inahiitaji Zanzibar zaidi. Uliza hilo!!Kuna watu wanasema kuna kero za muungano, mimi nafikiri kuna kero ya Zanzibar!!! Kwanini tusiachane nao wajue hamsini zao?? Tunachotafuta ni nini hasa? Tutaendelea kuwabembeleza mpaka lini?
Hiki kizazi cha wazee wanaong'ang'ania muungano kitapita muda sio mrefu, then tutasahau yote haya!
Bara hamhusiki. Yapo kila pembe ya Unguja na Pemba Tena yapo katika eneo la Bahari Kuu ( ambalo ni Economic exlusive zone ya Zanzibar siyo Tanganyika) Upo hapo.Ayo mafuta ya kujipaka yako pemba au unguja au bara? Mtu ambaye anajua eneo please
Ndugu yangu Mwiba, usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Baada ya kuwapa umeme bila kulipia kwa miaka yote, na fedha ya kuendesha serikali yenu, badala ya shukrani ndio unatuita 'wezi' kwa sababu ya mafuta ya 'alinacha?!.
Wazanzibari (baadhi) mna viburi, jeuri, na lugha za ****** linapokuwa ni jambo la maslahi ya Zanzibar, siye bara tumekuwa waungwana, wastaarabu na wavulivu sana wa chokochoko zote za kuubeza Muungano toka kwenu kama mke mdogo afanyae visa ili apewe talaka.
Kwa taarifa yako, Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano yenye uhuru wa kujitawala kwa mambo yake ya ndani. Zanzibar siyo dola haina nguvu za dola na kamwe haitazipata. Zanzibar haina Polisi, Jeshi wa UT.
Huo msimamo na jeuri ya Baraza la Wawakilishi utaishia Bunge la Muungano. Namuhurumia sana Nahodha, ndio keshapoteza chance yake kuwa rais Zanzibar. Sasa rais Zanzibar, ama Seif Khatib ama Mwinyi Jnr.
Wewe Mwiba utaendelea kulia kwa machungu ya moyo kama uliochomwa na mwiba kwa matarajio safari hii labda hamtapokwa kitumbua mdomoni. Mpewe muuvunje muungano!.
Leo Cuf na CCM mmeungana katika suala la mafuta, unganeni pia kwenye siasa kuumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili amani na ustawi wa kiuchumi uchanue mtutuwe mzigo siye wabara.
Mimi ni miongoni mwa wabara tunaokubali Zanzibar ipewe kila inachotaka ili tuache kuibeba. Amini usiamini, hiyo amani mnayojivunia, iko mikononi mwa bara, mngeachwa ingekuwa ni kuchinjana kwa majambia kwa kwenda mbele.
Mafuta kwetu bara siyo hoja, hoja ni kibri, jeuri na majigambo ambayo mwisho wake ni ndani ya Bunge. Hivi Baraza la Wawakilishi ni nini mbele ya Bunge?. Ni kama baraza la madiwani wa halmashauri ya mkoa wa visiwani, mamlaka yake ni by law tuu, siyo sheria huku bara.
Leo anza kicheko, wakati wa kilio, nitakukumbusha tena. Kutuita wezi ni kosa, kuomba msamaa ni ustaarabu ambao kwa kibri, jeuri, jazba na majigambo yenu hauwezi kukubali, na tusubiri atakaye cheka mwisho.
Binafsi nimeshajiuliza sana swala la Zanzibar. Ni kweli hawa ni ndugu zetu, pia ni kweli muungano wetu kama ulivyounganishwa na Nyerere na Karume unautata, vile vile ni kweli kuungana ni kitu kizuri katika kukuza uchumi na mahusiano baina ya zilizokuwa nchi mbili. Hatahivyo kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajibiki na hao wanaosuruhisha maswala ya muungano.
Haikuniingia akilini nilivyosikia Zanzibar ilikuwa inatumia umeme toka Bara bila kulipa mpaka ilipoingia Net Group Solution ambapo waliambiwa walipe or else wanakatiwa umeme. hapo ndipo nilipochoka maana walipiga mkwala kuwa wakikatiwa umeme wanavunja muungano, ukweli ni kwamba serikari ya bara ililipa lile deni la Zanzibar na mambo yakawa shwari. Hata hivyo bado hawa jamaa wanalazimisha tuvunje muungano lakini CCM haitaki na imekula yamini kuulinda kwa nguvu zote.
Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Hataukimpa offer nyingi nyingi kama hana mapenzi na wewe itakuwa ngumu kuwa rafiki yako. Kinachoendelea Zanjibar na Bongo sasa hivi ni kama baba na mtoto. Zanzibar kila itakachotaka Bara itabidi tukikubari ili mulinda muungano. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????
muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.
muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.
Nimefurahi kusikia CCM na CUF wamekubaliana kwa asilimia 100% kwenye hili. Nasubiri kuona kama na mpasuko watauziba kwa asilimia 100% nani ya baraza hilohilo la wawakilishi. Vinginevyo ndiyo ile hadithi ya kujenga jumba la kifalme hewani.
Chonde chonde tuazime busara sasa..huu muungano una umuhimu mkubwa sana kwa zanzibar kuliko wanavyojidanganya
Muda mwingine watu wanakubaliana kutokukubaliana. Hebu jiulize kama Zanzibar or Tanganyika si nchi bali Tanzania, na kama huu muungano ni halali kwanini suala la mafuta yaliyoko zanzibar iwe ni mali ya zanzibar peke yake???? Binafsi hainiingii akilini hapa kuna kauhuni fulani kanaendelea hakajawekwa wazi. Mbona resource zote zinazopatikana Tanganyika huchukuliwa kama mali ya Tanzania (Tanganyika & Zanzibar)na watanganyika wala viongozi wake hawalalamiki???????????
Hivi, hawa Wazenj wakija kuta kwamba chimbuko la hayo mafuta (ambayo kwa sasa ni mafuta hewa) ni Tanga, watachimba shimo hadi Tanga? Kwa nini tunaanza kuhesabu vifaranga il hali hata yai halijakomaa?
Kama ni kweli, ichagueni CUF, iyakane Mapinduzi matukufu, ivunje Muungano na hatimaye muanze kuchinjana!. Siye bara hatumo!.