Ndugu yangu Mwiba, usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Baada ya kuwapa umeme bila kulipia kwa miaka yote, na fedha ya kuendesha serikali yenu, badala ya shukrani ndio unatuita 'wezi' kwa sababu ya mafuta ya 'alinacha?!.
Wazanzibari (baadhi) mna viburi, jeuri, na lugha za ****** linapokuwa ni jambo la maslahi ya Zanzibar, siye bara tumekuwa waungwana, wastaarabu na wavulivu sana wa chokochoko zote za kuubeza Muungano toka kwenu kama mke mdogo afanyae visa ili apewe talaka.
Kwa taarifa yako, Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano yenye uhuru wa kujitawala kwa mambo yake ya ndani. Zanzibar siyo dola haina nguvu za dola na kamwe haitazipata. Zanzibar haina Polisi, Jeshi wa UT.
Huo msimamo na jeuri ya Baraza la Wawakilishi utaishia Bunge la Muungano. Namuhurumia sana Nahodha, ndio keshapoteza chance yake kuwa rais Zanzibar. Sasa rais Zanzibar, ama Seif Khatib ama Mwinyi Jnr.
Wewe Mwiba utaendelea kulia kwa machungu ya moyo kama uliochomwa na mwiba kwa matarajio safari hii labda hamtapokwa kitumbua mdomoni. Mpewe muuvunje muungano!.
Leo Cuf na CCM mmeungana katika suala la mafuta, unganeni pia kwenye siasa kuumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili amani na ustawi wa kiuchumi uchanue mtutuwe mzigo siye wabara.
Mimi ni miongoni mwa wabara tunaokubali Zanzibar ipewe kila inachotaka ili tuache kuibeba. Amini usiamini, hiyo amani mnayojivunia, iko mikononi mwa bara, mngeachwa ingekuwa ni kuchinjana kwa majambia kwa kwenda mbele.
Mafuta kwetu bara siyo hoja, hoja ni kibri, jeuri na majigambo ambayo mwisho wake ni ndani ya Bunge. Hivi Baraza la Wawakilishi ni nini mbele ya Bunge?. Ni kama baraza la madiwani wa halmashauri ya mkoa wa visiwani, mamlaka yake ni by law tuu, siyo sheria huku bara.
Leo anza kicheko, wakati wa kilio, nitakukumbusha tena. Kutuita wezi ni kosa, kuomba msamaa ni ustaarabu ambao kwa kibri, jeuri, jazba na majigambo yenu hauwezi kukubali, na tusubiri atakaye cheka mwisho.