Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Kuna watu wanasema kuna kero za muungano, mimi nafikiri kuna kero ya Zanzibar!!! Kwanini tusiachane nao wajue hamsini zao?? Tunachotafuta ni nini hasa? Tutaendelea kuwabembeleza mpaka lini?

Hiki kizazi cha wazee wanaong'ang'ania muungano kitapita muda sio mrefu, then tutasahau yote haya!
 
Pasco, nimekusoma vizuri. Kwamaneno mengine as long as CCM iko madarakani no way CUF itashinda. Suruhisho, Piga chini CCM ruhusu ushindi kwa CUF, funua muungano weka mezani tafuta suruhisho la kudumu.
Kukaa upya mezani na kuujadili muungano ndiyo suluhisho la kudumu litakalo toa haki sawa na kumaliza shida zote. Kwa sasa kuna nyufa ukutani, serikali ya CCM imeamua kutia viraka, dawa ya ufa sio kiraka bali kubomoa na kuziba ufa. Kuiondoa CCM haiwezekani, ni kusubiri tuu mpaka ukuta ubomoke ndipo ujenzi mpya uanze.

Tiba ya Muungano ni kidonge kigumu sana kumeza kwa serikali ya CCM na CUF wanaonyesha kila dalili ya kutoimeza dose ya CCC kwa tiba ya muungano na ndio maana kila siku wanapokwa ushindi na mwakani ni vivyo hivyo, labda 2015, zamu ya Hamad Rashid au Juma Duni, lakini Mzee wa Sharubu anafafana sana wajihi na Sultan Jamsid hadi kuna mashaka ya nasaba.

Kwa 2010, tutake tusitake, ni yale yale.
 
Kukaa upya mezani na kuujadili muungano ndiyo suluhisho la kudumu litakalo toa haki sawa na kumaliza shida zote. Kwa sasa kuna nyufa ukutani, serikali ya CCM imeamua kutia viraka, dawa ya ufa sio kiraka bali kubomoa na kuziba ufa. Kuiondoa CCM haiwezekani, ni kusubiri tuu mpaka ukuta ubomoke ndipo ujenzi mpya uanze.

Tiba ya Muungano ni kidonge kigumu sana kumeza kwa serikali ya CCM na CUF wanaonyesha kila dalili ya kutoimeza dose ya CCC kwa tiba ya muungano na ndio maana kila siku wanapokwa ushindi na mwakani ni vivyo hivyo, labda 2015, zamu ya Hamad Rashid au Juma Duni, lakini Mzee wa Sharubu anafafana sana wajihi na Sultan Jamsid hadi kuna mashaka ya nasaba.

Kwa 2010, tutake tusitake, ni yale yale.
Wacha kasumba hiyo eti kuiondoa CCM haiwezekani nani kasema KANU itaondolewa nani alijua kuwa Kaunda ataondolewa nani alifikiria kuwa Soviet unio itaparaganyika na mifani mingi tu ,hivyo kusema CCM haitaondoka naona unakuwa mganga wa kienyeji sasa, mfano mdogo tu CCM imeangushwa Pemba tena imeangushwa kifudifudi ,sio CUF walioiangusha CCM bali ni wananchi ndio walioiangusha CCM ,hivyo basi wananchi hawahawa wa sehemu nyengine wanaweza kabisa kuiangusha CCM kama wenzao wa Pemba ,kule Pemba CCM ipo kwenye magwanda ya kuvaa tu ,utawaona watu siku ya sherehe wamekutilia magwanda ya kijani na manjano utafikiri ni wapenzi wa Yanga kumbe wana lao rohoni.

Hapo umesema sio mswaada ,sasa chochote kitakachokuwa ndio kimeshaamuliwa na WaZanzibari wanasema ndio ishatoka hiyo.
 
Nguvu za watu au nchi kadhaa huunganishwa pamoja ili kulinda maslahi ya pamoja. wenye nguvu Duniani bado wanampango wa kuunganisha nguvu zao kwa sababu ndoto zao za kuongeza maslahi kwa pamoja ni kubwa kuliko wakati wowote katika historia za nchi zao.

Sasa kama hakuna maslahi ya pamoja, tunaungana ili kufaidika na nini?

Wakati huo huo inawezekana kuna faida tele ndani ya muungano. Lakini je?
Iweje kwamba ni Nongwa ya kutishiwa kifo kuweka jaribio lolote la kujadili Muungano kwa uwazi bila uficho?

Mzeee Aboud Jumbe alinyamazishwa na kono zito la kijamhuri hadi leo na kupakaziwa kwa nguvu zote na Marehemu Mwalimu Nyerere kwamba amejenga hoja au mazingira ya kuchafua hali ya hewa ya kisiasa huko Zanzibar.

Alichotaka kujua MZee Jumbe kwa undani na uwazi ndicho kilicholindwa kwa gharama ya damu na Mzee Karume.

Muungano ni kwa Faida ya wanao Ungana Tanganyika na Zanzibar siyo kikundi cha Wahuni wachache walo jaa mvi za ufedhuri ndani ya CCM na serikali yake!
 
Ayo mafuta ya kujipaka yako pemba au unguja au bara? Mtu ambaye anajua eneo please
 
Wadau naona the way tunavyochangia tunakwenda Nje ya mstari...as if yanayotokea DUNIANI kote hatuyajui au hatuyafuatiliii.....

Bahati Mbaya mtu kama Mwiba unaonekana ni Mtetezi wa CUF, lkn kwa upande mwingine unaharibu image ya CUF kwa Jamii. i do believe members humu JF watamchukilia Mwiba kama mtu binafsi na si MSIMAMO WA CUF.

Unaleta Hoja makini lete hoja, usilete Hoja za Ubaguzi ohh wabara hivi...au Wazenj hivi....?Tunakwenda Wapi? Nini kitatokea leo ikiwa ZNZ ikiwa ALONE, then wapemba na Waunguja nao wagawane Kisiwa...?..wabara nao kila mtu na Mkoa wake...!!!!

Hivi Jamani hatuoni kwanini USA imekuwa powerful country?...Kwanini leo nchi za Ulaya zimekuja na kutengeneza EURO?....waarabu wana GULF nayo ni just nchi 7 tu...

I do believe Muungano una positive na Negative...Muhimu kuangalia mapungufu yaliyopo na kuangalia namna ya kusawazisha Tofauti Iliyopo. Viongozi wa Muungano nao wanataka kuongoza Kibabe ktk wakati watu wanasaka maendeleo....Tukae chini tujadili Muungano uweje...Tunaohubiri Ubara au Uzenji haumsaidii yoyote bali sote tunaonekana majuha.....!!!!

I do believe JK is the right person kuondoa matatizo ya Muungano, Mkutano wa Butiama kuna Genge la watu wamemsaliti.......kama si kusalitiwa kule...Leo hii tungekuwa tumefungua page Mpya kabisa ktk huu Muungano.....Tuna matatizo ya Husda.....kama JK angefanikiwa BUTIAMA...credits zingeenda kwake......hata Miradi Mingi ukiichunguza inafeli si tu kuwa Watendaji hakupewa chochote...lkn wanajua credits za kufanikisha huyo Mtendaji atakuwa Hayumo au Hatajwi............I do hope in the 2nd term atalimaliza hili.......Inshallah.
 
Kuna watu wanasema kuna kero za muungano, mimi nafikiri kuna kero ya Zanzibar!!! Kwanini tusiachane nao wajue hamsini zao?? Tunachotafuta ni nini hasa? Tutaendelea kuwabembeleza mpaka lini?

Hiki kizazi cha wazee wanaong'ang'ania muungano kitapita muda sio mrefu, then tutasahau yote haya!
Wewe kama kungekuwa na uwezo zaidi ningekwambia mfufue Mwalimu Nyerere (Kumradhi hapa) halafu akueleze kwanini Tanganyika iin'gan'ganie Zanzibar. Mpaka kati ya Zanzibar na Tanganyika kama unakuwepo? Tanganyika haina amani , haina uchumi, haina ustawi wa jamii. Ni Tanganyika ambayo inahiitaji Zanzibar zaidi. Uliza hilo!!
 
Uimara wa USA hautokani na Muungano wala Ukubwa wake kijiografia tu, bali unatokana na siasa za uwazi uvumilivu na uwezo wake wa kujadili mambo mengi kwa falsafa ya juu na nia yake ya kuwapa walio wengi uwezo wa kuamua mambo.

Ingekuwa ni kuungana na ukubwa wa nchi kijiografia, basi hata Urusi leo hii nayo ingekuwa na uchumi uliosawa na uchumi wa Marekani na huenda baadhi yetu tungekuwa tumezamia huko kubeba Box au aina nyingine ya konteina la kuhifadhia mizigo
 
Ayo mafuta ya kujipaka yako pemba au unguja au bara? Mtu ambaye anajua eneo please
Bara hamhusiki. Yapo kila pembe ya Unguja na Pemba Tena yapo katika eneo la Bahari Kuu ( ambalo ni Economic exlusive zone ya Zanzibar siyo Tanganyika) Upo hapo.
 
Ndugu yangu Mwiba, usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Baada ya kuwapa umeme bila kulipia kwa miaka yote, na fedha ya kuendesha serikali yenu, badala ya shukrani ndio unatuita 'wezi' kwa sababu ya mafuta ya 'alinacha?!.

Wazanzibari (baadhi) mna viburi, jeuri, na lugha za ****** linapokuwa ni jambo la maslahi ya Zanzibar, siye bara tumekuwa waungwana, wastaarabu na wavulivu sana wa chokochoko zote za kuubeza Muungano toka kwenu kama mke mdogo afanyae visa ili apewe talaka.

Kwa taarifa yako, Zanzibar siyo nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano yenye uhuru wa kujitawala kwa mambo yake ya ndani. Zanzibar siyo dola haina nguvu za dola na kamwe haitazipata. Zanzibar haina Polisi, Jeshi wa UT.

Huo msimamo na jeuri ya Baraza la Wawakilishi utaishia Bunge la Muungano. Namuhurumia sana Nahodha, ndio keshapoteza chance yake kuwa rais Zanzibar. Sasa rais Zanzibar, ama Seif Khatib ama Mwinyi Jnr.

Wewe Mwiba utaendelea kulia kwa machungu ya moyo kama uliochomwa na mwiba kwa matarajio safari hii labda hamtapokwa kitumbua mdomoni. Mpewe muuvunje muungano!.

Leo Cuf na CCM mmeungana katika suala la mafuta, unganeni pia kwenye siasa kuumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili amani na ustawi wa kiuchumi uchanue mtutuwe mzigo siye wabara.

Mimi ni miongoni mwa wabara tunaokubali Zanzibar ipewe kila inachotaka ili tuache kuibeba. Amini usiamini, hiyo amani mnayojivunia, iko mikononi mwa bara, mngeachwa ingekuwa ni kuchinjana kwa majambia kwa kwenda mbele.

Mafuta kwetu bara siyo hoja, hoja ni kibri, jeuri na majigambo ambayo mwisho wake ni ndani ya Bunge. Hivi Baraza la Wawakilishi ni nini mbele ya Bunge?. Ni kama baraza la madiwani wa halmashauri ya mkoa wa visiwani, mamlaka yake ni by law tuu, siyo sheria huku bara.

Leo anza kicheko, wakati wa kilio, nitakukumbusha tena. Kutuita wezi ni kosa, kuomba msamaa ni ustaarabu ambao kwa kibri, jeuri, jazba na majigambo yenu hauwezi kukubali, na tusubiri atakaye cheka mwisho.

WACHA JAZBA WEWE!!! Ivyo kuambiwa kitu cha kweli kwako inakuwa nongwa?
Mafuta yatakayotoka Zanzibar yaw ya nani? Hivyo wewe kidume mwenye wake wawili unataka ufanye udume wako kwa mali ya mke? Mali ya kwenu uliorithi unaleweya pombe na unachokijua ni kujisifu tu kuwa una mke wala huna huduma yoyote kwake na sasa amepata mali unakuja na shuka yako na fito yako kutunisha udume?
Huo uungwana na ustaarabu ndio uliokufanya kutowa matishio na majilabu? POLE WEEE!!!
 
Binafsi nimeshajiuliza sana swala la Zanzibar. Ni kweli hawa ni ndugu zetu, pia ni kweli muungano wetu kama ulivyounganishwa na Nyerere na Karume unautata, vile vile ni kweli kuungana ni kitu kizuri katika kukuza uchumi na mahusiano baina ya zilizokuwa nchi mbili. Hatahivyo kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajibiki na hao wanaosuruhisha maswala ya muungano.

Haikuniingia akilini nilivyosikia Zanzibar ilikuwa inatumia umeme toka Bara bila kulipa mpaka ilipoingia Net Group Solution ambapo waliambiwa walipe or else wanakatiwa umeme. hapo ndipo nilipochoka maana walipiga mkwala kuwa wakikatiwa umeme wanavunja muungano, ukweli ni kwamba serikari ya bara ililipa lile deni la Zanzibar na mambo yakawa shwari. Hata hivyo bado hawa jamaa wanalazimisha tuvunje muungano lakini CCM haitaki na imekula yamini kuulinda kwa nguvu zote.

Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Hataukimpa offer nyingi nyingi kama hana mapenzi na wewe itakuwa ngumu kuwa rafiki yako. Kinachoendelea Zanjibar na Bongo sasa hivi ni kama baba na mtoto. Zanzibar kila itakachotaka Bara itabidi tukikubari ili mulinda muungano. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????

Sio kweli kuwa Zanzibar wanalazimisha mambo bali Upande wa pili unalengo la kuuuwa zanzibar kiinchi. Muungano ni wa sehemu mbili na sehemu moja iliyokubwa inaendelea kwa hatuwa za haraka na kisehemu kilichobakia ambacho ni kidogo kinazidi kudidimia.
Nakupa challenge, iwapo wewe ni Rais wa Tanzania jambo hili halitokuingia akilini na kujiuliza kulikoni? Barabara za mkoa mmoja tu wa Bara zinatosha kujenga barabara zote za unguja naPemba.Hebu jiulize katika ukweli halisi Rais gani wa Tanzania ,hata Mwinyi, aliyechukua hatuwa kuliangalia hilo. Si mnataka tuelewe kuwa Serikali ya Muungano ni dhamana wa Zanzibar kwa vile si nchi bali sehemu ya Tanzania? Sasa jukumu la kuuimarisha Zanzibar litakuwa la nani? Iwapo serikali ya zanzibar ndiyo yenye jukumu jee mmeipa nyenzo na uhuru wa kutafuta njia za kujiendeleza?
Ni jambo la kusikitisha kuwa watendaji wengi wa Tanganyika wana roho kama za PASCO hapa, roho za changu changu chao chetu.
Hivyo mlikuwa hamjui kuwa mna wabia wenzenu wakati mlipoamua kutumia kipato cha rasilimali zinazotoka upande wenu bila ya kukasimu kwao? Madini na gesi zote mkazifanya zenu peke yenu na hata baada ya kuliburuza hili suala la mafuta na gesi kuwa la muungano mliendelea kujivunia peke yenu.
Hebu jaribuni kuvaa nyie viatu mlivyotuvalisha mgejiuliza maswali mangapi?
Sisi tunajiuliza maswali mengi pengine maswala kama haya yafuatayo mngetujibu;
- Je mnatuona tuna shida sana ya kulindwa na nyie?
- Je mnatuona vipofu?
- Je mnatuona hatuna elimu na hivyo ni mbumbumbu?
- Je wenzetu mna choyo na maendeleo yetu?
- Je mnaringia maguvu yenu?
- Je wenzetu hamtaki Udugu bali ukoloni?
Hayo ni baadhi tu ya maswali tunayojiuliza tukiwa ndani ya hivi viatu mlivyotuvisha. La kuelewa ni kuwa binaadamu ana tabia ya kuchoka na anapochoka hafanyi kwa ubishi au kwa jeuri bali nguvu zake za kustahamili jambo zinafika mwisho hivyo huubwaga tu na kubwaga kwa mtu aliechoka ni kwa kishindo.
 
muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.

pinda alipotowa solution kwa mauwaji ya ndugu zetu mlipiga kelele!!!!!!!!
 
muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.

pinda alipotowa solution kwa mauwaji ya ndugu zetu mlipiga kelele!!!!!!!!

K
 
Nimefurahi kusikia CCM na CUF wamekubaliana kwa asilimia 100% kwenye hili. Nasubiri kuona kama na mpasuko watauziba kwa asilimia 100% nani ya baraza hilohilo la wawakilishi. Vinginevyo ndiyo ile hadithi ya kujenga jumba la kifalme hewani.
Chonde chonde tuazime busara sasa..huu muungano una umuhimu mkubwa sana kwa zanzibar kuliko wanavyojidanganya


Kwa Wazanzibari tatizo sio kuitwa Watanzania, hilo hawalikatai bali wanachotaka NI HAKI ZAO.
 
Muda mwingine watu wanakubaliana kutokukubaliana. Hebu jiulize kama Zanzibar or Tanganyika si nchi bali Tanzania, na kama huu muungano ni halali kwanini suala la mafuta yaliyoko zanzibar iwe ni mali ya zanzibar peke yake???? Binafsi hainiingii akilini hapa kuna kauhuni fulani kanaendelea hakajawekwa wazi. Mbona resource zote zinazopatikana Tanganyika huchukuliwa kama mali ya Tanzania (Tanganyika & Zanzibar)na watanganyika wala viongozi wake hawalalamiki???????????

UPO LAKINI HUSIKI WALA HUONI. Zanzibar wamejenga hoja ya kuthibitisha kuwa rasilimali za Bara haziifaidii zanzibar.Pia serikali yako imekwishasema wazi kuwa madini si suala la Muungano ni mali ya Tanganyika ,sasa kama akili yake haina uwezo wa kutia akilini hayo basi itakuwa tatizo.
 
Hivi, hawa Wazenj wakija kuta kwamba chimbuko la hayo mafuta (ambayo kwa sasa ni mafuta hewa) ni Tanga, watachimba shimo hadi Tanga? Kwa nini tunaanza kuhesabu vifaranga il hali hata yai halijakomaa?

Tatizo TPDC hawakuanzia hiyo shughuli huko Tanga kwani wangeanzia huko wasingesimamishwa kama ilivyofanyika.
 
Back
Top Bottom