Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Hati za Muungano zipo, tatizo zimeandikwa kienyeji mno ndio maana zinafichwa. Zikipatikana kuna madudu mengi yatafichuka. Hati halisi zilisainiwa kabla ya hiyo April 26, '64. Baada ya hapo zikatarishwa nyengine zenye afadhali kidogo, Karume hakusaini.Hili ninavyoelewa mie ndowa yoyote ile ikiwa ya kisilamu au kikristo kunakuwa na shahada ya ndowa, lakini ndowa hii shahada zake zimeliwawa na mchwa.sasa itakuwaje wakati wa kurisiana pale mmoja akiondoka duniani , huoni kuna uwezekano mmoja kati yenu akapoteza urisi wake ?
Kwa kifupi hata Karume akifufuka leo, viongozi waliopo watasutwa. Msingi mkuu wa muungano ni kauli ya Karume 'Tuungane, wewe rais, mimi makamo' yaliyofuatia yote sio issue.
Kitendo tuu cha rais wa Zanzibar kuwa sio Makamu, hicho peke yake kinatosha kuuvunjilia mbali muungano, achilia mambo lukuki tuliyoyaongeza bila ridhaa ya Baraza la Wawakilishi.
Tulitumia utaratibu wa dini ya Kiislamu ukitaka kuoa mke wa pili, omba ridhaa ya mke mkubwa, hata akikataa, bado unaweza kuoa tuu, kama ni hivyo, ridhaa ya nini?.
Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano walitosha kuiwakilisha Zanzibar na mabadiliko yote ya katiba ni halali.
Inachofanya baraza kwa sasa ni chokochoko, bora 'wamchokoe pweza, binadamu bara watamshindwa!'