Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hili ninavyoelewa mie ndowa yoyote ile ikiwa ya kisilamu au kikristo kunakuwa na shahada ya ndowa, lakini ndowa hii shahada zake zimeliwawa na mchwa.sasa itakuwaje wakati wa kurisiana pale mmoja akiondoka duniani , huoni kuna uwezekano mmoja kati yenu akapoteza urisi wake ?
Hati za Muungano zipo, tatizo zimeandikwa kienyeji mno ndio maana zinafichwa. Zikipatikana kuna madudu mengi yatafichuka. Hati halisi zilisainiwa kabla ya hiyo April 26, '64. Baada ya hapo zikatarishwa nyengine zenye afadhali kidogo, Karume hakusaini.

Kwa kifupi hata Karume akifufuka leo, viongozi waliopo watasutwa. Msingi mkuu wa muungano ni kauli ya Karume 'Tuungane, wewe rais, mimi makamo' yaliyofuatia yote sio issue.

Kitendo tuu cha rais wa Zanzibar kuwa sio Makamu, hicho peke yake kinatosha kuuvunjilia mbali muungano, achilia mambo lukuki tuliyoyaongeza bila ridhaa ya Baraza la Wawakilishi.

Tulitumia utaratibu wa dini ya Kiislamu ukitaka kuoa mke wa pili, omba ridhaa ya mke mkubwa, hata akikataa, bado unaweza kuoa tuu, kama ni hivyo, ridhaa ya nini?.

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano walitosha kuiwakilisha Zanzibar na mabadiliko yote ya katiba ni halali.

Inachofanya baraza kwa sasa ni chokochoko, bora 'wamchokoe pweza, binadamu bara watamshindwa!'
 
jamani hivi kiswahili kigumu kiasi hichi na kufikia baadhi yetu hatukifahamu au kukisikia?kwani ni upande gani wanaolilia mungano kwa vitisho na silaha za kijeshi na mauwaji hakuna wengine isipokuwa ni serekali yatanganyika.
 
Kama ni kweli, ichagueni CUF, iyakane Mapinduzi matukufu, ivunje Muungano na hatimaye muanze kuchinjana!. Siye bara hatumo!.

CUF imeshachaguliwa zamani ila mafisadi kutoka Tanganyika ndio wanaochukua na kubadilisha matokeo ili wazidi kumega ,sasa kuna hatari ya njia hiyo mnayotumia kuondolewa kiaina na hapo ndipo tulipo na hatua kwa hatua zimeanza na dalili mnaziona na mengine yanaonekana waziwazi nyie endeleeni kumlea CCM atawalinda maisha.Si wanamlinda baba yenu wa Taifa misingi na hila zake ,wacha watafune kila kitu na nyie mnashangilia yanini kupiga mayowe kuwa wanakula hazina ya nchi.
 
baada ya commoro kuonyesha nia yao ya kujiunga na TZ, ZNZ wanajidai wanamafuta ili tuwaone wao wa maana
 
Hati za Muungano zipo, tatizo zimeandikwa kienyeji mno ndio maana zinafichwa. Zikipatikana kuna madudu mengi yatafichuka. Hati halisi zilisainiwa kabla ya hiyo April 26, '64. Baada ya hapo zikatarishwa nyengine zenye afadhali kidogo, Karume hakusaini.

Kwa kifupi hata Karume akifufuka leo, viongozi waliopo watasutwa. Msingi mkuu wa muungano ni kauli ya Karume 'Tuungane, wewe rais, mimi makamo' yaliyofuatia yote sio issue.

Kitendo tuu cha rais wa Zanzibar kuwa sio Makamu, hicho peke yake kinatosha kuuvunjilia mbali muungano, achilia mambo lukuki tuliyoyaongeza bila ridhaa ya Baraza la Wawakilishi.

Tulitumia utaratibu wa dini ya Kiislamu ukitaka kuoa mke wa pili, omba ridhaa ya mke mkubwa, hata akikataa, bado unaweza kuoa tuu, kama ni hivyo, ridhaa ya nini?.

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano walitosha kuiwakilisha Zanzibar na mabadiliko yote ya katiba ni halali.

Inachofanya baraza kwa sasa ni chokochoko, bora 'wamchokoe pweza, binadamu bara watamshindwa!'

Pasco kama unaaccess na hizi nyaraka tafadhari tuwekee hapa tuweze kupata ukweli halisi. Kama wanatambua kuwa hizo nyaraka ni feki siwayamalize kiutuuzima??? si dhambi kukiri kosa isitoshe unakiri kosa kwa niaba ya mtu mwingine ambaye hayupo duniani.
 
Kama ni kweli, hilo ni kosa kubwa la kikatiba la bara. Tatizo la sisi bara ni ubabe, jee unajua makabrasha yaliyotayarishwa na Wolfgang Dourado na kuridhiwa na Aboud Jumbe kuhusu haki ya Zanzibar akijitayarisha kuishitaki Tanzania UN yalisababisha nini?. Hali ya kisiasa ilichafuka na watu wakafungwa midomo.

Ubabe ndicho mkitakacho na punde si punde mtakipata na kujua kama maharage ni mboga au futari.

So Pasco unakubaliana nami kuwa Tanganyika kupitia CCM tunainyanyasa Zanzibar yaani tunaitawala ndivyosivyo.
 
baada ya commoro kuonyesha nia yao ya kujiunga na TZ, ZNZ wanajidai wanamafuta ili tuwaone wao wa maana

Comoro wajiunge na Tz ,hilo hawalikubali hata siku moja ,aidha ikiwa watajiunga na kuwa kama Kenya na Uganda na ambavyo Rwanda na Burundi zimeomba uwanachama Lakini Zanzibar imeshatafunwa na nyoka ,hivyo kwa vyovyote vile madai ya Zanzibar hayakuanza leo wala jana ni madai ya zamani kabisa hayahusiani wala hawana habari na Comoro na hata wakijiunga basi hapatadumu kitu labda mkaikalie kimabavu/kinguvu kiulaghai na kitapeli.Na mafisadi wenu wengi watahamia huko itakuwa ni safe heaven kuliko Zenji maana Zenji kumoto na hakutabiriki kwa kuishi mafisadi.
 
baada ya commoro kuonyesha nia yao ya kujiunga na TZ, ZNZ wanajidai wanamafuta ili tuwaone wao wa maana

Hivi kumbe inauma kuona zanzibar wajiweka mbali nanyi?isitoshe ni serekali gani inayopelekea vitisho vya mauwaji au hata kufikia kuwauwa na kubaka raia wa zanzibar?hakuna nyingine isipokuwa ni ile iliyochangulia na watanganyika , kwa kisingizio eti mungano usife ?kifo cha nyani kinapowadia miti yote huteleza. only time will tell 😕
 
Hi ninyi, wazenji wamewapa nini mnawanganinia siku zote wee? Zenji ni zigo jamani, masikini Nyerere (RIP) akaacha watu kama wamalawi, wanyaruanda au waburundi ambao niwachap kazi, wanapiga shule fresh akaenda tafuta wapiga maneno matatizo ya ndo za mkeka ndiyo hayo. Waacheni waende zao tutajipange upya, kama zenji itageuka Somalia hilo halituhusu sisi, mombasa ni karibu watakimbilia...Tanganyika shule ipo tukiitumia vyema tunaweza kuwa kama South Korea au hata Japan, kwani Japan wanategemea mafuta? Dhahabu tunachimba, Almas tunachimba, Gas tunachimba, Tanzanite tunachimba, mafuta tulichimba japo mapipa 90, sasa ya nini kungania plots ambazo not even confirmed kama kuna hayo mafuta....eti muungano wetu ni mfano wa kuigwa dunia, we took the wrong people or side of the world. Zenj haina natural resources, it's a weak market so huwezi uza kitu kule, hakuna uzarishaji, hakuna ajira bali wamechukua ajira, tunagawa umeme wakati wenyewe tunauhitaji..Bora ulee kilema au yatima mungu atakukumbuka lakini siyo Zenj, please please, leave them alone we dont need them anyway . Rais bora ni yule atakaye ahidi kuungalia upya muungano...jumba lina nyufa kibao unaishia kuzibaziba, si ubomoe tu ujenge mpya mpaka likudondokee?
 
So Pasco unakubaliana nami kuwa Tanganyika kupitia CCM tunainyanyasa Zanzibar yaani tunaitawala ndivyosivyo.

Hili halina ubishi, hata muungano wenyewe una matatizo toka kwenye fundamental pillars zake. Prof. Issa Shivji aliuchambua Muungano na kuuvua nguo katika andiko lake la 'The Legal Basis of Union Between Tanganyika and Zanzibar'. Andiko hili alilitoa mwaka 2004 wakati wa miaka 40 ya Muungano. Andiko hili linapatikana Maktaba Kuu ya UDSM, sehemu ya Sheria

Profesa alizungumzia udhaifu wa Muungano kisheria jinsi ulivyokiuka sheria tangu mwanzo kwa Watanganyika wote kuburuzwa na Bunge la chama cha Tanu na Wanzanzibari wote kuburutwa na Baraza la Wawakilishi la ASP vyombo ambavyo havikuwa na mamlaka. Muungano halali ulitakiwa kuundwa kwa white paper, halafu kuundwa kwa constituent assembly na sio vyama. Badala yake ni Bunge na Baraza la Wawakilishi yalijigeuza Constituent Assembly na kuupitisha Muungano kwa papara. Kilichofuatia ni kuongeza vipengele kwa vipengele kwa njia za kibabe bila kuvipitisha Baraza la Wawakilishi kuridhia.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado aliyagundua mapungufu hayo ya Muungano
Akakuta Katiba imeweka ribit hakuna namna yoyote, wala mahakama yoyote nchini yenye mamlaka ya kusikiliza shauri lolote la malalamiko ya Muungano. Katika inatamka ni lazima uindwe mahakama ya katiba.
Taratibu za kuundwa mahakama hiyo ni mlolongo mwingine na rais wa Muungano bara ndiye aliyeshika mpini.

Dourado akamshauri Jumbe wakaishitaki Tanzania kwenye UN. Wakatayarisha makaratasi wakajipanga vizuri tuu, wakati huo jamaa wa UT wanaripoti kila kitu kwa Nyerere. Wakati muafaka uliwadia, Jumbe akaitwa Dodoma kwenye CC na NEC, akapata kibano cha nguvu. Dourado akaozea kiziuzini, Jumbe nae kizuizi cha nyumbani. Taifa likatangaziwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya siasa za Zanzibar zilizopolekea mabadiliko ya uongozi Zanzibar.

Hizi kelele za Baraza na Nahodha wanauchokoa tena Muungano. Mohamed Seif Khatib ni mkongwe na anaelewa somo, Nahodha ni kinda la juzi tuu, subirini walete azimio hilo muone jinsi watu watakavyopigwa dafrao. Hata Dr. Salmin alitaka kulea chokochoko, alichokipata wapambe wake akina Twahir Ali wanajua kilichowapata na vimbelembele wao kina Castico.

Siasa za Zanzibar ni ngumu, zina shari, jazba, chuki, vijembe, chuki, husda, kibri na kila aina ya ubabe, dawa ikawa ni ubabe tuu na ndicho kitachofuatia katika hili suala la mafuta-alinacha.
 
kuna kipindi kinafika inabidi ukweli tuukubali tu, kwa kweli zanzibar kabla ya muungano walikuwa juu sana kimaendeleo hata kuliko bara na kulikuwa na programms ambazo zilikuwa zinaworkout na hata kuna kipindi serikali ya bara ilishachukua mkopo kutoka zanzibar(kama kuna m2 mwenye kumbukumbu na hili),
ukweli uliowazi hao watu wa zanzibar wako commited kusaidiana na kweli kama muungano ukivunjika na zanzibar kukawa na amani ya angalau miaka mitatu zanzibar itakuwa mbali sana kimaendeleo bila hata kuchimba hayo mafuta, kwa sekta ya utalii pekeyake zanzibar ni maarufu sana duniani kuliko serikali ya muungano,kilimanjaro hata serengeti
mimi nadhani muda muafaka wa kuvunja muungano ndio huu kwa sababu tutakapoiona zanzibar ina prosper within short time hapo ndipo tutakuwa na akili nzuri ya kuchagua viongozi wazuri na dawa sahihi ya mafisadi itapatikana, mimi naona hapa ni kugawana umaskini tu kati ya bara na visiwani
 
Pasco kama unaaccess na hizi nyaraka tafadhari tuwekee hapa tuweze kupata ukweli halisi. Kama wanatambua kuwa hizo nyaraka ni feki siwayamalize kiutuuzima??? si dhambi kukiri kosa isitoshe unakiri kosa kwa niaba ya mtu mwingine ambaye hayupo duniani.
Hiyo access niipate wapi masikini wa Mungu mimi?. Hizo ni data zinatolewa na mashuhuda wa mambo ambao wamejinyamazia. Kuna wengi wanajua mambo ila wamejinyamazia.

Je ni wangapi mnajua kuwa Hayati Karume hakushiriki Mapinduzi?. Je wangapi wanajua mapinduzi hayakutumia risasi, mwenye bunduki akiwa mmoja tuu Mganda John Okelo?. Je wangapi wanajua waliouwawa waliuawa kwa Jambia kwa kukatwa vichwa kuanzia Baba wanawake na watoto, hata wa mama wajawazito?.
Kwa mujibu wa kitabu cha History of Afrika, walikufa watu zaidi ya Elfu 64. Kuna watu wanajua walizikwa wapi?.

Hata sababu za Kuuwawa Karume zinajulikana bali zinafichwa fichwa tuu ili kupunguza machungu ya mapinduzi.

Hivyo kwenye siasa za Zanzibar, kuna watu wana machungu, usongo na dhamira ya kulipiza visasi ndio maana hata wakishinda akina fulani, na watashinda tena lakini kamwe hawapewi nchi ili kudumisha muungano na kuepusha shari.
 
Baraza la wawakilishi ni sawa na braza la madiwani...jambo likianzia huko mwisho wake bungeni....ati mambo yaliyoamuliwa bungeni mpaka yakubaliwe baraza la wawakilishi!? ebooo!Wale wanatakiwa kutunga sheria za zanzibar kufutatana na katiba ya zanzibar.....ni sawa na bylaws tu. Bunge la Muungano ndiko kunakomalizikia kila kitu.....hata hao wawakilishi wabwateje.
Kama kweli ndugu zetu chokochoko za kuvunja muungano ni kwa sababu ya mafuta....basi vichwa vyao lazima vinawalakini. Hakuna duniani popote kunakuwa-declared uwepo wa mafuta bila ya kuyachimba na ku-flow hayo mafuta...tena ku-evaluate kama kuna comercial quantity.

Yakhee..mafuta yapo atii....wanakula urojo barazani.......Shit!
 
Mimi hizi hoja za wazanzibari huwa zinanikera sana.Natamani siku ambayo huu muungano utavunjwa. Najua viongozi (Marais) wote wanaogopa historia kuwahukumu lakini tunahitaji kupata Raisi ambaye atasema sasa inatosha wazanzibar nendeni kwenu sasa basi.
 
Hi ninyi, wazenji wamewapa nini mnawanganinia siku zote wee? Zenji ni zigo jamani, masikini Nyerere (RIP) akaacha watu kama wamalawi, wanyaruanda au waburundi ambao niwachap kazi, wanapiga shule fresh akaenda tafuta wapiga maneno matatizo ya ndo za mkeka ndiyo hayo. Waacheni waende zao tutajipange upya, kama zenji itageuka Somalia hilo halituhusu sisi, mombasa ni karibu watakimbilia...Tanganyika shule ipo tukiitumia vyema tunaweza kuwa kama South Korea au hata Japan, kwani Japan wanategemea mafuta? Dhahabu tunachimba, Almas tunachimba, Gas tunachimba, Tanzanite tunachimba, mafuta tulichimba japo mapipa 90, sasa ya nini kungania plots ambazo not even confirmed kama kuna hayo mafuta....eti muungano wetu ni mfano wa kuigwa dunia, we took the wrong people or side of the world. Zenj haina natural resources, it's a weak market so huwezi uza kitu kule, hakuna uzarishaji, hakuna ajira bali wamechukua ajira, tunagawa umeme wakati wenyewe tunauhitaji..Bora ulee kilema au yatima mungu atakukumbuka lakini siyo Zenj, please please, leave them alone we dont need them anyway . Rais bora ni yule atakaye ahidi kuungalia upya muungano...jumba lina nyufa kibao unaishia kuzibaziba, si ubomoe tu ujenge mpya mpaka likudondokee?

Sungura alipo zikosa zabibu alitowa maneno kama yako zabibu gani mbichi mbovu haziliki sababu tu amezikosa sasa any way shukurani zangu za zati nazipeleka kwa wabunge mashuhuri waliochagulia kwa imani ya wananchi nitawataja wachache hapa lowasa ,rostam,marehemu Bilal ,chenge (visent) etc wewe mtowa maoni endelea hivyo hivyo by the way usije ukajisahau sana
 
Hili halina ubishi, hata muungano wenyewe una matatizo toka kwenye fundamental pillars zake. Prof. Issa Shivji aliuchambua Muungano na kuuvua nguo katika andiko lake la 'The Legal Basis of Union Between Tanganyika and Zanzibar'. Andiko hili alilitoa mwaka 2004 wakati wa miaka 40 ya Muungano. Andiko hili linapatikana Maktaba Kuu ya UDSM, sehemu ya Sheria

Profesa alizungumzia udhaifu wa Muungano kisheria jinsi ulivyokiuka sheria tangu mwanzo kwa Watanganyika wote kuburuzwa na Bunge la chama cha Tanu na Wanzanzibari wote kuburutwa na Baraza la Wawakilishi la ASP vyombo ambavyo havikuwa na mamlaka. Muungano halali ulitakiwa kuundwa kwa white paper, halafu kuundwa kwa constituent assembly na sio vyama. Badala yake ni Bunge na Baraza la Wawakilishi yalijigeuza Constituent Assembly na kuupitisha Muungano kwa papara. Kilichofuatia ni kuongeza vipengele kwa vipengele kwa njia za kibabe bila kuvipitisha Baraza la Wawakilishi kuridhia.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado aliyagundua mapungufu hayo ya Muungano
Akakuta Katiba imeweka ribit hakuna namna yoyote, wala mahakama yoyote nchini yenye mamlaka ya kusikiliza shauri lolote la malalamiko ya Muungano. Katika inatamka ni lazima uindwe mahakama ya katiba.
Taratibu za kuundwa mahakama hiyo ni mlolongo mwingine na rais wa Muungano bara ndiye aliyeshika mpini.

Dourado akamshauri Jumbe wakaishitaki Tanzania kwenye UN. Wakatayarisha makaratasi wakajipanga vizuri tuu, wakati huo jamaa wa UT wanaripoti kila kitu kwa Nyerere. Wakati muafaka uliwadia, Jumbe akaitwa Dodoma kwenye CC na NEC, akapata kibano cha nguvu. Dourado akaozea kiziuzini, Jumbe nae kizuizi cha nyumbani. Taifa likatangaziwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya siasa za Zanzibar zilizopolekea mabadiliko ya uongozi Zanzibar.

Hizi kelele za Baraza na Nahodha wanauchokoa tena Muungano. Mohamed Seif Khatib ni mkongwe na anaelewa somo, Nahodha ni kinda la juzi tuu, subirini walete azimio hilo muone jinsi watu watakavyopigwa dafrao. Hata Dr. Salmin alitaka kulea chokochoko, alichokipata wapambe wake akina Twahir Ali wanajua kilichowapata na vimbelembele wao kina Castico.

Siasa za Zanzibar ni ngumu, zina shari, jazba, chuki, vijembe, chuki, husda, kibri na kila aina ya ubabe, dawa ikawa ni ubabe tuu na ndicho kitachofuatia katika hili suala la mafuta-alinacha.

Pasco, nimekusoma vizuri. Kwamaneno mengine as long as CCM iko madarakani no way CUF itashinda. Suruhisho, Piga chini CCM ruhusu ushindi kwa CUF, funua muungano weka mezani tafuta suruhisho la kudumu.
 
Asalamu alaykum.

habari za siku nyingi takriban mwezi wa tatu huu sipo mtandaoni kutokana na tatizo nililokuwa likinikabili ambalo nilifanyiwa upasuaji wa mguu hata hivyo nashukuru kwa wale wote ambao wamenifariji kwa njia moja au nyengine kwa kunitakia dua za kheri na sasa nimepona bila ya shaka tupo pamoja katika majadiliano.

Naomba nichangia hii mada ila kwa hakika kilichoandikwa juu kabisa kwamba baraza la wawakilishi hatimae limepitisha mswaada wa suala la mafuta sio sahihi. ama ni kweli wajumbe wa CCM na CUF kwa umoja wao wamependekeza baadhi ya mambo lakini sio mswada ni kuishauri serikali

Kwani hakuna mswaada uliopitishwa kilichokuwa kikijadiliwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kwa takriban wiki mbili sasa sio mswaada ni taarifa ya serikali kuhusiana na mapendekezo ya mshauri mwelekezi david reading kutoka uingereza ambayo alipewa kazi ya kuzishauri serikali zote mbili juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na namna ya ugawaji.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi walijadili na mwisho kutoka na maazimio ya baraza na kuishauri serikali ya mapinduzi zanzibar kama ifuatavyo.

Wiki iliyopita, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliwasilisha taarifa katika Baraza ikitaka maoni ya Wawakilishi kuliondoa au kulibakisha suala la mafuta na gesi asilia kwenye mambo ya Muungano.

Mapendekezo mengine ya SMZ ni kuwa, Ardhi na bahari ya ndani ya Zanzibar, maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibat sura ya kwanza 2(1) ni milki ya Zanzibar, katika maeneo hayo usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe wa Zanzibar pekee.

Pendekezo la pili ni kuwa , sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na mengineyo yanayoendana na hayo , chombo hicho kitakuwa sawa na lile Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC).

pendekezo la mwisho kuwa kwa upande wa bahari kuu(EEZ), Serikali inashauri kukubali mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa eneo hilo pekee kwa makubaliano maalum na sio muundo wa sasa wa Taasisi na sheria kwamba Zanzibar itakuwa ni mshiriki sawa.

kwa maana hiyo mswada bado hajawasilishwa katika kikao kwanza hadi bunge lijadili na kufikia mwafaka wa suala hili.
 
Stonetown,
Pole sana kwa kuuguwa na asante kwa kurekebisha makala ya Sultan wa CUF.
Pasco, nakubaliana na wewe kwa saana juu ya swala la Muungano. Hili swala ni gumu sana na labda kujua inabidi kwenda kuangalia chimbuko lenyewe.

Warusi walitaka kujenga base yao Zenji na wakati huo USA wana base yao Kenya. Hili jambo CIA hawakulipenda. Basi wakafanya trick moja ya kitoto sana kuwa, Zanzibar iunganishwe Tanganyika na Mrusi alie. Waunganishaji hawakufiria zaidi kwenye kuunganisha nchi kwa faida ya wananchi ila kwa faida ya UK na USA.

Kwenda kupekecha haya mafaili kutaumbua mengi. Utashangaa hata kifo cha huyo Okello mwenyewe. Na ubabe wake wote, aliishi maisha ya ajabu baada ya kufukuzwa Zenji na Tanganyika. Kama kweli alisaidia mapinduzi kwa nini alifukuzwa? Kifo cha karume baadaye. Je USA hadi leo wana lao jambo hapo Zenji au ni katika kuficha siri? Je Zenji mkienda UN (USA) kwenda kuishtaki Tanzania na hapohapo muimbue USA, mtasikilizwa? Hamuoni mnapigana nje na ndani ya Tanzania? Tena heri ya Tanzania, JKN hayupo tena ila huko USA, mhhhh soo la nchi.

Haya kama kesi ya baba ngedere mwampelekea mtoto wa ngedere, na mnategemea kupata solution basi kila la kheri. Nafikiri hili jambo Zenji mnalifanya kwa hasira. Mngejipanga vizuri na kutumia diplomat chanels zaidi kuliko kutumia maguvu naona mngelifanikiwa. Haya, kama mwaona nje ya Muungano mtafanikiwa zaidi kuliko ndani ya Muungano, go for it. Nakutakieni kila la kheri na Mungu atakuwa nanyi ili hatimaye muondokane na utawala wa Watanganyika wachache. Sisi pia ngoja tuendeleze vita yetu juu ya watawala haohao ambao hata Tanganyika wanaitawala (kama mlikuwa hamjui).
 
Asalamu alaykum.

habari za siku nyingi takriban mwezi wa tatu huu sipo mtandaoni kutokana na tatizo nililokuwa likinikabili ambalo nilifanyiwa upasuaji wa mguu hata hivyo nashukuru kwa wale wote ambao wamenifariji kwa njia moja au nyengine kwa kunitakia dua za kheri na sasa nimepona bila ya shaka tupo pamoja katika majadiliano.

Naomba nichangia hii mada ila kwa hakika kilichoandikwa juu kabisa kwamba baraza la wawakilishi hatimae limepitisha mswaada wa suala la mafuta sio sahihi. ama ni kweli wajumbe wa CCM na CUF kwa umoja wao wamependekeza baadhi ya mambo lakini sio mswada ni kuishauri serikali

Kwani hakuna mswaada uliopitishwa kilichokuwa kikijadiliwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kwa takriban wiki mbili sasa sio mswaada ni taarifa ya serikali kuhusiana na mapendekezo ya mshauri mwelekezi david reading kutoka uingereza ambayo alipewa kazi ya kuzishauri serikali zote mbili juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na namna ya ugawaji.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi walijadili na mwisho kutoka na maazimio ya baraza na kuishauri serikali ya mapinduzi zanzibar kama ifuatavyo.

Wiki iliyopita, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliwasilisha taarifa katika Baraza ikitaka maoni ya Wawakilishi kuliondoa au kulibakisha suala la mafuta na gesi asilia kwenye mambo ya Muungano.

Mapendekezo mengine ya SMZ ni kuwa, Ardhi na bahari ya ndani ya Zanzibar, maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibat sura ya kwanza 2(1) ni milki ya Zanzibar, katika maeneo hayo usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe wa Zanzibar pekee.

Pendekezo la pili ni kuwa , sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na mengineyo yanayoendana na hayo , chombo hicho kitakuwa sawa na lile Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC).

pendekezo la mwisho kuwa kwa upande wa bahari kuu(EEZ), Serikali inashauri kukubali mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa eneo hilo pekee kwa makubaliano maalum na sio muundo wa sasa wa Taasisi na sheria kwamba Zanzibar itakuwa ni mshiriki sawa.

kwa maana hiyo mswada bado hajawasilishwa katika kikao kwanza hadi bunge lijadili na kufikia mwafaka wa suala hili.

pia ikumbukwe mada hii kupelekwa bungeni ni ukikwaji wa katiba kwani hakuna kumbukumbuyoyote ileinayoonesha pande hizi mbili serekali zilitiana saini au kukubali kuwa mambo ya mafuta kuwa ni ya mungano sasa utapeleka vipi swali hili ambala halijakuwapo ndani ya mambo ya mungano kutokea huko mwanzo, huu ni ujanja ambao kwa njia moja au nyingi unaendelea kutumika ,utagunduwa kuwa wazanzibar wameligunduwa hilo sasa baada ya mika nenda rudi ya hewala bwana na wanatumiliwa kama chombo cha Tanganyika kusafiria na kukamilisha kile walichokidhamiri .
 
Halafu mtu kama wewe eti ndiyo uje uwe kiongozi. Naona Wazenji wataruka ,,,,, na kukanyaga........ Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom