Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mimi siku zote huwa naona kuwa Zanzibar waachiwe waamue mambo yao hata wakitaka kujitenga wawe na hiari wakitaka kubaki karibu na mafuta yao waachiwe na hata gas yao waachiwe pia.
Ila nionavyo mimi kama mimi nawaona wabinafsi si kwa wabara tu hata wao kwa wao.
Hebu wapewe wakitakacho labda watajitambua kuwa kweli wanahitaji muungano au laa kama muungano ni mzogo kwao basi watakuwa wamechagua njia sahihi kama wanauhitaji basi wataamua la kufanya.
 
Wadanganyika wataendelea kuosha vinywa kila siku kwamba wanaibeba Zanzibar.
Zanzibar ni mzigo kwa muungano.
Iweje kitu kinachokutia hasara uking'ang'anie.

Kama ni umeme Zanzibar ilianza kupokea umeme kutoka bara kwenye uongozi wa awamu ya pili [mzee Jumbe]

Je huo muda wa nyuma walikua hawana umeme?

Halafu wadanganyika kiburi chao ni umeme wakati wazanzibari wala hawakijali.

Kwani Zanzibar lazima inunue umeme kutoka bara tu?
 
wale wazee walionda un kudai pemba iwe nchi walienda wenyewe tu hamna hata mmbunge mmoja wa cuf aliyoambatana nao, na Cuf wananguvu sana pemba wakitaka kufanya chochote wanafanya na hata ccm z'bar wakitaka wanafanya lakini, hawataki kutoka muungano na sasa hivi wameshasikia kuna nyumba ndogo(commoro) hofu zimewajaaaaa
 
Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi...mi nafikiri mustakabari wa Zanzibar wanao wazenji wenyewe..waache waende. Nina uhakika hawata kwenda mbali sana kabla ya kusambaratika
 
Jamani wapeni nchi yao hee!, mnataka mpaka wawaambiaje ndio muelewe kuwa wanataka nchi yao?.
 
Jamani wapeni nchi yao hee!, mnataka mpaka wawaambiaje ndio muelewe kuwa wanataka nchi yao?.

Sio kupewa bali kurejeshewa nchi yao iliyoporwa na wadangayika
The delegation of Zanzibar seated in the United Nations General Assembly during meeting
Picture1.jpg


Prime Minister Muhammad Shamte of Zanzibar delivering a statement before the General Assembly on the occasion of Zanzibar's admission to the United Nations

Picture2.jpg


Secretary - General U Thant (left centre) congratulates Prime Minister Muhammad Shamte of Zanzibar on the admission of Zanzibar to the United Nation. Others in the photograph include (left) Chief of Protocol Pierre de Meeulemeester, and foreign Minister Ali Muhsin of Zanzibar

Picture3.jpg
 
Last edited:
Hapana,

Hatutaki tafrani hapa jirani..na pia hatutaki wakimbizi wakianza kuchinjana wenyewe kwa wenyewe!

Mapinduzi tu waliuana watu zaidi ya 15,000!

Visiwani ni sehemu ya Jamhuri Kikatiba!
 
Wadanganyika wataendelea kuosha vinywa kila siku kwamba wanaibeba Zanzibar.
Zanzibar ni mzigo kwa muungano.
Iweje kitu kinachokutia hasara uking'ang'anie.

Kama ni umeme Zanzibar ilianza kupokea umeme kutoka bara kwenye uongozi wa awamu ya pili [mzee Jumbe]

Je huo muda wa nyuma walikua hawana umeme?

Halafu wadanganyika kiburi chao ni umeme wakati wazanzibari wala hawakijali.

Kwani Zanzibar lazima inunue umeme kutoka bara tu?
Zanzibar walikuwa na umeme wa kumwaga tokea miaka ile ya 1800!
i61_DarajaniBridgeLightsc1910.jpg

Darajani miaka ile, daraja likiwa limepambwa na taa nzuri za umeme
 
Ndio hivyo biashala ya mafuta imeshapigwa na chini si ya Muungano tena ,sasa hivi wanajiandaa kuunda Shilika lao litakalojulikana kama ZPDC ile T ambayo wanasema sio Tanzania bali inawakilisha Tanganyika.
Na kalibu wataanza kuchimba mafuta ,na kuwawacha Tanganyika wakinyang'anyiana ulaji ,si tunafaamu kama madini ni dili kubwa na viongozi wote wa Tanganyika wanabiashala zao za ndani ila wakigongana kwenye dili inakuwa mtafaluku nchi nzima ,maji wanafunga ,umeme wanauzima kwa wakati watakao yaani wanadai eti mteremko wa mitokuelekea baharini umezidi hivyo mvua zikinyesha maji hayakai kwenye mito na mabwawa yanatiririrka baharini na kusababisha vina vya maji kupungua inabidi waongeze ununuaji wa majenereta yaani miaka 50 baada ya uhuru Nchi inategemea magenereta wakati kuna Uranium toka na kabla uhuru inachunguzwa ,hakuna la maana hata moja linalofanywa likaonekana ,zaidi ya wakati huu tulionao wezi kujidhihirisha bila ya aibu na CCM chama tawala kikitetea eti wasilumbane nje ya mikutano yao ya ndani watawababaisha na kuwajulisha wananchi nini kinaendelea , Wazenji sasa wamesituka na kuona viongozi wa Tanganyika hawana maana hata moja kwani ni wachumia matumbo tu na longolongo nyingi kumbe wanabiashala kibao zipo nyuma ya mapazia ,Mwakiembe aliewambia Wazanzibar hawana adabu kumbe akisema vile kulinda maslahi yake , akionyesha utawala wa king'ombe ng'ombe alieko mbele ndie anaetingisha kichwa kulia na kushoto. Akionyesha kuwa yeye ni kiongozi shupavu amejisahau kuwa nae ni ng'ombe kwa maana mambu anayoyasemea wenziwe nae anayo.
 
Kitu kimoja najiuliza kila siku kuwa hawa Serikali ya Muungano na Zanzibar huwa hawakai pamoja na kuelezana ukweli au vipi . Nzanzibar inapata 4.5% kutoka kwenye kodi ya mapato ya Muungano ambayo yanakusanywa Tanzania bar, wakati yale yanayokusanywa Tanzania Visiwani yanabaki huko Visiwani kwa 100%.

Mapato yanayotokana na Gas yote hukusanywa na TPDC na kupelekwa hazina, Mapato yanayotokana na kodi za madini hukusanywa na Wizara ya Nishati na Madini na kupelekwa Hazina.

TPDC pekee yake inakusanya mapato yasiyopungua 17 Billion Ths kwa mwaka , je 4.5% ya 17 Billion Tshs ni ngapi???? na Je , Wanzanzibar wanaopewa huo mgao ni % ngapi ya Wa Tanzania wote. Kwa hiyo hadi hapo inaonesha kuwa mapato ya Gas wanapata na Mapato ya madini wanapata by 4.5% hilo halina mjadala.

Labda kama kuna agenta ingine inayofanya Gas na mafuta viwe vyao lakini isiwe kwenye mapato ya Gas na Madini.

Mkuu nana kakwambia kuwa kodi inayotozwa Zanzibar inabaki Zanzibar? Kila kitu kinaenda Bara na baadae kurejeshewa hiyo 4%. Pahala kama uwanja wa ndege mapato yote yanakwenda Tanzania aviation na kuacha kiwanja hakina hata pahala pa kufanyia checking wasafiri. Ni aibu juwa na mvua ndio zao wasafiri. Pia kuna wakati maafisa wa TRA wakija Zanzibar kwa Boti asubuhi na kurudi na mapato boti ya kurudi saaa 10.jioni.
Mnapoelezwa kuwa upande mmoja wa Muungano hauna nia njema mnakaidi lakini mambo yanayofanyika huwezi kusadiki unapoambiwa.
 
Kitu kimoja najiuliza kila siku kuwa hawa Serikali ya Muungano na Zanzibar huwa hawakai pamoja na kuelezana ukweli au vipi . Nzanzibar inapata 4.5% kutoka kwenye kodi ya mapato ya Muungano ambayo yanakusanywa Tanzania bar, wakati yale yanayokusanywa Tanzania Visiwani yanabaki huko Visiwani kwa 100%.

Mapato yanayotokana na Gas yote hukusanywa na TPDC na kupelekwa hazina, Mapato yanayotokana na kodi za madini hukusanywa na Wizara ya Nishati na Madini na kupelekwa Hazina.

TPDC pekee yake inakusanya mapato yasiyopungua 17 Billion Ths kwa mwaka , je 4.5% ya 17 Billion Tshs ni ngapi???? na Je , Wanzanzibar wanaopewa huo mgao ni % ngapi ya Wa Tanzania wote. Kwa hiyo hadi hapo inaonesha kuwa mapato ya Gas wanapata na Mapato ya madini wanapata by 4.5% hilo halina mjadala.

Labda kama kuna agenta ingine inayofanya Gas na mafuta viwe vyao lakini isiwe kwenye mapato ya Gas na Madini.

Usichofahamu kuwa hiyo 4% inayopewa Zanzibar haitoki hazina bali ni marejesho ya kile kilichovunwa kwa jina la Muungano ikiwa pamoja na misaada ya kibajeti kutoka nchi wahisni.
Ingekuwa Zanzibar wanapewa 4% ya pato zima la hazina mbona pesa hizo zingekuwa nyingi kiasi cha kuifanya Zanzibar isiombe misaada na mikopo nje.
Kama hali ingekuwa kama hivyo matusi si yangezidi kwani hapo ingekuwa kweli Zanzibar inabebwana Bara lakini mapato ya Zanzibar yanagawiwa na baadae kupewa kasehemu kidogo kwa madai ya kuhudumia shughuli za muungano.
 
Hapana,

Hatutaki tafrani hapa jirani..na pia hatutaki wakimbizi wakianza kuchinjana wenyewe kwa wenyewe!

Mapinduzi tu waliuana watu zaidi ya 15,000!

Visiwani ni sehemu ya Jamhuri Kikatiba!

Kipi kigeni kwenu kuhusu uchinjaji na mauwaji? Mbona mifani mingi tu ipo humo mwenu na hata kwa jirani wenu kule Pemba. Vipi Tarime, Monduli na Balaa kwa ndugu zetu Maalbino. Hebu temea mate mbali!
 
Baada ya kujinyakulia Bendera sasa ni hazina ,step by step.
Baada ya purupushani za hapa na pale na kupandishiana jazba na kujibizani katika magazeti hatimae msaada wa kuanzishwa shirika la mafuta Zanzibar umepitishwa rasmi katika baraza la wawakilishi kwa nguvu zote za wawakilishi wa ccm na cuf na kutoa maagizo kwa serikali kuanzishwa kwa shirika hilo mara moja na kuwa suala la mafuta ni mali ya Zanzibar na shirika hilo litashughulikia shughuli zote za uchimbaji wa mafuta na nyaraka zote zilizopo TPDC zirudushwe mara moja katika himaya ya Zanzibar au itahesabika kama ni wizi na utapeli wa mchana.
Bado suala lipo kwa upande wa pili watanganyika watasema nini ? Ili suala hili kungoka katika mikono ya walowezi wa kitanganyika linahitaji hoja kali na kujikaza kwa wazanzibari kupambana na mbinu zozote zitakazoletwa na wajanja wa kitanganyika hongera wawakilishi wetu kamba ndio hiyo hiyo tumechoka na wezi hawa ambao wamekwiba kwao na kugawana na sasa wanavamia nchi jirani.
 
Ndugu yangu Mwiba, usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Baada ya kuwapa umeme bila kulipia kwa miaka yote, na fedha ya kuendesha serikali yenu, badala ya shukrani ndio unatuita 'wezi' kwa sababu ya mafuta ya 'alinacha?!.

Wazanzibari (baadhi) mna viburi, jeuri, na lugha za ****** linapokuwa ni jambo la maslahi ya Zanzibar, siye bara tumekuwa waungwana, wastaarabu na wavulivu sana wa chokochoko zote za kuubeza Muungano toka kwenu kama mke mdogo afanyae visa ili apewe talaka.

Kwa taarifa yako, Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano yenye uhuru wa kujitawala kwa mambo yake ya ndani. Zanzibar siyo dola haina nguvu za dola na kamwe haitazipata. Zanzibar haina Polisi, Jeshi wa UT.

Huo msimamo na jeuri ya Baraza la Wawakilishi utaishia Bunge la Muungano. Namuhurumia sana Nahodha, ndio keshapoteza chance yake kuwa rais Zanzibar. Sasa rais Zanzibar, ama Seif Khatib ama Mwinyi Jnr.

Wewe Mwiba utaendelea kulia kwa machungu ya moyo kama uliochomwa na mwiba kwa matarajio safari hii labda hamtapokwa kitumbua mdomoni. Mpewe muuvunje muungano!.

Leo Cuf na CCM mmeungana katika suala la mafuta, unganeni pia kwenye siasa kuumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili amani na ustawi wa kiuchumi uchanue mtutuwe mzigo siye wabara.

Mimi ni miongoni mwa wabara tunaokubali Zanzibar ipewe kila inachotaka ili tuache kuibeba. Amini usiamini, hiyo amani mnayojivunia, iko mikononi mwa bara, mngeachwa ingekuwa ni kuchinjana kwa majambia kwa kwenda mbele.

Mafuta kwetu bara siyo hoja, hoja ni kibri, jeuri na majigambo ambayo mwisho wake ni ndani ya Bunge. Hivi Baraza la Wawakilishi ni nini mbele ya Bunge?. Ni kama baraza la madiwani wa halmashauri ya mkoa wa visiwani, mamlaka yake ni by law tuu, siyo sheria huku bara.

Leo anza kicheko, wakati wa kilio, nitakukumbusha tena. Kutuita wezi ni kosa, kuomba msamaa ni ustaarabu ambao kwa kibri, jeuri, jazba na majigambo yenu hauwezi kukubali, na tusubiri atakaye cheka mwisho.
 
Pasco ! nafikiri na wewe umepandwa na jazba ,kumbuka kwa nini baadhi ya viongozi wa nchi hii wamepewa majina kama mafisadi ?Mafisadi maana yake nini? ukishapata jawabu lake hapo rudi na ujiulize maana ya mtu mwizi nini?hao viongozi wanoitwa mafisadi wamemuibia nani?wananchi wamefurahiswa na ufisadi huo(wizi) uliofanywa na viongozi ambao wananchi wamewachagua?ni miongoni mwa viongozi wanaotuongoza ndio mafisadi (wezi )wa mali ya uma na jamii kwa ujumla lakini hilo wewe hulioni na wala halikuumi inawezekana unatokana na familia ya hao wanaomiliki uchumi wa nchi kwa maslahi yao .mwiba aliposema wezi watanganyika kwa mtu mwenye akili yake timamu anaelewa anamainisha ni akina nani hakuna wengine isipokuwa hao waliokua wanafisidi uchumi wa nchi bila kuwa na huruma ya wananchi waliowachagua kwa imani nzuri na kama utasoma kuna sehemu mwiba ameandika kuwa Mafisadi wamefidi Tanganyika na sasa wanakuja nchi ya pili hapa alikuwa anzungumzia hao wenyewe uwezo wakufisidi na kuchota mali za uma na sio watu wakawaida unajaribu ku twisti isssue
 
Binafsi nimeshajiuliza sana swala la Zanzibar. Ni kweli hawa ni ndugu zetu, pia ni kweli muungano wetu kama ulivyounganishwa na Nyerere na Karume unautata, vile vile ni kweli kuungana ni kitu kizuri katika kukuza uchumi na mahusiano baina ya zilizokuwa nchi mbili. Hatahivyo kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajibiki na hao wanaosuruhisha maswala ya muungano.

Haikuniingia akilini nilivyosikia Zanzibar ilikuwa inatumia umeme toka Bara bila kulipa mpaka ilipoingia Net Group Solution ambapo waliambiwa walipe or else wanakatiwa umeme. hapo ndipo nilipochoka maana walipiga mkwala kuwa wakikatiwa umeme wanavunja muungano, ukweli ni kwamba serikari ya bara ililipa lile deni la Zanzibar na mambo yakawa shwari. Hata hivyo bado hawa jamaa wanalazimisha tuvunje muungano lakini CCM haitaki na imekula yamini kuulinda kwa nguvu zote.

Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Hataukimpa offer nyingi nyingi kama hana mapenzi na wewe itakuwa ngumu kuwa rafiki yako. Kinachoendelea Zanjibar na Bongo sasa hivi ni kama baba na mtoto. Zanzibar kila itakachotaka Bara itabidi tukikubari ili mulinda muungano. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????
 
Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????

Muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za Katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la Uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.
 
Muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za Katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la Uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.

Hili ni zuri hapa naimani viongozi na wanachi wa kule ZANZIBAR litwafika kama ulivyoliongelea .sasa hapa unataka kutwambia kuwa wakatoliki ameowana na waisilamu na ndowa yao ina base mamuzi ya kikatoliki?pia tueleze who`s dady and who`s mumy?ndani ya ndowa hii ?ninavyoelewa mie ndowa yoyote ile ikiwa ya kisilamu au kikristo kunakuwa na shahada ya ndowa, lakini ndowa hii shahada zake zimeliwawa na mchwa.sasa itakuwaje wakati wa kurisiana pale mmoja akiondoka duniani , huoni kuna uwezekano mmoja kati yenu akapoteza urisi wake ?
 
Back
Top Bottom