Mtaimba sana tu maana ngonjera za wafuasi wa Sultani CCM ndio utamaduni wao ila kwa mafuta mtamaliza kwaya zote hapatolewi kitu.

Halafu fikiria kinachopatikana kwenye mafuta ya nafaka na kinachopatikana kwenye mafuta ya ardhini naona unafananisha mpapai na mnazi 😀
 

1. Heee -- kumbe rais wenu anazunguka na umati mkubwa huo wa mawaziri -- kwa maendeleo gani yanayofanyika huko kutokana na hao?

2. Wewe tutakuamini vipi kama unasema ukweli?
 

Mambo yote mambo gani yataje halafu tulinganishe tuone isije kuwa watu wanaisabu nazi wewe unaisabu makumbi ?

Kwa taarifa yako karafuu imegunduliwa kuwa inauwa na kuyeyusha maradhi ya saratani ,process underway to produce mass drugs for cancer treatment semeni basi karafuu ziwe za muungano ,ikiwa mmeshindwa kuvuna matunda kamili ya mali asili na madini mtayaweza mafuta au ni kutafuta njia za kupachika mirija baada ya huko kuanza kuvutana mashati itabidi muuwe kama mlivyouwa Pemba ili kumsimika Sultani CCM kwenye madaraka sio Karume ,CCM maana karume mshamuona hafai kuwa Raisi wa Tanganyika aka Tanzania ,ilikuwaje mkamuweka awe Raisi wa Zanzibar kama si kutaka kumwibia. Au uongo jamani ?
 
Wamekutana na uamuzi wa mazungumzo yao ni kuwa waskubali kwa hila zozote zile kuyafanya mafuta kuwa katika Muungano hata wabara wakija na kutaka kuyaweka madini katika Muungano hilo ndio kabisa walifanye haliwezekani tena kwa sasa kwani hayo madini wameshagawana na wamegusia mfano wa Green Belt kule Mwanza kuwa umeshauzwa kwa wawekezaji kwa bei poa.Hivyo wasitetereke walipokamata ndio hapo hapo na zaidi ikiwezekana kuulizia uhalali wa Muungano katika vyombo vya kimataifa.Kazi mnayo waBara katika kuisaka hazina ya Zanzibar mafisadi lazima mtoke ndevu za ulimi.
 
Hivi hili swala la Tanzania kutaka mafuta ya zanzibar ni tetesi ama kunania hiyo kweli? Imejidhihirisha wapi? Kuna any official statements?
 
Hivi hili swala la Tanzania kutaka mafuta ya zanzibar ni tetesi ama kunania hiyo kweli? Imejidhihirisha wapi? Kuna any official statements?
Si suala la Tanzania lutaka Mafuta ya Zanzibar , uelewe kuwa kinachopiganiwa hapa ambacho WaZanzibari na Serikali yao wapo pamoja ni mgawo ambao utafaidisha serikali ya Zanzibar katika kuweza kujiendeshea mambo yake ,katika ufukunyuzi imeonekana kuwa tokea dili la utoaji leseni hakuna kilichoingia katika serikali ya Zanzibar mpaka kunatafutwa mikakati ya kuyabukua mafuta hayo Zanzibar haina habari kwa maana haina washiriki katika hiyo unayoisikia TPDC ina mjumbe hazimi wala hawashi yumo tu akibeba mifuko akifanyacho hakijulikani ,ila Zanzibar walikuwa wanatupia jicho harakati za TPDC Tanganyika Petroleum Development Company na waliizuia kampuni moja kufanya au kuendelea na uchunguzi baada ya kubainika haina ridhaa ya kupekua eneo la Zanzibar kusaka hazina ,na kampuni hiyo ilisimama sasa wewe watafute uwahoji hao waliosimamishwa au mkuu wa hiyo TPDC umuulize kwa nini aliridhia kampuni ile isimamishwe wakati ilipata baraka za serikali ya Muungano hapo utapata jibu litakalokuridhisha au kamuulize yule mzee aliekuwa akifanya kampeni za urasi kwa mahelikopta ilikuwa aliambiwa helikopta yake ikionekana katika anga za Zanzibar itadunguliwa ,ni ubabe tu wa utawala wa Sultani CCM hivyo uelewe hizi nchi mbili yaanio Tanganyika na Zanzibar zinaendeshwa na sheria za macowboy katika kugombea hazina ,sasa hapa tulipofikia macowboy wetu wamefikia ile stage ya kila mmoja anakimbia na fuko la fedha.
 
Sina tatizo na na wazanzibari kung`ang`ania kuwa mafuta si jambo la muungano ila nawaomba wajue kuwa hata suala la chakula si suala la muungano kwa hiyo wajiandae kununua chakula kwa dola au hela za kigeni kila kilo ya mahindi na mchele na vyakula vyote kutoka Tanzania bara kwani vitu hivyo si suala la muungano.

Wafanyabishara wa nyanya ,mchele,unga na kadhalika anzeni kuwalazimisha wazanzibari wawalipe kwa hela za kigeni kwani vyakula si sehemu ya muungano inabidi wawalipe kwa hela za kigeni maruhuni wa kizanzanzibari na msiwaonee huruma.

Wafanyabiashara wa Tanzania Bara Amkeni huu ni wakati wa kujipatia hela za kigeni.

Wao wanasema Zanzibar ni Nchi hivyo wauzieni kwa hela za kigeni vyakula VYOTE Toka bara wakiwemo pweza.
 
Lazima mjifunze kupanda mtumbwi ili kuja kuuza vyakua vyenu la si hivyo vitaozeana hapo sokoni pweza wanatoka msumbiji kawaulize watu wa mtwara kila asubuhi boti kutoka msumbiji zinafika na frozen pweza ila sijui kama kuna ushuru wa bandari unajua mipaka yetu ipo open jamaa wanaingia na kutoka kwenye shamba la Babu Nyerere.
 

1. Umeambiwa kwamba visiwani hawana chakula mpaka wanunue kutoka bara?
2. Kama wadanganyika wananunua ma-apples kutoka afrika ya kusini wazanzibari watashindwaje kununua chakula nchi nyingine?
3.Wazanzibari chakula chao wanaongezea tu lakini kuna vyakula ambavyo hata bara hawana.
4. Kama ni njaa watakula mashelisheli yao na pweza kutoka bahari ya zanzibar.
5 Kama unajua nikwamba chakula kikuu cha wazanzibari ni wali je unajua mchele unakotoka? tukiacha baadhi ya baadhi ya mchele unaotoka bara ambao ni asilimia hata kumi haifikii.
6. Unaijua Zanzibar au unaisikia tu kwenye radio na TV?
 
Mwiba,
Katika swala la mafuta nipo pamoja na serikali ya Zanzibar isipokuwa tu kinachonishinda kuelewa ni kwamba huyo Sultan CCM (baraza la Mapinduzi) ndiye mgongo wa hoja hii kwa Wazanzibar.
Katika mfumo wowote ule wa Muungano au serikali za Majimbo, mali inayopatikana ktk nchi au jimbo moja huwa ni mali ya eneo hilo isipokuwa hutoa mchango wake kwa serikali kuu...Serikali zote kwa ujumla hufaidika na kodi inayokusanywa hivyo kuwepo kwa kodi ya serikali kuu na ile ya nchi ni muhimu ktk kuondoa matatizo ya milki..Ni matatizo ambayo tunayaona kila kona toka Nigeria, Sudan hadi nchi ambazo hazijajenga mfumo bora wa Kiuchumi zaidi ya muungano wa Kisiasa.
Ikiwa leo hii dhahabu ya Bulyanhulu ni mali ya bara na bara tunawakatia Zanzibar ktk fungu la jimbo iweje sisi tuanze kudai mali itakayo patikana Zanzibar ni yetu wote!..
Zanzibar ni nchi na ina RAIS wake, muhimu sana tuheshimu kitu hicho kwa kukubali kwamba Zanzibar ina serikali yake ktk maswala ya Zanzibar...
Pia ni muhimu sana tufahamu nafasi ya Zanzibar ktk Muungano badala ya kuchanganya maswala yote ktk sahani moja..
 


Hivi Maalim seif alikuwapo ndani ya lile baraza la wawakilishi waliokuwa wanajadili na kukubaliana kuwa mafuta yabaki ya wazanzibari?wacha hizo za kuleta zisizokuwa na kichwa wala miguu zungumzia nini kinazungumzwa sasa ndani ya SMZ na baraza tukufu la wawakilishi. (PILI PILI USIO ILA WEWE INAKUWASHIANINI)
 
naend kusaka data za mafuta ya zanzibzr najua ni tiki tu ,sasa ka mndai kidogo ,ndio tumeshawambia tutajipaka
 
The oil in Tanzania's coastal belt was discovered in the 1960s but it is only recently, with western governments searching for alternative sources to the Middle East, that these paradise isles are being taken seriously as drilling sites. With negotiations on Zanzibar bogged down between the island and the mainland over which should benefit (semi- autonomous Zanzibar is unhappy with a proposed 60:40 split of profits), Mafia and its tiny neighbour Chole seem likely to be the first to see exploration, perhaps within a year.

Mafia and Zanzibar are part of a lush reef-based network of islands and atolls dotted along Tanzania's Indian ocean seaboard. A slowly growing tourist destination, Mafia is about 30 miles (50km) long and 10 miles (17km) wide, surrounded by a host of tiny islets. It has a population of 50,000. The capital, Kilindoni, is a one-horse, or half-a-horse town. There are no telephones and only a few cars
 
Tena wazanzibari Bwana-Masikini jeuri- wanasema huo mchele wenu wa Bara unanuka kupuo hausarifiki kwa pilau wala biriani, Hivyo wanaubeza wanapendelea wa Thailand.
 
Hakuwepo Bwana, Lakini CUF wana siasa za uharamia. Hili suala la mafuta wanataka kufanya mtaji wao. Wanatumia sera zile zile za ku-capitalize on public ignorance. Lakini kwa hili CCM (hasa CCM Zanzibar au niwe wazi SMZ) wako macho. Kuna tofauti kuhusu mafuta yanavyozungumzwa kati ya CUF na CCM Zanzibar (au labda niwe wazi SMZ). Kwa sasa wote wanaonekana kuwa na mbiu moja lakini njia zao ni tofauti kabisa. SMZ hailengi katika kuvunja Muungano hata siku moja-hata iweje vile. Lakini inatetea maslahi ya Wazanzibari , kwani hilo si ndio jukumu lake?
 
Kwa maneno mengine una maana kuwa CUF wana ajenda ya kuvunja muungano kupitia mafuta?
 
we Pakacha vp bwana! nani kakambia kuwa cuf wanalifanya suala la mafuta mtaji wao? suala hili limeingizwa na vibaraka wa Nyerere katika Muungano kabla ya chama cha CUF kuundwa siku hizo, na wazanzibar tokea siku hizo walikuwa wakipinga, sasa hii ni ajenda ya SMZ au ya wazanzibar. Ujue Pakacha ww usianze kuvuja mpaka mzigo wa nazi, Hata kama SMZ haitakuwapo taifa la zanzibar litakuwapo, Hata kama CUF haipo zanzibar itakuwapo, hata kama CCM haitakuwapo zanziba palepale na wazanzibari watakuwepo, Suala la mafuta ya zanzibar ni ajenda ya wananchi wa zanzibar na si CCM,CUF au vibaraka wa ukoloni wa Tanganyika (SMZ).
 
Zanzibar ilijitegemea kwa chakula kabla ya muungano,wala zanzibar haitakufa njaa ikiwa Tanganyika haitauza hata kipande cha mkate wa Bakhressa.Ukisikia zanzibar kuna ziki ujue imeletwa na huo unaoitwa muungano wa kinafiki.Leo hi muungano huu ukurekebishawa na kuwezesha zanzibar kujitaftia yenyewe, hatakuwa mbali na Singapore.Ila nynyi mtalazimika kumba viza kuja zanzibar na ubalozi wa kwa kuombea visa utawekwa Nairobi.
 
Kweli kabisa huu Muungano unazifanya nchi mbili hizi kuzidi umasikini ,faida inayopatikana ni kwa mafisadi wachache ,ila baadhi ya wafuasi wa Sultani CCM hufaidika kwa kugaiwa vyeo uchwara na kupata mshahara mnono ambao akifukuzwa kazi havuki hata miaka miwili anarudi na kuwa ombaomba au zaidi ,wapo kibao ambao walikuwa Walikuwa wafuasi wa Sultani CCM katika safu ya Ujeshi.upolisi na kwengineko leo hii huwezi amini kama walikuwa wakubwa pale walipokuwa wakitumika. Hakuna pension wala nini ,na ukienda kudai wanakuitia polisi kama wewe ulikuwa sie mwenzao.

CUF italiondoa tatizo hilo na kusahaulika kabisa unamaliza kulitumikia Taifa basi taratibu za kisheria ni haki yako kutimiziwa , maana Serikali ya CCM haiwathamini tena hata wale veteran waliokwenda kupigana Uganda wapo kibao ambao hadi leo hawajalipwa na wengine walipoteza viungo na hawapati msaada wowote ndio faida ya kuitumikia CCM kwa hali na mali ukichanganya na roho ila sera zao huna thamani wewe ni mtu wa kutumika tu wakifaidika wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…