Pakacha, unajua Unguja na Pemba ziko ndani ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania. Lakini nyinyi(Wanzanzibari) hamlijui hilo. TPDC ni chombo kinacho shughulikia maswala yote yanayohusiana na maswala ya mafuta yaliyoko Tanzania.
Sasa hicho chombo kingine kinachotoka kuundwa kwa ajili ya mafuta ya Zanzibar kinatoka wapi. Kwa kifupi mikataba yetu ya madini haikuwa mizuri kunatokana na TAMAA za vionozi wetu wakasaini mikataba mibovu. Hakuna kodi ila kuna Royality ya 3% kwa kisingizio kuwa makampuni ya madini hayapati faida.
Sasa tunapokuja kwenye swala la mafuta linakija swala la Tanganyika na Zanzibar, na mnasahau kuwa Zanzibar inaitwa hivyo kwa sababu ya muungano, nje ya muungano hakuta kuwa na kitu kinachoitwa zanzibar, Wapemba watakuja juu na kusema mafuta ni ya kwao kwa sababu ndiko yanapopatika. Mwishoe mtabaki na Unguja na Pemba kila mtu kivyake vyake.Wanzanzibari jaribuni kutumia hata muda kidogo kufikiri kuhusu swala hili na sio kukurupuka tu na kuanza kusema tuanzishe chombo cha usimamizi wa mafuta ya Zanzibar. Utafiti umefanywa na serikali ya muungano sasa kumeonyesha dalili za upatikanaji, nyie mnaanza kusema mafuta ni ya Visiwani na sio ya Tanzania Bara.