Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Wazanzibar kama wanataka hayo mafuta yawanufaishe wao Wazanzibar peke yao na si Watanzania wote tuwaachie tu hayo mafuta, kwanza wafahamu dunia sasa hivi inayakimbia mafuta ya kuchimbwa polepole na badala yake inawekeza katika green energy, baada ya muda si mrefu mafuta yatazalishwa kwa nafaka n.k, Kule Tanganyika kuna ardhi kubwa na ya kutosha ya kulima hizo nafaka, je ikifika hatua hiyo Wazanzibari mtataka vyote vilivyo bara na viswani?. Chao Chetu , Chetu Chetu!
hii inanikumbusha lile shairi kwenye DIWANI YA MLOKA
"Kuku akipata nyama hukimbia ale peke"
"Japo watamuandama wenzie waishike"
"Kuitupa hakubali mdomoni idondoke"
"Palipo na ubinafsi hapakosi kuwa choyo"
"na upeke wa nafusi na chuki katika moyo"
"Haukosekani wivu maringo pia tamaa"
"Kadhalika na ubovu wa moyo usiofaa"
Mtaimba sana tu maana ngonjera za wafuasi wa Sultani CCM ndio utamaduni wao ila kwa mafuta mtamaliza kwaya zote hapatolewi kitu.
Halafu fikiria kinachopatikana kwenye mafuta ya nafaka na kinachopatikana kwenye mafuta ya ardhini naona unafananisha mpapai na mnazi 😀