Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Sasa wanasema tunauza mbuzi!
Mbuzi yupo ktk gunia!!!
Fungua basi gunia mbuzi tumwone???
Je kuna mafuta kweli????
Yaani mnasahau hata lugha ya Taifa na misemo yake ,nikiwakumbusha labbda mtafunguka masikio , ...Panapofuka moshi panaficha moto. Sasa hizi kelele unazosikia au mnazozisikia hazikuzuka tu kama uyoga , mafuta yapo ya uhakika sio mchezo na hayakugunduliwa jana wala juzi ,tokea wakati wa Mfalme ,na nyaraka za wakati huo zipo ,ila kutokana na utajiri wa Zanzibar enzi hizo mfalme aliposhauriwa kuyachimba alisema haina haja anawawachia generation zijazo ni hazina yao ,Mfalme ,kwa kiswahili sanifu tunasema alikuwa hana shida ya kuchimba mafuta ,serikali yake ilikuwa na feza kedekede iliyotokana na ushuru waliokuwa wakilipa WaTanganyika waliokuwa wakileta wenzao kuwauza (Ni wakati wa utumwa) na wengine wakileta mazao kuuza yaani Zanzibar ilikuwa ni Hub ya kibiashara kwa east & central east ya Afrika Hebu kasomeni kitabu kijulikanacho kama Modern Tanganyika kinapatikana kwenye mtandao humo mtafaidika sana na haya Mambo ya Zanzibar na hata kuwajua ni akina nani wakipelekana kuuzana Zanzibar ,naona mkisoma si lazima kitabu chote lakini fukua tu na hutakosa kufaidika na kuja hapa na heshima na adabu kama alivyosema Mwakiembe iwepo heshima.Maana mnavyosema mtafikiri Tanganyika ilikuwepo mwanzo kabla ya Zanzibar kumbe ni kajinchi cha juzijuzi tu ,hilo nalo mnatakiwa mlielewe tena mlielewe sana ili mjue nyinyi wenyewe ni akina nani.
Kile kiwanda cha kusafishia mafuta ghafi kilijengwa kwa kutegemeakusafisha mafuta ya Zanzibar ,sijui kama hilo mliwahi kuambiwa na Baba yenu Nyerere lakini WaZanzibari wakamwambia baba kwa hilo tutasameheana mwanangu ,tutasafisha mafuta yetu pale ambapo tutapata kwa bei poa , Oman inachimba mafuta lakini nimeambiwa kuwa mafuta yanayotumika ndani ya nchi hiyo yananunuliwa kutoka nchi nyengine yao wao huwa ni grade nzuri na wanayauza kwa bei ya juu ,sijui kama ni ukweli au jamaa alikuwa kashiba tende kutoka huko kwao ,alinikuta pale Tabora nikiwa natengeneza baiskeli mbovu na zingine nakodisha.