Pakacha unamfahamu vizuri Mwalimu wakati huo unaouzungumzia(1984), baada kuona Wazanzibar wanahoji muundo wa Muungano, na mambo kama hayo ya mafuta kuingizwa kinyemela, alitengeneza "confusion" aliyoiita "mchafuko wa hali ya kisisa zanzibar" na kama utakumbuka sawa sawa ni katika miaka hiyo akina Jumbe na wenzake walifukuzwa kama "paka mwizi" na kufuatiwa na akina Seif na jopo lake, hayo aliyafanya Mwalimu kuzima "longolongo" ya wazanzibar katika mambo mbali mbali yaliyokuwa yakiendeshwa kitirigivyogo katika muungano likiwemo hilo la mafuta, na tokea hapo hakuna mtu aliyethubutu kuhoji kwa kuhofia yasijemkuta ya akina Jumbe na Ramadhn Haji na Seif. Si kuwa Mwalimu hakusikiliza malalamiko bali aliyazima kabisa kwa gharama ambayo mpaka Jumbe kwa uchungu akatunga kitabu kuyasema maovu na dhulma ile ili vizazi vitakavyokuja Zanzibar vijuwe pumba na mchele, muda wote Jumbe akisimulia dhulma ile ya Nyerere viongozi wa SMZ wameona porojo tu, leo ukweli umedhihiri baada ya Mizengo pinda kuwatanabahisha na kump"rove" Jumbe. Pakacha, kama Mwalimu alisikiliza kilio cha Wazanzibar tokea siku hizo bila ya kufanya hila na khiyana zote hizo, suala hili na mambo mengine yanayoitwa kero za muungano yangekuwapo?