Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hebu niambie kina Ali Ameir, Mohammed seif khatib na wengine mnawangojea wafe madarakani kwa vile hamna wengine wa kuchukua nafasi zao?
Nakushauri jamaa yangu muache kupanga nani ni mzanzibari zaidi ya mwengine ili mfanikiwe katika harakati za kudai haki zenu.
Wengine wapo , tena kibao kupitia katika majimbo yao ya Uchaguzi. Lakini tatizo ni system (au utamaduni) siyo mzuri unaotumika. Wapiga kura huwa wanazongwa na kuambiwa kuwa msimamo ni mtu fulani apite. Sasa wanafanya hivyo. New Generation itapenya wapi hapo. Ninao marafiki zangu mimi (hao new generation) wenyeji wa majimbo ya Uzini na Donge -lakini hawathubutu kujitokeza huko kuomba kura kwa wazee wao na vijana wenzao- Hawana pa kupenya mpaka , labda kama unavyosema wakati wa vigogo ufike na Mola awachukue. Nani ni Mzanzibari zaidi ya mwengine ni suala pana hilo. Kuna makosa kwa pande zote. Kwani na CUF nao hawawakubali Wazanzibari wenye asili ya Bara (Tanganyika) kama ni wazanzibari safi -hili huoni kuwa ni jambo la kushangaza?
 
Ni vizuri kuwa tunayakubali makosa na kutafuta sababu zake. Ni kweli kuwa CUF wanawaona Wazanzibari wenye asili ya Bara kuwa si Wazanzibari halisi lakini kwa hili tutakuwa tunageneralize suala tukisema hivyo. Kwanini? Kwasababu si kila mwenye asili ya Bara anachukuliwa kuwa si Mzanzibari halisi. Niliwahi kusema huko nyuma kuwa Uzanzibari si kuzaliwa Unguja au Pemba pekee lakini pia unashirikisha hata wale waliohamia lakini wakakukubali kuiona Zanzibar ni nchi yao na kuionea uchungu. Unapokosa sifa ya kuionea uchungu Zanzibar na ikitokea kuwa wewe si mzaliwa wa Visiwa hivi wenye visiwa watakataa kukuona kuwa u miongoni mwao. Historia ya Zanzibar inaonyesha kuwa wengi wa wakaazi wake wana msingi kutoka Bara au nchi za Kiarabu na wengine ambao ushahidi umeshapotea wanatoka Persia. Sasa utawezaje kuwakataa karibu asilimia 70 ya Wazanzibari kuwa si wazanzibari halisi? Isipokuwa huu mtindo wa sasa uliopo wa kumfanya mtu aliekuja kwa kibaruwa cha kondeni kuwa ana haki ya kushiriki katika masuala ya uchaguzi na kumuacha alietoka kisiwa cha pili asipige kura ndiyo inayoleta hii fitina ya kuanza kubaguwana. Inasikitisha kuona mtu hata lugha ya Kiswahili hajui vizuri anapokelewa moja kwa moja kuorodheshwa kuwa ni Mzanzibari kwa dhana ya kuwa huyu hatoipigia kura CUF na kunbeza yule anaezungumza moja ya lahaja za Zanzibar kwa hisia kuwa wote wanaozungumza lahaja hiyo wanaisapoti CUF.Ndugu yangu unafikiri hata ungekuwa wewe kati ya hao wanaotumia lahaja hiyo ungemuonaje yule anaependelewa na kupewa haki iliyokuwa yako?
Kwa mtaji huu ipo siku Wazanzibari mtakuja kujuta, hapo mtakapoambiwa mpige kura ya maoni na washiriki ni Wazanzibari wenye vitambulisho, kazi kwenu walio na uchungu na visiwa mshawanyima nafasi. Mjisahihishe ili mpiganie haki katika Muungano.
 
Si mweledi sana kuhusu sheria za uchaguzi. Lakini nafikiri kamwe hazimnyimi Mzaliwa wa Zanzibar kupiga kura na zikampa tu Mkazi Mhamiaji. Kama yupo kisiwa cha kwanza na anatoka kisiwa cha pili- na hajatimiza muda unaohitajika kukaa pale kisiwa cha kwanza hanyimwi kupiga kura bali huambiwa akapigie kura katika sehemu ya kisiwa cha pili anakotoka- Jee huko pia akirudi hukataliwa? na jee huko kurudi kupiga kura kunamgharimu kiasi gani au kuna usumbufu wa kiasi gani? Hata halazimiki kupanda ndege. Usizungumzie mambo juu juu tu na kulaumu Ndugu yangu -hayo ya kurusha lawama zisizo na msingi ni msimamo wa mrengu nule wa watani.
 
Pakacha, uhali gani gani? Kwa hadidu rejea hizo hizo unazotaka wewe hebu fikiria kwa Zanzibar ukiondowa huu umri wetu nani hakufanya makosa katika hali hii tuliyomo sasa ya Muungano? Karume Mkubwa ndiye alieiuza nchi kwa kuhofia kuondoshwa madarakani. Watu kama Seif Bakari waliwauwa wenzao kwa kupinga muungano huu na baadae wao wenyewe walipotanabahi na kuidai haki wakafungwa. Aboud Jumbe aliiuwa ASP na kuipeleka Zanzibar Tanganyika na alipotanabahi akataka kujitowa kwenye muungano nae akaangamizwa.Wazanzibari wenyewe walishangiria kuuliwa ASP baada ya kuona inawabana Kidemokrasia na wakiwaonea choyo Watanganyika, sasa kweli imedhihirii wanaitaka ASP irejee, Seif Sharifu na kundi lake walimsaliti Aboud Jumbe nao walipotanabahi wakapigwa na chini. Marehemu Dr Ali Juma aliwasaliti Wazanzibari kwa nafasi ya Umakamo wa Rais na mungu amempenda hakuwahi kuvuna usaliti wake. Salmini aliwatia uhaini wenzake kwa kudai hadhi na haki ya Zanzibar nae aliishia kivyake. Na hata Karume Mdogo (Amani) alipopewa madaraka akaipeleka Zanzibar Tanganyika na sasa anarudi kiguu nyuma.
SASA nieleze kati ya Wazanzibari ukiondowa Generation hii mpya nani hana mkono wake katika kuifisadi Zanzibar kwa kisingizio cha Muungano na nani mwenye haki na asie na haki katika kuitetea nchi yake? Pakacha mrengu wako pengine ndio waliokosa sifa za kutetea haki za Zanzibar kwa hili la mafuta kwani ni nyie mnaofadhiliwa na hao mnaowaambia kuwa waachane na mafuta yenu. Nina hofu kuwa mrengu wako hamko serious na hili jambo kwani ni nyie mnaowapa uwezo wa kuwa na sauti kwa kitu kisicho chao. Kauli yako ya kubaguwa wapiganaji wa haki hiyo inathibitisha kuwa mnafanya kiini macho kwa Wazanzibari wenzenu. Kinyume cha hayo hebu wachieni Wazanzibari waamue kwa haki katika uchaguzi unaofuata na muweke nguvu ya pamoja katika kudai haki yenu.
Nilisema awali kuwa ni bora kila aliyetarayari kupigania haki ya wazanzibar na aingie kundini hakuna haja ya kutafutana ww nani na ulikuwa vipi, mfano tumeuona BLW kwanini tusianzie pale? tukianza ww unahitajika na yule hafai tutayafanya mambo magumu, safari bado haijaanza saivi wazanzibar hawaogopi tena "kukatwa vichwa", yapo mambo mengi tunahitaji kukaaa pamoja "kuyamezua" kutoka katika muungano ambayo hayakustahiki kuwamo,mbali na hili la mafuta, haya yanahitaji umoja and no time to waste.
 
Ni vizuri kuwa tunayakubali makosa na kutafuta sababu zake. Ni kweli kuwa CUF wanawaona Wazanzibari wenye asili ya Bara kuwa si Wazanzibari halisi lakini kwa hili tutakuwa tunageneralize suala tukisema hivyo. Kwanini? Kwasababu si kila mwenye asili ya Bara anachukuliwa kuwa si Mzanzibari halisi. Niliwahi kusema huko nyuma kuwa Uzanzibari si kuzaliwa Unguja au Pemba pekee lakini pia unashirikisha hata wale waliohamia lakini wakakukubali kuiona Zanzibar ni nchi yao na kuionea uchungu. Unapokosa sifa ya kuionea uchungu Zanzibar na ikitokea kuwa wewe si mzaliwa wa Visiwa hivi wenye visiwa watakataa kukuona kuwa u miongoni mwao. Historia ya Zanzibar inaonyesha kuwa wengi wa wakaazi wake wana msingi kutoka Bara au nchi za Kiarabu na wengine ambao ushahidi umeshapotea wanatoka Persia. Sasa utawezaje kuwakataa karibu asilimia 70 ya Wazanzibari kuwa si wazanzibari halisi? Isipokuwa huu mtindo wa sasa uliopo wa kumfanya mtu aliekuja kwa kibaruwa cha kondeni kuwa ana haki ya kushiriki katika masuala ya uchaguzi na kumuacha alietoka kisiwa cha pili asipige kura ndiyo inayoleta hii fitina ya kuanza kubaguwana. Inasikitisha kuona mtu hata lugha ya Kiswahili hajui vizuri anapokelewa moja kwa moja kuorodheshwa kuwa ni Mzanzibari kwa dhana ya kuwa huyu hatoipigia kura CUF na kunbeza yule anaezungumza moja ya lahaja za Zanzibar kwa hisia kuwa wote wanaozungumza lahaja hiyo wanaisapoti CUF.Ndugu yangu unafikiri hata ungekuwa wewe kati ya hao wanaotumia lahaja hiyo ungemuonaje yule anaependelewa na kupewa haki iliyokuwa yako?
Kwa mtaji huu ipo siku Wazanzibari mtakuja kujuta, hapo mtakapoambiwa mpige kura ya maoni na washiriki ni Wazanzibari wenye vitambulisho, kazi kwenu walio na uchungu na visiwa mshawanyima nafasi. Mjisahihishe ili mpiganie haki katika Muungano.
you remind me of those Mfaranyaki, Abdul aziz A.K Twala, O.Shariff,Ubwa Jaha, A. Majura walikuwa wazalendo licha ya baadhi yao uasili wao kuwa wa mbali na visiwani.
 
Isipokuwa huu mtindo wa sasa uliopo wa kumfanya mtu aliekuja kwa kibaruwa cha kondeni kuwa ana haki ya kushiriki katika masuala ya uchaguzi na kumuacha alietoka kisiwa cha pili asipige kura ndiyo inayoleta hii fitina ya kuanza kubaguwana. Inasikitisha kuona mtu hata lugha ya Kiswahili hajui vizuri anapokelewa moja kwa moja kuorodheshwa kuwa ni Mzanzibari kwa dhana ya kuwa huyu hatoipigia kura CUF na kunbeza yule anaezungumza moja ya lahaja za Zanzibar kwa hisia kuwa wote wanaozungumza lahaja hiyo wanaisapoti CUF.Ndugu yangu unafikiri hata ungekuwa wewe kati ya hao wanaotumia lahaja hiyo ungemuonaje yule anaependelewa na kupewa haki iliyokuwa yako?
Zenj kuna utaratibu mzuri tu wa kuingia kwenye Shehia, unachotakiwa kufanya ni kuripoti mara moja kwa Sheha wa Shehia husika mara tu unapoingia katika Shehia yake.
Sheha anabuku la waakazi wake ambalo ndio linotumika kujua sifa ya mpiga kura visiwani humo. ZEC hupokea majina toka kwa Masheha ili kuweza kuandikishwa kwenye buku lao na kuweza kupiga kura.

Umuhimu wa Sheha katika ZEC ulikuja mara baada ya kutangazwa kwa mfumo wa vyama vingi hapo Tanzania. Marehemu Dr. Omar Ali Juma alitangaza sifa ya anayestahili kupiga kura Zenj kuwa awe ameishi ndani ya kisiwa hicho kwa miaka mitano mfululizo. Sifa hii iliweza kuwabana Wazenj wenyewe na wahamiaji ambao walikuwa bado kutimiza miaka mitano tokea kuhamia kwao.

Ikumbukwe kuwa hata kama unasafiri nje ya Zenj unapaswa kumuaga Sheha wako. Kimbembe kilikuja pale mtu fulani toka Pemba(huu ni mfano) kahamia katika Shehia ya Tomondo bila kutoa taarifa kwa Sheha, na ameishi zaidi ya miaka mitano, lakini kwa kuwa Sheha hana kumbukumbuku katika buku lake jamaa huyu alipoteza sifa ya kupiga kura. Hali kadhalika kwa wale ambao walikuwa wanaishi labda niseme Bara kwa ajili ya biashara zao za muda maalumu na maskani/nyumbani kwake bado ni visiwani, lakini kwa kuwa hajaishi miaka mitano mfululizo alipoteza haki yake ya kupiga kura. Hapa ndio tatizo la malalamiko ya kunyimwa haki ya kupiga kura lilipoanzia.
 
Hamna tatizo lolote lile ,kura mnakwiba na kutangaza matokeo batili ,mnatangaza matokeo kwa mtutu wa bunduki ,hilo linajulikana Zanzibar nzima ,kwani hao wana andikishwa kutoka bara wakifika kwenye sanduku la kura hawaipigii CCM ,na CCM wanalijua hilo ila hawana la kufanya zaidi ya kujipa moyo ,jamani hakuna anaeitaka CCM iendelee madarakani watu wamesha choka nayo huna la kuwambia wala la kuwalisha kinachotakikana Zanzibar ni tume ambayo itakubali kuuwawa lakini itangaze matokeo kwa mujibu wa matokeo sahihi ya uchaguzi. Ndio mkasikia hata mkiwaamsha waZanzibari manane ya usiku iwe wanapiga kura huku wana maruerue au wamelewa ulevi wa tende basi kura yao haiendi kwa CCM si Unguja si Pemba na hilo CCM wanalielewa.
 
Si mweledi sana kuhusu sheria za uchaguzi. Lakini nafikiri kamwe hazimnyimi Mzaliwa wa Zanzibar kupiga kura na zikampa tu Mkazi Mhamiaji. Kama yupo kisiwa cha kwanza na anatoka kisiwa cha pili- na hajatimiza muda unaohitajika kukaa pale kisiwa cha kwanza hanyimwi kupiga kura bali huambiwa akapigie kura katika sehemu ya kisiwa cha pili anakotoka- Jee huko pia akirudi hukataliwa? na jee huko kurudi kupiga kura kunamgharimu kiasi gani au kuna usumbufu wa kiasi gani? Hata halazimiki kupanda ndege. Usizungumzie mambo juu juu tu na kulaumu Ndugu yangu -hayo ya kurusha lawama zisizo na msingi ni msimamo wa mrengu nule wa watani.

Ndugu yangu ni bora unyamaze yaishe iwapo hutaki kuukubali ukweli. Ninayokwambia ni yakweli nawe mwenyewe unajuwa hilo. Ukianza kushutumu na kusema kuwa niyasemayo ni uongo bas pengine kama ulivyosema mwenyewe nitaacha kusema juujuu na kuingia ndani zaidi lakini bado nitaenda nawe kwa mujibu wa hadidu rejea unazozipenda.

Sawa! Sheria za uchaguzi zinasemaje huko kwenu kwa mtu aliekuwa si mkaazi wa pahala anapotaka kupigia kura? Sheria inasema kuwa mtu huyo hatopigakura ya mwakilishi tu bali mbunge na Rais atakuwa na ruhusa ya kujiandikisha na kupiga kura. Sasa hili la mtu wa kisiwa cha pili kuambiwa arudi alikotoka linakujaje na akienda kule alikozaliwa anaambiwa yeye si mkaazi hivyo hana haki ya kujiandikisha. Hii inafanyika kwasababu hao wa kisiwa cha pili nyota ya kijani imechelewa sana kufika huko hivyo wao ni wengi. Aidha huko wao hawana starehe kama mlizonazo kisiwa kikubwa.
Pakacha nina wasi wasi kuwa itikadi inakufunika macho lakini hao wenzenu mnawahitaji sana kuliko hao unaojaribu kuwatetea. Wapo wapi mliokuwa nao kwenye nafasi za juu, wengine hapo awali walisema ni Wapemba lakini baadae wakajitambulisha kuwa wao ni kutoka Tabora, wengine wamerudi kwao na tambo 'mtu kwao' na wengine mliwajengea nyumba kwa dhana ya kuwaona Wazanzibari lakini wameacha magofu yakaliwe na vizuu huku wakituma watoto wao waje kutafuta ukubwa kwa wajinga. Wasio na kwa kwenda na hata wakienda popote wanafuatana na JINA lao mnawabeza, shauri yenu 'mtumai cha ndugu.......'
 
Hamna tatizo lolote lile ,kura mnakwiba na kutangaza matokeo batili ,mnatangaza matokeo kwa mtutu wa bunduki ,hilo linajulikana Zanzibar nzima ,kwani hao wana andikishwa kutoka bara wakifika kwenye sanduku la kura hawaipigii CCM ,na CCM wanalijua hilo ila hawana la kufanya zaidi ya kujipa moyo ,jamani hakuna anaeitaka CCM iendelee madarakani watu wamesha choka nayo huna la kuwambia wala la kuwalisha kinachotakikana Zanzibar ni tume ambayo itakubali kuuwawa lakini itangaze matokeo kwa mujibu wa matokeo sahihi ya uchaguzi. Ndio mkasikia hata mkiwaamsha waZanzibari manane ya usiku iwe wanapiga kura huku wana maruerue au wamelewa ulevi wa tende basi kura yao haiendi kwa CCM si Unguja si Pemba na hilo CCM wanalielewa.
Mara ya mwisho CCM kupigiwa kura na wazanzibari ni mwaka 1990 katika uchaguzi wa NDIYO(ndo huyohuyo) na HAPANA(isipokuwa huyo),pale komandoo SALMINI alipokuwa ndo kwanza MWARI.
 
Zenj kuna utaratibu mzuri tu wa kuingia kwenye Shehia, unachotakiwa kufanya ni kuripoti mara moja kwa Sheha wa Shehia husika mara tu unapoingia katika Shehia yake.
Sheha anabuku la waakazi wake ambalo ndio linotumika kujua sifa ya mpiga kura visiwani humo. ZEC hupokea majina toka kwa Masheha ili kuweza kuandikishwa kwenye buku lao na kuweza kupiga kura.

Umuhimu wa Sheha katika ZEC ulikuja mara baada ya kutangazwa kwa mfumo wa vyama vingi hapo Tanzania. Marehemu Dr. Omar Ali Juma alitangaza sifa ya anayestahili kupiga kura Zenj kuwa awe ameishi ndani ya kisiwa hicho kwa miaka mitano mfululizo. Sifa hii iliweza kuwabana Wazenj wenyewe na wahamiaji ambao walikuwa bado kutimiza miaka mitano tokea kuhamia kwao.

Ikumbukwe kuwa hata kama unasafiri nje ya Zenj unapaswa kumuaga Sheha wako. Kimbembe kilikuja pale mtu fulani toka Pemba(huu ni mfano) kahamia katika Shehia ya Tomondo bila kutoa taarifa kwa Sheha, na ameishi zaidi ya miaka mitano, lakini kwa kuwa Sheha hana kumbukumbuku katika buku lake jamaa huyu alipoteza sifa ya kupiga kura. Hali kadhalika kwa wale ambao walikuwa wanaishi labda niseme Bara kwa ajili ya biashara zao za muda maalumu na maskani/nyumbani kwake bado ni visiwani, lakini kwa kuwa hajaishi miaka mitano mfululizo alipoteza haki yake ya kupiga kura. Hapa ndio tatizo la malalamiko ya kunyimwa haki ya kupiga kura lilipoanzia.

Laiti hao masheha wangekuwa na utaratibu kama huo unaouzungumza pengine hali isingekuwa mbaya kama ilivyo huku kwetu. Ni Masheha wangapi wana uadilifu wa kuweka daftari la wakaazi wote ndani ya shehia zao?
Kwanza masheha wote lazima wawe makada wakereketwa wa CCM na wanafuata maagizo ya CCM. Kuna wakati Masheha waliagizwa kupitia nyumba hadi nyumba kuandikisha wakaazi wa nyumba hizo lakini sikun za kuandikisha Daftari la uchaguzi majina ya nyumba za watu fulani hayakuonekana.
 
Si lazima sana Sheha kuwa kada wa CCM, nawafahamu Masheha kadhaa ambao sio makada wa CCM na wanaendelea na kazi zao kama kawaida. Wengi wanafikili kuwa Sheha lazima awe kada na kwa kuwa labda ana bendera ya Taifa nyumbani kwake au kwa kuwa anachaguliwa na Mkuu wa Mkoa.

Moja ya tatizo la Masheha wengi ni kushindwa kuwashirikisha wajumbe wake 10 kwenye maamuzi muhimu kama la kuandikisha wakaazi wa Shehia yake.
 
Ndugu yangu ni bora unyamaze yaishe iwapo hutaki kuukubali ukweli. Pakacha nina wasi wasi kuwa itikadi inakufunika macho lakini hao wenzenu mnawahitaji sana kuliko hao unaojaribu kuwatetea. '
Sawa. Ndugu yangu kwa mawaidha yako- ni muwafaka. Lakini mimi sina itikadi, sina chama cha siasa kwa hivi sasa (kwa maana ya CUF au CCM) hata nikisoma hiyo historia kama ningekuwa mtu (mzima) wa zama hizo nisingekuwa mwanachama wa ZNP (Hizbu) wala ASP (Afro-Shirazi Party) au ZPPP. Lakini kama tunaanzia na historia ningekuwa ni mwanachama wa Zanzibari Shirazi Party (ZSP) ingekuwa wazee wamefanikiwa kuunda hiyo , lakini wapi walizongwa tokea wakati huo- Hiyo inamaanisha kuwa mimi ninawashabikia na kuwatetea wale unaoweza kuwaita (sahau mambo ya ubaguzi) ni wazalendo asilia wa Zanzibar nao ni Wapemba vyoko. Watumbatu, na Wahadimu - ambao wote hao walijipachika kasumba ya ushirazi. Hawa wamekuwa victims kwa muda mrefu katika historia ya Zanzibar na wanendelea kuwa victims. Siwezi kuwatupa wenzangu asilia. Lakini hapa panahitajika kazi kubwa na hasa kuigomboa new generation katika mazonge haya. Wanababaishwa sana hivi sasa - tena katika kambi zote mbili husika.
 
Kuna wanasiasa wanatumaia ujinga wa baadhi ya ndugu zetu kuchoche itikadi hizi potofu za kibaguzi, kwa manufaa yao, tazama wakati mfumo wa vyanga vingi unaanza wapo wanasiasa waliojaribu kuuhusisha mfumo huu na harakati za vyama vya upinzani kumrudisha sultan, wengine walihusisha hata vyama vya siasa na u-hizbu na u-ASP, angalia kitabu cha "1964 ZANZIBAR REVOLUTION AND ITS ACHIEVEMENTS" by Mapuri, O.R, humo utakuta kabisha mnazungumzwa U-PEMBA NA U-UNGUJA, U-HIZBU NA U-ASP, na hata kuhusisha mfumo wa vyama vingi wa uliorejeshwa 1990s na itikadi hizo. Wazanzibar walitumiwa wakapotoshwa na mambo hayo ambayo si mwandishi tu aliyekuwa akiyahubiri bali hata chama chake kwa kuwa alikuwa mwanasiasa. Mambo haya hayana nafasi tena katika kujenga zanzibar mpya.
 
Nafikiri kuna haja ya kuweka vugu nvugu jipya sasa kukikomboa kizazi hiki kipya. Hapo zamani waliokuwa wanaweza kusema wakibanwa. Lakini sasa alhamdullillah. sasa mnaoweza kutoa maoni mshirikiane mkizindue kizazi kipya. kielewe ubabaishaji huu ambao umefanyika katika zama za ukoloni na vyama vyote hivyo- vikatumia nguvu za wazalendo (washirazi wa Kipemba, Kihadimu na kitumbatu) kujiimarisha. Baadaye mapinduzi nasikitika kuwa mapinduzi hayo hayakuwanufaisha ipasavyo hao Washirazi wazalendo
bali wameburuzwa tu huku Waafrika wakishika himaya, na sasa katika mfumo wa vyama vingi naona Washirazi hao wanaburuzwa tu(ama wawe CCM ama wawe CUF). Ukweli wao ndio wenye nguvu kutokana na wingi wao,lakini wapi bado ni victims tu. sasa hawa ni hao walioko Chokocho. Paje, Kidoti, Fumba na kadhalika siyo wenye jamaa zao Dubai, Songea, Anjuwani, Mombasa au hadharamut au London au Scandinavia.
 
Tukianza tu kuweka mipaka basi tutakuwa tukizunguka humo kwa humo. Lengo liwe kuwatetea Wazanzibari bila ya kujali kuwa hawa ni Waafrika , Washirazi, Watumbatu au wana asili ya Dubai.
Kwanini? Waafrika hawana tena kwao huko walikotoka Bara, Washirazi hawajui sehemu hasa walipotokea< Watumbatu hawana pahala pa kujinasibu zaidi ya Zanzibar< Wapemba watabaki Wapemba tu na hata hao walio na asili ya Dubai hawana pa kwenda isipokuwa Zanzibar.
Zanzibar Kihistoria ni pahala ambapo watu wa sehemu mbali mbali waliweka makazi na Zanzibar ina bahati kuwa hata katika zama hizi za sasa anakuja huwa anapenda aweke makazi, hivyo kuishi kwa historia si sahihi.
Hili suala la Waafrika kuchukuwa madaraka na kuwaacha Wazanzibari asilia linaletwa na nguvu kutoka upande wa pili wa Muungano na wanafanya hivyo kwa faida zao wanazozijuwa. Wengi wape na ni jukumu la wengi kupigania haki ya kuwa na sauti katika nchi yao lakini kama ulivyosema wanasiasa wanawatumia wananchi kwa uasilia wao kupata manufaa yao.
Well, haya ni matatizo ya ndani ya Wazanzibari lakini kwa sasa wanatakiwa wawe pamoja kukabiliana na tatizo linalowakabili la kunyimwa haki zao kwa kisingizio cha Muungano. Pengine ingekuwa vizuri kama tofauti za Wazanzibari zingetatuliwa kwanza na kupata nguvu ya kuikabili upande wa pili wa MuunganolLAKINI muda huo haupo na hivyo wapambane na kurejesha haki zao kwanza na baadae wakae na kuondosha tofauti zao.
 
kwanza wakae waondoshe tofauti zao wakubaliane kufanya siasa za maendeleo ya watu, ambazo hazitatazama PEMBA imekosa ngapi na UNGUJA imepata ngapi bali ZANZIBAR inapata ngapi na WAZANZIBARI wa UNGUJA na PEMBA wanafaidika vipi.Kupambambana na maadui wa zanzibar(ujinga, maradhi na njaa n.k) kusihusishwe na itikadi ya chama chochote bali itikadi za wananchi za kutaka maendeleo, WAZANZIBAR wapewe fursa ya kuchagua wanachokitaka ambacho wanaamini kitawanufaisha. Haya yanaweza kufanyika kama kizazi kipya kitafuta sumu mbaya zilizopandikizwa na wazee wetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
 
Unajua hawa wazanzibari bi bora wajitoe kwenye huu muungano, kila siku tunapiga kelele kuhusu muungano. Tanzania bara iachane na hao wazanzibari tuone kama hata hayo mafuta watayachima. Namshangaa sana Maalim Seif anapiga kelele sana kuhusu haya mafuta. Yani hii yote inaonyesha kuwa hawa wanzanzibari ni wabaguzi sana kwa nini tuna wang'ang'ania??????
 
THE FARMER,
kama umesikia "kelele" za mafuta basi hakupiga Maalimu Seif, "kelele" hizo wamepiga wazanzibar wote kwa pamoja kupitia WAWAKILISHI wa majimbo yao,"kelele" hizo zimekuzibua masikio yako mpaka unapandisha munkari hivyo na kutaka Muungano uvunjwe.Pengine kweli WAZANZIBAR wabaguzi lakini kwasababu tu wamesema "nyinyi mmetunyima almasi zenu na gesi na kutubagua katika mapato yake na sisi tuwachieni mafuta yetu japo robo kikombe" wala WAZANZIBAR hawan'gan'ganii Muungano bali wana'nga'nganiwa kubaki katika MUUNGANO, na wamewekewa chombo cha kuwalazimisha(ccm)
 
Nimekupata Junius, lakini kitu ambacho Wazanzibari hakijui nikwamba wananufaika na haya Madini yaliyoko Tanzania bara kupitia serikali ya Jamuhuri ya Muungano. umeme umetoka huku Bara. Wanataka kila kinachotoka huku waambiwe fungu limetoka kwenye sector gani???
 
nimekupata junius, lakini kitu ambacho wazanzibari hakijui nikwamba wananufaika na haya madini yaliyoko tanzania bara kupitia serikali ya jamuhuri ya muungano. Umeme umetoka huku bara. Wanataka kila kinachotoka huku waambiwe fungu limetoka kwenye sector gani???
hebu nieleweshe zaidi hapa, kama wenyewe huko tanzania bara wananchi wanalalamika kuwa hawafaidiki na rasilimali hizo, itakuwa zanzibar!?
 
Back
Top Bottom